Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Matatizo yapo kotekote, Polisi na Mahakama pia,

tuangalie tusije tukaingia ktk kesi ya kuku na yai ya kwamba kipi kilianza.

Jamani lets give JK credit where he deserves, kateua majaji na muundo wa polisi unaendelea kubadilishwa, tusubiri matokeo yake maybe another year or two.

Kuharakishwa kwa kesi ya braza Ditto, wakati kuna kesi nyingi on queue ni UONEVU WA HALI YA JUU kwa wanaosota rumande na ndugu zao.

Mwendapole
hebu tumegee kidogo haya mambo yanakuwaje kuwaje
 
Ogah sasa unaleta majibu rahisi kwa maswali magumu. Hivi Marais waliopita walikuwa wanashindwa nini kuteua judges wakati wa vipindi vyao? Tatizo kulikuwa hakuna wenye sifa nyakati hizo? Au tatizo lilikuwa resources? Au hakukuwa na kesi nyingi wakati huo? Baada ya uteuzi huo ni kanda ngapi za mahakama kuu zimeongezwa au kuundwa au wote wameendelea kuwa Dar? Lakini zaidi tatizo letu lipo kwa idadi ya ma-judge? Yale yale ya kujenga vyumba vya madarasa nakudai mafanikio katika sekta ya elimu.
Kuhusu hilo la polisi muundo wake kubadilishwa hebu tupe mfano wake maana hapo sasa naona unakuja na hekaya zile zile za watawala.
Suala la Dito kama kesi imeharakishwa well and good, bila shaka hilo si tatizo hapa, suala ni mashtaka yake. Hiyo kesi ilitakiwa kuanza kuunguruma ndani ya mwezi mmoja na wala siyo miezi minne kama ilivyo sasa.
 
Ogah sasa unaleta majibu rahisi kwa maswali magumu

Lets not complicate some issues ambazo ziko soo obvious and simple!!

Hivi Marais waliopita walikuwa wanashindwa nini kuteua judges wakati wa vipindi vyao? Tatizo kulikuwa hakuna wenye sifa nyakati hizo? Au tatizo lilikuwa resources? Au hakukuwa na kesi nyingi wakati huo?

Good questions........ningefurahi sana kama ningekuwa na uwezo wa kujibu hayo maswali hapo juu.

Sasa baada ya kujiuliza hayo maswali, sasa pata picha; kaja JK kateua majaji...........

Baada ya uteuzi huo ni kanda ngapi za mahakama kuu zimeongezwa au kuundwa au wote wameendelea kuwa Dar?

kuongeza kanda its a next step after uteuzi huo, ingechekesha ikiwa angeanzisha kanda bila ya kuwa na Judges

Lakini zaidi tatizo letu lipo kwa idadi ya ma-judge?

to some extent, Ndio, hivyo kukawa na umuhimu wa kuteua majaji, pia kuna msongamano wa kesi nyingi mahakama kuu

Yale yale ya kujenga vyumba vya madarasa nakudai mafanikio katika sekta ya elimu.

Nafikiri hapo ni kinyume chake kwani JK kateua halafu "nina Imani" kanda "madarasa" zitaongezwa kinyume cha hapo ninaweza kuuita uamuzi huo "NONSENSE"

Kuhusu hilo la polisi muundo wake kubadilishwa hebu tupe mfano wake maana hapo sasa naona unakuja na hekaya zile zile za watawala.

Kama utakumbuka....Mzee Mwanakijiji.....nafikiri ilikuwa kule BCS alipendekeza muundo maalumu wa utendaji kwa jeshi letu la polisi, na tumeshuhudia juhudi za forum kama hii kuzaa matunda hayo ambayo tumeyaona yameanza kufanyiwa kazi "Kanda ya Dar es salaam" kamanda ni Tibaigana.

Suala la Dito kama kesi imeharakishwa well and good, bila shaka hilo si tatizo hapa,

Ndugu yangu.......... ni 'well and good kwa Ditto!!! however, HILI NI TATIZO kwetu sisi wananchi tulio na ndugu zetu wenye kesi za "kuku" wanaosota bila kujua hatma za kesi zao miaka nenda miaka rudi. Ninachoweza kusema ni kuwa kama walitaka kumsaidia 'mwenzao" basi wangeharakisha kufanya uchunguzi wa kesi zilizo mbele ya hiyo ya Ditto ili nayo ifanyiwe maamuzi kwa wakti wake. May be FIFO doesn't apply in LAW.....Mwendapole hebu tuelimishe hapo!!

suala ni mashtaka yake (Ditto).

