Mkutano wa pili wa umoja wa mabaraza ya habari Afrika

Mkutano wa pili wa umoja wa mabaraza ya habari Afrika

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

View: https://www.youtube.com/live/TESsdXCNBrU?si=zVojh8cRb2WhaVBx



Mkutano wa Pili wa Mabaraza ya Habari Afrika 2025 umeelezwa kuwa ni fursa ya kihistoria kwa vyombo vya habari barani Afrika kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kukuza matumizi ya teknolojia mpya, na kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya sekta ya habari.

Katika mkutano huo unaofanyika Arusha, viongozi mbalimbali wakiwemo Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, wamesisitiza umuhimu wa kuwa na mifumo madhubuti ya udhibiti na usimamizi wa vyombo vya habari itakayolinda uhuru wa habari, kukuza uwajibikaji, na kuongeza imani ya umma kwa tasnia ya habari.

Aidha, mjadala mkubwa umejikita kwenye changamoto za kidijitali, hasa ongezeko la maudhui yanayozalishwa na akili bandia (AI), na haja ya kuwa na mifumo ya ukaguzi na uhakiki Taarifa na ukweli (fact-checking) ili kudhibiti upotoshaji. Mkutano huu unaonesha dhamira ya Afrika kuunda mfumo thabiti, unaojitegemea na unaoendana na maadili ya Kiafrika katika uendeshaji wa vyombo vya habari
 
Back
Top Bottom