Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

This case is closed.!!!

Kwa vile Ditopile ni mtu wa serikali na ndiyo hiyo hiyo inayomshitaki, ni wazi kuwa marehemu Mbonde hana mteteaji katika hili; amekufa kibudu na Mheshimiwa Ditopile atarudi mitaani kimyakimya tu.

DPP amehalalisha matumizi ya silaha hadharani. Yaani leo hii ukiwa na kisu (wananchi hawatembei na bastola) halafu mtu akakutukana huyo ni halali yako kuchinja. Ditopile alikuwa mwepesi sana wa matusi, kwa hiyo na yeye kumbe alikuwa halali ya aliokuwa akiwatukana. Sidhani kama DPP alitumia utaalamu wake sawasawa wa sheria au labda alishinikizwa kutafuta maarifa ya kumpunguzia mheshimiwa kosa. Ninadhani kuwa alishinikizwa na ndiyo maana akakimbilia kujitetea.



Ninapenda sheria ya Florida: Inaitwa 10 - 20 -LIFE.

Ukimlenga mtu kwa bunduki: miaka kumi jela.
Ukifyatua risasi hata kama haikumpaa mtu : miaka 20 jela
Ukimjeruhi mtu kwa risasi: Unafungwa maisha.
Ukiua Unanyongwa kwa sindano ya sumu.
 
In Tanzania, the CCM politicians are above the law; they can do everything illegal but the law will be bent in their favour!
 
Mwendapole,
you may be right, however umeeleweka. sasa je, hakuna kipengele cha kumbana/kumuadabisha mtu anyeenda kinyume na process ya kimahakama? tena akiwa mfanyakazi wa serikali!!
 
Ni sawa DPP kuanza "kutoa ushahidi" kabla ya kesi kuanza?

Mbona inakuwa kama anamtetea mtuhumiwa?

Si angeacha maswali na majibu huko huko mahakamani?


Mwanagenzi

Pokea 5. Huyu DPP ametokea dunia gani...mbona anamtetea Mtuhumiwa kwenye vyombo vya habari bila hata kesi yenyewe kuanza kusikilizwa...??? Hivi kweli hajavunja sheria kwa kusema hayo aliyoasema, ningekuwa mimi ndiye Mlalamikaji kwa kweli hii kesi ningeachana nayo tu kwa moyo upande na huzuni maana hapa hakuna watakachoambulia..hakuna JUSTICE hapa.

Tanzania Yetu hii kweli safari ni ndefu.
 
niwape mfano, wewe ni mvuta sigara na unatembea na kibiriti, umetoka kununua mafuta ya taa (kwa matumizi ya nyumbani) ukiwa njiani jirani yako mmoja ambaye alikuwa na kisasi na wewe akaanza kukupaka.. Mwisho anaishia kukutukana matusi ya kila aina (ya mama yako na ya nguoni) unakasikirika kweli, unataka kumpiga, jirani anakimbilia ndani ya nyumba yake na kufunga mlango. Kwa vile umekasirika hutaki kuendelea na safari yako... unaamua kumwagia nyumba ya jirani huyo mafuta ya taa, unachomoa kiberiti, unachukua njiti na kuamua kuiwasha nyumba ya jirani moto...!! Unahakikisha kuwa hatoki mtu humo.. na baadaye wanakuta mwili wa jirani ukiwa umeungua vibaya! Marehemu ameacha mtoto mmoja. Unakamatwa hapo hapo... kwa maelezo ya DPP... huwezi kushtakiwa kwa kuua kwa kukusudia kwani tendo ovu (actus reus) halitakunguliwa na nia ovu (mens rea). Uliua kwa bahati mbaya kwani hukutembea na kiberiti na mafuta ya taa kwa lengo la kuua mtu...! Sasa kama hukuwa na nia ovu (ya kuua) ilikuwaje umwagie mafuta ya taa nyumba, kuchomoa kiberiti na kuwasha njiti? Ulitarajia kuwa nyumba ikianza kuwaka, yatatokea maua?!!!

DPP amekosea siyo tu kisheria bali pia kiukweli (the learned DPP has erred in law and in fact)!
 
Mwanakijiji,
'DPP amefanya makusudi. Kwanza bastola ilipotea. Sasa anasema kulikuwa na majibizano ya matusi. Alete mashahidi waliokuwemo kwenye daladala tuwasikie walichoona na kusikia. Huyu anaandaa jamvi la kutamka nolo prosecui.
 
