Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Napenda tena kukishukuru Chama cha Chadema kumpa nafasi TUNDU LISSU ya kugombea Urais katika uchaguzi huu.

Mungu alimuokoa na kifo na Mungu ana makubwa juu yake
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!...
Huyu alitakiwa kuwa campaign manager wa chama chake badala ya kuwa referee wa wote.

Tanzania mbona tunakuwa natume ya karne iliyopita?
 
Aisee! Hivi ndugu Nkuugenzi(in Sambaaz voice) ni wa kanda maalum ee
 
Hovyo kabisa huyu. Ni kwa mamlaka ipi anawasemea raia? Double standard
 
zero kabisa, yani mnatetea mtu anaetaka kuweka rehani ardhi yetu? Unajidai upo deep kumbe umejaza manyoya tu kichwani. Mkiona hamuwezi kuisapoti CCM bora mkae kimya kuliko kutetea uovu.
Ardhi yetu na madini yetu yalishawekwa rehani na hao hao Ccm. Tena kwa mikataba mibovu ya miaka 100 ambayo haiwezi kuvunjwa. Hata Maghufuli hawezi kuvunja.
 
Wanasheria chukueni taadhari,kuna haja ya Ku-note sehemu flani kwa msaada wa baadae ikibidi. Pia kama kuna mtu mwenye video crip ya huyu bwana kada wa ccm aliye jivika ngozi ya NEC tunaiomba hapa pls.
Zama Twitter, inasambaa sana kule
 
Unampangia Lissu cha kunadi kwa wananchi?
 
Hali ni ngumu ndani ya CCM, Bashiru amepwaya sana na Polepole amepagawa.
Njia iliyobaki imeonekana ni kwa Mkurugenzi wa NEC ambaye bila kujua anatazamwa na Balozi zote na nchi wahisani kuingia kwenye timu ya kampeni ya ccm.

Refa akiamua kuweka filimbi mfukoni na kucheza midfielder njia sahihi ya kufanya ni kumpiga kiatu bila kujali unatengua nyonga au kuvunja mguu.
Kudadeki!
 
Kwa maneno yake mwenyewe, huyu ni mkurugenzi wa NEC ama nayexni sehemu ya timu ya kampeni ya CCM? Hawa vikaragosi wa CCM ifike wakati wakutane na hukumu ya umma, ukiwachekea hawa, itakuwa ni sawa kabisa na kuwaachia nyani shamba la mahindi, ni bayana tu kuwa utaambulia mabuwa.

Imefika kipindi sasa wameanza kuvuka mstari wa uvumilivu. Katika kipindi ambacho kampeni zimepamba moto, wanafanya kila hila kumtoa Tundu Lissu kutoka ktk reli.

Wakati jeshi la polisi likionekana wazi likifanya kazi zake kwa weledi na pia likitii matakwa ya umma. CCM ilitegemea kuwa jeshi la polisi lingekuwa upande wa udhalimu wao, na kwa makusudi kukwepa kuwajibika kwa kutokuruhusu mikutano ya wapinzani kwa kutoa visingizio vya sababu zitokanazo na intelejesia na usalama mdogo.

Kimbilio lao kuu ovu na pekee lipo sasa kwa msajili wa vyama na viongozi wa tume ya uchaguzi. Hii taarifa ya kuwaita maDED nchi nzima wala siyo ya kuipuuzia hata kidogo. Pengine kwa kuepuka "physical movements" ambazo zingaliweza kustukiwa.

Kutoka na uwepo wa ICT kuna uwezekano mkubwa wa kufanya mkutano huo kupitia "tele conference" mathalani "Zoom or Skype meetings"
Nia yao ovu imeweza pia kushtukiwa kwa kuwa ndani ya watendaji wa vyombo na usalama wapo wazelendo wa kweli wenye kutimiza wajibu wao kwa weledi, maadili na uadilifu mkubwa.

CCM ni lazima wakumbuke ya kwamba, teknolojia huwa haziongopi. Ukweli wote utawekwa bayana.
 
Jamani maji yamezidi unga,maji yako shingoni ,binafsi imebidi nicheke kwa hiki kioja Cha jamaa wa tume,kwamba sasa hata time waungane na ccm hakuna kitakachobadilika watzn wameshaamua Kama mbwai na iwe mbwai
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£ Kwa kweli nimeamini mwananchi sio wa mchezo mchezo ,seems huyu jamaa Yuko kwenye shinikizo kubwa kwa Nini walipitisha jina la TL ,huwezi kushindana na Mungu kwa vioja hivyo
Basi tufanye ccm huwa wanachimba madini na kugawia wananchi.Aisee watu wamepanic kinoma na bado kadiri tarehe ya uchaguzi tutazika wengi kwa pressure
 
Mwaka huu tutaelewana tu
Kmmk watuletee uhajisi wao hawataamini
 
Dooh, kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauna!
Mkurugenzi si aanzishe chama chake tu.
Asitupangie watanzania tunataka nini.
Sisi wengine tunataka ubwabwa tu, sio Barabara nzuri wala ndege.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…