Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Mwenyekiti.
ninatoka nje kidogo kunusa ugoro maana zogo la humu ndani, hatusikilizani.
ntarudi punde

Ohooo, yamekuwa hayo tena? Hivu ugolo si madawa ya kulevya?
 
Mwenyekiti hebu tuwekee pannel yako ya wanamajumuisho maana unaposema kutakuwa na mjumuisho hapo unaniacha njia panda kwani sijajua nani ni nani ktk mjadala huu

Hahaaa msanii, kuna watu wanakimbia maajukumu hapa, nadhani kwa kuwa hakuna posho. Iko hivi:
Dark City = katibu lakini inaonekana amechomoa
WoS= Mwenyekiti ya Kamati ya kuhusu utawala bora na kama wahujumu wanyongwe au la. Kachomoa na kunipigia kelele eti atanifikisha mahakamani. Alimtumia pia lugha ya matusi mazito ya kawaida na ya nguoni pamoja na kejeli na kashfa.

Habari ndo hiyo, kinachoniweka hapa ni uzalendo tu.

Sasa nasubiri warudi niwaulize kama watafanya hiyo kazi au la.
 
Mwenyekiti naona hiki kikao kilikuwa kilikuwa cha dharura sana, Maana wengine tunavile vikao vya posho na hatuwezi kuvikwepa si mnajua jamani hii desturi ya posho nyingi nyingi? Kwa hiyo hivi vikao visivyo na posho huwa tunapiga chenga , lakini hiki ni KIKAO MUHIMU KULIKO POSHO, Mwenyekiti naomba samahani kwa kuchelewa mkutanoni!

Mimi Hoja yangu ya Msingi iko kwenye TUME YA UCHAGUZI, Uchaguzi unaweza kuwa huru na wa haki kama tume itakuwa chombo huru kisichofungamana na chama chochote, hivyo watendaji wakuu katika tume hii wachaguliwe na vyama vyote vilivyoandikishwa na msajili wa vyama vya siasa, lakini pia hata Msajili wa vyama vya siasa awe anaomba nafasi na kusailiwa na hatimaye kupewa kazi na Mashirika au Taasisi za elimu ya Juu zenye utaalamu na uzoefu wa kudahili wafanyakazi , Na katika hili sitegemei chochote kipya kwenye rufaa ya Dkt. Slaa dhidi ya Mgombea wa CCM.
 
Bajaji ni ambulance za kisasa zaidi, Comfortable na zinafika kwa urahisi zaidi kijijini kuliko mjini. Zimetengenezwa kwa uimara zaidi. Na kubwa zaidi RAISI Wa Tanzania wa awamu ya 10 atakuwa mama yake alipelekwa dispensary pale kijijini na BAJAJI maana lazima awe na akili za ziada!

Haaa haaaa haya Mkuu, nimekuelewa!
 
Msanii safi sana . . . huwezi kupata soft copy uzibandike hapa? hatufanyi mchezo na agenda hizi. Tukimaliza tunachapisha na kukabidhi kwa serikali ijayo.

Naomba kuwakilisha.
Ninazifuatilia mkuu, nikipata naziweka sawia hapa jukwaani tuangalie na kupima
Msanii, kwanza karibu tena. Mkuu umetukuna sana kwa pointi zako. Zinatuweka vizuri kuongezea zilizopita hasa suala zima la katiba.

Hili la tano Msanii, unaweza kulitolea ufafanuzi wa kina?
Ninaposema maabara ninalenga kuwa serikali iboreshe maabara za mashule hasa kuanzia shule za msingi, pia kila mkoa kama si wilaya kuwepo na maabara hizi. tusisahau katika majeshi yetu ya ulinzi na polisi waboreshewe maabara pia
Aina za maabara siyo zile za kutest litmus paper bali za majaribiop ya kisayansi, kwa mfano maabara zinazohusu masuala ya electronics na components zake, pia zinazohusu masuala ya fizikia hasa mashine na mitambo ili kuwezesha wavumbuzi kujitokeza na kuleta changamoto za maboresho. Nakumbuka nilipokuwa shule nilimwomba mwalimu wa fizikia nifanye jaribio la kurusha roketi (niliambulia kibano). Maabara za masuala ya arts hasa sisi tunaotumia rangi za kuchorea tunaweza kuvumbua aina ya rangi kutokana na malighafi za hapa nchini hivyo tukaongeza pato la taifa (nakumbuka nilipokuwa najifunza uchoraji sikuweza kupata rangi na matirio nyinginezo, nilitumia majani na maua kupata rangi na manyoya ya wanyama kutengeneza brush), hivyo pamoja na maabara waandaliwe watu wa kuziendesha na kumaintain.
Nimeeleweka?
 
Chaiman, ni kwlei nin can ya beer (LOL) maana siye kwetu ni kinywaji kama maji ,,,,,

Hili la muungani linanikera manake kila siku linaibuka kwa sura tofauti

nina uhakika tukiitisha referendum sasa hivi na watu wakipewa civic education, mwenyekiti watu watasema bora kila mtu ajue mji wake!

baada ya hayo, naomba kuwaaamkua umati uliofurika hapa jangwani!

Asante sana Kijana wangu. Hili litazingatiwa.

