Kwa wanaoita hayo mapigano "show" wajue Tanzania ilikaa njaa miaka mitano baada ya 1979, tukapewa unga wa yanga na USA, petroli tulikuwa tunanunua kwa kibali na kwa foleni, na sabuni na sukari ni kwenye duka la kaya.Baada ya show!!
Majenerali wa USA ambao hawajawahi kushindwa vita wanasema hakuna mjeda anaependa vita. Na kitu kigumu kwa marais wao huwa wanasema ni kupeleka watoto wa watu vitani
Sasa sisi ambao tunaweza kusondekwa vitani kwa kikao kimoja cha Halmashauri Kuu tuendelee kuchekelea na kufanya mizaha kwenye mitandao. .