Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Jana wakati natoka Manyara kuelekea Tanga nikapita Arusha, sasa nikakutana na matangazo kuwa mkutano wa 153 wa IPU unafanyika kuanzia kesho jumatatu tarehe 5 mpaka tarehe 9 Oktona, pale katika ukumbi wa AICC Arusha na baadhi ya wabunge wawakilishi kutoka nchi washiriki wamekwisha kuwasili jijini Arusha tayari kwa ajili ya mkutano huo.
Kila kona na makutano ya jiji la Arusha kuna maafisa wa polisi wa kutosha, kuanzia usalama wa taifa mpaka migambo.
Ingawa sijajua ajenda za mkutano huu ila najua kuwa Mheshimiwa Zungu ndio mwenyeji kwa maana ya kuwa yeye ndio Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ila najaribu kujiuliza je kupitia jukwaa hili la wabunge wa IPU pale AICC wataweza kweli kuongelea suala la Uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2025, au watajizima data?
Moja ya tukio ambalo liliacha majonzi, vifo pamoja na damu mitaani, lakini bunge letu tukufu linasherehekea "demokrasia" kana kwamba wanatunga sheria za kupika pilau na biriani, huku likidai kuwa waliouawa sio watanzania.
Wengi tunafahamu kuwa Bunge letu ni tawi la CCM hilo lipo wazi kabsa. Bunge ni tawi tu la kusaini na kupitisha amri za "Rais Samia" kutoka juu. Linapiga makofi kwa kila kitu kama mazuzu, likisahau kuwa wananchi waliuwawa na kuzikwa "makaburi ya pamoja".
Wajumbe wa IPU waje Arusha wajionee wenyewe: hapa bunge lina uhuru wa sampuli moja tu pekee—uhuru wa kunyamaza na kukaa kimya! Wanajadili ulemavu wakati mfumo wote wa sheria ndio uliovunjwa uti wa mgongo, miguu pamoja na mikono.
Kama wajumbe wa IPU hawana ujasiri wa kuuliza kuhusu maiti na risasi zilizoondoa uhai mitaani mwaka jana, huu mkutano hautakuwa zaidi ya kikao cha kunywa kahawa na kula "kitimoto pale Gran Melia.
Tunafahamu kama watanzania kuwa Bunge letu linaendeshwa kama ofisi ya tawi la CCM; ukipiga chafya bungeni, ukasema Mama anaupiga mwingi, basi Rais inakupa barua ya uteuzi usiku kwenye mkeka wake mpya.
Je, IPU itakuwa na ujasiri wa kuikumbusha Tanzania kuwa bunge linatakiwa kuwakilisha wananchi badala ya kuwa sehemu ya Ikulu?