Ila suala la kinywaji kuwa makini . . . maana tuko katika mkutano, na wewe kila ukishika mic una glass yako . . . unanikumbusha mambo ya John walker . . . . Haaa haaa
 
Kama walivyosema wadau wengine, elimu ni kipaumbele cha vipaumbele vyote. Hata hivyo ni ngumu sana kuja na recipe ambayo ni muafaka sasa hivi. Niliwahi kusema huko nyuma kwamba ili hii nchi iende, inabidi kila kitu kipigwe chini na kuanza upya (to overhaul the main system and subsystems). Kwa upande wa main system, ndo hapo wadau wanaweka mkazo kwenye kuandika katiba mpya (nasisitiza tena na tena, kuandika katiba mpya). Kwenye sub-systems (sectors) kama elimu, ni muhimu kukaa chini bila kukurupuka na kuandaa education master plan (au road map) ambayo itakubaliwa na wadau mbali mbali. Kwa sasa ni vigumu kueleza ni mfumo gani wa elimu unafaa zaidi ingawa baadhi ya maoni ni mazuri sana.

Nawasilisha,.....DC

Swadata! Nimekusoma DC! karibu tena!
 
Mwenyekiti naona hiki kikao kilikuwa kilikuwa cha dharura sana, Maana wengine tunavile vikao vya posho na hatuwezi kuvikwepa si mnajua jamani hii desturi ya posho nyingi nyingi? Kwa hiyo hivi vikao visivyo na posho huwa tunapiga chenga , lakini hiki ni KIKAO MUHIMU KULIKO POSHO, Mwenyekiti naomba samahani kwa kuchelewa mkutanoni!

Mimi Hoja yangu ya Msingi iko kwenye TUME YA UCHAGUZI, Uchaguzi unaweza kuwa huru na wa haki kama tume itakuwa chombo huru kisichofungamana na chama chochote, hivyo watendaji wakuu katika tume hii wachaguliwe na vyama vyote vilivyoandikishwa na msajili wa vyama vya siasa, lakini pia hata Msajili wa vyama vya siasa awe anaomba nafasi na kusailiwa na hatimaye kupewa kazi na Mashirika au Taasisi za elimu ya Juu zenye utaalamu na uzoefu wa kudahili wafanyakazi , Na katika hili sitegemei chochote kipya kwenye rufaa ya Dkt. Slaa dhidi ya Mgombea wa CCM.

Kijana kwanza karibu sana renegade katika Mkutano . . . Ila tafadhali tumia lugha ya kistaarabu maana matusi haturuhusu, unaweza ukasababisha TBC wakakata matangazo. Tuko zaidi Kiuzalendo na Kitaifa kuliko mambo ya Chama.

Sasa turudi kwenye hoja, tunakubaliana na wewe 100%. Iliongelewa kuwa katiba iainishe kuwe na tume huru ambayo itawajibika bungeni na si serikalini.

Hili la msajili wa vyama ni jipya na limekaa vizuri. unaweza kulitolea ufafanuzi wa kina ili wadau walielewe kwa uwazi?
 
Kwa kuwa suala la katiba limeonekana kuwa kero ya wengi wa waliohudhuria, ni vema hapo baadae tujadili tunataka katiba ya aina gani ili itakapofika kupiga kura za "Ndio" na "La" kieleweke. Mimi naogopa kutumia sana energy ya ubongo sasa hivi nisiije kuishiwa sukari nikadondoka wakati nachangia mada, swaumu imeshanchanganya!
 
Ninazifuatilia mkuu, nikipata naziweka sawia hapa jukwaani tuangalie na kupima

Ninaposema maabara ninalenga kuwa serikali iboreshe maabara za mashule hasa kuanzia shule za msingi, pia kila mkoa kama si wilaya kuwepo na maabara hizi. tusisahau katika majeshi yetu ya ulinzi na polisi waboreshewe maabara pia
Aina za maabara siyo zile za kutest litmus paper bali za majaribiop ya kisayansi, kwa mfano maabara zinazohusu masuala ya electronics na components zake, pia zinazohusu masuala ya fizikia hasa mashine na mitambo ili kuwezesha wavumbuzi kujitokeza na kuleta changamoto za maboresho. Nakumbuka nilipokuwa shule nilimwomba mwalimu wa fizikia nifanye jaribio la kurusha roketi (niliambulia kibano). Maabara za masuala ya arts hasa sisi tunaotumia rangi za kuchorea tunaweza kuvumbua aina ya rangi kutokana na malighafi za hapa nchini hivyo tukaongeza pato la taifa (nakumbuka nilipokuwa najifunza uchoraji sikuweza kupata rangi na matirio nyinginezo, nilitumia majani na maua kupata rangi na manyoya ya wanyama kutengeneza brush), hivyo pamoja na maabara waandaliwe watu wa kuziendesha na kumaintain.
Nimeeleweka?

jamani tuache utani, hivi mmepitia points zote toka mwanzo? Aisee mnatisha JF na sijui kama Serikali inajua kuna vichwa hapa.

Mimi nimekuelewa sana na naomba tuliweke hivi: Kwamba serikali inayokuja "Ifanye kila jitihada za kuendeleza Utafiti, sayansi na Technolojia mabyo itachochea kuleta maendeleo ya Nchi"

hapo vipi?
 
Ukibofya hapa http://www.hakielimu.org
utakuta hii meseji inakungoja
We are sorry for inconveniences,
For any details please contact:
HakiElimu
Plot # 739, Mathuradas Street
P. O. Box 79401
Dar es Salaam
Tanzania
Tel: +255 22 2151852/3
Fax: +255 22 2152449
sijui ndo wamefulia?
bado nasaka soft copies za ahadi za ccm 2005
 
Sijamuelewa huyu jamaa ana zungumzia nini, bora unge andika kwa lugha moja kuliko hivi unavyo mix swahili na ki-English, fool!
 
