Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Mkuu mimi napenda kufahamu tumefikia wapi na suala la katibu kabla ya kuendelea kuangusha point halafu zipotee hewani.
Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi nahisi alipendekezwa Dark City lakini mjadala kutoka kwake kuikataa nafasi hiyo ukawepo mda mrefu.
Labda WOS anajua suala la katibu lipo vipi.
Lakini unaweza kujitolea kuwa katibu maana hata huyu mwenyekiti wetu kajitolea pia.

jamani kuna anayepinga???

Naona kimya chenu kinaashiria tumempata katibu

Hongera Ambassador nakuomba uchukue nafasi yako ya ukatibu.
Turudi ktk mjadala sasa
 
AGENDA NO:1

  • KATIBA MPYA
AGENDA NO:2

  • KUPUNGUZA MAWAZIRI IDADI 20 TUU.
AGENDA NO:3

  • STOP UNUNUZI WA MASHANGINGI.
Nawakilisha mheshimiwa mwenyekiti kwa Heshima.
 
mkuu Kiby
umenena vyema ila kuhusu suala la mapenzi katika katiba mhhhh!
ngoja tumsubiri mtaalam wa masuala ya katiba atushauri namna ya kuliweka sawa suala hili.
Kuhusu nanihii nadhani akirudi mwenyekiti ataipambanua

.
Sawa mkuu navuta subira. Ila nikunongoneze sikioni kabla ya m/kiti kuja na wala sitaki mjumbe yeyote asikie, ikiletwa hoja ya jinsia moja kuruhusiwa kupumuliana walahi naapa nitapindua meza potelea mbali hata kama mkutano utanikabizi kwa Kova. Unajua mkuu rasilimali watu ni mtaji tosha wa maendeleo kwa taifa makini. Sitavumilia kuona mwendelezo wa uzao ukikomeshwa. NITUNZIE HII SIRI MKUU! SIVYO??
 
nashukuru sana mwenyekiti kwa kunipa fursa ya kutoa maoni

kwanza kabisa nitoe salama
kwa mwenyekiti ,katibu ,meza kuu kwa pamoja, wajumbe kutoa vyama mbalimbali , wagombea uraisi wote mliofika wote kwa pamoja nasema mungu awabariki kwa kuonyesha upendo wenu kwa nchi yetu tanzania.

ndugu mwenyekiti nina hoja 3 kuu ambazo ningependa zifanyiwe kazi

hoya zenyewe ni
1.Dira ya taifa kwa miaka 20 ijayo
2.katiba mpya
3 elimu


Dira ya taifa kwa miaka 20 ijayo
hili suala naomba katika uongozi ujao lifanyiwe kazi kwa umakini sana

ningependekeza kuwa chama kitakacho ingia madarakani kifanyo ifuatavyo

kuitishe kongamano la wataalam kutoka kila sector yaani uchumi ,sayansi na nyinginezo hapa naomba kutoa angalizo wanasiasa wasihusishw ewataalam hao watengewe sehemu na kupewa mda kututengenezea dira ya tanzania kwa miaka 20 katika hio miaka ishirini waigawanye katika miaka mitano mitano then wagawe tena katika kila mwaka nini kinatakiwa kifanyike. kumbuka wanaotakiwa kutengeneza ni wasomi na iwe ni dira ya taifa sio ya chama baada ya hopo ipitiwe na ikubalikwe hilo zoezi lipelekwe kwenye vyama na wasign kuifuata hio dira endapo kitapata nafasi katika miaka hio ishirini .

katiba mpya
itengenezwe katiba mpya ambayo pamoja na mambo mengine itaweka mkazo kwenye dira hio jinsi ya kusimamia kuanzia waziri mpaka mkuu wa nyumba hii itasaidia kwani tunatengeneza katiba tukijua tuna nia ya kwenda wapi au hii katiba inatusaidia kufika wapi.

