Mkuu wa Mkoa Songwe ni Mtanzania? Jina kama Mkongo au Mrundi?

Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe
Francis Kasavubu Michael...ni Mtanzania??niliposikia jina hili wakati yupo katibu wizara ya sayansi. Nilijiuliza hili swali..ni Mtanzania?mbona jina kama Mcongo au mrundi?...


Kuna anaemjua vizuri hapa JF?
Ukabila utakuua wewe, ndio maana hupati afya unakonda tu sababu ya gubu!!!!
 
The Boss watu wakawaida hawataelewa msingi wa swali lako.

Kasavubu ni jina nadra sana Tanzania lakini lenye deep profile miaka ya 1960 huko DRC.

Mimi nakuelewa sana.
Kasavubu aliwahi kujitangazia Uhuru miaka ya 1960s jimbo LA Katanga lijitenge na Congo. Mwulizaji naona anasumbuliwa na historia. Anapaswa kufahamu kuwa majina mengi ya kibantu hufanana
 
Kasavubu aliwahi kujitangazia Uhuru miaka ya 1960s jimbo LA Katanga lijitenge na Congo. Mwulizaji naona anasumbuliwa na historia. Anapaswa kufahamu kuwa majina mengi ya kibantu hufanana
Kuuliza sio ujinga
 
Kw
ewe mwenyewe ikute ni mmalawi. Kwani Bashe ni Mtanzania ?Maana ana jina la kisomali .
Kwani msomali hawezi kuwa mtanzania!!
 
Kwa Ulimwengu wa sasa jina halimtambulishi mtu origin yake ,leo nilikuwa nasikiliza njia panda clouds fm walikuwa wanamuhoji mtu aliyejulikana kwa jina lake alilopewa na wazazi wake kama Osama na pia nilishawahi kukutana na mtoto anaitwa mandela(amezaliwa tanzania 1996) ,hapa nasemaje Osama sio muafhganistan au mandela siyo msouth bali ni waTZ.

Hata huyo jamaa haitwi Kasavubu bali ni Kasabubu.

 
Mkuu kwani huyo Osama unayemsema ni jina lake la ukoo, au huyo Mandela ni jina lake la ukoo?
Nimesoma na jamaa anaitwa Saddam Hussein ila jina lake la ukoo ni la kibongo, hapa hatusemi majina ya kuokoteza uko Ulaya na Uarabuni au wapi. Tunasema jina la ukoo ambalo ndio uhalisia wa mtu.

Hivihivi tulijikuta tuna Kanali wa JW ni Mnyarwanda na anatuma taarifa kwa Kagame, alitoroka na sasa ana cheo kikubwa uko kwao. Hivi hivi Syria ilijikuta na Eliyahu Cohen Myahudi pure aliyejifanya anaitwa Kamel Amin alafu akawa mshauri wa usalama na mmojawapo wa vigogo serikalini. Mtu anauliza kujua background ya kiongozi serikalini anatokea muuza gongo analalamika. Hii nchi imejaa vilaza watupu.

Congo hawakuuliza uraia wa maofisa wao serikalini wakajikuta wamejaza Wanyarwanda kila idara. Last month mshauri wa Rais kapigwa msako kakutwa na passport ya siri kutoka Rwanda na ana documents za nyumba anazomiliki uko, yuko under arrest.
 
Tangu alambishwe asali enzi za JPM, alibadilka sana huyu Mheshimiwa. Kiufupi hana tofauti na akina Slow slow.
 
Kweli...ila ni wa huko jikoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…