Mkuu wa Mkoa, jukumu la kuwaondoa Wamachinga ni lako. Usilikwepe

Mkuu wa Mkoa, jukumu la kuwaondoa Wamachinga ni lako. Usilikwepe

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Mkuu wa Mkoa kuagiza Wakuu wa Wilaya wawaondoe wamachinga barabarani ni kuwapa mzigo wasiouweza asilani.

Hawa wamachinga walikwisha pewa jeuri na viongozi wakuu wa taifa na tumeshuhudia waliojaribu kuwaondoa waliondoka wao!

Wewe binafsi uliwahi kuwapa muda wa kuondoka kwenye eneo la ujenzi wa mwendokasi lakini bado wapo hivyo kuwakwaza wajenzi.
 
Katika vitu ambavyo ulipaswa uende navyo taratibu tena kwa Umakini mkubwa mno ni hili Suala la Wamachinga ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nilidhani kuwa Wewe ni Mtoto wa mjini kweli tena wa Kawe na hili ungelishtukia upesi.

Kama kuna Kitu ambacho Rais na CCM hawataki Kukisikia ni Wamachinga Kubughudhiwa hapa nchini.

Hakuna asiyejua kuwa Mtaji Mkuu ( Mama ) wa Kiushawishi na Kisiasa wa CCM na ni hawa Wamachinga.

Kwakuwa ulipoteuliwa ghafla ulionekana hufai kuwa RC wa Dar sasa Watu wamekutega nawe umeingi mazima mazima.

Sikushauri tena kuwa uachane na huu Mpango wako, ila ninachojua umeshatoa Sababu ya Wewe Kutumbuliwa rasmi.

Upo uwezekano Mkoa wa Dar es Salaam akapewa Mwanamke au Kijana mwenye Msimamo na Ushawishi ndani ya CCM.

RC Amos Makalla napenda sana ubakie kuwa RC wa Dar ukizingatia ni mwana Simba SC Mwenzangu ila unaondolewa.

Unawaondoa Wamachinga kama ulivyoahidi ila Wamachinga hawa hawa watamfanya akutoe.

Wabaya wako ndani ya Mkoa, System na CCM wamekutafuta na wakakudanganya kuhusu Wamachinga nawe umeuvagaa.

Ni Suala la muda tu, ila Unatumbuliwa!
 
Ni wazi anakwenda kutumbuliwa. Hawezi kuvuka hicho kisiki.
Kilichonisikitisha zaidi ni kwamba RC Amos Makalla ni Mtoto Mjini hasa sasa nimeshangaa ni kwanini ameshindwa Kushtuka mapema kuwa hatakiwi Dar es Salaam na kwamba kuna Watu Maalum wametumwa Kumdanganya Kimaamuzi ili akosee kama watakavyo na Bi. Hangaya amle Kichwa (amtumbue) mazima.
 
Mmh,acha tuone mwisho wake!
Labda akaroge na akatambike zaidi pale Kwao Kawe Ukwamani nyuma ya Hotel ya Ghorofa ya Victoria alipozaliwa na Kukulia pia, ili Mizimu imuokoe ila hili la Wamachinga ndilo linaenda Kumuondoa kama RC wa Dar es Salaam muda wowote kutoka sasa.
 
Kwa taarifa tu ni kuwa hakuna serikali ya wanyonge Tena

Maazimio ya TISS ni Kila kitu kirudi kama zamani

Hata michango ya shule January inarudi

Mama Samia anajua kila hatua inayofanywa juu ya machinga nyie mtapiga kelele.

Akijitokeza ni kupigilia msumari Kama alivyofanya kwenye tozo.

Huyu Mama ni TV tu walioshikiria remote ni watu wengine.

Huu ni utawala mwingine kabisa mnyonge Hana chake shauri yenu msiseme hatukuwaambia.
 
Labda akaroge na akatambike zaidi pale Kwao Kawe Ukwamani nyuma ya Hotel ya Ghorofa ya Victoria alipozaliwa na Kukulia pia, ili Mizimu imuokoe ila hili la Wamachinga ndilo linaenda Kumuondoa kama RC wa Dar es Salaam muda wowote kutoka sasa.
HAPANA kabisa hivi hao Wamachinga watabaki mpaka lini?
wamefunga mitaa,
wamefunga barabara
wamezinga maduka ya wanaolipa Leseni
wamefunga mpaka njia za wenye nyumba
NAONA MAKALLA ATAONESHA MFANO NA RAIS yupo naye Mwendazake alikosea sana kutaka kura za hisani wala sio Mama Rais Samia Suluhu Hassan
 
Jamaniiii atumbuliwe tena kwa lipi?

Wamachinga hawajazuiwa kufanya biashara ila wametakiwa kufuata utaratibu. Na huu ndio wakati wa watendaji kufanya kazi zao bila kuchafua serikali

Issue ya wamachinga iko wazi kabisa, ni swala la viongozi husika wa maeneo yao kuhakikisha hakuna madhara
 
HAPANA kabisa hivi hao Wamachinga watabaki mpaka lini?
wamefunga mitaa,
wamefunga barabara
wamezinga maduka ya wanaolipa Leseni
wamefunga mpaka njia za wenye nyumba
NAONA MAKALLA ATAONESHA MFANO NA RAIS yupo naye Mwendazake alikosea sana kutaka kura za hisani wala sio Mama Rais Samia Suluhu Hassan

Ni maamuzi mazuri ya RC na ni kufuata na kusimamia sheria za miji zilizowekwa. Kinachotakiwa ni njia zipi zitafuatwa kulitekeleza. Hili leo linaloitwa tatizo limefanywa na serikali ya ccm na ufumbuzi unatakiwa ufanywe na serikali ya ccm.

Mwendazake alikuwa wa CCM msijitoe ufahamu na aliikuta CCM ikificha jezi zake kwenye sandarusi na mkizomewa mitaani na hawa hawa machinga kama vibaka. msijisahaulishe na kuleta lawama za kijinga.

Kuonesha hamjui mnachokifanya wewe unazungumzia wenye fremi hii leo! Wenzako baada ya kuona machinga wanaziba fremu ili waishi na biashara zisife asilimia kubwa wameunda a symbiotic business relationship na machingas. Wako wenye fremu tena wa kutosha wanaonufaika na huu utaratibu wa machinga ulivyo sasa.
 
Pedeshee Amos Makalla,baba Gabriel,mzee wa mvomero kwa sauti ya Nyoshi al sadaat au Pablo masai.

Ila jamaa akumbuke alipotoka kutoka kuwa mfyatua matofali na ulinzi wa petrol station.

Machinga pia binadamu na wana watu wanaowategemea nyuma yao.

Naunga mkono.
 
Jamaa km umemsikiliza msala na mpira amewapa Wakuu wilaya na Wakurugenzi yeye kajitoa kweny hili sakata ili likibuma lisimkute
 
Machinga wanakuwaje mtaji wa mtu ambaye anakuambia ukipeleka kura kwengine basi umeunga kijiko cha sukari baharini/ziwani; vyovyote vile, yeye ndiye mwenye kuunda serikali?

Mwendazake alitaka kuvuruga miji ili kukamilisha azma yake ya kuhakikisha wazee wa mujini wanaishi kama mashetani. Hakuhitaji kura za machinga, labda kusifiwa na kuabudiwa tu.
 
Back
Top Bottom