elimu

itolewe elimu ya uraia na katiba kwa wananchi wote hili ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo mfano ilisha wahi kufanyika katika nchi mojawapo barani ulaya karine ya 18 wananchi wote walifundishwa ustaarabu na thamani yao Mfano unakuta mtu anaakili yake anaelimu ya chuo kikuu anakula mhindi na kutuma gunzi barabarani ukimuuliza atakuambia si tunalipa kodi wapo watu kwa ajili ya kufagia barabara mtu kama huyu teyari ana elimu ila hajui ustaarabu.

kwa leo naomba tuishie hapo.

mwenyekiti naomba uniruhusu nitoe mapendekezo kwa ajili ya kikoa kijacho kwani naweza kukosa mda tena

nashukuru wajumbe kwa kutii wito wa huu mkutano kwa vyile ni mara ya kwanza siwezi kuwalaumu ila nawapongeza zaidi ya yote ningependekeza angalau mara mbili kwa mwaka tuwe tunafanya mkutano kama huu online. na minute zitolewa report itumwe bungeni,na jumuia nyingine ambazo tutaziona zinafaa katika mikutano ijayo kuwe kuna daraja kabla post haijawekwa mbele hio itasaidia kuondoa watu wanaofanya joking na kuupuuzia mfano mimi nina changia baada ya kuonana kutuma lakini mwenyekiti na katibu wanazipitia then ndio inawekwa buplic bila kuchujwa kama inaonekana ni mbaya(naamaanisha utani masihara haiendani na mkutano)automatic mnaipeleka kwenye agenda zilizo tupwa kwenye mkutano yaani page nyingine kwa hiyo mtu akilalamika amechangia ila point yake imepuuzwa wajumbe wataiona kwenye page nyingine ila sio hii cream nashukuru wajumbe wote asanteni
 
Kwanza tunachangia tuuu hata lunch hatupewi ruksa! Sijasikia sitting allowance ni dola ngapi!
Mheshimiwa mwenyekiti natoa hoja
 
Sasa naomba niwaite wafuatao watoe maoni yao. Tafadhali njooni jukwaani. kamata Microphone please:
The Good
Ambassador
Dark City
Lubaluka
payuka
Misterdennis
Chesty
Mujuni2
Kabengwe
mlachake

Sawa kwangu mimi naomba yafuatayo.

1. Katiba iandikwe upya kama wajumbe wengine walivyosema.

2. Nchi ianze kujengwa upya nikiwa na maana kuwa yaundwe mashirika yakishirikiana na mabenki ambayo yataanza kupanga upya miji. Sehemu zote ambazo ni unplanned zinakuwa bulldozed watu wanalipwa fidia zao na nyumba bora zinajengwa. Hii ni pamoja na miundombinu ya maji safi, maji taka, barabara, umeme, nk.

3. Jeshi la polisi liundwe upya, liwe na vifaa vya kutosha kama magari ya patrol kwenye highways na hayo magari yawe na mitandao ya satellite so they can be seen wherever they are ili kuepuka rushwa.

4. Mapato yapatikanayo na madini yahusike moja kwa moja kuhakikisha kuwa watoto wanasoma bure na watu wanapata matibabu kwa kuchangia kidogo sana.
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi nahisi alipendekezwa Dark City lakini mjadala kutoka kwake kuikataa nafasi hiyo ukawepo mda mrefu.
Labda WOS anajua suala la katibu lipo vipi.
Lakini unaweza kujitolea kuwa katibu maana hata huyu mwenyekiti wetu kajitolea pia.

jamani kuna anayepinga???

Naona kimya chenu kinaashiria tumempata katibu

Hongera Ambassador nakuomba uchukue nafasi yako ya ukatibu.
Turudi ktk mjadala sasa
Teh teh teh! Akirudi Superman hapa utamueleza kwa nini umefanya mabadiliko! Kwani amekuachia full madaraka?
 
