Uchaguzi 2020 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM: Dkt. Hussein Ally Mwinyi achaguliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM. Membe afukuzwa rasmi

Ccm naowajua wakitaka mtu fulani atapita hata kwa kupindua meza. Mm nilimuona yule Doc kama yuko matured kidogo kuliko mwinyi
Kalpana hebu ifafanue hyo maturity tujibwedee hapa....
 
Ccm ni Mali binafsi mmiliki wake ndie mwenye maamuzi nani agombee Nani asigombee,
 
Karume Baba, Karume Mtoto, Mwinyi baba na sasa Mwinyi mtoto. Twende nao, nitaulizwa " Mbona tulikua na Bush Baba halafu Bush Mtoto?" nitajibu nini mimi. Nasikia jamaa hata JKT alikwepa, sijui wana mpakazia. Sasa tusilalamike sana labda Maalimatapata upenyo ni wazanzibar kuamua, au kuna jecha mwingine kajificha mahala?
 
Rais wao anachaguliwa zanzibar, huko dodoma hao ni ccm ndio wamekaa huko kuchaguana, hao ni ccm, sio wazanzibari
 
Vuai alikuwa kama raia tu kwa miaka 10 iliyopita. Siasa usipotokea kwenye vyombo vya habari, ndio basi tena. Hakuwa na cheo cha kumfanya aonekane mara kwa mara. Hata kuingia kwenye 3 bora sikutegemea.

Facts.
 
Oh ho wamenuna CCM Zanzibar , maskani manung'uniko- oh Usultani siyo lazima mwarabu.
 
Vuai alikuwa kama raia tu kwa miaka 10 iliyopita. Siasa usipotokea kwenye vyombo vya habari, ndio basi tena. Hakuwa na cheo cha kumfanya aonekane mara kwa mara. Hata kuingia kwenye 3 bora sikutegemea.
Wamemuweka kwenye 3 bora kama rubber stamp tu ya Dr Mwinyi.
 
Afanye siasa gani zaidi wakati amekuwa mbunge wa Jimbo la kwahani Unguja kwa vipindi vitatu mfululizo 2005-2020, amekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa na mjumbe wa kamati kuu ya CCM kutokea Zanzibar kwa muda mrefu sifa hizo zinatosha kuijua siasa ya Zanzibar
 

Mbona hushangai Mwenyezi Mungu kuwapendelea wana waISRAEL?!!!

Itakuwa sisi BINADAMU.....

Yaani sijui siasa zenu za kiliberali zenye WISHFUL THINKING ziliasisiwa pale ACUTE WARD NO.14 HOSPITALI YA MIREMBE JIJI LA DODOMA?!!!

Imeisha iyoooo twende na Dr Mwinyi.
 
Kwa sababu hiyo hiyo, ndio maana Mbarawa hakuingia kwenye 3 bora. Kama angeingia kwenye 3 bora, angekuwa tishio kwa chagua lao (Mwinyi). Kura ingeweza kulalia upande wowote.
Wamemuweka kwenye 3 bora kama rubber stamp tu ya Dr Mwinyi.
 


Mungu hapendelei kiumbe yeyote , hayo ni makosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…