Mkuu wa majeshi Israel amgomea netanyahu kuishambulia iran

gallow bird

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2024
Posts
14,889
Reaction score
18,593
Mkuu wa majeshi wa Israel, bwana zamir,amemgomea waziri mkuu wa Israel Benjamin netanyahu kuishambulia iran siku moja kabla ya uchaguzi mkuu Israel

Bwana zamir alimtaka netanyahu asaini nyaraka rasmi za amri hiyo Ili atekeleze Ili baadae mkono wa Sheria usimkute

Netanyahu ana Hali ngumu ya kisiasa,huenda asishinde,na akikaa nje ya madaraka ni rahisi kwake kuukwepa mkono wa Sheria dhidi ya kesi yake ya ufisadi
Juzi ndege vita za Israel ziliruka hadi mpaka wa iraq-iran wakitaraji Iran ishambulie wapate sababu ya vita na hivyo kuahirisha uchaguzi
In ‘unprecedented confrontation,’ IDF chief said resisting Netanyahu's order for military action tied to Iran | The Times of Israel https://www.timesofisrael.com/in-un...g-military-action-tied-to-iran-ordered-by-pm/
 
Chai☕️ ☕️
 
Hivi Bibi unamchukuliaje huyu mtu sijawahi kumuona wala kufika Israel ila nimeangalia vlogs nyingi mno za waisrael na wapalestina pamoja na watu wa nje wanaokwenda huko ambao wako neutral

Aisee Bibi ni story ingine
Bibi ni zero tu nyie ndio mnamkuza. Hivi unajua chaguzi iliyopita alishinda kwa 20% pekee ya kura? Maana yake 80% ya raia wa Israel Walimkataa ila bahati mbaya waziri mkuu anachaguliwa na bunge sio wananchi so akaungana na vyama vidogo vidogo akawa waziri mkuu ila alikua na wabunge kma 22 pekee.

Kingine Netanyahu ana kesi ya ufisadi na rushwa sema anaisogeza mbele kwa kisingizio cha vita hivyo bila vita ataenda jela. Ila msiojitambua mnadhani anapigana vita kisa kupigania wayahudi au kupambana na ugaidi.

Kumbuka pia ana kesi ICC hivyo hawezi kanyaga ulaya tena maisha yake yote.

Nashangaa wewe unamsifia ila huko Israel hana hiyo heshima unayodhani anayo
 
Bora Netanyahu kiasi flani anauoga, huyu mpinzani wake Gadi Eisenkot wa moto kinoma.

Wagombea wote lengo ni moja wanatofautiana approach kuhusu Gaza/Hamas, Lebanon, Iran, Turkey, Damascus & Yemen.
Gadi ni reasonable sijui hii mindset kuwa ni hatari kuliko Netanyahu inatoka wapi. Kumbuka kambi ya Netanyahu kuna Israel katz, bezalel Smotrich na Itamar Ben Gvir hawa ni hatari sana kwa amani ya middle east.
 
Huyu hawamuwezi ni kelele tu za kisiasa, Iran imewashinda kupindua serikali ndio sembuse uturuki inayowazidi Israel kila kitu kijeshi
Wote baba yao mmoja, Turkey anamsikiliza Mmarekani na Israel anamsikiliza Mmarekani ndo maana hata Israel aliposhambulia Abu Al Duhur Air base Turkey akaishia kulalamika tu.
 
Wanachikitafuta kwa Muajemi ipo siku watakipata

hakuna “muajemi” tena, wote walikimbia au kuuliwa na muslims waliovamia persia, zoroastrians ni dini iliyokuwepo persia kabla ya uvamizi wa muslims, na zoroastrians wote were wiped out na waliobahatika walikimbia na kuhama, wengi walikimbilia india.

hivyo islamic republic of irani ≠ uajemi …
 
Acha blah blah,waajemi wamesilimu kama waturuki walivyoacha ukristo na kusilimu
 
Nyie hamuwajui wanasiasa uyodingi ana ushawishi mkubwa sana Marekani lazima waibe uchaguzi ashinde tu hao ndio wauni wenyewe wakizayuni
 
Mkuu wa majeshi wa Israel, bwana zamir,amemgomea waziri mkuu wa Israel Benjamin netanyahu kuishambulia iran siku moja kabla ya uchaguzi mkuu Israel

Bwana zamir alimtaka netanyahu asaini nyaraka rasmi za amri hiyo Ili atekeleze Ili baadae mkono wa Sheria usimkute

Netanyahu ana Hali ngumu ya kisiasa,huenda asishinde,na akikaa nje ya madaraka ni rahisi kwake kuukwepa mkono wa Sheria dhidi ya kesi yake ya ufisadi
Juzi ndege vita za Israel ziliruka hadi mpaka wa iraq-iran wakitaraji Iran ishambulie wapate sababu ya vita na hivyo kuahirisha uchaguzi
In ‘unprecedented confrontation,’ IDF chief said resisting Netanyahu's order for military action tied to Iran | The Times of Israel https://www.timesofisrael.com/in-un...g-military-action-tied-to-iran-ordered-by-pm/
Hawa wenzetu wanawezaje miaka yote wapo vitani na bado nchi inaendeshwa kidemocrasia hii ingekuwa africa hapo aingetoka mtu kwenye madaraka sanasana angeingiza watoto wake majeshini ili warithi uongozi.
 
Back
Top Bottom