Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Bado ninasimamia point yangu kuwa Mkono, anatumwa na "mkono mzito" kusimamia hii kesi, pamoja na sababu ya kimsingi ya dada wa Blaza Dito kuwa ofisini kwake,

Muulize Dr. Kitine, nani anaye-run the show bongo kati ya sheria na wanasiasa, ni wanasiasa wa CCM ndio wanao-run the show bongo, kitendo cha Mkono kuingia kichwa kichwa hii kesi ni lazima kina baraka toka kwa some politician au a politician, kwa sababu ni kitendo cha kuweka career yake politically, kisheria, na biashara zake kwenye line!

Na yeye binafsi anaijua bongo kuliko, kwa hiyo haiwezekani kabisaaa kuwa ameingia tuu for the sake ya utetezi kwa sababu ni mwanasheria, No Way! na tunajua better, isipokuwa tu chenye mwanzo huwa lazima kiwe na mwisho, na kwa bahati mbaya mwisho wa viongozi corrupt huja bila barua,

Unless, prosecutors wasifanye kazi yao kwenye hii kesi, maana ukweli ni kwamba kuna pattern ya Blaza Dito na Bastola, tena siku moja kabla hajaitumia alikuwa tayari amemtishia nayo mkewe, na huko nyuma tayari alishawahi kupiga risasi matairi ya gari la mwananchi mmoja, halafu tena alishawahi kuzipiga hewani kuwatisha wananchi, kwa hiyo nilitegemea Mzee kama Mkono atakuwa makini kutojiingiza na kitu kama hiii ambayo wazi kuwa imekuwa ni tabia ya Blaza Dito kucheza cheza na Bastola,

Lakini tunajua kuwa Mzee Mkono sio mjinga, ni lazima ana baraka za mzito mmoja au wengi, lakini aangallie usije ukawa mtego wa panya ambao huingiza waliokuwemo na wasiokuwemo, ARROGANCE ndiyo imemfikisha Blaza Dito hapo alipo, I hope siyo the same ARROGANCE inayomfanya Mzee Mkono aingie kichwa kichwa,

maana kama Human Right Watch Dogs & NGO's walivyomwambia Rais JK, kuwa kwenye hili wote wako macho kuona haki inatendeka!

Ni haki ya Mkono kumtetea Blaza Dito, lakini pia ni haki ya wananchi kuuliza Mwanasheria mbunge, anapokwenda kumtetea Mkuu wa Mkoa, aliyeuwa kwa makusudi!, tena dereva wa basi la walalahoi!



by the way hakuna sheria inayomkataza kutomwakilisha dito regardless of how people think ....na kama kuna mtu ana UPUPU wa MR MKONO then aanzishe separate thread ambako najua wataalam watakuja na mitazamo tofauti

Sula lingine usisahau kuwa ma Prosecutors kule kwetu ndio wenyewe kwa kuboronga sasa nchi ina wasomi wasiosoma small print then what else do you need?

Wangapi waluliwa kule Bulyankulu na mpaka leo nani aliwajibishwa? Mv Bukoba nani aliwajibishwa?
 
Hiyo mzee wangu ilikuwa ni awamu ya tatu, sasa tuko ya nne ya kasi mpya ndio maana wananchi wana hamu ya kuona je awamu hii itakuwaje?

Ni kweli ma-prosecutor wetu wana tabia ya kuharibu either kwa kutokujua ambayo ni only 10%, wakati 90% huwa ni kwa ajili ya rushwa,

So far kwenye hii kesi wako sawa isipokuwa bado sijaelewa kuhusu kupotea kwa bastola, aliyoitumia Blaza Dito, lakini otherwise tuko nyuma yao, na ninarudia ni haki ya Blaza Dito kutetewa na wakili yoyote duniani hata kama ni Blair au Clinton, lakini pia ni haki ya wananchi yaani sisi kuuuliza kulikoni Mzee Mkono Mbunge wa serikali kjiingiza kwenye kesi aliyoisema wazi mkuu wa polisi Dar, Mzee Tibaigana, kuwa ni home run kwa serikali?
 
awami hii ya tatu si ndio imekuja na maskendo ya RICHI-MONDI?

sasa unashangaa nini

na hii bado...kuna hicho kiwanja kipya cha ndege au hijasikia hiyo?
 
Yamempata makubwa na mzito. kuna mazingatio makubwa mno kwenye kadhia nzima hii ya mpaka yeye kuwa Keko rumande badala ya kwenye hekalu lake kama mkuu wa mkoa akilindwa na kuhudumiwa kwa matashi yake. Zingatio kubwa ni kuwa Mungu yupo, yeye ndio mwenye uwezo wa kutoa na kuondosha ufalme wa mtu. Binadamu hawana jeuri ya uwezo,maisha na hata uhuru wao.
Fundisho kwa wenye hadhi na nafasi kama aliyokuwa nayo mzee wetu Ditto, tumuogope Mungu.
Ushauri wa nasaha kwake na kwa watu wake wa karibu mno
-Aombe msamaha kwa wafiwa kwa kosa alilolifanya. Tena bila ya woga wala kuhofia kama atazidi kujiingiza kitanzini kwenye kesi yake.
- Kama alivyosema mheshimiwa Raisi, amuombe Mungu msamaha.
- Aondoe jopo lote la mawakili, wanaosimama eti kumtetea. Amefanya kosa kubwa mno, na hata hao mawakili kwa kutumia utaalamu wao ikitokea kama ataonekana hana hatia au kupewa hukumu ya 'afadhali', unadhani wanaweza kusimama pia mbele ya Hakimu wa mahakimu wote (Mungu mwenye Enzi)?, muumbaji wa huyo aliyemuuwa al marhuum Hassan.
Ahsante,
kingwele.
 
