Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Haya ndiyo matatizo ya kuajiri watu wenye elimu ya mtandaoni (fani imevamiwa).

Cha kushangaza mpaka sasa hivi sijaona Jaji Mkuu (Chief Justice) na hata Mwanasheria Mkuu (Attorney General) akimkosoa DPP kwa kosa alilofanya. Na waziri wa Sheria na Katiba naye kimya.

Mkjj: Naomba umtafute Rev. Mtikila atusaidie kufungua kesi mahakamani, mimi binafsi nitatoa Milioni Mbili kuona haki inatendeka. Jamani tusikae kimya kuona mnyonge ananyongwa.
 
mwanzoni nilikuwa na hamu sana ya kuona kuwa tunaisaidia familia ya marehemu kuajiri wakili mahiri kumtetea lakini baada ya kuona vitendo vya viongozi wa serikali na rambirambi zao nilijua kabisa ya kuwa familia imeenda kutulizwa na hawatapigania haki kutendeka wakati wamekatika fedha za pole na Rais mwenyewe!! Wakili yoyote mzuri kama hajipendi Tanzania basi ajiingize kwenye kesi hii.

Kuhusu majaji usiwe na shaka, nina uhakika wataona BS hii toka mbali. Binafsi ningefurahi kuona Mwendesha Mashtaka wa Polisi hakubaliani na DPP na kusema hajaona sababu ya kubadilisha mashtaka ya awali na kujitoa amwache DPP aje aendeshe mashtaka hayo yeye mwenyewe.! Haiwezekani kuwa DPP amesikiliza ushahidi wa watu hao na bado akasema jamaa alifanya hivyo kwa kutokukusudia!!

NB*

1: Nenda ukurasa wa pili wa thread hii usome maelezo ya waandishi ya wakati ule na ulinganishe na maneno ya mashahidi

2. Kuna mtu mmoja ambaye ni muhimu sana katika kesi hii. Katika ripoti za awali kulikuwa na abiria wanne kwenye gari la Dito na madai hayo yamerudiwa kwenye ushahidi hapo juu. Upande wa utetezi wanasema walikuwa watu watatu. Toka mwanzo nilihoji, who was the fourth person.. mwanamama huyo ni nani? Under penalty of perjury dereva wa Dito lazima abanwe kuhusu hilo, na kama huyo mama yupo atiwe moyo ajitangaze hadharani. She is a very important witness for either side.

3: Muda. Ajali ilitokea saa moja za jioni, ilikuwaje polisi wapate taarifa za nani alifanya usiku wa manane? Hivi toka Dar hadi Bagamoyo siku hizi unatumia muda gani?

4. Kwanini Dito hakujisalimisha Bagamoyo "alikokimbilia" na kusubiri kujisalimisha Dar tena kwa kumuita mkuu wa polisi nyumbani kwake? Kwanini hakukwenda kituoni?
 
Jamani hivi vikundi vya Wanasheria na NGO vinafanya nini au navyo vimeshavamiwa na Mtandao.

Swala la msingi hapa ni: Je DPP anaweza kubadilisha kesi au mahakama ndiyo hupitia ushahidi na utetezi wa kosa na kuamua na kutoa hukumu.

Huyu DPP anataka kusema mimi nikimshitaki mtu kwa kuniibia, yeye anaweza kuabdili shitaka na kuwa mimi ndiye niliyeiba.

Nadhani ndiyo maana wakati mwingine nadhani "MOB JUSTICE is BETTER than our JUSTICE SYSTEM"

Nadhani wananchi wamepewa ushauri tosha kabisa kuwa "mwenye kosa aadhibiwe papo hapo" kwani kumpeleka polisi ni kupoteza muda na unaweza kugeuziwa kesi bure"
Wangetakiwa wa"Dito" pale pale kama vibaka wanavyofanyiwa.

