Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Mkurugenzi wa kampeni anampigia kampeni mgombea wa kampeni

Nchi imeoza hii inanuka
 
Labda tumuulize kazi yake nini? Nikuwapangia wagombea cha kuongea, je yule mwingine aliye sema hawazi peleka maendeleo kwa watu ambao hawakuchagua upande wake NEC inamzungumziaje?
Kwani huyo mkurugenzi anagombea urais kupitia chama gani? Watanzania tuna masikio, hayo matusi ya Lissu anasikia peke yake tu?
 
Huyo mkurugenzi wa tume anaonyesha wazi kuwa wao tayari wana matokeo kwenye mikoba yao na wanafanya uchaguzi kama formality tu.

Lakini tulisema siku nyingi huko nyuma kuwa hii sio tume inayoweza kusimamia uchaguzi wowote wa maana kwani inaundwa na wanachama hai wa ccm na wako pale kukihakikishia chama chao ushindi.

Mwaka 2021 lazima tuhakikishe tunakuwa na tume huru kabisa ambayo rais hatahusika ktk uundaji wake la sivyo huko tuendako tutakuja kuchinjana. Inavyoonekana ccm na tume yao tayari wamepanga kuhujumu huu uchaguzi.
 
Mkurugenzi atulie, sisi ndio tunajua tunataka nini
 
Mkurugenzi wa kampeni anampigia kampeni mgombea wa kampeni

Nchi imeoza hii inanuka
 
Mkurugenzi ana ujecha fulani na ameuonyesha mapema hata kampeni hazijakwisha. Itabidi tutafute njia ya kumlalamikia huyu mkurugenzi kwenye vyombo vya sheria kabla ya hii tume haijaharibu uchaguzi. Kwa kweli kuna dalili ya baadhi ya watu wanataka kuuharibu huu uchaguzi na kibaya zaidi wanaweza hata kuwatoa kafara baadhi ya ndugu zetu.

Lazima tujue kuna maisha baada ya uchaguzi, tujaribu kufuata sheria, kanuni, taratibu na mipango tuliyojiwekea ili tumalize hili zoezi kwa salama. Ikiwa wachaguzi ni wananchi basi waacheni wenyewe wachague nini wanataka. Tume ya uchaguzi inatakiwa isimamie uchaguzi huru wa haki na amani.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Rais Mkapa ameuza madini madini ya hii nchi kiasi gani ?

Kama nchi tumepata faida kiasi gani?
 
Kwenye kamati ya maadili, huyu hatakiwi kuwepo, period. Ushahidi ni hiyo clip. Ngoja tumuone mwenyekiti wake ambaye ni Jaji mstaafu atasemaje juu ya hili; kama huyu mkurugenzi anaweza kuwa mwamuzi sahihi
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!...
Huyu ni Mkurugenzi wa Tume ya CCM, sio wa Tume ya Uchaguzi. Mara zote wakurugenzi hawa wanakuwa ni makada wa CCM na wanajaribu sana kuficha ukada wao hadharani lakini huyu wa sasa ameamua kujianika wazi.

Kwa kauli zake hizi za kikada, ipo haja ya uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi badala ya hii Tume ya CCM. Inasikitisha sana, tena sana aisee. Sijawahi kuona Mkurugenzi asiyeweza kuficha ukada wake kama huyu msukuma.
 
Atimae tume yapanda jukwaani kumnadi mgombea wao still watapigwa asubui mapema
 
Watanzania wapi hao anaowasemea! Asubiri show tarehe 28 October 2020.
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!...
Sasa kwa kauli kama hii Mkurugenzi haoni kama anaonyesha anaegemea upande gani. Unapokuwa refa hata kama ina mapenzi na timu shindani basi jitahidi kutokuexpose mapenzi yako ili kubalansi mchezo.
 
Mimi sio mwana siasa hata kama Lissu atauza nchi sidhani NEC kama inahusika
Wangejaribu kua neutral
kusema kwamba mgombea inabidi atetee rasilimali za nchi na awe mzalendo sio kua neutral? Kwamba kwa kusema hivyo basi wanampigia kampeni mgombea wa CCM? Ukiona mtu ana react kwenye hili ujue mgombea wake sio mzalendo wala mtetea rasilimali za nchi.
 
Zero kabisa, yani mnatetea mtu anaetaka kuweka rehani ardhi yetu? Unajidai upo deep kumbe umejaza manyoya tu kichwani. Mkiona hamuwezi kuisapoti CCM bora mkae kimya kuliko kutetea uovu.
Unazungumzia CCM ipi, CCM ya zamani au CCM mpya - MATAGA!
 
Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje
Kwani sasa hivi madini yanachimbwa na wasukuma na kuuzwa soko la Kariakoo? Huyu jamaa amekula maharage ya wapi? Ninachojua mimi ni kwamba madini yanachimbwa na wageni na yanauzwa huko huko nje kwa wageni.
 
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?...
We liache liwajaribu watanzania
 

Ahaaaa ahaaaa, halafu eti tume ya uchaguzi inajiita iko huru huku kiongozi wa tume anaghani mashairi ya ccm. Magufuli ameishurutisha hiyo tume wamtangaze yeye na chama chake kwa 90%+, hivyo tume wanatuandaa kisaikolojia.

Kitendo cha Lisu kusema haramiachia Mungu kinaichanganya tume maana wana matokeo tayari kabla ya kura halisi. Nimecheka sana eti hawataki mtu atakayepeleka madini yao nje kwa wazungu, kwani mpaka wanaochimba ni kina nani, na baada ya kuyachimba wanayapeleka wapi kama sio kwa wazungu? Kweli tume hii imeshapoteza uhalali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…