Kitengo maalumu cha kueneza na kusimika siasa za magharibi kwa masrahi ya mataifa yao makubwa. Ni aina flani ya mtego ambao asiyeunga mkono ataonekana ni adui wa ulimwengu kumbe hayo hayo mataifa makubwa ndo maadui wakuu wa ulimwengu na nchi maskini.
Mataifa yote ya Afrika kuwa masikini sio bahati mbaya wala amri ya Mungu, bali sababu ya aina moja iliyowekwa kwa ustadi mkubwa inayosababisha yawe hivyo. Kwa bahati mbaya viongozi wetu wa Afrika hawaonekani kuhangaika kwa pamoja kujinasua na sababu hiyo. Sababu hiyo ni kati ya hizi zifuatazo:
1. Viongozi wa Afrika kupenda misaada kutoka kwa wakoloni wao.
2. Viongozi wa Afrika kupenda sana kwenda ulaya na marekani
3. Elimu hafifu inayotolewa kwenye mataifa ya kiafrika
4. Viongozi wa Kiafrika kupenda kusifiwa na wazungu.
5. Viongozi wa Afrika kuacha kufuata ushauri wa wataalamu wao kwenye maamuzi, hawaamini utaalamu.
6. Nchi za Afrika kuuziana wenyewe kwa wenyewe bidhaa kidogo sana.
7. Nchi za Afrika kutokuwa na msimamo wa pamoja kuhusu hatima yao
8. Nchi za Afrika kuwa na sera mbaya
9. Waafrika kuacha kuthamini vitu vyao
10. Ukoloni mamboleo: Zile sababu zilizowasukuma wazungu watafute makoloni miaka ya 1880's bado wanazo hadi leo. UN, commonwealth na taasisi nyingine zenye sura ya kimataifa kuvalishwa agenda za siri.
11. Viongozi wetu wa Afrika kufurahishwa na sera za wazungu za divide and rule: Mfano, Kenya inafurahi kuondolewa vikwazo vya kusafiri na waingereza kwa masuala ya covid 19 katikati ya nchi zote za Afrika mashariki na kati, lakini wamefurahia kitu kama hicho.