Wanajamvi salama?
Wakati joto la uchaguzi likizidi kupanda hatimaye mkuu wa mkoa wa Morogoro bwana Loata Sanare amediriki kuwa nje ya kituo chake cha kazi mwezi mmoja sasa.
Nilizozipata asubuhi ya leo kutoka vyanzo vyangu zinàsema tokea ateuliwe amekuwa akisononeka sana moyoni na kuanza kumlaumu mh Rais kwa kumteua kuwa RC Morogoro kwani uteuzi huo ni sawa na kumkosesha ubunge wa Monduli.
Habari zadi zinasema tokea atoroke kwenye kituo chake cha kazi amekuwa akifanya vikao usiku kwa usiku lengo ni kumhujumu mbunge mh Julius Kalanga huku akijiapiza kuwa hatakama yeye Rc hatogombea atahakikisha mbunge wa sasa hatorudi bungeni.
Habari kutoka Morogoro zinaeleza tokea ameaga anaenda msibani Monduli hadi leo hajarudi kwenye kituo chake kazi huku mgogoro wa wakulima na wafugaji ukizidi kufuka moshi kwenye mkoa wake.
Habari zaidi zinasema wiki nzima amekuwa akitumia gari ya serikali kupita vijijini kuonana na wajumbe kuwashawishi kuwa wasije msahau kwani naye anaingia kwenye kinyanganyiro cha ubunge wa monduli huku uongozi wa chama wilaya ukimfumbia macho.ameendelea kujitapa zaidi kuwa hata rais na katibu mkuu wa chama wamempa baraka zote.
Ninaomba chama wilaya watoe tamko kuhusu huyu Sanare kwani amekuwa anafanya kampeni za wazi wazi kabla ya ratiba za bunge kuvunjwa.
Rc amekuwa akivuruga chama kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa na mtakumbuka baada ya yeye kuteuliwa kura RC bado alirudi kuhakikisha anampinga mwenyekiti wa sasa wa mkoa wa arusha mh zelothe lakin bado hakufanikiwa.
Naomba chama Wilaya waliangalie hili kwa macho matatu kwani RC huyu anaivuruga wilaya ya Monduli badala ya kurudi kwenye kituo chake cha kazi kutatua migogoro inayofukuta moshi ndani ya mkoa wake