Kwa kuwa suala la katiba limeonekana kuwa kero ya wengi wa waliohudhuria, ni vema hapo baadae tujadili tunataka katiba ya aina gani ili itakapofika kupiga kura za "Ndio" na "La" kieleweke. Mimi naogopa kutumia sana energy ya ubongo sasa hivi nisiije kuishiwa sukari nikadondoka wakati nachangia mada, swaumu imeshanchanganya!

Mkuu, tumekusoma sana na tuko pamoja.

Tunaomba wanaomfahamu Dr. Mvungi (PhD mambo ya katiba) atuwekee soft copy ya ile waliyoiandaa ili tuanze kuichambua hapa. tupate kazi ya kufanya.
 
jamani tuache utani, hivi mmepitia points zote toka mwanzo? Aisee mnatisha JF na sijui kama Serikali inajua kuna vichwa hapa.

Mimi nimekuelewa sana na naomba tuliweke hivi: Kwamba serikali inayokuja "Ifanye kila jitihada za kuendeleza Utafiti, sayansi na Technolojia mabyo itachochea kuleta maendeleo ya Nchi"

hapo vipi?
hapo sawa!
 
Sijamuelewa huyu jamaa ana zungumzia nini, bora unge andika kwa lugha moja kuliko hivi unavyo mix swahili na ki-English, fool!

Mnganyizi; kwanza karibu kikaoni, haalafu lete hiyo Mic kwanza.

Tumesema maadili hayaruhusu lugha ya matusi. tuko live TBC au unataka wakate matangazo?

Sasa turudi kwenye hoja yako, nani hujamuelewa?

Wana JF tafadhali tusichakachue lugha. Tutumie kiswahili tu, lugha yetu ya taifa.
 
