Mkuu wa Majeshi wa Uingerleza ameyataka Majeshi yake kujiandaa kuingia vitani ndani kwenye ardhi ya Urusi

Mkuu wa Majeshi wa Uingerleza ameyataka Majeshi yake kujiandaa kuingia vitani ndani kwenye ardhi ya Urusi

Wakurya wana methali "vita ni vita" vita haichukuliwi kwa wepesi hata siku moja ndio maana putin hajaigeuza majivu Ukraine [emoji1255] mpaka leo. Although mimi ni mcremlin pure ila nakiri kuwa shughuli itakuwa pevu ukizingatia uingeleza ndie baba wa "mayuenking" wote duniani
Wewe sio mkremlin
Maana hata kujua kwamba hatupo vitani na UKRAINE
Unatushangaza MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakurya wana methali "vita ni vita" vita haichukuliwi kwa wepesi hata siku moja ndio maana putin hajaigeuza majivu Ukraine [emoji1255] mpaka leo. Although mimi ni mcremlin pure ila nakiri kuwa shughuli itakuwa pevu ukizingatia uingeleza ndie baba wa "mayuenking" wote duniani
Mkuu , tofautisha Vita ya Ukraine na vita hiyo Kama itatokea , Vita ya Ukraine mrusi anapiga kwa taadhari na anaongoeza nguvu kutokana na na uhitaji na bado anatumia silaha ya mwaka 60, maana yake URUSI hayupo vitani yupo kwenye opereshen maalum Kama ile ya Syria. Sasa ikitokea Vita ya Uingereza kaa ukijua silaha chaguo na moja itakua nyuklia na makombora hypasonic kwahiyo ikipigwa bomu moja tu hata marekan akiingilia tayari sio Uingereza tena.
 
Ajaribu kwanza Iran kabla ya kwenda Urusi
Wanajeshi wa Uingereza walikuwa Afghanistan wakisaidia USA kijeshi - mnajuwa kilicho tokea mwaka juzi? Ngoja niwachekeshe kidogo, ni hivi: Wamerikani walipo ona wamelemewa kwenye mapigano yao ya muda mrefu na Wataliban, Wamerika wakatuma ujumbe wa siri kwa Wataliban kwamba wakutane huko Qatar kwa lengo la kumaliza tofauti zao na kusitisha Vita.

Kikao/mkutano huo ulifanyika kwa siri kubwa bila ya kuwashirikisha Waingereza wala kushirikisha viongozi wa Serikali ya Afghanistan ambayo Merikani na washirika wake ndio waliiweka madarakani!! Katika mkutano huo wa siri huko Qatar, Wamerikani na Wataliban wakakubaliana kumaliza vita baina yao

Sasa kichekesho: Majenerali wa jeshi la Marekani walipo wasili mjini Kabul baada ya kikao/mkutano huko Qatar hawakuwambia chochote maafisa wa majeshi yaliyo kuwa yanasaidiana na jeshi la Merikani kupigana na wanamgambo wa Taliban huko Afghanistan, hata Serikali ya Afghanistan haikuelezwa chochote wala maafisa wa jeshi la Uingereza nao hawakuambiwa chochote kuhusu kikao hicho- Amerika ilikaa kimya kabisa, ikawa inafanya mpango wa siri kuwaondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan - siku ya kuwaondoa wanajeshi wake kwa ndege za kijeshi, Wamerikani wali sepa fasta kwa kupanda ndege ya kijeshi,waka wasahau wanajeshi wa kutoka Uingereza ambao ni marafiki wa karibu sana na Wamerikani (remember special bond baina ya US na UK)

Baadae, Waingereza walilalamika sana kuhusu kitendo hicho cha jeshi la USA kuwasahau wanajeshi wa Uingereza huko Afghanistan na kutowambia chochote kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano na Wataliban!!

By the way, hata Ukraine ili contribute wanajeshi wake kusaidiana na jeshi la USA kupigana vita na Wataliban huko Afghanistan - bottom line is: US hana rafiki wa kudumu - watu wanasema hata Ukraine itakuwa hivyo hivyo, Amerika ita jadiliana kwa siri na Urusi kusitisha vita bila ya kushirikisha serikali ya Zelensky, EU wala NATO - ndio Uncle SAM alivyo - hatabiriki.
 
Kinacho endelea duniani ni kama vita kati Ya Tanzania na mkoa wa Burundi
 
Back
Top Bottom