Hata mimi nilikuwa nafikiria "kwani hakupatiwa hukumu ya kifo pale pale," nikawa sipati jibu. Sasa nimejua ni kwa sababu dereva wake alitoka na bastola pia. This is disgusting. Ati alitaka kumpeleka hospitali, hospitali gani siku hizi wanafufua wafu?
 
Hii inatisha risasi mbili kichwani na silaha iliyotumika haieleweki kama ipo au vipi? Huyu DPP ni uchwara hafai na sijui alisomea wapi?
 
Wanabodi,
Hivi ile bastola imesha patikana?...
Kama bado vipi jamaa kadai kuwa bastola ilikuwa Automatic!... meaning what? kwamba kesha iona hiyo bastola!..

Guy's huwezi kumwambia mtu ashuke toka ndani ya gari ili mzungumze huku umeshika bastola!.. Kitendo cha kutoka na bastola toka ndani ya gari, hii ni kukusudia kabisa kwa sababu marehemu hakutukana (kama alitukana) wakati Dito akiwa bado ktk gari lake.
 
Haya ndiyo matatizo ya kuajiri watu wenye elimu ya mtandaoni (fani imevamiwa).

Cha kushangaza mpaka sasa hivi sijaona Jaji Mkuu (Chief Justice) na hata Mwanasheria Mkuu (Attorney General) akimkosoa DPP kwa kosa alilofanya. Na waziri wa Sheria na Katiba naye kimya.

Mkjj: Naomba umtafute Rev. Mtikila atusaidie kufungua kesi mahakamani, mimi binafsi nitatoa Milioni Mbili kuona haki inatendeka. Jamani tusikae kimya kuona mnyonge ananyongwa.

Hiyo milioni 2 watalamba na bado watafanya wanavyotaka wao.
Ni kitu gani hapa kinachotakiwa kujadiliwa zaidi kwani kama ni mimi ndiyo jaji na mahakama hiyo ya jana inaruhusa ya kutoa hukumu basi ningemhukumu Ditopile kama sheria inavyosema.Huyo MUUNGWANA AMEUA KWA KUKUSUDIA KWANI KABLA YA KUUA ALICHUKUA MUDA MWINGI KUFANYA VITENDO VYA KIBABE KWA WAHUSIKA KADHAA NA HATA KITENDO CHA DEREVA KUJIHAMI ILI ASIFIKWE NA MADHARA ALIKIPUUZA NA BADO ALIFYATUA RISASI.Hata kama ilikuwa automatic kama anavyotaka tumuelewe hivyo Lakini si alikoki kwani hata gari kuwa automatic haimanishi litakwenda bila ya kuongozwa.
 
Kazi ndiyo kipimo cha Utu,
Maneno yako kweli kabisa na mfano wa gari Automatic ni mfano bora hakuna kingine. Bastola ya Utomatic hufanya kazi sawa kabisa na gari Automatic yaani toka risasi ya pili na kuendelea ni yenyewe inamimina maadam kidole chako kipo ktk trigger, lakini risasi ya kwanza ni lazima uiweke ktk chamber kwa kukoki.
Kisha, shahidi yule kijana kasema Dito alikoki bastola yake, sijui hapo alikuwa bado hajakusudia ama ndio bado ktk kutishia!
 
Kazi ndiyo kipimo cha Utu,
Maneno yako kweli kabisa na mfano wa gari Automatic ni mfano bora hakuna kingine. Bastola ya Utomatic hufanya kazi sawa kabisa na gari Automatic yaani toka risasi ya pili na kuendelea ni yenyewe inamimina maadam kidole chako kipo ktk trigger, lakini risasi ya kwanza ni lazima uiweke ktk chamber kwa kukoki.
Kisha, shahidi yule kijana kasema Dito alikoki bastola yake, sijui hapo alikuwa bado hajakusudia ama ndio bado ktk kutishia!

