Mkurugenzi wa NIDA atakiwa kujieleza kwanini asifutwe kazi

Mkurugenzi wa NIDA atakiwa kujieleza kwanini asifutwe kazi

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola amemwagiza Mkurugenzi wa NIDA kukutana naye kwenye ofisi za NIDA Lindi tarehe 11 January, huku akiwa na maelezo ya kutosha kuhusiana na ucheleweshaji wa vitambulisho ili asifutwe kazi.

Chanzo: Watetezi TV
Debe tupu .....

Wahenga walisema
 
Nchi haina hela

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati wakitangaza zoezi hili la kusajili line zote za simu walitumani ungetokea muujiza mbele kwa mbele kuwamilikisha watu vitambulisho vya utaifa? Fine waziri mwenye dhamana atamuwajibisha mkurugenzi, naye anaweza kuwajibishwa na aliyemteua, mwisho wa siku hata wa mwisho kuwajibisha naye atalazimika kujiwajibisha kwa kuidhinisha miradi ambayo haikufanyiwa upembuzi wa kina kabla haijawa implemented!
 
Mmepatia budget ya kutoa vitambulisho? asilimia kubwa ya uchelewaji kutoa vitambulisho ni serikali kushindwa kutoa fungu bhana , vitambulisho vimewashinda miaka mitano sasa mmeamua kukimbilia kutoa namba , vitambulisho hadi vitoke makao makuu wapi na wapi? kwa nini msiwe na centralized system nchi nzima katika vituo vya polisi au uhamiaji? kubalini watu wa cyber cafe wawatolee pindi wakipata namba kutoka kwenu ni haraka na rahisi, mtu apate namba aende akapige passport size aende cyber kutengenezewa kitambulisho dakika chache tu Mambo yanakamilika , akili za IT hamna mnatumia ubabe tu kila mahali.
 
Mawaziri wa namna hii ndio wanashusha hadhi ya uwaziri. Aliwasema makamanda wa polisi wafukuzwe, wakabaki. Leo anamsema mkurugenzi wa NIDA.

,
 
Kuna ile link waliolazimisha watu ku-share kuhusu yao kupitia watu nane WhatsApp, lazima ku-share au mtu huwezi kupata details zako. Sijui nani aliwaambia wananchi wote wanatumia WhatsApp!!!

Hadi leo kuna watu wameshindwa kucheki info zao
 
Mmepatia budget ya kutoa vitambulisho? asilimia kubwa ya uchelewaji kutoa vitambulisho ni serikali kushindwa kutoa fungu bhana , vitambulisho vimewashinda miaka mitano sasa mmeamua kukimbilia kutoa namba , vitambulisho hadi vitoke makao makuu wapi na wapi? kwa nini msiwe na centralized system nchi nzima katika vituo vya polisi au uhamiaji? kubalini watu wa cyber cafe wawatolee pindi wakipata namba kutoka kwenu ni haraka na rahisi, mtu apate namba aende akapige passport size aende cyber kutengenezewa kitambulisho dakika chache tu Mambo yanakamilika , akili za IT hamna mnatumia ubabe tu kila mahali.
Nimekupa line sio kwamba nimeelewa ulichoandika, ila nimeona umeandika 'kiprofeshno'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili nililitegemea maana hata ukifanya utafiti usio rasmi ni kwamba watu wengi wamekamilisha zoezi hili kwa kutumia namba za NIDA za watu wengine of which halikuwa lengo la zoezi husika!

shida nyingine niliyo iona ni kuwa, watu wakishamaliza process zote, za kujiandikisha waanaambiwa warudi majumbani, namber watapatiwa baada ya mwezi mmoja. hili lipo karibu kila wilaya

kwahiyo dhana yakusema vitendea kazi hamna, haiingi akilini, maana system ingeweza kumpa mtu namba akaendelea na process zingine huku akiendelea kusibiri id itoke huko siku za mbeleni.

sasa, mtu amejiandikisha ndani ya muda uliowekwa, kumwambia asubiri siku 30 ndiyo apate just namba na siyo id, hilo ni mapungufu ya nida siyo serikali.
 
Sijui ni mawazo yangu ama laa, kama lengo ni kujua mmiliki halali la chip ya mtandao na kwamba watu wengi wametumia vitambulisho ama namba zisizokuwa zao kwa sababu ya urasimu uliopo NIDA basi tutaraji watu wengi sana kubeba kesi zisizokuwa zao mara line walizosaidia wengine kusajili zitakapotumika kinyume na matakwa ya watawala!
 
Namfahamu sana Dr. Kihaule sio mtu creative na ni mwoga kufanya maamuzi. Hata kabla nafasi aliyoshikilia Director of Planning ilikua ni mtu wa kuelekezwa tu pale ARU.
 
Muda wote huo Leo ndio amejua mkurungezi ndio tatizo la kumaliza zoezí la kujiandikisha ajitafiti yeye Kwanza kwanini 2020 ameanza na hili
 
Back
Top Bottom