Nakubaliana na wewe only if una maanisha kubadilishwa kwa Kosa kuwa "Kuua bila kukusudia" ya kwamba si haki!!
Huu mimi nauita UHUNI!! na ni DHAMBI KUBWA Mbele ya MOLA WETU. Mzee Kichuguu alitoa mfano mzuri saana wa Kleruu, nafikir kilichompata muuwaji wake ndicho kilichotakiwa kumpata huyu Ditto

Hiyo kesi ilitakiwa kuanza kuunguruma ndani ya mwezi mmoja na wala siyo miezi minne kama ilivyo sasa.

NO!!, nafikir ilitakiwa iungurume kama zilivyo za wengine wanaosota rumande hadi leo miaka nenda miaka rudi.
Hata hivyo NAFARIJIKA YA KWAMBA DITTO IS NO BODY MBELE YA MOLA WETU NA ATAKULA HAKI YAKE TU HIYO SIKU

Mgomo wa mahabusi wasambaa Dar

Na Waandishi Wetu

MGOMO wa mahabusu wa kupinga kucheleweshewa kesi zao ulioanza katika Mahakama ya Kisutu juzi, umeendelea jana na kusambaa katika mahakama nyingine jijini Dar es Salaam na mjini Arusha.

Jijini Dar es Salaam, mahabusu hao waligoma kwa mara ya pili kushuka katika karandinga, wakishinikiza Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Mary Nagu, atoe tamko juu ya kesi zao ambazo wanadai zimechukua muda mrefu bila ya upelelezi wake kukamilika.

Mgomo huo uliingia siku ya pili jana, baada ya juzi mahabusu hao kukataa kushuka katika karandinga kwa ajili ya kusikiliza kesi zao, wakishinikiza upelelezi wa kesi zao ufanywe haraka kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila ya kukusudia.

Mgomo huo ambao unaonekana kuishika pabaya serikali, uliendelea tena jana kwa nyakati tofauti katika mahakama ya Kisutu na mahakama za wilaya za Ilala na Temeke ambako mahabusu waligoma kushuka huku wakisisitiza kuwa hawatafanya hivyo hadi hapo serikali itakapotoa tamko kuhusiana na madai yao.

Wakiwa ndani ya makarandinga ya polisi katika mahakama hizo, mahabusu hao waliendelea na staili yao ya kuimba nyimbo za kudai haki na kuishutumu serikali kuwa inafanya upendeleo katika kushughulikia kesi za vigogo na walalahoi.

Walimtaka Dk Nagu na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) watoe tamko litakalofafanua muda ambao mtuhumiwa wa mauaji anastahili kukaa mahabusu wakati upelelezi wa kesi yake ukiendelea kwa kile walichoeleza kuwa upo upendeleo wa dhahiri katika kushughulikia kesi hizo.

Walisema tatizo zaidi linakuwa katika kesi zinazohusisha vigogo wa serikali na watu maarufu, huku zile zinazowahusu walalahoi zikipuuzwa na upelelezi wake ukichukua muda mrefu na kuwaacha wakiteseka gerezani bila ya kupatiwa haki za msingi.

Pia walimtaka Waziri Nagu, atembelee magereza aweze kujionea mwenyewe hali halisi, ili ajue kuwa kuchelewesha kesi hizo ni kuwaumiza na kuwapa mateso makubwa mahabusu.

Katika Mahakama ya Kisutu, jana, karandinga la kwanza lililochukua mahabusu kutoka Gereza la Keko lilifika saa 3.30 asubuhi na kama ilivyokuwa juzi, waligoma kushuka na baada ya muda mfupi walirudishwa gerezani.

Karandinga la pili lilifika saa 4.38 asubuhi, likiongozwa na gari la polisi namba T 220 AMV Land Rover, lakini mahabusu waliokuwamo pia waligoma kushuka na kurudishwa mahabusu.

Katika mahakama za wilaya za Ilala na Temeke, kesi zote zinazohusu mahabusu waliotoka katika magereza ya Keko na Segerea, ziliahirishwa jana baada ya mahabusu kugoma kushuka kwenye karandinga wakidai kucheleweshwa kwa upelelezi wa kesi zao.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya mahabusu waliokuwa wakitarajia dhamana, waliangua kilio baada ya kuwaona ndugu zao waliofika mahakamani hapo kwa ajili ya kuwawekea dhamana.

Katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, waliobahatika kushuka kwenye karandinga ni mahabusu wanawake kutokana na wao kuwekwa katika chumba tofauti na wanaume ndani ya gari lililowafikisha mahakamani hapo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Joyce Minde, alisema kuwa amewasiliana na polisi ili wafuatilie suala hilo.