HALAFU tukumbuke Ditopile kitaaluma anauwezo wa kumiliki silaha,Pili Toka anaitoa silaha alikuwa anajua ni Automatic na alielewa kabisa madhara ambayo yangeweza kusababishwa na silaha kitaaluma na hasa kwa aina ya silaha yenyewe,sasa kwanini aliamua kuitumia kugongea kioo cha dirisha la gari ?Huyu Aliua kwa kukusudia na Nachelea kusema hata hiyo tabia ya kutishia silaha haikuwa mara ya kwanza alishazoea na Hatujui wangapi huko nyuma alishawahi kuwafanyia hivyo?Kitu kingine kinachonifanya niamini hawa jamaa silaha kwao ilikuwa nje nje ni ile ya hali hata ya dereva wake kuwa anamiliki silaha.
 
msisahau kuwa watu watatu walitishiwa na bastola... imagine....the scene when mkuu wa mkoa guns down three unarmed young men.. and the DPP says it was "unintentional"....

Swali: Je mheshimiwa na dereva wake wanamiliki bunduki kihalali? Je polisi wanaweza kutuambia Bastola ya mheshimiwa iliyopotea ni namba gani kuna mtu kaokota bastola..!
 
Waungwana,

Naona hapa tayari haki ya mtu imeshapotea na mashahidi tayari wameshapata cold feet. Inaelekea Ditopile atatolewa nje siku si nyingi
akisubiri case yake iendelee. Hii inatisha kweli kweli. Soma hapa chini:

Katika maelezo yao, ilidaiwa kuwa, Ditopile alianza kumpigia simu Kamanda Mssika akimtaka waonane kwa kuwa tukio lilitokea njia panda ya Kawe la mtu kupigwa risasi, lilimhusu yeye.

Baada ya kuonana na Mssika na kumsimulia tukio hilo, ilidaiwa kuwa, walikwenda nyumbani kwa Kamishna Tibaigana saa 8:00 usiku ambapo baada ya kufika na kukaribishwa alijibu ``Mimi si Mheshimwa, ni muuaji, miaka yangu ya kazi imepotea bure,`` alidai Kamanda Tibaigana.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa, risasi iliyomuua dereva wa daladala, Hassan Mbonde, ilifyatuka wakati Ditopile akigonga gonga dirisha kumtaka dereva huyo atoke nje.

Ulidai kuwa, dereva huyo alimjibu Ditopile vibaya kuwa suala hilo limeshatoka na kumsonya na ndipo ghafla aliposikia watu wakisema kuwa, ameuua.

Ushahidi wa kondakta, Bw. Thomas Mwita ambaye alikuwa na marehemu siku ya tukio, ulidai kuwa, Novemba 4, mwaka jana, saa 1:40 usiku, eneo la njia panda ya Kawe, wakiwa kwenye gari lao kutoka Mwenge kuelekea Tegeta, kulikuwa na msongamano wa magari.

Alidai kuwa, waliliona gari lingine likipita katika barabara ya dharura na kusimama mbele yao kwa kuwa njia ilikuwa imefungwa kutokana na msongamano.

Hata hivyo, alidai kuwa, moja ya matairi ya gari hilo la ziada liligongwa na gari lao ambapo dereva aliteremka kuangalia.

Alidai kuwa, baada ya dereva huyo kuona lake halijagongwa, alirudi tena kwenye gari lakini alitoka mtu mwingine mweupe ambaye hakumtambua na kumtishia kondakta mwingine aliyekuwa akitazama kama gari limegongwa kwa kumwekea bastola kichwani akitaka kujua anafanya nini hapo.

``Mara alimgeukia dereva wa daladala na kumtaka ashuke kwenye gari, lakini alimueleza kuwa, akishuka gari lingeweza kuserereka na kuwaua abiria kwa kuwa lilikuwa kwenye mteremko,`` alidai.

Hata hivyo, maelezo ya kondakta yalisema Ditopile alimfokea na kutaka kujua kama dereva huyo anajali zaidi abiria wake kuliko gari lake.

