Katika vitu ambavyo ulipaswa uende navyo taratibu tena kwa Umakini mkubwa mno ni hili Suala la Wamachinga ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nilidhani kuwa Wewe ni Mtoto wa mjini kweli tena wa Kawe na hili ungelishtukia upesi.
Kama kuna Kitu ambacho Rais na CCM hawataki Kukisikia ni Wamachinga Kubughudhiwa hapa nchini.
Hakuna asiyejua kuwa Mtaji Mkuu ( Mama ) wa Kiushawishi na Kisiasa wa CCM na ni hawa Wamachinga.
Kwakuwa ulipoteuliwa ghafla ulionekana hufai kuwa RC wa Dar sasa Watu wamekutega nawe umeingi mazima mazima.
Sikushauri tena kuwa uachane na huu Mpango wako, ila ninachojua umeshatoa Sababu ya Wewe Kutumbuliwa rasmi.
Upo uwezekano Mkoa wa Dar es Salaam akapewa Mwanamke au Kijana mwenye Msimamo na Ushawishi ndani ya CCM.
RC Amos Makalla napenda sana ubakie kuwa RC wa Dar ukizingatia ni mwana Simba SC Mwenzangu ila unaondolewa.
Unawaondoa Wamachinga kama ulivyoahidi ila Wamachinga hawa hawa watamfanya akutoe.
Wabaya wako ndani ya Mkoa, System na CCM wamekutafuta na wakakudanganya kuhusu Wamachinga nawe umeuvagaa.
Ni Suala la muda tu, ila Unatumbuliwa!