Mjini Arusha, mahabusu wanaokabiliwa na kesi mbalimbali nao waligoma kushuka katika karandinga katika viwanja vya Mahakamani Kuu wakitaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa jirani na mahakama hiyo, ilipo Ikulu ndogo wakilalamikia kucheleweshwa kesi zao.

Mahabusu hao wanaokaridiwa kufikia 70, walipaza sauti wakilalamikia kuachiwa kwa dhamana kwa Ditopile huku wao wakiachwa wateseke gerezani.

Mahabusu hao baadaye walianza kuimba kwa sauti kubwa "polisi wanataka nini...wanataka rushwa na Ditopile kawapa nini, kawapa rushwa" hatua ambayo ilizuwa tafrani kubwa mahakamani hapo na kwa maafisa wa usalama ambao walikuwa viwanja vya Ikulu.

Tukio hilo lilianzaa majira ya saa 3.30 mara baada ya mahabusu hao kuwasili katika gari lao lenye namba za usajili STG 9266 na lilidumu hadi saa 4.11 pale maafisa kadhaa wa polisi walipowasili na kuamuru mahabusu hao kurejeshwa magerezani.

Maafisa wa polisi wakiwa katika gari lenye namba za usajili T638AJR na polisi wengine wa kutuliza ghasia wakiwa katika gari lenye namba za usajiri T 447 APF waliwaondoa mahabusu hao kupitia njia tofauti na ambayo hutumika, hivyo kukwepa Rais Kikwete asisikia kelele hizo.

Awali, mahabusu hao huku wakipiga mayowe, walikuwa wakilalamikia polisi kuchelewesha kesi zao na hasa upelelezi, hatua ambayo inachangia kukaa muda mrefu magerezani.

Hata hivyo, hakuna hakimu ambaye alikuwa tayari jana kuongelea tukio hilo kwa maelezo kuwa wanaolalamikiwa ni polisi na sio wao.

Katika mgomo wa juzi katika mahakama ya Kisutu, Mahabusu wanaokadiriwa kuwa kati ya 250 hadi 300 wakitokea katika magereza ya Keko na Segera, waligoma kushuka ndani ya magari ya polisi STH 3058 na STJ 903 wakilalamikia ucheleweshwaji wa upelelezi wa kesi zao.

kazi kwelikweli.........
 
Majaji wangapi walioteuliwa na wangapai waliostaafu ama kufa? Je, hilo siyo suala la kata mti. panda mti?
 
Message sent kwa wapelelezi
Siku zote wakazi wa Dar huyaogopa makarandiga ya Polisi yakiwa yamebeba wafungwa kutokana na mitusi ya nguvu wanayoporomosha, ila jana walikuwa wanawashangilia na kuwapungia mikono.

Mabadiliko hayo ya mioyo ni hatua ya kuwaunga mkono kwa uamuzi wao wa kugoma kushuka katika Mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi zao.

Wakati mgomo huo ukiendelea raia waliojazana Mahakama ya Kisutu waliungana na watuhumiwa hao wa mauaji kuimba wimbo wa 'parapanda italia parapanda.....'

Kilichoibua mgomo ni hatua ya Mahakama kuharakisha uendeshaji wa kesi ya Dito kwa miezi mitatu na hadi kuachiwa kwa dhamana kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Kibao kiligeuka na raia kushangilia mgomo wa wafungwa..

Malalamiko ya watuhumiwa hao ni kutokana na baadhi yao kukaa
lupango kwa miaka 10 na bado kesi zao hazijasikilizwa.

Kushindiliwa kwenye karandinga kupita kiasi hadi kufikia 170 kwa gari moja (lenye uwezo wa kubeba watu 30) huku wakidai kuwa huletwa mahakamani saa 12:00 asubuhi na kurejeshwa gerezani saa 11:00 jioni bila ya chakula wala maji ya kunywa.

Waliendelea kutema cheche kuwa hata ndugu zao huzuiwa kuonana nao na baadhi ya ndugu zao wa uraiani walishawekwa mahabusu kwa siku mbili kwa kisa cha kuwaletea chakula.

Mgomo huo ulidumu hadi saa 5:00 asubuhi hadi Hakimu Mwangesi
alipoamua warejeshwe magerezani huku message ikiwa sent
 
habari, tatizo siyo mahakama..! kesi imeharakishwa na DPP na maafisa wa polisi.. Mahakama husikiliza kesi baada ya ushahidi kukamilika....
 