Shahidi huyo alidai kuwa, alimshauri dereva huyo afunge dirisha lake ambapo alifanya hivyo na Ditopile alimtishia kuwa angepiga kwa risasi matairi ya gari hilo huku akigonga gonga dirisha kwa kutumia bastola yake na ndipo mlio mkubwa wa risasi uliposikika na kumpiga dereva.

Hata hivyo, ushahidi wa Bw. Mwita ulitofuatiana na ushahidi wa watu wengine kwa kuwa ilidaiwa kuwa, gari lao ndilo lililogonga gari la Ditopile mara mbili na hivyo kusababisha ateremke kwenye gari lake.

Hakimu Luguru alimshauri Ditopile kusubiri kesi hiyo ipangwe Mahakama Kuu atakapotoa utetezi wake na kuomba dhamana.
 
Tibaigana, Mssika wasimulia alivyojisalimisha polisi
Na Ester Bulaya

KONDAKTA Thomas Mwita aliyeshuhudia kifo cha dereva wake, amedai kuwa mshitakiwa Ditopile Mzuzuri (58), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, alimzaba vibao na kumtishia kwa bastola dereva wa akiba kabla ya kumuua Hassan Mbonde.
Mbali na Mwita abiria aliyekuwa amekaa kiti cha mbele katika basi hilo, Masasi Luenge, alidai Ditopile alimtishia kumpiga risasi na kumtukana baada ya kumueleza aache kumuamuru dereva Mbonde ashuke chini.
Kauli hizo ni maelezo ya mashahidi wa upande wa mashitaka yaliyosomwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Michael Luguru aliyesikiliza maelezo ya mashahidi hao 24 yatakayotumika katika kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa Mahakama Kuu.
Akisoma maelezo ya Mwita, Mwendesha mashitaka Gilvanus Muhume alidai Luenge alizambwa vibao baada ya kushuka kuangalia jinsi gari la Ditopile lilivyoharibika baada ya ajali hiyo.
" Aliposhuka alikutana na mshitakiwa (Ditopile) aliyemuuliza unafanya nini, ambapo Luenge alimjibu 'samahani mzee naangalia tulipo gonga' ghafla Ditopile alimzaba vibao na kumuamuru aondoke huku akimuonyeshea bastola kichwani," alidai Mwita katika maelezo yake.
Mwita ambaye ni kondakta wa daladala hilo lenye namba za usajili T 816 AGT, alidai siku ya tukio walikuwa wakielekea Tegeta saa moja usiku njia panda ya Kawe, wakati wakiwa kwenye foleni lilikuja gari aina ya Prado ambalo lilienda 'kuchomekea' ghafla mbele ya gari yao, ambapo kwa bahati mbaya gari lao liligonga tairi ya akiba iliyokuwa nyuma ya gari.
Alidai baada ya kuona mwenzake amenyooshewa bastola, aliondoka na kuingia ndani ya gari, huku Ditopile akizunguka dirisha alilokuwa amekaa dereva na kumlazimisha ashuke.
Mwita alidai Mbonde alimjibu: "Samahani mzee siwezi kushuka kwa kuwa gari lipo kwenye kilima na breki siyo nzuri hivyo nitaua abiria."
Kwa mujibu ya maelezo ya Mwita, baada ya marehemu kujibu hivyo, Ditopile alimwambia kuwa anajali abiria kuliko gari lake na kumlazimisha asishuke ambapo alipandisha vioo na 'kuloki' mlango wake.
Ditopile baada ya kuona hivyo 'alikoki' bastola na kumfyatulia dereva Mbonde risasi mbili za kichwa.
Alidai baada ya kumpiga risasi, abiria walianza kulia huku wakipiga kelele kuwa ameua ndipo mshitakiwa alipoingia na kumgusa dereva huyo.
Mwita alidai abiria walianza kumzonga huku yeye akimshika kwa nguvu asitoroke kwa ajili ya kumpeleka polisi.
Alidai wakati wakimzuia, alitokea dereva wa Ditopile ambaye naye alichomoa bastola na kuwanyooshea huku akiwakataza kumshika bosi wake na hivyo kufanikiwa kuondoka naye katika eneo la tukio.
Shahidi Masasi Luenge ambaye alikuwa abiria katika daladala hilo, alidai dereva wa Ditopile ndiye 'aliyechomekea' na kusababisha ajali hiyo.
Luenga ambaye alikuwa amekaa kiti cha mbele alidai baada ya marehemu kupigwa risasi alimuangukia na kufa papo hapo.
Alidai kabla ya kushambuliwa, marehemu alimuomba msamaha na kueleza sababu za kutoshuka.
Hata hivyo, alidai Ditopile alimtukana na kumuelekezea bastola.
Kwa upande wake, dereva wa akiba katika daladala hiyo, Edward Girvas ambaye siku hiyo alikuwa kama kondakta, alidai alitishiwa kupigwa risasi ya kichwa na Ditopile, baada ya kushuka na kumuomba msamaha wakati marehemu alipogonga gari lao.
