Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kisheria nchi yetu imekwisha haribika.Majambazi pia yanaua bila ya kudhamiria kwani wanafyatua na kusambaza risasi ovyo ovyo bila ya kulenga mtu maalum!
serekali ya awamu ya nne imeingia majaribuni kwa mara nyingine bila yenyewe kujijua , hili ni tukio la aina yake kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu tangia JK kuingia madarakani , sasa na sisi wenzetu tuna jiuliza itakuwaje kama itakuwa serikali imejivua nguo barabarani?
tusaidiane katika hili na tumsaidie JK na wafungwa wake......
Haki sawa kwa wote na sheria ni msumeno unakata huku na huku!
serekali ya awamu ya nne imeingia majaribuni kwa mara nyingine bila yenyewe kujijua , hili ni tukio la aina yake kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu tangia JK kuingia madarakani , sasa na sisi wenzetu tuna jiuliza itakuwaje kama itakuwa serikali imejivua nguo barabarani?
tusaidiane katika hili na tumsaidie JK na wafungwa wake......
Walikuwa na madai ya msingi kwanini awahukumu kwa kudharau mahakama!Leo majira ya saa tano asubuhi, wafungwa waliokuwa wameletwa kuendelea na kesi zao kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam walikataa katakata kushuka kwenye karandinga.
Karandinga zilikuwa mbili zikiwa na mahabusu wa Keko, Ukonga na Segerea, walipofikishwa mahakamani pale wakaamriwa kama kawaida washuke kwenye karandika ili waswekwe kwenye sero ya pale! Walikataa kwa kupiga kelele na kuimba kwamba hawashuki kwa sababu mahakama za Tanzania haziwatendei haki mahabusu na wafungwa. Aidha wamelalamika kesi zao kuchukua muda mrefu wakiwa wanaachwa rumamnde bila kupata dhamana.
Maaskari baada ya kuona jambo hilo limeanza kuleta mvuto wa ajabu kwa raia ambao walikuwa pale mahakamani kwa kuwasupport ilibidi defender isafishe njia na makarandinga hayo yakatokomea kurudi Keko, Ukonga na Segerea. Waliondoka wanimba wimbo wa "Parapanda ....... !
Kazi kweli kweli, nguvu ya mnyonge labda itaweza kuwaamsha walio katika usingizi wa fofofo!!
Binafsi naona wamefanya kitendo ambacho ni positive, na hata kama haki haitapatikana mapema ila ujumbe wao umefika.
Wasiwasi wangu ni je, wakija tena mahakamani hakimu anaweza kuwahukumu kwa kutoiheshimu mahakama? Ngoja tuone....
Kulikoni!Naam wengi wenu pia mnaangalia suala hili la kesi kishabiki sana.
Hapa kuna masuala mawili yapo as much related as they are different.
1.ditopile kaachiwa kwa dhamana baada ya mashtaka yake kubadilishwa.
Baadhi wanadai kwamba kwanini kesi yake inaenda spidi ukilinganisha na washtakiwa wengine wa kuua bila kukusudia, in fact wengine wana-argue kwamba kwanini mashtaka yabadilishwe?
HAPA MAJIBU NI KAMA IFUATAVYO:
Ditopile alipofanya kitendo ambacho mpaka sasa ameshtakiwa kwacho mahakamani, alifanya jitihada mwenyewe za kujisalimisha. Akakamatwa na pia aliamua mwenyewe kabla hajawahiwa kujiuzulu nafasi zake serikalini.
Then kakaa rumande mpaka hapo ilipoangaliwa mazingira ya kesi mashtaka yakabadilishwa na kuwa kuua bila kukusudia, ni jambo ambalo unastahili kupata dhamana, kafuata masharti ya dhamana na kutolewa.
Kwa nini Kesi yake inaenda haraka sana:
Kuna kesi ambazo mazingira ya tukio na participation ya mshtakiwa yanapelekea kesi hizo kuendeshwa haraka, hili halina shaka.