Mkuu Superman
Nimefanikiwa kwa ombi lako kusaka kwenye net na kukuta hii kitu itakayotuongoza kuchambua ahadi za Kikwete 2005. Nimeweka ilani kwanza kama walivyoiweka wenyewe kisha nasaka ahadi ambazo hazikuwekwa kwenye ilani
Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005 kwa muhtasari.
UTANGULIZI
1. Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM cha tarehe 15 Agosti, 2005 kilichofanyika Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Benjamin William Mkapa, miongoni mwa mengine kilipokea rasimu ya Ilani ya uchaguzi kwa Ajili ya uchaguzi Mkuu wa 2005. Rasimu hiyo iliwasilishwa na mwenyekiti wa Kamati ta Ilani ya CCM, Ndugu Kingunge Ngombale-Mwiru. Halmashauri Kuu ilipitisha rasimu hiyo baada kuifanyia marekebisho machache na sasa tayari ni Ilani kamili. Halmashauri Kuu pia ilipokea kitabu cha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tatu na Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2000. Aidha, Kamati ya Kampeni ya CCM imeandaa Muhtasari wa Ilani ya CCM ya 2005.
SIASA NA SERA ZA MSINGI ZA CHAMA.
2. Siasa ya Chama Cha Mapinduzi ni ya ujamaa na kujitegemea inavozingatia mazingira ya wakati. Mwelekeo wa sera za msingi za CCM za kujenga ujamaa kwa kipindi fulani huzingatia ukweli na hali halisi ya wakati huo. Ndiyo maana katika mwelekeo wa sera za CCM katika miaka ya Tisini ulioandaliwa katika mazingira ya mageuzi makubwa na kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyoikumba dunia nzima mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzoni mwa tisini, CCM ilibainisha ifuatavyo katika ibara za 5 na 6 za mwelekeo huo:-
5. Siasa ya msingi ya Chama Cha Mapinduzi itaendelea kuwa UJAMAA NA KUJITEGEMEA kwa kuzingatia kwamba ndiyo iliyotuundia mazingira ya amani, utulivu na umoja wa Taifa letu, na ndiyo siasa inayolinganana matarajio ya mwananchi walio wengi.
6. Lengo la Ujamaa na kujitegemea katika miaka ya tisini litakuwa kuhakikisha kwamba wananchi wenyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi yetu, mmoja mmoja, kwa kupitia vyama vyao huru vya ushirika wa aina mbalimbali, kwa kupitia makampuni ya wananchi na ya ubia ambamo maelfu ya wananchi watanunua hisa....Kwa mtazamo huu wa CCM, sehemu kubwa ya uchumi wa nchi inakusudiwa umilikiwe na wananchi wenyewe ili kuinua hali ya maisha yao na kutosheleza mahitaji yao ya msingi. Dola....itaendelea kushika nafasi ya muhimili wa uchumi wa Taifa.
7. Ikumbukwe kwamba kabla ya hapo, ujenzi wa ujamaa ulisimama juu ya msingi wa wananchi kumiliki uchumi wa Taifa kupitia dola, na siyo moja kwa moja.
8. Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2000 hadi 2010 ambao ndio sera ya msingi ya CCM ya wakati huu, ni mwendelezo wa malengo makuu ya mwelekeo wa sera za CCM katika miaka ya Tisini. Katika ibara zake za 11, 12, na 13, mwelekeo huo (wa 2000-2010) unabainisha ifuatavyo.
"11. Malengo makuu ya mwelekeo wa sera za CCM katika miaka ya Tisini yalikuwa mawili. Kwanza mwelekeo ulitamka kuwa lengo la Ujamaa na kujitegemea ni ni kuhakikisha kuwa uchumi wa Tanzania unamilikiwa na kuendeshwa na wananchi wenyewe kwa njia mbalimbali. Hii ni sera ya msingi ambayo utekelezaji wake ni wa muda mrefu na unaohitaji mipango na mikakati thabiti."
"12. Pili, mwelekeo wa miaka ya Tisini ulisisitiza kwamba lazima nguvu na uwezo wetu uelekezwe kwenye kuinua kiwango cha nguvu na uwezo wetu uelekezwe kwenye kuinua kiwango cha nguvu za uzalishaji mali ili kuinua uchumi wa taifa. Hivyo, kazi iliyo mbele yetu ni kuwajenga wananchi (watenda kazi) kwa elimu na maarifa ya kisasa, kueneza matumizi ya zana za kisasa (vitendea kazi) na kujenga miundombinu ya uchumi wa kisasa."
"13. Malengo haya makuu ya mwelekeo wa sera za CCM za miaka ya Tisini yanatuunganisha na majukumbu ya mwelekeo wa sera za CCM za miaka ya 2000 hadi 2010. Kwa kuendeleza malengo hayo mawili kazi iliyo mbele yetu ni kujenga msingi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea na uwezeshaji wa kiuchumi wa wananchi.
5. Hii ndiyo inatupeleka kwenye chimbuko la Ilani ya sasa
CHIMBUKO LA ILANI YA UCHAGUZI YA 2005.
6. Chimbuko la Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 ni mwelekeo wa sera za CCM katika miaka ya 2000 hadi 2010. Ilani hii itakuwa ni kipindi cha pili na cha mwisho cha utekelezaji wa mwelekeo huo. Kwa hivyo, imeandaliwa kwa kuzingatia majukumu makuu mawili yafuatayo ya mwelekeo huo:-
(a) Kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea; yaani modenaizesheni ya uchumi.
(b) kutekeleza sera ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TATU NA AZMA YA KUYAENDELEZA
7. Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya Awamu ya Tatu chini ya uongozi wa Rais Benjamin Mkapa imepata mafanikio makubwa sana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii na utawala bora katika kipindi chake cha miaka 10 toka 1995 hadi 2005. Katika kipindi chake hicho, Serikali hiyo ilitekeleza Ilani mbili za Uchaguzi za CCM, yaani Ilani ya 1995 iliyotokana na mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya Tisini na Ilani ya 2000 hadi 2010. kwa hivyo mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hicho yameisogeza nchi kuelekea malengo mawili makuu ya mielekeo hiyo. Ni azma ya CCM kupitia Ilani hii, kuyaendeleza mafanikio hayo na kuanzisha mengine. Ni kwa madhumuni ya kutekeleza azma hiyo, ndiyo CCM kupitia Mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu Jakaya mrisho Kikwete imebuni kaulimbiu ya:- Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya.
KUJENGA MSINGI WA UCHUMI WA KISASA WA TAIFA LINALOJITEGEMEA.