Kwanza tunachangia tuuu hata lunch hatupewi ruksa! Sijasikia sitting allowance ni dola ngapi!
Mheshimiwa mwenyekiti natoa hoja

.
Nahisi harufu ya uccm kwa mbaali. Ama labda ni upepo umelipiga jengo la makao makuu Lumumba kuelekea huku jangwani tuliko?
JAMANI TUZINGATIE UTAIFA WETU KULIKO CHOCHOTE.
 
Napendekeza kuwa vipaumbele katika Uchaguzi wa 2010 viwe kama vifuatavyo;


  1. Katiba: Katiba ya nchi ina mapungufu mengi na makubwa. Katiba ndio dira ya uongozi na ustawi wa jamii huru. Katiba haiwezi kutungwa kwa matakwa ya wachache wenye mahitaji ya kujitwalia kila lililo bora katika nchi. Katiba ni lazima ijenge usawa na haki kwa watu wote bila kujali nafasi zao katika jamii. Katiba lazima ijenge heshima kwa wananchi kati yao na kwa nchi yao. Katiba ni lazima ijenge uwajibikaji. Serikali ijayo ihakikishe kuwa wananchi wote wenye uwezo wa kushiriki katika kuandaa na kutunga Katiba wanashirikishwa (kwa kuchagua) katika utungaji wa Katiba ya nchi. Kuachia kundi la wanasiasa wachache kutunga Katiba ni kunyima haki na kuondoa usawa muhimu kwa Taifa.
  2. Afya: Jinsi gani serikali ijayo itakavyohakikisha afya za wananchi wake zinaboreshwa. Hii inahusu zaidi mapambano ya nguvu dhidi ya Malaria, maambukizo ya ukimwi, na magonjwa mengine, uboreshaji na uongezaji wa hali na idadi ya hospitali/zahanati, madaktari, vitendea kazi na dawa baridi
  3. Elimu: Jinsi gani serikali ijayo itakavyo hakikisha elimu inatolewa kwa wote wenye kuihitaji ili kuondokana na ujinga na kuongeza uwezo wa uzalishaji, ubunifu na kuepukana na umasikini. Wananchi wenye elimu nzuri wanaweza kuliingizia taifa mapato makubwa kwa kutumika katika juhudi za maendeleo na pia kukodisha wataalamu kwa nchi zinazohitaji utaalam huo.
  4. Miundombinu: Serikali ijayo inahakikisha vipi kuwa barabara, njia za reli na usalama wa majini zinaboreshwa na kuwa za viwango vya juu ili kuwezesha unafuu wa uchukuzi wa mazao ya kilimo na urahisi wa usambazaji wa huduma za jamii ikiwemo ulinzi na usalama, elimu na afya na kadhalika. Vile vile, ili kuwezesha kupunguza ajali zinazoligharimu Taifa kutokana na upotevu wa maisha ya wananchi wake, upungufu wa nguvu kazi kutokana na muda wa matibabu na hata kupunguza uwezo wa wahusika kwenye ajili hizo kuzalisha kwa kiwango kizuri kama inavyotakiwa.
  5. Kilimo cha kisasa: Kwa kuwa Taifa lina ardhi nzuri yenye rutuba na ukubwa wa kutosha, serikali ijayo ifanye jitihada kuhakikisha ardhi hiyo inatumika vizuri katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara ili kuwezesha nchi kuzalisha chakula cha kutosha na kuongeza pato la Taifa kutokana na kilimo. Kwa kutumia kilimo, wakulima wataweza kujikimu na hali ngumu ya maisha kwa kuweza kuhakikisha ustawi wa familia zao na kujemga Taifa huru zaidi lenye kujitosheleza kwa chakula na bidhaa nyinginezo za mashambani. Vile vile kilimo kitapunguza tabia ya watu kuwa wachuuzi kwa bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.
  6. Viwanda: Serikali ijayo itakuwa na mpango gani wa kuanzisha viwanda vya usindikaji wa mazao ya wakulima na uzalishaji wa bidhaa nyingine za majumbani, maofisini na sehemu nyingine kama zinavyohitajika na jamii? Kwa kukuza viwanda, serikali itaweza kuhakikishia wakulima soko la mazao yao, kuongeza ushindani na bidhaa za nje, kuongeza ajira kwa watu wake na kuongeza pato la Taifa. Vile vile, viwanda vitaifanya nchi iwe na heshima duniani kwa kuwa na watu wenye ujuzi na ubunifu na wenye kipato kinachoridhisha zaidi.
  7. Ulinzi na Usalama: Serikali ijayo inatakiwa iwe na uwezo wa kuhakikisha kuwa mali na hali za watu wake zinalindwa kila wakati ili kuwawezesha kuzalisha zaidi, kufurahia mafanikio yao na kujenga uzalendo kwa nchi yao. Nchi salama ina uwezo mkubwa zaidi ya kukua kiuchumi na kujenga jamii yenye umoja.
  8. Ushirikishwaji wa Umma: Tanzania itajengwa na watanzania. Serikali ijayo ihakikishe kuwa watanzania wa rika zote, wenye uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa Taifa wanashirikishwa ipasavyo katika kuamua, kujenga na kufurahia matunda ya nchi yao.
  9. Na mengine yoyote kama yatakavyochangiwa na wengine.
 