Alidai mshitakiwa kabla ya kumonyeshea bastola alimpiga vibao na kumtaka aondoke haraka.
Shahidi mwingine aliyetoa maelezo yake mahakamani hapo ni daktari Mgaya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, na kuthibitisha kuwa marehemu aliuawa kwa kupigwa risasi mbili.
Alidai risasi hizo zilipitia upande wa kulia na kutokea kushoto na kwamba kipande cha risasi kilibaki katika kichwa cha marehemu.
Kamishna msaidizi wa polisi, Abdallah Mssika, katika maelezo yake alidai Ditopile alimueleza kwamba hakudhamiria kumuua dereva Mbonde, lakini bastola aliyokuwa akimtishia ilifyatuka na kusababisha mauaji hayo.
Akisoma maelezo ya shahidi huyo (Mssika), aliyemhoji Ditopile, Muhume alidai katika maelezo hayo, mshitakiwa alimueleza kuwa
hakuwa na nia ya kufyatua risasi bali alishtukia risasi zimetoka zenyewe baada kugonga dirisha.
Kulingana na Ditopile, hali hiyo ilisababishwa na bastola hiyo ambayo ni 'Automatic'.
Alidai kitendo cha yeye kutoa bastola hiyo, kilitokana na marehemu (dereva) kumsonya na kugoma kushuka, baada ya kumgonga huku kondakta wa akiba akimtamkia maneno kwamba 'mzee hiyo ndiyo imetoka' matamshi aliyoyaona ni dharau kwake.
Mssika aliendelea kudai katika maelezo hayo kuwa Ditopile, baada ya kugundua risasi imefyatuka, aliamua kutoa risasi zote katika bastola yake ili isilete madhara zaidi.
Alidai baada ya kuhakikisha bastola yake iko salama, aliingia ndani ya basi hilo kuangalia jinsi dereva alivyoumia ili aweze kumsaidia ikiwa ni pamoja na kumpeleka hospitali.
Mssika alidai katika maelezo yake kwamba, Ditopile hakupata ushirikiano kutoka kwa abiria na badala yake walianza kumzonga na kumuambia 'umeua mwenyewe na umbebe kumpeleka hospitali' huku wengine wakimpiga.
Alidai katika kujiokoa kondakta wa gari hilo, alichukua chuma na kutaka kumpiga kichwani, lakini mshitakiwa alifanikiwa kukinga kwa kutumia mkono wake.
Kutokana na hilo, mshitakiwa alilazimika kukimbia huku akipiga kelele kuomba msadaa kutoka kwa dereva wake.
Mssika alidai kabla ya kuchukua maelezo ya Ditopile, mshitakiwa alimpigia simu kwa lengo la kutaka kujisalimisha na kumueleza juu ya tukio hilo.
Kamanda Mssika alidai baada ya kujisalimisha alichukua maelezo yake mbele ya wakili wake Ringo Tenga.
Akisoma maelezo ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, Mwendesha mashitaka Naima Mwanga alidai Tibaigana alieleza kushangazwa kumuona mshitakiwa akifika nyumbani kwake usiku wa manane akiwa na Mssika.
Naima alidai Kamanda Tibaigana alimkaribisha Ditopile kwa kumueleza 'Karibu Mheshimiwa na yeye alijibu kuwa mimi siyo mheshimiwa tena bali ni muuaji' na kuanza kumsimulia tukio hilo na kusisitiza kuwa hakuwa na nia ya kufanya hivyo.
Tibaigana alidai kuwa lalamiko kubwa la Ditopile ni kitendo cha dereva (marehemu) kumtukana na kukaidi kushuka ili waweze kufikia makubaliano.
Mbali na maelezo ya mashahidi hao, pia upande wa mashitaka utawasilisha vielelezo vitano ikiwemo taarifa ya daktari, maelezo ya ungamo la mshitakiwa, taarifa ya uchunguzi wa ripoti ya mlio wa risasi, ramani ya eneo la tukio na fomu ya gwaride la utambulisho.
Hata hivyo, upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili Nimrod Mkono, uliomba dhamana kwa mteja wao, na kumueleza hakimu kuwa ana uwezo wa kutoa dhamana ingawa hana mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hata hivyo Hakimu Lugulu alikataa kusikiliza ombi hilo na kuwataka kuliwasilisha Mahakama Kuu.
Ditopile ambaye jana alikuwa akiendeleza mtindo wake wa kuingia mahakamani huku akiwa amevaa 'pama' kuficha uso jana alisomewa shitaka jipya la kuuawa bila kukusudia.
Katika shitaka hilo, anadaiwa kuwa Novemba 4, mwaka jana, njia Panda ya Kawe na Bagamoyo alimuua bila kukusudia Hassan Mbonde.
Awali, alishitakiwa kwa kosa la mauaji kabla ya kubadilishiwa shitaka hilo na Mkurugenzi wa Mashitaka mwishoni mwa Januari.
 