8. Mafanikio ya serikali ya Awamu ya Tatu katika utekelezaji wa jukumu la kujenga msingi wa uchumi wa kisasa taifa linalojitegemea yanajidhirisha kwa ujumla katika kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 3.6 mwaka 1995 hadi asilimia 6.7 mwaka 2005. Lengo la Ilani hii katika kuyaendeleza mafanikio hayo ni kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2010 kwa kutumia mikakati iliyomo katika mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini Tanzania (MKUKUTA).
KUTEKELEZA SERA YA UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI.
9. Lengo la kukuza uchumi wa nchi ni kwamba hatimaye manufaa ya kukua huko kwa uchumi yawafikie wananchi. Kuna aina mbili za manufaa wanayotarajia kuyafaidika kwa pamoja kwa njia ya huduma zilizoimarishwa za kijamii na miundombinu kama vile elimu, afya, maji, barabara, umeme, mawasiliano n.k. Aina ya pili ya manufaa ya kukua kwa uchumi yanayotarajiwa na wananchi ni ile ambapo mwananchi mmoja mmoja anafaidika kwa njia ya kuongezeka kwa kipato chake na cha familia yake.
10. Katika lugha ya wanaharakati wa mapambano dhidi ya umaskini, aina ya kwanza ya manufaa huhusishwa na kupunguza kile kinachoitwa umasikini usiokuwa wa kipato na ile aina ya pili huhusishwa na kile kinachoitwa umasikini wa kipato.
11. kwa kutumia ukuaji wa uchumi wa taifa uliopatikana katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Serikali ya Awamu ya Tatu imefanikiwa sana kuimarisha huduma za jamii na miungombinu, mafanikio ambayo yanaonekana kwa macho nchi nzima. Kwa hivyo, kwa ujumla, watanzania wamenufaika kwa pamoja kwa kiasi kikubwa na kukua kwa uchumi. Kwa maneno mengine umasikini usiokuwa wa kipato umepungua kwa kiasi ambacho jamii nzima ya Watanzania inakihisi.
12. Jitihada pia zimefanyika na zinaendelea kufanyika za kukabiliana na umasikini wa kipato, yaani kuwafikishia wananchi manufaa ya kukua kwa uchumi kwa wao kufaidika mmoja mmoja. Hili ndilo hasa eneo ambalo sera ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi inahusika nalo. Agenda kuu katika eneo hili ni:-
(a) uwezeshaji
(b) Kupambana na umasikini
(c) Kushiriki katika uchumi wa nchi, na
(d) Ajira.
13. Eneo hili la kuyafikisha kwa wananchi manufaa ya kukua kwa uchumi wa nchi ndilo agenda kuu na changamoto ya msingi ya Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005. Na mbinu kuu za kuikabili changamoto hii ni pamoja na zifuatazo ambazo zote ni sehemu ya MKUKUTA:-
(a) Kuendelea kukua kwa uchumi wa nchi kwa kasi kubwa zaidi (kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2010).
(b) Kuongezeka kunakoendelea, kwa wingi na ubora wa huduma za jamii hasa elimu, afya, maji n.k. na miundombinu hasa barabara, madaraja, mawasiliano, umeme n.k.
(c) Modenaizesheni ya harakati mbalimbali za kiuchumi zinazowapatia ajira za kujiajiri na kipato wananchi, hjasa kilimo, ufugaji, viwanda vidogo, uvuvi, uchimbaji madini, n.k.
(d) Kuzipa uhai rasilimali mfu za wananchi ili ziweze kutumika kama dhamana za kujipatia mikopo, kwa kutumia mkakati wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA). Mkakati huu utachangamsha ajira za wananchi za kujiajiri wenyewe.
(e) Kuwawezesha wananchi kutumia fursa mbalimbali za maendeleo zilizopo kujiongezea kipato na kushiriki katika uchumi wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kumiliki hisa katika makampuni mbalimbali, kama ilivyokwishaanza kwa mfuko wa umoja.
(f) Mkakati wa uanzishaji wa maeneo maalumu ya uchumi ( Special Economic Zones Strategy) kama unaotumiwa na nchi Asia ambao utazalisha ajira nyingi za kuajiriwa katika sekta rasmi, na za kujiajiri. Kwa jina jingine, mkakati huo unaitwa The Tanzania Mini-Tiger Plan.
(g) Kuimarisha taasisi zinazotoa mikopo kwa wananchi.
14. Kwa vile lengo la juhudi zote hizi zinazobainishwa na ilani ni kuyafanya maisha ya watanzania wawe bora zaidi, CCM imebuni kaulimbiu mbili zifuatazo.:-
(a) "Maisha bora kwa kila Mtanzania",
(b) "Kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, Tanzania yenye neema tele inawezekana."
KUZINGATIA DIRA ZA 2025 NA 2020 NA MALENGO YA MAENDELEO YA MILENIA.
15. Ilani hii ya mwaka 2005 imezingatia pia malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2020. Imetumia pia vigezo vya malengo ya maendeleo ya milenia (Millenium Development Goals-MDGs) kwa kadiri ilivyowezekana, katika kuweka malengo yake.
DONDOO ZA YALIYOMO KATIKA ILANI.
16. Dondoo za mambo yaliyomo katika ilani hii ya uchaguzi zinatolewa hapa sura kwa sura.
(a) Sura ya Utangulizi
Sura hii imeshambua hali ilivyo duniani wakati huu na kuiweka Tanzania katika muktadha wa ulimwengu wa utandawazi. Hoja imejengwa kwamba utandawazi si suala la hiari ya nchi au ya viongozi wa nchi. Utandawazi ni suala la hali halisi. Utandawazi una madhara mengi kwa nchi zinazoendelea za kusini ikiwemo Tanzania. Lakini pia utandawazi unatoa fursa nyingi kwa nchi zinazoendelea ambazo kama zitazitumia vyema fursa hizo, nchi hizo zinaweza kujikwamua kimaendeleo. Mkakati wa Ilani hii ni kuzitumia kwa kadiri iwezekanavyo, fursa hizo zinazotolewa na utandawazi na kujipunguzia kwa kadiri iwezekanavyo madhara ya utandawazi.
(b) Sura ya kwanza.
Sura hii inabainisha kwa muhutasari mafanikio ya kiuchumi na kijamii ya miaka 10 ya serikali ya Awamu ya Tatu. Mafanikio hayo yameelezewa kwa uchambuzi zaidi katika kitabu cha mafanikio ya serikali ya Awamu ya Tatu na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000.
(c) Sura ya pili.
Sura hii imeweka mkakati wa kuendeleza utekelezaji wa jukumu kuu la kwanza la mwelekeo wa sera za CCM katika miaka ya 2000 hadi 2010, yaani jukumu la kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea. Inasisitiza umuhimu wa mapinduzi ya kilimo (pamoja na ufugaji na uvuvi) ambacho ndicho sekta msingi wa uchumi wetu, na pia mapinduzi ya viwanda ambavyo vinatambuliwa na Ilani hii kama sekta kiongozi wa uchumi wa kisasa. Sura hii hatimae inaweka malengo makuu ya jumla ya Ilani kuwa ni haya yafuatayo:-
(i) Kukuza uchumi kwa kiwango cha zaidi ya asilimia kumi (10%) kwa mwaka ifikapo mwaka 2010 kutoka ukuaji wa sasa wa asilimia sita sukta saba (6.7%).