.
Nahisi harufu ya uccm kwa mbaali. Ama labda ni upepo umelipiga jengo la makao makuu Lumumba kuelekea huku jangwani tuliko?
JAMANI TUZINGATIE UTAIFA WETU KULIKO CHOCHOTE.

Mkuu ni nani wa sasa anajali hili taifa. limebakia kama yatima! Kila mtu anajichukulia chake mapema tu. Ukiamka oooh yule ana meli, ooo huyu ana hotel ya 5 star south, ukienda kule ooh kiwira ni ya mang'anya. Tukubali tukatae hii nchi imebinafsishwa na hakuna mwenye uchungu nayo. Mwenyekiti allowance hakuna ama tufanye uzalendo tu? ni swali tu Mh. Munyakiti
 
Mwenyekiti kaingia mitini bila kuahirisha kikao wala kumuachia kaimu nini? Nasikia harufu ya futari, baadae kidogo.
 
Ok nimepata taarifa toka kwa mwenyekiti wa dharura kuwa amepatwa na dharura hivyo atakuja kwa dharura baada ya kumaliza dharura. Ni majibu ya dharura baada ya dharura hii.
 
Nyunyu karibu sana. Toka jana nilituma watu wakutafute nikaambiwa umekwenda kule nanihii . . . kunanihiii . . . shughuli muhimu.

Siku nyingine ukisikia kikao muhimu kama hiki jitahidi kuwahi. Na siku hizi kuna Boda Boda so, kuwahi siyo issue ya foleni tena.

Turudi kwenye hoja sasa:

Hili na katiba liko sawa na limekaa vema. Tusaidiane kumtafuta dr. Mvungi atuletee draft tuanze kuipitia hapa.

Hili na Elimu nadhani ni Muhimu ila mpaka sasa hatujaliweka sawa. Kuna moja alisemaa elimu ya msingi iwe hadi kidato cha nne. Je baadaa yaa hapo itakuwa imemwandaa kijana wa Kitanzania kukabiliana na maisha?

wale waliobahatika kuhudhuria Silivan Summit mlimsikia Rais wa Mozambique akiongea kuwa yeye Mpango Mzima wa Elimu ni kujenga Vocational training Centres mapka level ya kata. ameshafanya hivyo kila wilaya sasa. Na akasema vijana wakimaliza wanaingia moja kwa moja katika soko la ajira ya kazi za mikono na uzalishaji.