2. Kuna mtu mmoja ambaye ni muhimu sana katika kesi hii. Katika ripoti za awali kulikuwa na abiria wanne kwenye gari la Dito na madai hayo yamerudiwa kwenye ushahidi hapo juu. Upande wa utetezi wanasema walikuwa watu watatu. Toka mwanzo nilihoji, who was the fourth person.. mwanamama huyo ni nani? Under penalty of perjury dereva wa Dito lazima abanwe kuhusu hilo, na kama huyo mama yupo atiwe moyo ajitangaze hadharani. She is a very important witness for either side.

Duh!
Jamani habari za Ditto ni nyingi:
Kwanza alitoroka kituo chake cha kazi, yaani, aliondoka bila kutoa taarifa au kuomba ruhusa kwa mwajiri wake.
Pili, huyo mwanamama aliyekuweko nae habari za uhakika zinadai ni mamdogo wa nyumba ndogo. This explains why she does not feature anywhere
Tatu, Ditto ni mzoefu wa makeke...ukijumlisha uwepo wa mamdogo pembeni..he was trying to impress her
Hivyo ndivyo dhambi inavyozaa dhambi!

4. Kwanini Dito hakujisalimisha Bagamoyo "alikokimbilia" na kusubiri kujisalimisha Dar tena kwa kumuita mkuu wa polisi nyumbani kwake? Kwanini hakukwenda kituoni?[/QUOTE]

Acha Ditto, mi nimewahi kushuhudia mfanyabiashara akimuita OC/CID, na RCO nyumbani kwake kumpeleka mtuhumiwa wake waliyemkamata, na walimpeleka! mfanyabiashara 'akamuhoji' mtuhumiwa mbele yao, akamnasa kibao kisha akawa-discharge!
 
