Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Gairo akamatwa na Polisi kwa tuhuma ya wizi wa mabati

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Gairo akamatwa na Polisi kwa tuhuma ya wizi wa mabati

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Morogoro.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale anashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma ya wizi wa mabati 1,100 mali ya halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Muslimu amesema hayo leo Jumanne Agosti 24, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Muslimu amesema kutokana na wizi huo watu wengine saba wanashikiliwa na wanadaiwa kushirikiana mkurugenzi huyo na wanaendelea kuhojiwa.

Awali Mwambambale alikuwa mkurugenzi wa halmamshari ya Kilosa kabla ya kuhamishwa halmashauri ya Gairo.

Wizi wa mabati hayo ulifanyika Juni 17, 2021 eneo ya ujenzi kitongoji cha Mvumi B wilayani Kilosa katika stoo ya halmashauri hiyo ambayo haikuvinjwa ambapo stoo hiyo haikuvunjwa.

mkurugenzipicc.jpg

 
Daah uchunguzi ufanyike hii inaweza kuwa imetengenezwa.
 
Tatizo ni la aliyewateua. Mtu anagombea nafasi ya kisiasa kwa kuamini anastahili kuwa mwansiasa, rais anamteua kuwa mkurugenzi, nafasi ya utendaji serikalini. Hata hivyo si tunaona sasa uelewa na rais wetu? Powa!
Mweupe sana huyu mtu.
 
Kwani makada wa CCM huwa mnachagua cha kuiba?

Mwizi ni mwizi tuuu na mwizi ni mwizi tuu sio itikadi, imani wala kabila
Kule chadema hawana mabati lakini; wanaiba pesa, mwanaibwa wao na wenye pesa, hadi uwanaume na uwanamke kule unaibwaaa
 
Back
Top Bottom