Jasusi, siyo hivyo tu bali pia wametengeneza mazingira ya kesi kuwa dismissed for prosecution misconduct.. I can see Mkono na timu yake wakichekelea...
 
Yaani DPP kaamua kumsema uongo marehemu ? Kweli kutukanwa Ditto can justify his shooting ? Ama kweli madaraka . Wenye matumaini na JK mko wapi ?Maana mlisema kaja kiongozi wa wanyonge . Wanyonge wapi ?
 
halafu kinachoudhi ni kuwa ni yale yale wanamlaumu Marehemu...! Hivi kweli kama ingekuwa ni marehemu ndiye ametukanwa na kuchomoa bastola kumlipua mkuu wa mkoa .. hivi kweli mnafikiri serikali ingekuwa na mashaka juu ya "kusudio" la mtuhumiwa? Ama kweli ukitaka kumuua nyani, usimtazame usoni...!! Mwendesha Mashtaka aachie ngazi kwa kujaribu kupinda sheria, na kushona mashtaka ili yamtoshe mtuhumiwa!! This is a classic example of grand travesty of justice!
 
Mimi naamini kabisa kuwa Ditto atafungwa,albeit miaka labda miwili hivi.Lakini concern yangu kubwa ni kwamba,huyu DPP katoa kibali kwa watu kuua madereva wa daladala sasa!In other words,yule dereva wa daladala naye angemuua Ditto,wangesema hakukusudia? Yaani kesi ya Ditto inafananishwa na dereva aliyeuwa kwa ajali.They are terming as an accident,thats a bloody joke!

Hii ni high profile case ndio maana wote tunaisoma kwenye magazeti kila siku,lakini kwa mtu wa kawaida mwenye bastola yake,hatutasoma kama hivi,na kwa mwendo huo basi madereva wengi watauawa au wataua,according to what the DPP has said,kwani nani hajawahi kutukanana na dereva wa daladala? Kumbe naweza kumuua na ikawa sijakusudia?? Nikihonga pesa kiasi flani hata mahakani haifiki,kwa sababu DPP alisha set precedent!!Maana polisi wetu tanajua wanavyohongeka kiurahisi.I think this is just too wrong.

Lakini sishangai sana,huko nyuma kuna mama mmoja alikuwa mke wa Liundi(4ma msajili wa vyama) aliua watoto wake wawili na mmoja akasevu kwa sababu ya wivu.Yule mama nafikiri alihukumiwa maisha,cha ajabu Mwinyi akamsamehe,na sasa yuko nje anaendelea na maisha yake.Lakini vipi those innocent souls who lost their lives at a tender age? Is that justice kweli? Kuna faida gani ya kuwepo na hukumu kama hizo,kama anaweza kuja kiongozi na kuzitengua kwa sababu za kijinga tu.Haya basi,kama yalishafanyika yatafanyika tena,kuna uwezekano mkubwa sana Ditto akasamehewa kwa sababu za kiajabu tu,lakini mahakama inakuwa haina lawama maana 'ilitenda haki'.
 
Mzee MJJ,
Heshima yako mkuu,
Mimi nimejaribu kuonyesha sheria vile niijuavyo, na ndiyo position ilivyo.
Kwa suala la kukusudia, nimejaribu kuaininsha vipengele vinavyoangaliwa na sheria; ila yooote yanategemea sana USHAHIDI unasemaje.
Kuhusu mens rea; wewe mwenyewe umesema ..ukiwa njiani jirani yako mmoja ambaye alikuwa na kisasi na wewe .. sasa swali la kisheria hapa litakuwa..je, marehemu alikuwa na kisasi/ Ditto alikuwa na kisasi na marehemu?

Simtetei Ditto kabisa; in fact I hate his guts for more reasons than one, but am trying to look at it from a legal point of view..
 
