Mkuu wa Majeshi ajuta na kuwaomba radhi wananchi wa Marekani kwa kuambatana na Rais katika ziara yenye utata ikihusishwa na siasa!

Mkuu wa Majeshi ajuta na kuwaomba radhi wananchi wa Marekani kwa kuambatana na Rais katika ziara yenye utata ikihusishwa na siasa!

Alisema: "Sikustahili kuwa hapo. Uwepo wangu hapo wakati wa tukio hilo ilionesha taswira kwamba majeshi yanajihusisha na siasa za ndani ya nchi.

"Kama afisa mkuu wa majeshi ilikuwa makosa na nimepata funzo, natumai nimejifunza kutokana na tukio hilo."

Jenerali Milley aliongeza kusema: "Lazima tuhakikishe tunatenganisha jeshi letu na siasa ilituendelee kudumisha sifa yetu."
Daah . . . . nchi nyingine zimestaarabika sana. Yaani mkuu wa majeshi anaomba radhi wananchi? mmmhhh sio Africa aisee
 
Naam, ndivyo ilivyo kwa nchi zinazoheshimu Katiba. Kiapo cha mwanajeshi ni utii kwa Katiba na si utii kwa Rais.
Aisee..! Yaani huyo kamanda hawajibiki kwa Rais au?

Trump kama Amiri jeshi mkuu angetakiwa kuvaa kombati kwenye hiyo ziara (kama viongozi wetu wakuu wanavyofanya).
 
Mzukulu,

Our level of professionalism is below evarage.hivyo tusamehe bure kwa kuwa hatujui tulitendalo,si wakuu wetu wa majeshi, Marais wetu Wala wananchi wa shithole countries
 
Kwa sisi wazee wa kuchumia tumbo, uwepo wetu karibu na "mkulu" ni jambo la kitukufu na heshima kubwa kabisa.
 
Kwanini unataka wanaume wengine wakupigania vita yako? Si upambane mwenyewe kama umekwazwa na mtu fulani.
 
Mkuu wamajeshi nchini Marekani amekiri kuwa alikosea kuungana na Rais Donald Trump wakati wa alipotembea kuenda kanisa lililopo karibu na Ikulu ya Marekani ambalo liliharibiwa na waandamanaji.


Tukio hilo la Juni tarehe moja na ambalo lilizua utata lilionesha "taswira kwamba jeshi linajihusisha na siasa za ndani ya nchi", Jenerali Mark Milley alisema.

Bwana Trump alitembea hadi kanisa hilo na kupiga picha akiwa ameshikilia Bibilia baada ya maandamano ya amani ya kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd kuvunjwa kwa nguvu
Tukifika hatua hii, maendeleo yanakuja yenyewe
 
GENTAMYCINE yuko wapi siku hizi[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Unataka waige nini kati ya hayo uliyoandika?
Waige kusema kuwa na wao wanasikitika kuambatana na wakuu wao wa nchi kwenda kanisani au waige kuambatana na wakuu wao wa nchi kwenda kanisani?

Maana hayo mambo yote mawili huyo mkuu wa majeshi wa marekani kayafanya. Sasa ndugu mtoa mada unataka waige kipi hapo?
 
Unategemea wakiiga kutakuwa na amani? Msilazimishe kukopi Kila kitu, mfumo wa kijeshi, katiba na kiwango Cha ufahamu Cha wamarekani Ni tofauti na wa kwetu huku, Marekani Ni taifa kubwa Sana na liko mbele yetu mara dufu katika Kila nyanja za maisha.

Tumia vizuri akili zako!
 
Sijui unamaanisha nini unaposema ,, Trump amekosa ushawishi” kwenye Majeshi, D.Trump ni Raisi wa USA na commander in chief wa US military, sasa sielewi unachomaanisha, ...
Mohamed Morsi rais wa Misri alikosa ushawishi jeshini. Raia walipoanzisha maandamano jeshi likalinda raia dhidi ya serikali.
 
Huyo ni four star general. Ukiona hivyo ujue Trump amekosa ushawishi na utashi. Juzi niliona Collin Powell akiunga mkono jeshi kutomkubali Trump hasa baada ya kuruhusu National guard mitaani.

Ukiona hivyo ujue Trump hana ushawishi wa kisiasa, utashi, uwajibikaji au uzalendo kwa raia wake. Ingekuwa nchi za dunia ya tatu Trump would have been no more.
Trump is not a war monger,ameondoa majeshi Syria na amekata budget ya kupigana vita Afghanistan.Kitendo cha kuondoa majeshi Syria walitofautiana sana ma Jim Matis hadi kupelekea kumwambia ajiuzulu.Trump sera yake ni kupunguza globalism na kutumia fedha kulijenga upya jeshi la USA,Kama unakumbuka obama alipunguza sana budget ya Jeshi na hata idadi pia..Sasa sera hii imefanya baadhi ya majenerali kutofautiana nae sana,Labda Joint Chief Chairman Gen Mike Milley nae inawezekana hakubaliani na baadhi ya Sera Za Trump...Ila in politics hayo ni mambo ya kawaida na yana muda pia...
 
Mohamed Morsi rais wa Misri alikosa ushawishi jeshini. Raia walipoanzisha maandamano jeshi likalinda raia dhidi ya serikali.


Kwa hiyo unamaanisha Jeshi la USA halichukui Amri kutoka kwa Raisi D.Trump? Isitoshe unafananisha Misri na USA?
 
Kwa hiyo unamaanisha Jeshi la USA halichukui Amri kutoka kwa Raisi D.Trump? Isitoshe unafananisha Misri na USA?
Sijamaanisha ulichosema hapa. Ninachomaanisha Trump kakosa ushawishi siyo kwamba kakosa amri.
 
Sijamaanisha ulichosema hapa. Ninachomaanisha Trump kakosa ushawishi siyo kwamba kakosa amri.


Tofauti ni nini? Bado sijaelewa unachomaanisha unaweza kufanunua kama ukipenda, kama ni commander in chief US Military ana anaweza practice power yake muda wowote ule kwa mujibu wa Katiba ya USA, ni kipi kingine anataka kama Commander in Chief ? Huo ushawishi unaoungelea ni upi na unaathiri vipi majukumu ya Commander in chief?
 
Back
Top Bottom