MWANAKIJIJI JE MWAPACHU AMEKUCONVINCE AU NI YALEYALE

juu
 
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/3/14/makala7.php

Mimi kinachonisikitisha ni kuwa wakati Mtikila anataka kufunguwa kesi ya ditopile upya ndugu na jamaa wa marehemu wapo kimya kabisaa kama hawapo. Hata mashtaka yalipobadilishwa kutoka kuua kwa kukusudia kuwa kuua bila kukusudia pia walikuwa kimya. Au kimya chenyewe kinatokana na ziara za viongozi wetu zilizo wazi na zisizo wazi pamoja na rambi rambi walizopewa? Hivi kumbe siku hizi roho inaweza nunuliwa bei rahisi hivyo.
 
joo wane karibu tukate ishu na tuendeshe nchi...

mimi ninao ushauri mmoja kwa muheshimiwa rais..katika juhudi za kurudisha hadhi ya idara ya mahakama kwa ajili ya rafiki yake ditto ...kitendo ambacho forum hii ilikijua tangu anakamatwa hasa BAADA ya rambi rambi yake na zilizofuatia kwenye msiba wa mbonde..werevu walishajua kuwa pale UHAI ULISHANUNULIWA...

Muungwana anatakiwa achukue hatua za haraka kuhakikisha wale nduggu zake ditto waliopiga waandishi mahakamani wanafikishwa mahakamani na kushitakiwa...

anatakiwa yeye binafsi alikemee hili suala....

hatua ya haraka ichukuliwe kuhakikisha suluhisho la kudumu la PP na CID na ikiwezekana hivi vitengo vipewe bajeti zaidi na vitendea kazi..

hii agalau itarudisha imani iliyopotea...
 
Hapo ndipo wakati mwingine huwa nakubaliana na wakenya kuwa sisi watanzania ni watu wa aina yake! Hii kesi ingechukua sura ingine kabisa kama ndugu wangeonesha kidogo tu kujali roho ya ndugu yao. Lakini hawa wamethamini sana zile ziara za wakubwa wa hapa duniani.

Inabidi turejee tena zile safari tujiulize hivi hawa walikuwa wanaenda kufanya nini kule Kawe kwa ndugu wa marehemu? Ni kutoa pole tu kweli? Kama ni pole tu mbona athari zake zimekuwa kubwa namna hii kwa ubinadamu wa hawa ndugu?
 
Kweli wadanganyika tupo tupo tu. Hivi hizo "ngo" za haki za binadamu zipo wapi zinashindwa hata kuaandaa maandamano ya amani kupinga dhamana hiyo na jinsi mazingira ya kesi ilivyoendeshwa ukizingatia kuna watuhumiwa wamekaa miaka 15 ndani. Si huwa nasikia kuna "ngo" za kwasaidia watuhumiwa/wafungwa au ndio zile zile za kuwasaidia waliozianzisha? Mpaka watuhumiwa/wafungwa wanagoma ndio watu tulio nje tunashtuka na kujitia tunawasapoti. Jamani wanadanganyika wenzangu tuamke tupiganie haki za wafungwa/watuhumiwa kwani magereza yapo kwa ajili ya binadamu wote huwezi kujua ni siku gani unaweza kuteleza ukajikuta upo ndani ya gereza
 
Joo wane
nakubaliana nawe kabisa . NGO zikijitokeza watakiona cha moto kama kile cha Hakielimu .

Lakini bado we need them to out.
 
hata kama ndugu wa marehemu watakaa kimya, tusife moyo, hii yaweza kusabiswa na uelewa mdogo wa mswala ya kisheria au sababu nyingine....

kesi inayomkabili dito haijafunguliwa na ndungu wa marehu bali ni Jamuhuri ya muungano vs Dito jamuhuri ni wewe na mimi.

jambo la msingi ni kuumuunga mkono Mtikila ili mashitaka yabadilishwe, ili dito kesi yake iwe ni kuua kwa kusudia
 
Joo wane,

Hata mimi nakusupport mzee, hizi NGO zinafanya kazi gani??

Mtu unakaa unasubiri kesi yako kwa muda wa miaka 15? duh!!! this is too much - wana haki ya kugoma
 
hivi mnajua ni kiasi gani serikali imekuwa karibu na familia ya Marehemu Mbonde? mtashangaa!!
 
Chakusikitisha baada ya miaka 15 ya kukaa mahabusu na miaka 4 ya kesi unaambiwa na jaji huna makosa upo huru. Duu umetumikia kifungo cha miaka 19 bila kosa uuuuuh ndio Tanzania hiyo nchi ya domokrasia na waumiani ( sorry demokrasia na amani)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…