Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,363
Debe tupu .....Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola amemwagiza Mkurugenzi wa NIDA kukutana naye kwenye ofisi za NIDA Lindi tarehe 11 January, huku akiwa na maelezo ya kutosha kuhusiana na ucheleweshaji wa vitambulisho ili asifutwe kazi.
Chanzo: Watetezi TV
Wakati wakitangaza zoezi hili la kusajili line zote za simu walitumani ungetokea muujiza mbele kwa mbele kuwamilikisha watu vitambulisho vya utaifa? Fine waziri mwenye dhamana atamuwajibisha mkurugenzi, naye anaweza kuwajibishwa na aliyemteua, mwisho wa siku hata wa mwisho kuwajibisha naye atalazimika kujiwajibisha kwa kuidhinisha miradi ambayo haikufanyiwa upembuzi wa kina kabla haijawa implemented!
Nimekupa line sio kwamba nimeelewa ulichoandika, ila nimeona umeandika 'kiprofeshno'Mmepatia budget ya kutoa vitambulisho? asilimia kubwa ya uchelewaji kutoa vitambulisho ni serikali kushindwa kutoa fungu bhana , vitambulisho vimewashinda miaka mitano sasa mmeamua kukimbilia kutoa namba , vitambulisho hadi vitoke makao makuu wapi na wapi? kwa nini msiwe na centralized system nchi nzima katika vituo vya polisi au uhamiaji? kubalini watu wa cyber cafe wawatolee pindi wakipata namba kutoka kwenu ni haraka na rahisi, mtu apate namba aende akapige passport size aende cyber kutengenezewa kitambulisho dakika chache tu Mambo yanakamilika , akili za IT hamna mnatumia ubabe tu kila mahali.
Aisee hili swali ni la muhimu sana!!Swali ninalojiuliza hivi tunawahi wapi na hizi biometrics. Why are we in a hurry? Wakati bado logistics zote hazijakaa sawa.
Ninja ameanzaWaziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola amemwagiza Mkurugenzi wa NIDA kukutana naye kwenye ofisi za NIDA Lindi tarehe 11 January, huku akiwa na maelezo ya kutosha kuhusiana na ucheleweshaji wa vitambulisho ili asifutwe kazi.
Chanzo: Watetezi TV
Nini kifanyike?Watu wengi hawana vigezo vya kupata NID CARDs
Duh kumbe unapingailifahamika mapema kwamba lazima adondoshewe jumba bovu , hata yeye mwenyewe alishasoma alama za nyakati
Aisee!!Duh kumbe unapinga
unajua maana ya jumba bovu ? unamtoa mkurugenzi wa Nida kwenye hili ili iweje ?
Hili nililitegemea maana hata ukifanya utafiti usio rasmi ni kwamba watu wengi wamekamilisha zoezi hili kwa kutumia namba za NIDA za watu wengine of which halikuwa lengo la zoezi husika!
Sijui ni mawazo yangu ama laa, kama lengo ni kujua mmiliki halali la chip ya mtandao na kwamba watu wengi wametumia vitambulisho ama namba zisizokuwa zao kwa sababu ya urasimu uliopo NIDA basi tutaraji watu wengi sana kubeba kesi zisizokuwa zao mara line walizosaidia wengine kusajili zitakapotumika kinyume na matakwa ya watawala!shida nyingine niliyo iona ni kuwa, watu wakishamaliza process zote, za kujiandikisha waanaambiwa warudi majumbani, namber watapatiwa baada ya mwezi mmoja. hili lipo karibu kila wilaya
kwahiyo dhana yakusema vitendea kazi hamna, haiingi akilini, maana system ingeweza kumpa mtu namba akaendelea na process zingine huku akiendelea kusibiri id itoke huko siku za mbeleni.
sasa, mtu amejiandikisha ndani ya muda uliowekwa, kumwambia asubiri siku 30 ndiyo apate just namba na siyo id, hilo ni mapungufu ya nida siyo serikali.