Iwapo kesi ya Ditto ingepangwa kusikilizwa mwisho wa mwaka huu wengi humu mngehoji KULIKONI? lakini mwenye katoa ushirikiano wa kutosha kwa waendesha mashtaka na pia mazingira yake yalikuwa ni rahisi kupatikana ushahidi unaotakiwa kuendesha kesi hivyo ndio maana mashtaka yamechukua kile kinachoonekana haraka kuliko wengine.
Kwa Nini kesi nyingine zinachukua muda nk
Hili nalo ni jambo linashughulikiwa na serikali kwa kushirikiana na mamlaka husika. Kulikuwa na msongamano wa kesi kwa vile majaji wachache, Kikwete kateua majaji lukuki kwa uwezo na kesi zitaanza kupungua soon.
Hakuna anaewekwa kwa muda zaidi ya mazingira yalivyo, kuna kitu kwenye judiciary tunaita CASE FLOW MANAGEMENT committee nayo ni kamati inaongozwa na jaji kuangalia uendeshaji wa kesi, mashtaka na treatmend ya remandees nk na kwa dar yalipotokea masaibu haya kamati ilikwishapitia kesi zote na kutoa maelekezo ya waliotakiwa kushughulikiwa nk na hatua zinaendelea.
Of course mahabusu kugoma katika karandinga is a sorry state which should n't have taken place lakini sisi sio kama zimbabwe hatukuwapiga watu hawa kwa kugoma bali mahakimu na wadau wengine walikwenda na kusema nao na makubaliano yamefikiwa tayari.
Nimearifiwa hivi punde kwamba Arusha kesi zinaanza rasmi kusikilizwa jumatatu baada ya mahakimu kuongea na mahabusu na kufikia muafaka.
Hapa hamna budi ku-appreciate hatua za kiungwana tulizochukua kabla ya kushambulia,
Our judiciary needs changes, everyone agrees that lakini hilo sio kosa la establishment ni sehemu ya our continous efforts to make things better...
Ninyi mnakalia tu ooh wameanza wenyewe wataipata safari hii nk....
Fuatiliani mambo with a neutral eye ndio mtoe analysis sio mtoe conclusion ndio mfuatilie mambo, hiyo inakuwa bias!
Kulikoni judiciary wanahusika vipi na kutafuta ushahidi na kuendesha kesi?
Kulikoni!Of course you are right on that lakini huna budi kukumbuka kwamba tunahitaji masuala mengi kubadilika.
Waiting lists ni jambo linalosumbua wengi katika sekta mbali mbali kwa kukosa masuala mengi, uzito wa makosa unahitaji kupimwa.
This has nothing to do with government, wasiliana na JUDICIARY mimi nilikupa yale ambayo serikali inafanya kurekebisha tatizo kwenye eneo linalotuhusu.
MKJJ
Kama mtu kweli amekaa miaka sita na ushahidi bado basi hakimu/jaji ana uwezo wa kufuta hiyo kesi ikiwa kila siku ikienda mahakamani inapigwa tarehe na prosecutors.
Ikiwa haijakwenda mahakamani wapitia majalada na kucross check na wafungwa i.e. CASEFLOW MANAGEMENT COMMITTEE basi majaji ndio wadau hasa husika ambao wanaweza kumshauri DPP kuwa kesi hii imeshakosac merit ifutwe nk...
I hope you get my point.
Tatizo lililokuwepo awali ni kuwa majaji walikuwa wachache na watendaji wa kisheria, majaji tumeteua wengi tu sasa ama kuhusu wanasheria ni vigumu serikali kuintervene quickly enough kwani huwezi kuteua mwanasheria ni jitihada za wananchi tumesawasaidia kwa kuanzisha vyuo extra lakini safari ni ndefu sana...
Hivi unajua kwamba tanzania tuna less than 1000 qualified advocates? my last count was december 2005 na tulikuwa na 735 lawyers in total...