Mkuu Poor brain, mateso ya Mama wa Kambo hauko peke yako, tumeyapitia wengi

Mtoto anadeliver kile alicholishwa, ni wachache wenye uthubutu wa kupambana.
Na wengi hukata tamaa zaidi akiona baba anamsikiliza zaidi mama kuliko yeye.
Sahihi mkuu, tujitahidi kuchagua wenza wa maisha japo waliosahihi kuepukana na kadhia kama hizo zisiwatokee vijana wetu cc Ushimen
 
Mtoto anadeliver kile alicholishwa, ni wachache wenye uthubutu wa kupambana.
Na wengi hukata tamaa zaidi akiona baba anamsikiliza zaidi mama kuliko yeye.
Sahihi mkuu, tujitahidi kuchagua wenza wa maisha japo waliosahihi kuepukana na kadhia kama hizo zisiwatokee vijana wetu cc Ushimen
 
Njoo inbox
 
Kwa asilimia kubwa wako hivyo hasa hao masingo Maza, mama wa kambo singo Maza ni kirusi zaidi
 
Kuna dogo huko ngara alipoona mateso yamezid alienda kujitafta mwanza.
Lakin huko home mamake wa kambo akawa anawaambia watu kwamba huyo Daniel hawaez kutoboa maisha hata iweje nikiwa hai.

Nahuko dogo ikawa ni majanga juu ya majanga. Alipo ambiwa hayo maneno ya maza yake wa kambo dogo aliumia saana akasema pamoja na kuniharibia maisha na kuamua kumkimbia bado ananifuatilia tena hata nikiwa mbali??
Sasa kwenye harakati za mishe huko mwanza dogo alkuwa na marafiki wenye asili ya rwanda na burundi. Asee dogo akaongea na na rafiki yake wa burundi akampa connection.

Dogo alitoka mwanza kimyakimya akatimba burundi akakodi mguu wa kuku akazama nao mpaka home ili akamalize kazi. Kwao wakati huo walijua yuko mwanza.
Kwahyo dogo alitaka kufanya tukio bila kujulikana sema kwa bahat mbaya akakuta mamake wa kambo yuko na shaz la wanawake wakiwa wanasukana.
Dogo akasuburi wee akaona kukaa na chuma mda mrefu anaweza kuwamwaga wote waliokuwepo pale na yeye kukamatwa, ikabidi avunge akasepa.
Kwahyo mama yake wa kambo akapona hivyo.
 
Mwambie dogo a move on afute mahusiano ya huko kwa mama yake kambo aondoe kinyongo. Mimi alishawahi Kuja nyumbani kwangu mtoto wake wa kike yani mdogo wangu upande wa baba amekaa sana kwangu hapa alivyoondoka nikamfungashia ZAWADI za vitenge, kanga, mashuka na blanketi awapelekee Mzee akajifunike na mke wake. Walivipokea akapiga sim kushukuru baadae alianza kupga sim kunisalimia nikawa sipokei mpaka Leo sipokei sim yake labda Mzee apige napokea nikiwa kwenye mudi nzuri vinginevyo sipokea kwakweli mnisamehe
 
Duuuh we jamaaa mbona una hatarerr hvo aiseee
Mkuu nilishasolve nikofresh japo sio kivile. Ndio maisha yenyewe ndugu yangu binadam tunapitia mengi. Na nikuambie nisingekuja town huku nikapambana nikapata pesa ya kujipambania nilikuwa tayari nishakufa kitambo bila hata kuweka alama yoyote hapa duniani
 
Usimlaumu mshukuru sana huyo mama wa mambo maana alikua anakujenga katika kuyazoea mazingira yote bila yeye kujua huo ni moango wa mungu juu yako hata Mimi nimepitia baadhi ya mambo kama hayo lakini baada ya kukua na kuyajua maisha nikagundua yule mama alikua mwalimu mzuri sana kwangu bila yeye kujua na watoto wake wamekua mafukara na walevi sana hatimae Mimi ndio nimekua tegemezi lao nashukuru sana mungu kwa njia alizonipitisha hatimae nikawa mtu tusipende kuwalaumu wamama wa jambo inawezekana ungelelewa na mzazi wako Leo hii ungekua marioo
 
Siwezi kumshukuru kwa lolote, wa kumshukuru ni huyu Mzee aliyenitoa bush kunileta huku japo alinilagai ananipeleka dsm kwa mwanae nakasimamie duka la ujenzi mwisho wa siku tumefika hapa nyumbani kwake akanikabidhi kwa kwa mkewe akanipa kazi ya kumuuzia vitumbua asubuhi, mchana barafu na maji ya kandoro na mshahara 15 elfu kwa mwezi imagine! Alinifunza sana life bahati mbaya akafariki mwaka wa kwanza nipo hapo nikawa nimebaki na huyo mke wake na ndoto ya kupelekwa dar kwenye mshahara mzuri ikawa imeishia hapo maana alikuwa hataki nitoke hapo kutokana na kazi na kipato nichokuwa namuungizia. Baadae nilichomoa betri dkt za jioni nikamwambia naacha kazi halafu mwanaume ninamshahara wa miezi mitatu. Akaniweka mezani akapiga hesabu zake za madeni anayodidai mara nilidondosha vitumbua kadhaa, mara nilivunja sahani, mara alinipa miche kadhaa za sabuni akakata kata madeni yake ikabaki 28 elfu nikasepa bila kujali itakuwaje huko nakoelekea. Huyo ndio wa kumshukuru sio huyo mama wa kambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…