TANZIA Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia

Kuna hii nyingine ya juzi juzi hapo baada ya Magufuli kudhibiti uuzwaji wa dhahabu nje ya wilaya.

Sasa Sauli alidakwa alikuwa na wenzake anatorosha hizo dhahabu.

Akawekwa jela wakati huo alikuwa akitamba na gari yake ya Amarok. Polisi wakai-seize hiyo gari wakati jamaa yupo jela.

Katika harakati za kuhangaika kutoka jela, jamaa akatoa toa hela mwisho wa siku akaachiwa.

Sasa wakati anaachiwa zile lile gari yake bado ikawekwa kizuizini.

Jamaa akamwambia afande "naomba unirudishie gari yangu kama ambavyo umenirudishia mkanda wangu wakati natoka jela"
 
Kesi iliyopo mahakamani polisi hawanaendelei ku seize mali ya mtuhumiwa inakabidhiwa Mahakama akishinda kesi anaerudisha mali ni mahakama polisi hana power ya kuzuia.
 
Kesi iliyopo mahakamani polisi hawanaendelei ku seize mali ya mtuhumiwa inakabidhiwa Mahakama akishinda kesi anaerudisha mali ni mahakama polisi hana power ya kuzuia.
Sidhani kama hata kesi hiyo iliamuliwa mahakamani, nadhani zilitembezwa hongo tu kwa mapolisi kuua soo.
 
Tumepokea taarifa ya ajali ya gari ndogo ambapo mmiliki wa Mabasi ya kampuni ya Sauli Luxury Solomoni Mwalabhila amefariki dunia kwenye ajali hiyo.

Tajiri huyo amepata ajali na kupoteza maisha Mlandizi karibu na lilipoungua moja ya basi lake mwaka Jana.

Alikua na Watoto na mke .


Sauli amefariki kweli ni mzawa wa chunya kata ya chokaa kijiji cha igodima mpk ss kijiji kina majonzi makubwa sana.

Pichani ni marehemu enzi za uhai wake.
 

Attachments

  • 1722772578501.jpg
    320.3 KB · Views: 7
Hiv serikali haijawahi kuwaza kuipanua Morogoro road at least kila mwaka km 30 tu...mwaka huu mnaishia mlandizi, ujao chalinze, ujao Bwawani, mwingine mikese, mwingine Morogoro...

Njia sita mpaka mlandizi...mnaachq njia kati kwa ajili ya BRT... then njia mbili mlandizi mpaka chalinze...mkikaribia mnapiga niia sita tena...then njia mbili mpaka Morogoro mkikaribia mnapiga njia sita tena.
Viongozi jengeni nchi yenu. Hapa ndo kwenu

Wamaweza ila hawajaamua tu
 
RIP Saul. Uliiheshimisha tasnia ya usafiri wa mabasi nchini Tanganyika.
 
Mmiliki wa Mabasi yaliyokua yakiitwa Sauli sio Tajiri wa Tukuyu Landmark?
 
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa kamili hapo chini

MMILIKI WA MABASI YA SAULI AFARIKI DUNIA

Mmiliki wa mabasi ya kampuni ya Sauli, Solomon Sauli (40) amefariki dunia leo Agosti 4, 2024 katika ajali ya gari iliyotokea mapema leo eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kufafanua kuwa ilihusisha magari matatu; moja aina ya Fuso lililo feli breki na kuligonga gari aina ya Jeep, ambalo nalo liligonga gari jingine aina ya Vowo lililokuwa limebeba kokoto.

Marehemu alikuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka minne, ambae amepata majeraha madogo na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Kituo cha Afya, Mlandizi.

R. I. P Boss😭😭😭😭
 

Attachments

  • 1722773468320.jpg
    463.5 KB · Views: 8
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…