Mkurugenzi wa NIDA atakiwa kujieleza kwanini asifutwe kazi

Mie huwa nashangaa sana
Nec ndani siku saba wana uwezo wa kuanikisha kanda moja yenye watu milioni tano,,sijui hawa NIDA wana tatizo gani
Unaweza kumpa mtu namba kwanza,ukigundua kuna makosa au uraia una utata unampoka tu namba akamalizane na uhamiaji kwanza,lakini wao wanaona ni bonge la kazi kutoa vitambulisho
 
Hivi Mh Kagi anataka kutuambia muda wooote hajui shida NIDA iko wapi?? /Akiwa waziri na hajui shida iko wapi basi hata yeye Kagi ana takiwa ajieleze kwetu kwanini na yeye Mh Rais asimfute kazi. Waache siasa kwenye mambo yanayo gusa jamii..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ningefurahi kusikia anayehusika aeleze kwa nini wahitimu hawaajiriwi na wamejaa mitaani huku kukiwa na upungufu wa wafanyakazi sekta mbalimbali.
Kwangu hili ni tatizo sugu. Na hili la NIDA halina shida kubwa laweza kusuasua hata miaka mia. Mbona NIDA ni ya juzi tu?
Mtu anaacha kukomaa na matatizo siriazi na kudili na mambo ambayo hata ukiyaaahirisha taifa halidhuriki kivile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola amemwagiza Mkurugenzi wa NIDA kukutana naye kwenye ofisi za NIDA Lindi tarehe 11 January, huku akiwa na maelezo ya kutosha kuhusiana na ucheleweshaji wa vitambulisho ili asifutwe kazi.

Chanzo: Watetezi TV

cheo ni Mkurugenzi Mkuu sio mkurugenzi maana wapo wengi halafu kwa Mkurugenzi Mkuu hafutwi kazi na Waziri never
 
Tunaambiwa kwamba tar 20 Jan ndo line zote zinazimwa,Kule Nida ukimaliza kujiandikisha ile namba huipati siku hiyohiyo,Sasa je wale ambao watajiandikisha siku ya mwisho tar 20 line zao itakuaje? Na je inawezekana tar hiyo 20 watu wote mpk vijijini wakawa wamepata hiyo namba?
 
Nchi inaendeshwa kama gari lililokatika senta bolti
 
NIDA iko chini ya nani?? Unaitenganishaje NIDA na Serikali??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

[emoji419]
 

Huelewi unachoandika....
 
Hii serikali ya kipuuzi kabisa, hivi kuna haraka gani na hili zoezi wakati wanajua kabisa hawana rasilimali za kutosha? Wamekwama hata kwenye kutoa hizo namba zenyewe, kwani kuna ugumu gani wa kumpatia mhusika namba yake siku hiyo hiyo wanapochukua vielelezo vyake?
Kuna Vijana wengi wataalam wa masuala hayo wapo mitaani tu, wangetumika angalau wakasaidia hata kuwezesha kupatikana kwa NAMBA YA NIDA tu, mara tu anapomaliza kuandikishwa mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…