Tuna shida kwani haapa vijiweni down town nawaona hadi university Graduates na wengine na Masters wakitafuta ajira. Wa diploma na advanced ndo usimseme, tayari nina CV 10 wakiomba niwatafutie ajira nami wala sijawapatia bado kwani hazipo.

Hebu tuelewane katika hili, tunataka nini hasa katika Elimu? Let us be brief and to the point.

Mwenyekiti Asante sana,

Unajua hapa mjini tuna wale wadhamini wanaohahakikisha tunacheka mwisho wa mwezi. Tehe teh tehe.... nilikuwa nawajibika huko mkuu.

ELIMU.
M/Kiti, ukiangalia mfumo wa elimu kwetu utashindwa hata ku-define objective ni nini!! Kuanzia timing kwenye mitaala, muda wa temu za shule, etc utachoka. Siku hizi Dar kumezuka wimbi la watoto kupelekwa shule za ST NANIII...; kuna watu ambao wanalazimika kufanya hivyo simply because watoto wa jirani zake wanasababisha watoto wake wachukie kwenda shule kwa kuwa wa jirani wakiwa likizo wake (wanaosoma shule zetu za msondo) wanaenda shule. Its just likizo za st nanii na shule za msondo ni tofauti!! Serikali ni lazima ilione hili kwa macho matatu, kwanza kuwe na uthibiti wa ada (for private) na pia term ziwe sawa, Wizara ya Elkimu ndo ielekeze mitaala ya kufindishia na itumike kwa shule zote. Hii itasaidia kuwa na mfumo sawa tofauti na sasa, st nanii wanatumia mitaala yao, kila mtu na lake, mwisho tutakuwa na elimu isiyokuwa na standard moja. Nasisitiza mfumo uwe mmoja kwa shile zote!!

VOCATIONAL TRAININGS
M/Kiti hii zamani ilikuwepo na ilikuwa derfined vizuri tu, ni serikali ya CCM ndo ilivuruga mambo. Kulikuwa na a good selections kwa watoto kwenda vocational trainings, technical schools, ualimu etc. Hawa jamaa wamevuruga, mwishowe siku hizi imekuwa failures ndo wanaoenda tech schools na vocationals!! Mfumo wa elimu unapswa kuwa na mechanism ya kuchagua wanafunzi wa high schools, tech schools voct schools etc. Hii itasaidia kila mtoto kwenda kwenye fani anayopenda, maana wanafunzi wapo wa aina nyingi, kuna ambao ni artist by nature, vipaji vitakuzwa toka chini!!

Mkuu kwa sasa naomba niwakilishe.
 
Order, order, order jamani! Mbona mna fujo hivi?

Kaimu Mwenyekiti kaenda wapi? Maana naona jukwaani simwoni hapa na watu wanaongea bila mpangilio . . .

Tusikilizane jamani!
 
Aiseee . . . .Nilifikia wapi tena . . .
 
HII KALI! Wiki hii sijacheka kama nilivyocheka baada ya kusoma post ya mwenyekiti wangu wa mkutano!
Jamani...kiswahili chaenda kikiwa kigumu.Kama haya ni matusi ya nguoni, je yale yenyewe ya nguoni yatakuwa nini?

Habari ndo hiyo . . . lakini sasa yamekwisha turudishe mshikamano!
 
Kwanza tunachangia tuuu hata lunch hatupewi ruksa! Sijasikia sitting allowance ni dola ngapi!
Mheshimiwa mwenyekiti natoa hoja

Sitting allowance wakati umesimama! wewe vipi?Jangwani hakuna sitting, standing wala sleeping allowance!
Mwenyekiti..naomba hili la mshiko nalo liwe mojaya ajenda ili mkakati wa kuondoa hizi rushwa halali uwekwe. Watu wameajiriwa kufanya kazi na sio kupokea malipo kwa kukaa!
 
Back
Top Bottom