Mwendapole, heshima na kwako,

Mimi pia naangalia kupitia mwanga huo huo wa sheria, na hoja yangu ya kuua kwa kukusudia sioni ni lazima kuwa na muda wa kupanga. Mojawapo la tatizo la sheria ya Tanzania ni kukosekana kwa madaraja ya mauaji ya kukusudia. Kama una pande mbili tu (kuua kwa kukusudia na kuua kwa kutokukusudia) basi unajikuta una wakati mgumu kuamua kirahisi kesi kama ya Dito. Je aliua kwa kukusudia kwa kushika bastola, kuweka kidole kwenye kifyatushi, kuelekeza kwa mtu mwingine aliyekuwa amejificha ndani ya gari, na kufyatua huku akilenga kichwa? Jibu ni ndiyo, kwani baada ya Mbonde kufunga mlango na dirisha la gari, Bw. Dito alikuwa na uhuru wa KUAMUA kuondoka na kupuuzia jambo hilo, alikuwa na uamuzi wa kukaa pembeni hadi polisi wafike, au kuendelea kumtaka kijana atoke kwenye gari wazungumze. Yeye ALIAMUA kuchomoa bunduki na kuiweka katika hali ya kufyatua. Upande mwingine kama NIA YA KOSA inajengeka baada ya muda na siyo papo kwa papo (kama unavyoashiria) basi ni kweli Dito hakuua kwa kukusudia kwani ulikuwa ni uamuzi wa papo kwa papo. Sasa katika kuamua jambo hili kitu kimoja tukisubiri mahakamani, je Dito alikuwa na silaha kiunoni alipotoka mara ya kwanza kwenda kuzungumza na dereva? Au alizungumza na dereva na dereva alipoamua kuingia ndani ya gari, Dito alirudi kwenye gari lake na kuchukua silaha na kisha kurudi (kitu kitakachoashiria kusudio la kudhuru).

Kwa vile mimi naweza kuitabiri serikali hii naweza kukuambia kabisa nini kitatokea. Mashahidi wote 23 wa upande wa mashtaka watakubaliana juu ya jambo moja.

a. Dito alikuwa na silaha kibindoni alipotoka ndani ya gari kwa mara ya kwanza na hakurudi kuichukua kwenye gari!

Hata hivyo, kuna watu wawili ambao watakuwa ni kiini cha kujua kusudio la mtuhumiwa nao ni dereva wa Dito na yule abiria mwingine ambaye hadi leo hajatajwa.

Swali jingine kutokana na hayo hapo juu ni kuwa je NIA YA KOSA inaweza kujengeka papo hapo bila kudhamiria? Nafikiri kutokana na kesi hii hatuna budi kuongeza madaraja ya makosa ya mauaji kama Murder in the 1st Degree, 2nd Degree, na 3rd Degree kuliko ilivyosasa.
 
Watu wote wanaopewa bunduki wanasheria kabambe na kali jinsi ya kutumia silaha hizo. Hakuna haja ya mizunguko ya sheria hapa DITO ni muuaji wa kudhamiria i.e. kwa nini alishuka kwenye gari lake na kumfuata mtuhumiwa huku akiwa ameikoki bastola yake? Tena huyu mtuhumiwa hakuweza hata kufungua dirisha lake, ilikuwa ni dhamira ya DITO kuua, hakuchukua hii bastola kwa ajili ya self defence, waache wazungushe wanavyopenda lakini the bottom line huyu ni muuaji, tena kwa sheria za Tanzania inabidi anyongwe kama Mwamwindi.
 
Dua,
Kwa kufuata kauli ya DDP huyu kishaepuka kitanzi. Sana sana ataswekwa lupango na baadaye kuachiwa kimya kimya.
 
Ni kweli Jasusi, kwa sababu haingii akilini mwa DPP kuwa mtu kama Dito anaweza kuwa muuaji!! Ila kama ingekuwa ni mmachinga amemuua Mbunge, au Mkuu wa mkoa katika mazingira yale yale.... mbona kitanzi kinaweza kuwekwa mahakamani!!!!
 
Tamthilia ndio imeanza hapa tutaona mengi sana.
Lilio wazi ni kuwa sasa Dito yuko huru baada ya miezi kama mitatu ijayo. Tutaambiwa aliuua bila kukusudia, anapewa hukumu huku ya miaka miwili jela, na kwa sababu ameshakaa jela muda mrefu (hausemwi) na kwa sababu hana rekodi mbaya basi atatumikia miezi sita kwisha.
Uzuri wa sheria unaweza kumanipulate unavyotaka na ikaonekana iko upande wako. Hili la Dito ni mauaji ya kukusudia pure and simple no matter what wanasheria na wengineo watasema nini.
Kama Mwamwindi alinyongwa kwa kumuua Kleruu katika mazingira yanayofanana na haya, huyo DPP anatuambiaje sasa hivi ati ukitukanwa rukhsa kumng'ofoa mtu roho?
 
Back
Top Bottom