Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Hilo kongamano limenisikitisha sana. Ni dhahiri viongozi wa dini wanaonesha upande. Namuunga mkono JPM lakini hii ni too much. JPM hahitaji yote haya kushinda
 
Kweli Mungu wetu ni mkuu na ndio maana amelifanya taifa la Tanzania kuishinda corona.magufuli ooyeeee!!!
Wanasema mungu wa yakobo ndio huyo mungu wa yohana mimi nakataa, Mungu aliyetupa amani na mungu wa maaskofu ukumbini leo ni wawili tofauti
 
Mungu wa isacka,Yacobo,Yohana ndo Mungu aliewapa hekima na busara viongozi wetu wa dini kuamua kukutana na Rais wetu kipenzi JPM.
Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi, hakuna hata mmoja aliyetokea hadharani kukemea jambo hilo hata angalao kulia pamoja naye.
Maiti zilipokuwa zinaokotwa kule ufukweni, hakuna hata mmoja aliyejitokeza kuhoji watawala watoe maelezo kuwa zilifijaje hapo, licha ya kitendawili kuwa ni za nani. Maiti zilizookotwa mto Ruvu sikuwasikia wakihoji. Mauaji ya Aquilina sikuwasikia. Kwamba Ben Saanane yuko wapi, Azori Gwanda , Simon Kanguye sikuwasikia hata viongozi wa madhehebu yao wakihoji. Amani wanayoiomba ni ipi? Nadhani wangeliomba kuwa haki itamalaki zoezi lote la uchaguzi. Nadhani wangelitubia dhambi ya rushwa iliyotamalaki katika zoezi la awali la watia nia, na kukukemea lisiwepo wakati wa uchaguzi. Nadhani wangekemea kauli kama zile za kutumia vyombo vya dola ili kubaki madarakani n.k. Hawa sio wa kweli wala wa haki wala sio wapenda amani ya kinaukweli. Yarabi tunusuru.
 
Na ninyi tumieni waganga kuingia ikulu
Ukimaanisha?

Kwamba ni halali kutumia dini kuingia ikulu mnavyofanya na unatushauri sisi tusiotumia dini tutumie waganga?

Hivyo ni kwamba una halalisha kutumia dini kupata madaraka?

Mzima kweli wewe?

Mkuu,tufata principles,we do not follow your immoral behavior mnaziofanya!

Wewe unatumia dini,full stop...mwache ambae hatumii huo ujinga,apate ikulu asipate wewe una presha gani nae?

Mnachofanya ni immoral na mnajua,kazi yetu ni ku-condemn what you are doing basi....fanyeni tani yenu concequences mtapata nyie nyie kutokana na matendo yenu
 
Kuna haja ya kuacha kwenda MAKANISANI.

MAKANISA yote Ni CCM
Hii Kamati ya Amani kama sikosei ni kamati ambayo inahusisha viongozi wa dini wa Dar es Salaam tu, si ya kitaifa. Kuna haja ya viongozi wa dini wa kitaifa kulisemea hili tukio kama na wao wamelibariki kwa jinsi lilivyo. Kama hawatafanya hivyo, kuna haja ya waumini kuomba viongozi wa kitaifa wa dini walisemee swala hili ili kufahamu msimamo wao, vinginevyo waumini wafanye protests za kutokwenda nyumba za dini mpaka pale maelezo sahihi ya huu msimamo uliogemea upande mmoja utakapopata maelezo yanayoridhisha.

Tumezoea kuona nyaraka za Kiaskofu ambazo zinaelezea mambo mbalimbali yatokeayo nchini ikiwemo yale yanayo hatarisha amani yetu na jinsi ya kurekebisha lakini kwa sasa imekuwa nadra sana kuziona na kuzisikia. Mara nyingi viongozi wakisemea mambo ya kisiasa na utendaji wa serikali ambao una sura ya hasi wamekuwa wakiambiwa kuwa wanaingilia mambo ya siasa, wabaki kwenye mambo ya dini tu. Je jambo hili la leo la kusifu na kupongeza si la kisiasa?
 
Wanachokifanya kitawagalimu sana.
Haiwezekani kiongozi wa dini hasa kipindi hiki mnakuwa na biases
Its so bad

Sujutii kutokwenda kanisani muda mrefu sasa, baada ya kujua huko kwenye nyumba za ibada ni sehemu ya kufichia waovu. Hao viongozi wa dini wanaokutana leo kusifu kazi za rais, wote walishuhudia kilichofanyika kwenye uchaguzi wa SM na chaguzi zote za marudio. Lakini walikaa kimya, na wale wote walioandika waraka waliitwa na kutishwa vibaya. Kwa sasa wengi wao wameshalainika. Nikikumbuka Mussollini alivyoitawala Italy kwa mgongo wa kanisa, naanza kuona picha kubwa ya kile kitakachofuatia.
 
Back
Top Bottom