Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Chalamila astuka , Atengua zuio la kufunga Bar kuzuia Corona

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Chalamila astuka , Atengua zuio la kufunga Bar kuzuia Corona

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ametengua agizo la kufunga baa saa 3:00 usiku alilolitoa Aprili 17, 2020. Amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wamiliki wa baa kuweka mikakati ya kudhibiti virusi vya corona (kuweka vitakasa mikono, kuzingatia umbali) kwenye maeneo yao.

Na nyie Watawala Siku zingine muwe mnatuliza Kwanza Akili zenu hasa pale mnapowateua Wasaidizi wenu hawa Tanzania hii.
Mkuu lakini wanywaji wengi huzingatia masharti na taratibu ktk awamu za ulabu. Zikiingia vyema kichwani huwa juu ya sheria, hivyo hujikuta wanavunja masharti na taratibu zote, kinachobaki ni kuongea lugha ya Kiingereza kwa saana tu, kutoa ahadi za ajira kwa warembo, kucheza mziki na kukumbatia hovyo warembo.

Lkn yote ya yote ni kuishia kwenye kale kamchezo ka baba na mama, tena pengine kavu kavu bila kinga ya VVU na hii sasa Corona. Ambapo naamini kutumia zana zote mbili za vita kwa pamoja inahitaji mbinu za medani na uvumilivu wa hali ya juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sms ya saa saba usiku ilisomeka namna hii;

Mkuu : Hivi wewe unavyopunguzia watu muda wa kunywa bia hizo kodi utaziripa wewe?
Chalamila : Samahani Mkuu nimekuelewa.
Mkuu: Na usinipigie simu tena.
Chalamila: Asante mkuu nimekuelewa nisamehe sana.
 
Huyu jamaa anachezea nguvu ya shetani!!!,

Shetani anataka watu walewe watende zambi afurahi.

Shetani anataka watu wapate corona wafe.

Taifa linasema tuombe Mungu alafu linaacha watu walewe kwenye mabaa.

Kwa maoni yangu ili maombi yetu yamfikie Mungu serikali ingezuia kabisa pombe nchini maana unaweza kuta laana ya ulevi ndio imeleta corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1422530

Hapo Jana Mh Chalamila aliweka utaratibu wa wanywaji wa Mbeya , kwa kutoa muda wa hadi saa 3 usiku wawe wamepukutika kwenye mabar , kwa hoja kwamba baada ya muda huo wengi wanakuwa wamelewa kiasi cha kukiuka kinachoitwa Social Distancing ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona .

Lakini katika hali ya kushangaza leo hii amefuta amri hiyo , na kwamba wanywaji waendelee kupiga kilaji mpaka watakapotosheka , ili mradi wachukue tahadhari .

#Tuendelee kunawa mikono kwa maji Tiririka ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona
Huyo mropokaji mpya huwa anajaribu kuvaa viatu vya mropokaji mkuu wa mzizima
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ametengua agizo la kufunga baa saa 3:00 usiku alilolitoa Aprili 17, 2020. Amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya wamiliki wa baa kuweka mikakati ya kudhibiti virusi vya corona (kuweka vitakasa mikono, kuzingatia umbali) kwenye maeneo yao.

Na nyie Watawala Siku zingine muwe mnatuliza Kwanza Akili zenu hasa pale mnapowateua Wasaidizi wenu hawa Tanzania hii.
Hata mteuaji mwenyewe ni shida tupu, kifupi mteuaji na mteuliwa wote akili zao ziko sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sms ya saa saba usiku ilisomeka namna hii;

Mkuu : Hivi wewe unavyopunguzia watu muda wa kunywa bia hizo kodi utaziripa wewe?
Chalamila : Samahani Mkuu nimekuelewa.
Mkuu: Na usinipigie simu tena.
Chalamila: Asante mkuu nimekuelewa nisamehe sana.

Kwa jinsi ninavyomjua huyo Mkuu kwa jinsi Matusi yalivyo Mlangoni mwa Mdomo wake na Viganjani ni lazima alimtukana tu.
 
Si kiherere ni tabia yake kukurupuka. Kama alivyowashambulia kimwili wale watoto wa shule
 
Back
Top Bottom