Suala la zima la Ditopile linaonyesha ni kwa sababu gani nchi zetu zitaendelea kuwa maskini . Hakuna nchi yoyote hapa duniani ambayo imeendelea na wakati huo huo inapuuzia utawala wa sheria . Mimi sidhani kama DPP hana kosa hapa kwani anapata tuu Directives kutoka kwa wakubwa .

Nauliza kitu kimoja ni kigezo gani kilichotumika kubadilisha shitaka toka murder to manslaughter.
 
umesikia utetezi wa kina Tenga na Mkono wakati wakiomba dhamana:

"Wadhamini tunao, tena wa maana… watano, hivyo mteja aliyepo mbele yako anastahili dhamana na kwa kuwa ni mtu mkubwa na mzito, hawezi kutoroka… tunaiomba mahakama yako tukufu impatie dhamana," alisema Nimrod. (Tanzania Daima)

umepata jibu la swali lako my friend?
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nahisi si vizuri kwa waheshimiwa wabunge kufanya kazi za uwakili wakati wanapokuwa na ubunge. Sidhani kama inaakisi vizuri dhana nzima ya utawala bora; unapokuwa na wakili ambaye ni sehemu ya judiciary na wakati huo huo ni mbunge ambaye ni mtunga sheria. Kichwani napata taabu kuelewa kama namsikiliza Mkono mbunge au Mkono wakili. Badala ya kufunga makampuni yao ya sheria wawapo wabunge, basi wabunge wanasheria hawa wasifanye kazi ya kutetea wazi wazi mahakamani. Naona haijatulia!
 
Thanx MKJJ ..kumbe kulikuwa na mjadala kuhusu wasiwasi wangu huko nyuma!
Anyway, ndiyo maana naona bora tukae chini tuandike KATIBA upya, kwa sababu tukiendelea kuweka viraka tu nguo halisi yenyewe nayo itaendelea kuchanika tena!

Nafikiri sasa Watanzania kwa ujumla wao wana uelewa mkubwa kufanya tuwe na katiba inayokidhi maisha yetu ya sasa na changamoto zake.
 
Karibu watanzania wengi wanaona umuhimu wa kuwa na KATIBA Nyingine itakayokidhi matakwa ya walio wengi kiubora.Lakini ni nani anakwamisha hili?
 
Ditopile may walk home today


gallery_image.php


The Front seat of the ill-fated 'daladala' spots blood stains after its driver, Hassan Mbonde, 33, (insert) was shot dead on Saturday night. The Ubungo-Tegeta bus is parked at the Kawe Police Station. (Photo by bernard Rwebangira)​




2007-03-08 09:32:59
By Rosemary Mirondo


The High Court of Tanzania in Dar es Salaam is to-day expected to resolve the issue of bail for former Tabora Regional Commissioner, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, who is charged with manslaughter. The matter, supposed to have been determined yesterday, was adjourned until to-day at 11:00 am because of what was described as inevitable circumstances. Moments before the court session began, many people converged at the court premises to hear what would happen to the former Tabora regional commissioner.

Adjourning the case yesterday, High Court Judge Augustino Mwaringa cited communication problems that ensued among prison officers, police and the court as the basic factor that led to a change of schedule. The accused was not brought to court in the morning.

By the time he appeared at 2:15 pm, the judge had already issued an adjournment order to the effect that the matter be heard to-day. Ditopile was taken back to remand prison where he has been living since he was arraigned allegedly for killing without malicious forethought Hassan Mbonde, a daladala driver.

It was claimed that the accused committed the offence at Bagamoyo and Kawe Roads junctions within Kinondoni District in Dar es Salaam on November 4, 2006. The bail consideration comes in the wake of a lesser offence for which he is being tried. Initially, the accused was charged with murder. However, the prosecution later altered the charge and substituted it with manslaughter, meaning killing without malicious forethought.

Earlier, committal proceedings were conducted by Kisutu Resident Magistrate's Court where he was not asked to enter any plea.

The Resident Magistrate`s Court has no jurisdiction to try and determine the case under existing laws.
 
Back
Top Bottom