Mkono anastahili kuchunguzwa ili afukuzwe Bungeni

Sheria ambazo inawezekana amezivunja makusudi ni:

1. Watu wenye madaraka serikalini kukoma utumishi wanapochaguliwa. Sheria ya 1992 Na. 4 ib. 23 sheria ya 1995 Na. 12 ib. 14 (ambayo ni lazima iwahusu chief executives wa private firms).

2. Masharti ya sheria ya maadili ya uongozi wa umma

3. Masharti ya kazi ya wabunge sheria ya mwaka 1984 Na. 15 ib 13


Kamati ya uongozi & kamati ya katiba, sheria na utawala ndizo lazima zishughulikie suala hili kama ilivyoelezwa katika
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania as specified kipengele 4 majukumu ya msingi na ya jumla ya kamati.

Kifungu 4.1 Bunge na kamati zake ndiyo darubini (oversight or watch-dog organ) ya kuhakikisha kwamba mambo yote ya uendeshaji wa kazi za dola unafanywa kwa kuzingatia katiba, sheria na kanunu zilizowekwa.

Wajumbe wa kamati hii ni :

1. Mwenyekiti –Spika
2. Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni
3. Kiongozi wa upinzani bungeni
4. Wenyeviti wa kamati za kudumu
5. Mwanasheria mkuu wa serikali

Hata kama itabainika kwamba hajavunja sheria kamati ya kanuni za bunge inaweza kufikiria na kutoa mapendekezo juu ya kufanya mabadiliko katika kanuni za Bunge – uchunguzaji huu utatokea iwapo taarifa ya kutoa pendekezo lolote na hususan hili hasa kutoka kwa wabunge wa opposition. (Mkono anafanya tenda nyingi kutoka serikalini na wakati huohuo yeye ni Mbunge)

Haya sasa wabunge wa upinzani hii ni changamoto kwenu. Tusikubali Mbunge kumtetea criminal.

________________________
Dua la kuku halimpati mwewe
 
Jamani nimeingia tena, nilikuwa na matatizo katika kulog in nikabakia kusoma tu bila uwezo wa kuchangia, lakini sasa imekubali tena.Mliyonikaribisha asanteni sana, am very happy to be here.

Kwa maoni yangu Mheshimiwa Mkono kama mtu wa serikali hapaswi kabisa kumuwakilisha Ditto kwa sababu Ditto anashitakiwa na serikali hapo lazima kuwe na conflicts katika interests, ni kama vile mtu awe wakili wa kampuni ya simu tanzania halafu kama mteja wa kampuni hiyo akiishitaki kampuni yule wakili hawezi kusimama katika upande wa mteja aliyeishitaki kampuni.Hata licence anaweza kunyang'anywa.

Anyway Ditto bwana halaiki ya watu imemuona akiua, kama bastola imepotea hiyo sio hoja kabisa kwasababu ushahidi sio kama mnyororo ambapo kipengele kimoja kikipotea basi ule mnyororo unakatika katikati, ushahidi ni kama kamba ya katani zile nyuzi zinakamatana kutengeneza kamba kwa hiyo kama nyuzi moja ikiachia kamba ile ya katani bado inaendelea kujishika na kubakia kamba!
Ditto amekwisha, iliyobaki ni kumpeleka kwa saikolojist aseme ilie ilikuwa "Temporary insanity" yaani kwa ule muda mfupi jamaa akili zilimruka kwa hiyo hakujua alichokua akikifanya, matokeo yake adhabu inaweza kupunguzwa badala ya life imprisonment akapewa labda miaka 25 au 30 hivi.
 
Tuendelee kupiga kelele ndugu zangu hadi vyombo vya nyumbani vilivalie njuga. Hivi Waziri ambaye ni mwanasheria anaweza kwenda mahakamani na kumtetea mshitakiwa kwa kisingizio tu kuwa yeye ni wakili? Sifikiri kuna sheria inayomkataza Waziri kufanya hivyo. Na ieleweke kuwa tatizo letu siyo Mkono kumtetea Dito, bali Mhe. Mkono Mbunge wa Bunge la JMT ambalo ndio chombo kikuu cha kutunga sheria kufanya kazi ya uwakili. Aidha aachie uwakili au ajiuzulu Ubunge!!
 
