Mkuu wa Majeshi aitembelea familia ya Sajent Mohamed Abdala Suleiman aliyefariki DRC

Mkuu wa Majeshi aitembelea familia ya Sajent Mohamed Abdala Suleiman aliyefariki DRC

Hili kundi,linaishi kwa kufanya kazi Gani, wanakula wapi? Wana mpango Gani kuhusu maisha Yao?wataoa lini na wataolewa lini?Wameajiriwa wapi? Wamesomea nini? Hili ni janga jingine!
Kwani hao wanajeshi wengine huwa wanayafanya saa ngapi hayo uliyoulizia?
 
Hakuna kurudisha amani hapo issue ni kwamba, Saa100 anamlinda mwenzake na ili likitokea la kutokea kwa Saa100 naye aweze kuja kumlindwa

..mkataba wa Sadc unasema nchi moja ikivamiwa nchi wanachama zinapaswa kutoa msaada wa kijeshi.

..mimi ni mkosoaji mkubwa wa Mama Abduli lakini siwezi kumlaumu kwa kuitikia wito wa kupeleka majeshi kurejesha amani DRC.

..ningependa AMANI irejee DRC na Tshisekedi na M23 washindane katika majukwaa ya kisiasa.
 
Hao yuvisisiemu kumbe walifariki wabeee tu!
..Jenerali Jacob Mkunda alipokwenda kutoa pole kwa familia ya marehemu Sajent Mohamed Abdala Suleiman.
===

"Mishoni mwa mwaka uliopita (2024) kikundi cha vijana wenye silaha wakijiita M23 walianza chokochoko na kuharibu kabisa amani ya mashariki mwa nchi ya Kongo. Kwahiyo vita ilitokea mnamo January 23, vijana wetu walipigana katika jukumu la kuwasaidia wenzao wa Kongo kurejesha amani mashariki mwa nchi ya kongo. Kwa bahati mbaya sana katika mapigano hayo tulipoteza vijana wawili katika kikosi cha Tanzania pekee, akiwemo kijana wetu Sajenti Mohamed Abdallah Suleiman. Yupo na mwingine private John ambay yeye anatokea kanda ya Mwanza."- General Jacob Mkunda, CDF Tanzania

Soma pia Askari wawili JWTZ wafariki dunia, wanne wajeruhiwa mashambulizi ya M23 huko Goma, DRC

 
Hata mimi imenistua kidogo.....sikumbuki matukio kama haya kuona au kusikia CDF mwenyewe anakwenda nyumbani kwa mfiwa kwa maelekezo ya rais. Anyway....
Niliona na ndugu wa marehemu anamuombea kazi ndugu yake ambaye yuko Kigoma, sijui aingizwe jeshini au vipi! ili asaidie familia
Jeshi la sokuhizi lina wapa ajira vijana ili kuzisaidia familia zao na siyo nchi, ndiyo maana tuna askari wa ajabu ajabu tu.
 
Mkuu umekosa uzalendo. Kumbuka huyu ni kijana wetu kaiwakilisha nchi yetu. Asante Jenerali Joseph Nkunda kwa kuitembelea na kuwafariji familia ya kijana wetu.

Nawachukia sana M23
Ndugu yangu kwa kifupi inauma sana, unaposema awe mzalendo unafikiri ni mbongo huyo? Moyo unaumia mno kuna pahala pamevuja vibaya mno mno tena😔😔😌😌
 
Ndugu yangu kwa kifupi inauma sana, unaposema awe mzalendo unafikiri ni mbongo huyo? Moyo unaumia mno kuna pahala pamevuja vibaya mno mno tena😔😔😌😌

..huyu askari amefariki ktk uwanja wa vita.

..pia ameuwawa na watu ambao sio Watanzania.

..pamoja na kwamba ni askari, lakini kifo chake kinatusikitisha wote.

..sasa hebu rudisha fikra zako hapa nyumbani.

..tunao vijana wa vyama vya upinzani wametekwa, wameteswa, wameuwawa, na Watanzania wenzetu.

..Mkuu wa majeshi ameomba radhi familia kwa kushindwa kuurejesha kwa wakati mwili wa Sajent Suleiman ili uhifadhiwe kwa taratibu za Kiislamu.

..Mwili wa Mzee Ali Kibao wa Chadema uliharibiwa na Watanzania wenzetu waliomteka na kumuua.

..nakuomba ufikirie machungu wanayopitia wapinzani. Je, ni halali kufanyiwa hivyo katika nchi yao?

..kama tuna hasira na M23 na Rwanda waliouwa askari wetu, je tunapaswa kuwa na hasira kiasi gani kwa Watanzania wanaoteka, kutesa, kuua, na hata kuharibu maiti za wapinzani?
 
Back
Top Bottom