(ii) Kuanza kupunguza umasikini wa kipato wa watu wetu kwa namna iliyo dhahiri.
(iii) Kuendeleza safari ndefu ya kujitegemea kwa kuwa na uwezo wa kulipia gharama za bidhaa tunazoziagiza toka nje zinazohitajika kusukuma maendeleo yetu, kwa kutumia mapato ya ziada yatakayotokana na ongezeko kubwa la thamani ya mazao na bidhaa tutakazouza nje ya nchi.
(d) Sura ya Tatu.
Sura hii inaweka malengo na mbinu za utekelezaji kwa sekta za uzalishaji mali, hasa kilimo, mifugo, uvuvi, wanyamapori, misitu, utalii, viwanda, madini, biashara na masoko. Mikakati yote inalenga katika kuongeza tija ya uzalishaji mali kwa kutumia maarifa ya kisasa (modenaizesheni). Serikali zitatakiwa kuongeza bajeti katika sekta hizi na kuwapatia unafuu wananchi, wa gharama za uzalishaji mali (hasa pembejeo za kilimo, ufugaji na uvuvi) ili waweze kushiriki kwa ari na ufanisi zaidi katika harakati kama hizo za kukuza uchumi wa nchi na kupambana na umasikini. Kwa upande wa Viwanda mkazo utawekwa katika kuongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo na maliasili zetu nyingine, kwa njia ya usindikaji N.k.
(e) Sura ya Nne.
Sura hii inabainisha malengo ya Ilani katika sekta za miundombinu na huduma za kiuchumi. Sekta hizo ni ardhi, nishati, barabara, usafiri, uchukuzi, mawasiliano na fedha. Miongoni mwa malengo makuu ni kurasimisha umilikaji wa ardhi na nyumba kwa watanzania wanyonge wenye rasilimali hizo bila ya kuzisajili. Zoezi hilo lenye lengo la kuwawezesha wananchi kutumia ardhi na nyumba zao kama dhamana za mikopo litafanywa chini ya mpango wa MKURABITA. Aidha, barabara kuu za kitaifa ambazo zitajengwa zimeorodheshwa katika sehemu hii ya Ilani. katika eneo la usafiri na uchukuzi, ni dhamira ya Ilani kuiandaa Tanzania ili iweze kufaidika kikamilifu na jiografia yake kama lango, kuu la ukanda wa maziwa makuu na kusini mwa Afrika. Kwa upande wa sekta ya fedha, lengo ni kuweka mazingira mazuri ya kujenga tabia ya kujiwekea akiba miongoni mwa wananchi na kurahisisha upatikanaji wa mikopo.
(e) Sura ya Tano.
Sura hii ya Ilani inajikita katika utekelezaji wa sera ya uwezaji wa wananchi kiuchumi. Sehemu ya utekelezaji wa sera hii inayomlenga mwananchi moja kwa moja, ni kuwaanda wananchi na kuwatengenezea mazingira mazuri ili waweze kuzitumia ipasavyo fursa zilizopo na zitakazoanzishwa na uwezeshaji kiuchumi. Maandalizi hayo ni pamoja na elimu na mafunzo, ujasiriamali, urasilimishaji wa rasilimali (MKURABITA) na kujiunga katika ushirika, hususani wa kuweka na kukopa (SACCOS).
Maeneo matatu mahususi ya uwezeshaji wa wananchi yamepewa uzito wa aina yake. Maeneo hayo ni kuwezeshana kupambana na umasikini.
(i) Ajira
Ajira ziko za aina mbili zifuatazo:-
*Aina ya kwanza ni ajira katika maana ya kazi ya kulipwa mshahara katika sekta ya umma (Serikalini na vyombo vyake) na katika sekta binafsi (iliyo rasmi na isiyo rasmi). Katika aina hii ya ajira, baada ya utafiti wa kina, inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba zitaweza kupatikana nafasi mpya zaidi ya milioni moja katika kipindi cha ilani. Tulifanya utafiti huo ili kujiepusha na kutoa ahadi ya njozi isiyotekelezeka kama ilivyotokea katika nchi jirani, ambapo wakati wa kuomba kura, vyama viliahidi kutengeneza ajira 500,000 kwa mwaka, lakini vilipoingia madarakani ikabainika kuwa lengo hilo lilikuwa kubwa mno.
Nafasi hizo mpya kwa upande wetu zitapatikana kutokana na kukua kwa uchumi ambako kutawezesha kuongezeka kwa harakati za kiuchumi na kupanuka kwa huduma mbambali za kijamii, ulinzi, miundombinu n.k. Katika sekta ya umma, pamoja na nafasi za ajira zitakazotokana na watu kustaafu na kufariki, kutakuwa na ajira mpya nyingi kwenye sekta ya ualimu kutokana na upanuzi unaoendelea wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu. Sekta ya afya pia itatoa ajira nyingi kwa upande wa waganga na wauguzi kwa vile sekta hii lazima ipanuke kukidhi mahitaji ya wananchi. Sekta ya ujenzi vile vile ina nafasi ya kutoa ajira nyingi mpya. Kwa upande mwingine katika sekta ya binafsi, serikali za CCM zitaendelea kuvutia wawekezaji katika viwanda, migodi, kilimo cha biashara (mashamba makubwa) n.k. ili nafasi za ajira ziendelee kuongezeka. Mkakati mpya wa serikali wa kuanzisha maeneo maalum ya uchumi (Special Economic Zones) umekusudiwa kuibua nafasi nyingi mpya za ajira.
*Aina ya pili ya ajira katika maana ya kujiajiri binafsi katika kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara, kuchimba madini, udereva, ufundi, ualimu, uhasibu, kuendesha mgahawa, ushonaji, uandishi, uanasheria, uhandishi, ukandarasi n.k. Eneo hili ndilo lenye nafasi tele za ajira katika nchi yetu. Katika kipindi cha Ilani hii, MGOMBEA urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete.
CCM itaweka mkazo kwenye kuwawezesha wananchi, hasa vijana na wanawake kwenye shughuli za kujiajiri vijijini na mijini. CCM inatoa wito kwa wananchi wajitokeze kuitikia wito wa kujiajiri na pia wakubali kutobagua kazi maana wahenga wanasema mchagua jembe si mkulima. Kwa njia hiyo ya serikali kuwawezesha wananchi walio tayari, nafasi mpya za ajira zitapatikana kwa mamilioni zaidi ya zile milioni moja za kuajiriwa, na kiwango cha ukosefu wa ajira (unemployment) kitapungua sana miongoni mwa vijana na wananchi wengine katika nchi yetu.
(ii) Eneo la pili la uwezeshaji litakaloibuliwa ni mifuko ya hifadhi ya jamii.
Pamoja na suala la kukaribisha wawekezaji nchini, kuna umuhimu wa kufikiria uwezekano wa kuutumia uwezo mkubwa wa fedha uliopo katika mashirika ya hifadhi za jamii (pensheni) yaani NSSF, PPF, LAPF na mfuko wa Pensheni wa serikali. CCM itaelekeza serikali kufanya mashauriano ya msingi na uongozi wa mifuko hii ili kupata njia muafaka za kuifanya mifuko hii ishiriki katika uwekezaji na hivyo kuliongeza nguvu taifa, ya kukuza uchumi wake kwa kasi zaidi na kuwawezesha wananchi wake kiuchumi kwa kuwaongezea nafasi za ajira.