What is up? hakuna kulala, sasa so far nimesikia kuwa Blaza Dito ana spend muda mwingi hospitalini, lakini almost kila siku, ila good news ni kuwa kila jioni hurudishwa lupango!
 
kuna taarifa za kuaminikakuwa huko hospitali anakoenda kuna watu wamemshauri so ana mpango wa kufanyiwe mpango ili apimwe ubongo[insanity test],kama atafanikiwa kukubaliwa na jaji awasilishe hicho kipimo itakuwa silaha moja kubwa kwake na iliyosalia ya kumuweka huru....hali ya akili ya mtuhumiwa huwa inazingatiwa sana na wanasheria kutoa mwelekeo wa kesi kama hizi....
 
Mtu asiyekuwa na akili timamu, hawezi kuandika barua ya kujiuzulu kwa rais baada ya kuua, na hawezi kutafuta wakili kama Mkono!, labda jaji akiwa Mahita!
 
HII BIASHARA GANI?

Kwa nini Dito anaruhusiwa kwenda hospitali kila siku? (Kama ni kweli?)

Kwa sababu Dito ni muuaji anapokwenda mahakamani huwa wamemfunga minyororo miguuni na mikononi maana yake wameanza kusema akili zake sio sawa, Je kwa wale waliopo DSM mnaweza kutueleza.

Huyu ni mtu hatari kwa hiyo lazima minyororo itumike.
 
Dua ushasahau kuwa impossibles are possible in bongoland?
 
Ukitaka kuweka posibilities za kujenga hoja ya "Not Fit to Stand Trial" au "Msamaha wa Rais kwa sababu za Kiafya" ni lazima uanzie mbali.

Hapa naona bro Dito anajiwekea options tofauti wazi, mapema kabisa ili later msije mkapigwa na butwaa akiwa off the hook kwa sababu za "Kiafya".

Pia mle ndani namo hakukaliki ati...
 
Na huu uwendawazimu (insanity) umemfika lini? Tangu aingizwe lupango au hata alipokuwa Ikulu ndogo pale Tabora?
 
Mzee Jeee!

I love it, yaani hii forum idumu maana saa moja hapa ni afadhali kuliko masaa 10 ya vikao vya kamati kuu za vyama vyote upinzani na CCM!

Huyu jamaa insanity ipi? Basi akachanganywe Mirembe angalau kwa one year tuone matokeo kama anaweza kukaa mle hata siku moja, licha ya lisaaa limoja?
 
Kama akiachiwa kwa madai ya insanity kweli basi hiyo itakuwa ni doa kubwa sana kwa Rais na serikali yake kwa jumla. Yaani Rais anaweza kumteua mtu insane kuwa Mkuu wa Mkoa! Au kwa maana nyingine ni kuwa kuna wateule wa Rais ikiwa ni pamoja na Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, na Mabalozi ambao ni insane!
 
Kichuguuu,
Ama kweli penye kichuguu hapakosi mchwa!...
Hiyo point bob na itamtafuna vizuri JK.... Haya vyama vya upinzani mmepewa tip! tena itakuwa proven by the court!... Patamu hapo?
 
Ditopile aanza kulalamika

na Irene Mark

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile-Mzuzuri, amelalamikia ucheleweshaji wa upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili.

Ameiomba mahakama iubane upande wa mashitaka ili upelelezi ukamilike, kesi ifikishwe Mahakama Kuu, aweze kuomba dhamana.

Ditopile, alisema hayo kupitia kwa wakili wake, Nimrod Mkono, anayemtetea mbele ya Hakimu Mkazi, Michael Luguru, baada ya Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Charles Kenyella, kudai kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

"Leo ni siku ya 32 tangu kupandishwa kizimbani kwa mteja wangu, naomba upande wa mashitaka uharakishe upelelezi…tunaomba uzembe huu ufanyiwe kazi ili twende Mahakama Kuu kwa ajili ya kuomba dhamana, huu si mwendo wa kasi, ari na nguvu mpya," alisema Mkono.

Akijibu maombi ya wakili huyo, Kenyella, alidai kwamba, mauaji ni kosa kubwa na mtuhumiwa huyo ni sawa na wengine, hivyo upelelezi wake unahitaji muda kwa kuchunguza mlipuko, silaha, na mazingira ya tukio.

"Msomi mwenzangu asiwe na haraka, wapo watuhumiwa wamekaa mahabusu kwa kesi za aina hii kwa miezi sita, tutafuata taratibu za upelelezi kama inavyotakiwa…hakuna aliye juu ya sheria," alisema Kenyella.

Baada ya maelezo ya pande hizo mbili, Hakimu Luguru, aliutaka upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba 18 itakapotajwa.

Ditopile-Mzuzuri aliingia mahakamani hapo akiwa amevalia shati la kijani, suruali nyeusi na baraghashia nyeupe, akiwa amezungukwa na maofisa wa polisi.

Mwanasiasa huyo anadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, dereva wa daladala, Hassan Mbonde, katika tukio lililotokea makutano ya Barabara ya Bagamoyo na Kawe, Dar es Salaam. Tukio hilo linadaiwa kutokea jioni ya Novemba 4, mwaka huu.
 
Back
Top Bottom