PreGE2025 Mkuu wa Majeshi, Jeneral Jacob Nkunda awaonya Askari wa JWTZ kujihusisha na siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,517
Reaction score
3,399
Mkuu wa Majeshi Jeneral Jacob Nkunda, amewaonya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutojihusha na masuala ya kisiasa na jeshi halitasita kumfuta kazi askari atakayebainika kujihusisha na katazo hilo.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Nkunda ametoa onyo hilo alipokuwa kwenye Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko, Msata Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo pia amepata nafasi ya kukagua miradi inayotekelezwa kwenye shule hiyo na kisha kuzungumza na askari wa jeshi hilo.
 
Kusikiliza kampeni na sera za wanasiasa na kupiga kura ni kujihusisha na siasa.
 
Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda amewaambia askari wa JWTZ kuwa askari yoyote atakayejihusisha na siasa basi watamchukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kumfuta kazi.

Jenerali Mkunda akaongeza, askari wa JWTZ mnaruhusiwa kupiga kura lakini sio kufanya siasa ambapo ni kinyume na taratibu za kijeshi.

Jenerali Mkunda ameyasema hayo alipokuwa anafunga mafunzo ya askari wapya katika Shule ya Mafunzo ya Kijeshi ya Kihangaiko iliyopo Msata, Wilayani Bagamoyo.
Hawa wanajielewa siyo kama akina Mulilo ambao ni Makada wa a chama cha CCM
 
Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda amewaambia askari wa JWTZ kuwa askari yoyote atakayejihusisha na siasa basi watamchukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kumfuta kazi.

Jenerali Mkunda akaongeza, askari wa JWTZ mnaruhusiwa kupiga kura lakini sio kufanya siasa ambapo ni kinyume na taratibu za kijeshi.

Jenerali Mkunda ameyasema hayo alipokuwa anafunga mafunzo ya askari wapya katika Shule ya Mafunzo ya Kijeshi ya Kihangaiko iliyopo Msata, Wilayani Bagamoyo.
Wazi afande, ongezea kabisa sauti 🫡
 
Muulize vipi kuhusu Jeshi kukaa kimya Katiba ikivunjwa wazi na Viongozi wa CCM na Serikali wakati kiapo chao ni kuilinda hiyo Katiba?
 
Back
Top Bottom