(iii) Eneo la tatu la uwezeshaji litakalopewa mwelekeo mpya ni Harambee za kuwezeshana katika kupambana na umasikini.
Watanzania wa asili mbalimbali wana jadi ya kuungana mkono kwa hali na mali, kuchangiana na kusaidiana kwa msingi wa udugu, urafiki, utani, ujirani n.k. Tabia ya watu kuungana mkono (solidarity) ni nzuri na inafaa ikaendelezwa lakini kwa kupewa mrengo wa kimaendeleo, badala ya mambo ya sherehe (Harusi, ngoma n.k.) pekee.
CCM itawahimiza wananchi kwenye michango (harambee) ya kuweseshana katika fani za elimu, afya na uchumi (mitaji) kwani hizi ni nyenzo za msingi katika kupambana na umasikini.
(g) Sura ya sita.
Sura hii inahusu malengo ya Ilani katika sekta ya huduma za jamii. Sekta zinazohusika ni elimu, afya, maji na maendeleo ya makaazi. Upanuzi mkubwa sana wa huduma hizi za jamii ulifanyika katika kipindi cha miaka 10 ya serikali ya Awamu ya Tatu. Malengo ya Ilani hii zaidi ya kuendeleza upanuzi huo (kufikia kuukamilisha katika elimu ya msingi) ni kuongeza ubora wa huduma hizi. Miongoni mwa malengo mahususi katika sekta hizi ni:-
(i) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa msingi watakaoendelea na elimu ya sekondari kufikia asilimia 50 ya watahiniwa wa Darasa la Saba upande wa Bara.
(ii) Kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 95 kwa watoto 100 wanaozaliwa hadi watoto 50.
(iii) Kuwafikishia huduma ya maji safi asilimia 90 ya wakazi wa mijini na asilimia 65 ya wakazi wa vijijini
(h) Sura ay Saba
Sura hii ni ya mazingitio maalum ya Ilani kuhusu Zanzibar. Baada ya kuyatambua mafanikio makubwa ya serikali ya mapinduzi ay Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Amani Abeid Karume katika maeneo ya uchumi, miundombinu, huduma za jamii na utawala bora, sura hii ya Ilani inabainisha malengo makuu yafuatayo:-
(i) Kuendelea kuyatambua na kuyaenzi mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari, 1964 kuwa ndiyo yaliyoleta uhuru kamili na heshima ya kweli ya wazanzibari.
(ii) Kuendelea kutambua kwamba mapinduzi hayo sio tu ni ngao ya uhuru wa wananchi wa Zanzibar, bali pia ndio moja ya misingi muhimu ya muungano wa Tanzania.
(iii) Kuendelea kuyalinda na kuyaendeleza kwa nguvu zote mafanikio yaliyoletwa na mapinduzi hayo, hususani katika sekta za ardhi, ustawi wa jamii, huduma za jamii kama vile elimu na afya, na kukuza uchumi na matumizi endelevu ya rasilimali pamoja na kuwajengea wananchi uwezo wa kutumia fursa zilizopo ili kupambana na umasikini.
(iv) Kuendelea kuheshimu haki za binadamu, demokrasia na utawala bora.
Malengo mahususi ya kisekta yamezingatia misingi hiyo na yamewekwa kwa mtindo ule ule kama wa Jamhuri ya muungano lakini kwa kuzingatia mazingira ya Zanzibar. Maelezo ya uchambuzi kuhusu sehemu hii ya Ilani yatatolewa na viongozi wa CCM wa Zanzibar.
(i) Sura ya Nane.
Sura hii inahusu maeneo mengine muhimu, hususani demokrasia, utawala bora, madaraka ya umma, mapambano dhidi ya rushwa, ulinzi na usalama, hifadhi ya mazingira, kukabili majanga, utafiti na maendeleo, vyombo vya habari, mambo ya nje, utamaduni, michezo, kuyaendeleza makundi mbalimbali na kuhamia Makao Makuu Dodoma.
Katika eneo la utafiti na maendeleo (R&D), CCM inalenga katika serikali kutenga asilimia 1.0 ya bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya utafiti. Msukumo maalum utatolewa katika kulinda hakimiliki za matokeo ya utafiti na kuyafikisha matokeo ya utafiti kwa wananchi ili wayatumie kujiongezea tija. Inatarajiwa pia Tanzania itaingia rasmi katika biashara ya uundaji wa magari kupitia shirika la Nyumbu.
Katika eneo la mambo ya nje, mkazo utaelekezwa katika utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya uchumi.
Katika eneo la kuyaendeleza makundi mbalimbali, yamelengwa makundi ya watoto, wanawake, vijana, wazee, walemavu, wafanyakazi n.k. Kwa makusudi kabisa ya kutoa msukumo kwa makundi kama hayo, CCM, kupitia Jumuiya yake ya wanawake (UWT), imetenga viti bungeni na katika baraza la wawakilishi, mahususi kwa VIJANA, WALEMAVU, WASOMI, WAFANYAKAZI, NGOs, mbali ya WANAWAKE wenyewe kwa ujumla wao.
(j) Sura ya Tisa.
Sura hii inahusu Chama chenyewe, hasa viongozi. Viongozi wa CCM wanahimizwa kuongoza kwa kuonyesha njia katika utekelezaji wa yote yaliyomo katika Ilani, hususani yale yanayohitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Ilani inatumbua muundo wa serikali mbili (yaani serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar) na pia itahimiza ushirikiano wa serikali hizo katika kuleta maendeleo. CCM itazielekeza serikali zote mbili kuanzisha miradi ya pamoja ya kiuchumi, miundombinu na ya kijamii visiwani Zanzibar na kuwashirikisha wawekezaji binafsi.
HITIMISHO
Ilani ua uchaguzi ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2005 imesheheni mambo yenye kuleta matumaini kwa wananchi. Imeandaliwa juu ya msingi wa nguvu ya hoja na si hoja ya nguvu. Inaahidi mambo iliyoridhika kuwa yatawezekana, kufuatia utafiti wa kina ilioufanya kabla. Kwa hivyo, wagombea wa CCM wa ngazi zote kama wataitumia ipasavyo, hawatokuwa na haja, wala muda wa kujishughulisha na siasa za matusi, ubabe, kuwasema watu wala malumbano na wapinzani. Ni kutokana na msingi huo ndiyo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kwamba CCM itaendesha kampeni za kistaarabu.
Kwa Ilani hii ya uchaguzi, CCM inaahidi mambo makubwa matatu ya jumla yafuatayo:-
* Maisha bora kwa kila Mtanzania
* Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya katika kukuza uchumi wa nchi na kupambana na umasikini.
* Tanzania Yenye neema Tele
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Idara ya itikadi na uenezi
CCM MAKAO MAKUU
Gazeti-Uhuru
ISSN 0876-3896
Tarehe: Alhamisi 25,2005
 
