TANZIA Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia

Attachments

  • FB_IMG_1722778676362.jpg
    FB_IMG_1722778676362.jpg
    58 KB · Views: 5
Mi pia nina mawazo kama ya kwako.
Barabara ya Morogoro imezidiwa sana.
Madereva wengi hasa wale wa masafa marefu wanaendesha wakiwa wamechoka sana.
Lakini mara kwa mara namsikia ndugu Kafulira anapigia debe kampuni binafsi zijenge barabara za aina hiyo kwa kulipia.
Kwanini tulipie wakati tuna serikali, inayokusanya kodi zetu.
Serikali ijenge hata km 50 kwa mwaka.
Wanaweza sema they don't care. As if Tanzania sio kwao....
Na mbaya zaidi hii barabara inawaua hata wao na mav8 yao wakipita.

Mimi toka SGR imefunguliwa sipandi tena magari kwenda Morogoro au Dodoma. Wacha nikate ticket hata week 2 kabla...
Maana siku hiz zinajaa hatari
 
Sema haya madude malori na magari ya mizigo ni kuwa makini mda wowote yanakutoa roho, hata hivyo barabarani ni kuwa makini napo sana, spidi kali wazee inaua acheni utani, Mimi huwa nashangaa sana dereva anaongea na simu barabarani au anaangalia video then yupo sehemu hatari sana aisee, mazoea huua...acheni mazoea, kufa utakufa lakini usijipeleke mwenyewe.

La mwisho, dereva lazima ujue TZ hii Kuna maeneo kama Yana laana vile, usipokuwa makini unakufa kweupe tena eneo la kawaida tu.
 
AJALI YAMUUA MMILIKI WA MABASI YA SAULI

Mmiliki wa mabasi ya Sauli, Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri.

Mwandishi wetu wa Pwani ameeleza kuwa ajali hiyo ilihusisha magari mawili yaliyokuwa katika sehemu moja gari namba T213 DQD aina ya Fuso.

Imeelezwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu ya kiufundi na kuligonga gari aina ya Jeep lenye namba za usajili T466EGW alilokuwemo mmiliki wa Sauli ambapo liligonga gari jingine aina ya Howo la kubebea kokoto.

Marehemu Sauli mkazi wa Mbeya alikuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka minne ambaye alipata michubuko na alipelekwa hospitali kabla ya kuruhusiwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti kituo cha afya Mlandizi.

Sauli alikuwa mmiliki mabasi ya Sauli yaliyowahi kufanya safari za Dar Es Salaam - Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

1000533551.jpg
 
Kibaha. Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Sauli, Solomon Mwalavila amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Mlandizi mkoani Pwani.

Akizungumza na kwa njia ya simu na Mwananchi Digital leo Agosti 4, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema Mwalavila amefariki leo baada ya gari lake kugongwa kwa nyuma na lori la mchanga.

"Ndiyo hilo tukio limetokea leo saa 12:30 asubuhi maeneo ya Mlandizi alikuwa anatoka Dar es Salaam kuelekea mikoani gari lake likagongwa na lori la mchanga kwa nyuma na akapoteza maisha papohapo," amesema.

Lutumo amesema ndani ya gari marehemu Mwalavila alikuwa na mtoto wake, Midrick Solomon mbaye amepata majeraha madogomadogo maeneo mbalimbali ya mwili wake.

"Huwa ana kawaida ya kusafiri na mtoto wake huyo kila anaposafiri hivyo wakati anapata ajali walikuwa wote" amesema.

Amesema wanamtafuta dereva wa lori la mchanga aliyesababisha ajali hiyo, Ramadhani Mkusa mkazi wa Zegereni Kibaha ambaye ametoroka.

“Tunamtafuta dereva huyo na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mlandizi Kibaha,”amesema.

©Mwananchi
 
Tumepokea taarifa ya ajali ya gari ndogo ambapo mmiliki wa Mabasi ya kampuni ya Sauli Luxury Solomoni Mwalabhila amefariki dunia kwenye ajali hiyo. Tunatoa pole sana kwa Kampuni ya Sauli Luxury.

Ajari ya barabarani imeondoka na roho ya mmiliki wa mabasi ya Sauli Luxury siyo mbali sana na ilipopata ajari basi yake mapema mwaka huu Kibaha na kuwaka moto na yeye pia mmiliki ajari imemwondoa maeneo ya Mlandizi leo hii asubuhi akiwa na gari binafsi

Atakumbukwa kwa kuleta upinzani wa huduma na kufikisha abiria kwa haraka kampuni zake kwa wasafri wa nyanda za juu kusini.

Hasa kwa sisi wanazi wa Scania tutamkumbuka sana mwamba kwa kuziheshimisha Scania road.

Rest in peace Mwilabila Sauli

======

Mmiliki wa mabasi ya Sauli, Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Mlandizi mkoani Pwani majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri.

Mwandishi wetu wa Pwani ameeleza kuwa ajali hiyo ilihusisha magari mawili yaliyokuwa katika sehemu moja gari namba T213 DQD aina ya Fuso.

Imeelezwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu ya kiufundi na kuligonga gari aina ya Jeep lenye namba za usajili T466EGW alilokuwemo mmiliki wa Sauli ambapo liligonga gari jingine aina ya Howo la kubebea kokoto.

Marehemu Sauli mkazi wa Mbeya alikuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka minne ambaye alipata michubuko na alipelekwa hospitali kabla ya kuruhusiwa.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti kituo cha afya Mlandizi.

Sauli alikuwa mmiliki mabasi ya Sauli yaliyowahi kufanya safari za Dar Es Salaam - Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Azam TV

Utajiri wa manyoka ndo tabia zake,ata biashara zake zitayeyuka sasa hvi
Apumzike kwa aman mwamba wa chunya
 
Back
Top Bottom