Katibu Tarafa
JF-Expert Member
- Feb 16, 2007
- 989
- 54
Tarehe 3/14/2007
MWANANCHI HABARI
Polisi wamtetea Ditopile, mahabusu wazidi kugoma
Na Nora Damian
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, ametaja sababu za kuharakishwa kwa upelelezi wa kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri.
Manumba alitoa maelezo hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi hilo kufuatia mgomo wa mahabusu unaoendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Dodoma.
Mahabusu hao ambao mgomo wao unaonekana kuchochewa na kuachiwa kwa dhamana kwa Ditopile, wanadai upelelezi wa kesi zao unacheleweshwa kwa makusudi wakati ule unaohusu kesi za wakubwa kama Ditopile, unaharakishwa.
Akijibu maswali kuhusiana na madai ya Ditopile, kupendelewa na kuharakishiwa upelelezi, Manumba alisema katika kesi za namna hiyo ambapo mtuhumiwa anajisalimisha mwenyewe, inasaidia kuondoa ugumu wa upelelezi na hivyo kuwasadia polisi katika kukusanya ushahidi na hatimaye kesi hiyo kuharakishwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya mashahidi yaliyosomwa mahakamani Kisutu, Ditopile alijisalimisha kwa polisi na kuelezea tukio la mauaji lilivyotokea.
Manumba alipinga kuwa ucheleweshaji wa upelelezi katika baadhi ya kesi unategemea hadhi ya mtu.
Alisema mara nyingi ucheleweshaji au uharakishaji wa upelelezi, unategemea sana mazingira ya kosa lenyewe lilivyotendeka, upatikanaji wa haraka wa mtuhumiwa na vielelezo, vitu ambavyo alisema vinawarahisishia polisi kupata ushahidi wa kile kilichotokea.
Kwa mujibu wa Manumba, kesi inaweza kumalizika au kusikilizwa haraka au kuchelewa kutokana na mazingira ya jinsi kosa lilivyotendeka, tabia na mwenendo wa mshtakiwa kabla na baada ya kutenda kosa, mashahidi walioshuhudia kosa likitendeka na vielelezo vinavyohitajika kuthibitisha kosa.
Akizungumzia kuhusu baadhi ya mahabusu kupelekwa kwa makarandinga na baadhi yao kwenda kwa usafiri maalum, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, aliyeambatana na Manumba, alisema kuwa suala hilo linatokana na uzito wa kesi husika na mshitakiwa mwenyewe.
Mfano kesi ya Ditopile ile ina mvuto kwa jamii hivyo anapokwenda mahakamani lazima tuhakikishe yuko salama ili asije akadhuriwa kwa sababu akiwa mikononi mwetu, ikitokeo hilo, sisi tutakuwa hatuna kazi. Tulikuwa tunafanya vile kwa sababu ya usalama wake, alisema Tibaigana.
DCI alikiri kuwa baadhi ya madai ya mahabusu ni ya kweli kwa kuwa Jeshi la Polisi lina udhaifu katika kushughulikia upelelezi wa baadhi ya kesi kutokana na matatizo ya uhaba wa vitendea kazi na upungufu wa taaluma ya upelelezi katika jeshi hilo.
Mgomo huu wa mahabusu sisi kwa kweli umetusikitisha, matatizo ya upungufu wetu, nyenzo na taaluma ndani ya upelelezi yapo, hivyo kuna uwezekano mambo mengine pia yakachelewa, lakini si kwa kudhamiria, alisema Manumba.
Alisema tayari wameshawaagiza makamanda wa polisi wa mikoa kwa kushirikiana na mahakimu wa mikoa, mawakili wa serikali walioko katika kanda na maafisa magereza, waende magerezani ili kusikiliza madai ya mahabusu nchi nzima ili yaweze kushughulikiwa.
Alisema wameagiza ucheleweshaji wa upelelezi unaotokana na sababu zisizo za msingi, uchukuliwe hatua na kwamba mahakimu wameagizwa watathmini uwekwaji wa watu ndani kulingana na taratibu za kisheria.
Aliwataka mahabusu waliopo katika mgomo kusitisha mgomo huo huku madai yao yakishughulikiwa ili kesi zao ziendelee kama kawaida.
Tunaomba washitakiwa wetu watumie busara, waheshimu sheria za nchi na waendelee kuhudhuria mahakamani kwa sababu hiyo nayo ni haki yao na wajue kuwa kugoma ni njia nyingine ya kuendelea kuchelewesha kesi zao mahakamani, alisema Manumba.
Wakati huo huo, mgomo wa mahabusu wa kupinga kucheleweshewa kesi zao, jana uliingia siku ya tatu katika mahakama zote za jijini Dar es Salaam, siku ya pili Arusha na ukasambaa zaidi hadi Dodoma.
Mahabusu hao waligoma kushuka katika makarandinga yaliyowapeleka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama za wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala wakishinikiza tamko la serikali kuhusiana na madai yao.
Walisema hawatamsikiliza kiongozi yoyote wala makamanda wa polisi wa wilaya na mikoa isipokuwa wanataka tamko hilo litolewe na Waziri Mkuu, Waziri wa Sheria na Katiba,Waziri wa Usalama wa Raia au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mjini Arusha, maafisa wa juu wa mahakama mkoa wa Arusha, wakiongozwa na Jaji mfawidhi na mahakimu na maafisa wa polisi jana, walikwenda kukutana na mahabusu waliopo katika gereza kuu la Mkoa wa Arusha ili kupata ufumbuzi kwa mgomo wao uliongia siku ya pili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Matei Basilio, alithibitisha mahabusu hao kutokufikishwa
mahakamani jana na viongozi hao kuwafuata kuzungumza nao.
"Ni kweli leo mahabusu hawajafikishwa mahakamani, lakini kuna kikao cha kupata ufumbuzi kinachoendelea huko magereza kikiongozwa na Jaji Bwano mimi sikwenda ila maafisa wangu wapo huko,"alisema Kamanda Basilio bila kutaja kilichokubaliwa.
Mjini Dodoma nako iliripotiwa jana kuwa mahabusu waliopelekwa katika mahakama za Mwanzo, Wilaya na ile ya Hakimu Mkazi, nao waligoma kuteremka katika karandinga na kurejeshwa Gerezani la Isanga.
nb ,hii ndio ile hadithi ya kila siku fisi alipokuwa ana fuatia mkono wa binadamu akifikiri unakaribia kuanguka.wacha tuishi kwa matumaini