Ndg M/Kiti,Ktb, na wajumbe wote mlikoko kwa kikoa hiki napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa michango yenu kwa dhati, bila kupoteza muda nina yangu machache kwa kuanzia tu kwa leo hii.


  1. Katiba ya nchi ile ndio ya kwanza kufanyiwa marekebisho
  2. Baaada ya kuundwa katiba ya nchi kuwepo na mustakabali wa nchi hii ni katika kusimamia kila sector za serikali na umma katka uwajibikaji wao katika nchii.
  3. Elimu- kuwepo na mustakabali wa nchi ndipo kutaisimamia mfumo mpya wa elimu kama wenzangu waliotangulia wakiitaji mfumo mpya wa elimu na itatuondolea ile hali ya kila waziri aingiapo wizara hiyo na kujiwekea mfumo wake wa kuiongoza wizara kwa kuifanya kama sarakasi
  4. Afya
  5. Miundombinu na mawasiliano
  6. Viwanda

 
Ninazifuatilia mkuu, nikipata naziweka sawia hapa jukwaani tuangalie na kupima

Ninaposema maabara ninalenga kuwa serikali iboreshe maabara za mashule hasa kuanzia shule za msingi, pia kila mkoa kama si wilaya kuwepo na maabara hizi. tusisahau katika majeshi yetu ya ulinzi na polisi waboreshewe maabara pia
Aina za maabara siyo zile za kutest litmus paper bali za majaribiop ya kisayansi, kwa mfano maabara zinazohusu masuala ya electronics na components zake, pia zinazohusu masuala ya fizikia hasa mashine na mitambo ili kuwezesha wavumbuzi kujitokeza na kuleta changamoto za maboresho. Nakumbuka nilipokuwa shule nilimwomba mwalimu wa fizikia nifanye jaribio la kurusha roketi (niliambulia kibano). Maabara za masuala ya arts hasa sisi tunaotumia rangi za kuchorea tunaweza kuvumbua aina ya rangi kutokana na malighafi za hapa nchini hivyo tukaongeza pato la taifa (nakumbuka nilipokuwa najifunza uchoraji sikuweza kupata rangi na matirio nyinginezo, nilitumia majani na maua kupata rangi na manyoya ya wanyama kutengeneza brush), hivyo pamoja na maabara waandaliwe watu wa kuziendesha na kumaintain.
Nimeeleweka?

Msanii,

Kuna wengine wanapinga kwa sasa na hasa hasa kwa nchi masikini kujiingiza kwenye tafiti za ugunduzi zaidi (sisemi wasifanye) ila wanadhani (hata mimi naamini hivyo) kwamba kuna level ya hali ya juu ya ugunduzi umeshafanyika na uko kwenye public domain. Kwa hiyo sisi tunatakiwa kujielekeza kwenye technology zaidi ili kutumia hivyo vitu kutegengeza products kwa ajili ya matumizi yetu na kwa kukuza uchumi wetu. Kwa mfano, Cuba wanazalisha zaidi chanjo nyingi (na hasa hasa zile chanjo muhimu za watoto kwa mpango wa EPI) kwa sababu wametumia elimu iliyokwishafanyiwa kazi na kuweka nguvu kwenye uzalishaji. Kwa sasa ni chanzo muhimu cha chanjo hizo kwa shirika la afya duniani (WHO). Pia nasi tunaweza kuangalia mahali pa kuziba pengo, mfano, chanjo ya kipindupindu au products za kifizikia zinazohimili joto la hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom