Tukijadili hili swala kwa maslahi ya taifa tufikirie kuhusu kesho yetu. Tusidhani tuko salama sana.
Nachokiona ni kutaka kuuza nchi kwa maslahi y na tamaa za madaraka.
Marekani wakiamua mtawala wa nchi fulani atawale milele bila vurugu inawezekana. Aliweza kuigeuza Saudu Arabia kuwa ya kifalme wakati ilikuwa na utaratibu mwingine wa kiutawala.
Kwa tabia za hawa marais wa nchi zetu pale wanapoona tishio ktk uongozi wao wako tayari kuweka nchi rehani ili wasaidiwe ulinzi na mataifa yenye nguvu. hilo kwa nchi ya USA, Ufaransa na Urusi wako vizuri sana.
Ktk nchi zote duniani ambako Marekani kwa visingizio vya udumavu au tishio la usalama waliingiza vikosi vyao vya kijeshi( US miltary bases) nchi hizo hazikubaki salama hadi leo hazijatengamaa.
Mifano iko mingi michachi ni kama Somalia, Afighanistan, Uganda na Ethiopia.
Maeneo mengi waliingia kwa sababu za kupambana na ugaidi. Hadi leo nchi hizo hazitawaliki, hazina amani, ugaidi na uharifu wa kibinadamu na rasilimali umeongezeka mara dufu.
Tangu habari za Mboww kukamatwa kwa movie ya Ugaidi tunaona Mabeberu wakimiminika nchini. Kibachonishtua ni hawa makamanda wa AFCOM.
Je mama anataka kuweka rehani nchi ili wale maadui wa ndani wasimzingue? je tutasalimika??