Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Wababodi,
Kidogo mwenzenu nimelewa hapa. Hiyo section 201 ambayo wanaitumia imeeleza vizuri visa ambavyo vinaambatana na provocation ktk section hiyo 203. Mwenzenu hapa sioni kitu kinacholingana wala kufanana na kisa cha DPP.
Ama ndio lugha tena inanipiga chenga?
 
Mkandara, ndio maana nilitaka kuhakikisha kuwa lugha hii siyo ngumu kama wanavyotutaka tuamini. Labda kama Bw. Mwendapole anasheria nyingine ndogo ndogo. Ila kama ni Kiingereza hiki hiki cha malkia (Queen's English) DPP itabidi atanue sana maana ya hivyo vipengele.. but then he'll be doing some real work..!
 
Now here is the kicker... did the accused (Dito) know that by him holding a gun, putting a finger on the trigger and fire it towards the deceased that his action would "probably cause the death" of that individual? The answer is an affirmative yes! because there is no way on earth that a loaded gun fired toward a person would "probably" not cause death!!!

According to this section, was Ditopile provoked? absolutely NOT for there was no such a relationship between him and Hassan that could have been interpreted as "immediate care" or "conjugal, parental, filial, or fraternal relation, or relation of master or servant". He (Hassan) was a total stranger to Ditopile and he to him.

Section 203 does not apply in this case.

The answer is NOT an affirmative yes! because it depends on where or on what part of the human body the loaded gun is pointed or fired at. Firing on the head is almost always going to kill but not the legs, arms, or shoulders. Another question that is not clear to me is whether Ditto fired his weapon at point-blank or not. What was the distance between him and the victim?
 
Mkandara, ndio maana nilitaka kuhakikisha kuwa lugha hii siyo ngumu kama wanavyotutaka tuamini. Labda kama Bw. Mwendapole anasheria nyingine ndogo ndogo. Ila kama ni Kiingereza hiki hiki cha malkia (Queen's English) DPP itabidi atanue sana maana ya hivyo vipengele.. but then he'll be doing some real work..!


Jeez! aint I treading on dangerous grounds here!
Am not trying to teach law, I dont even qualify for that, but I know that it takes 3-4 years of college to be able to interprete the law; thats why the judiciary is there for the sole purpose of interpreting the law- the law which is enacted by the parliament!
So my brothers, law is not read as plainly as a novel, its not a question of plain queen's english..it is a question of legal language..thats why it is couched the way it is...A law professor can break one paragraph there to make a subject for discussion for one whole week in his class..
What I did was just to show what the law is in this case.
I also added that there is caselaw..it is as important as the statutory law

And yes, there are other laws, i wont call them sheria ndogondogo,
they are also applicable..like The Law of Evidence- this will govern the issues of conduct, circumstances, the provocative words uttered etc...there is also The Criminal Procedure. Act..it is the one that provides for the powers of the DPP to control criminal proceedings...


Plus, there is the evidence itself... and lets not forget the judge himself..his way of interpreting the law...his ability and competency in assessing and evaluating the evidence...[should we include impartiality?]

Kwa kifupi ndugu zangu, najaribu kuwa-prepare for the eventuality..nionavyo mimi, kama hayo aliyosema Kaduma ndivyo alivyo, na kwa kuzingatia sheria kama ilivyo, na kwa kukumbuka kesi za namna hiyo zilizokwisha amuliwa,
I can bet..uamuzi wa mahakama utakuwa hivi

"...the evidence in its totality proves beyond any reasonable
doubt that the accused person had no malice aforethought;
..that he words uttered by the victim as well as his conduct, were
such that, any reasonable person in the position of the accused
would react the same way; that is to say, the accused was
provoked...
This court therefore finds the accused..Ditopile guilty of
manslaughter as charged."

Sentence
"...considering the age of the accused, the period he has stayed
in custody, his ill-health..and the undisputed fact that he has always
been a law-abiding citizen...and the fact that he has spent the
best part of his life serving the country in various govt posts,
I sentence him to twelve months conditional discharge.."

And, he will sign some stupid papers promising to behave himself within the twelve months, and go home flanked by green shirts & khangas bearing the words 'CCM nambari one'

Wanna bet?
 
Hii nayo imekaa vipi?

Mahakama yamwachia kigogo aliyejeruhi kwa risasi


Written by Irene Mark, Tanzania Daima
Thursday, 15 February 2007


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Diotraphes Mmary (6, aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za kujeruhi kwa risasi.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Neema Chusy, alisema mtuhumiwa huyo mkazi wa Masaki, ameachiwa huru chini ya kifungu cha 98 cha sheria za kanuni ya adhabu (CPA), baada ya majeruhi kuiomba mahakama kufanya hivyo.

Kabla ya kuachiwa kwa mtuhumiwa huyo, ilidaiwa na Inspekta Msaidizi wa Polisi, Maximillian Birigi, kuwa Oktoba 5 mwaka jana, eneo la Mbezi Juu, wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa alimpiga risasi ya mguu Benedct Valerian na kumsababishia majeraha.

Katika maelezo ya mlalamikaji, ilidaiwa kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alimpiga ngumi ya sikio, kumnyooshea bastola kichwani, kumtolea maneno ya vitisho na kumpiga risasi ya mguuni.

Maelezo hayo yanaonyesha kuwa siku hiyo mlalamikaji alikuwa na wenzake wakichota mchanga eneo hilo ndipo mtuhumiwa alipoamuru kazi hiyo isitishwe na kuanza kutoa vitisho kwa waliokuwapo eneo la tukio.

http://jambotanzania.net/v2/content/view/1047/2/
 
Duh!! ama kweli Tanzania yetu . Sijui bwana ila ninakata tamaa kila kukicha .
 
surely Mwendapole, i wouldn't even dare to bet...............when CCM is influencing....................ooohh no poor driver!!..............
 
Mwendapole, I won't take you on that bet... the cards are on your favor... binafsi sina tatizo which way the court gonna rule.. I hope that precedence ambayo wanaanzisha au wanafuata itakuwa inatumika hata pale mmachinga anapotukanwa na Mkuu wa Wilaya na kuchomoa bastola na kumlipua papo kwa papo!!
 
Mwanakijiji,
naungana na wewe kuonya kuhusu precedence itakayotokana na uamuzi wa DPP, pamoja na hukumu itakayotolewa. kesi hii inaweza kuwa na athari mbaya sana ktk mwenendo mzima wa uendeshaji mashtaka tanzania.

kinachonitatiza vilevile ni mwenendo mzima wa DPP pamoja na kauli zake. Kwa kweli DPP ana-act utafikiri ni wakili wa utetezi. DPP amejitwisha uwakili wa utetezi na amechomoka na kesi hii. Huo ndiyo mtizamo wangu kama mwananchi wa kawaida.

Ili haki ionekane ikitendeka, naamini DPP alipaswa kumshitaki Ditopile kwa kosa la kuua. Hata kama mashahidi wa kuthibitisha hilo hakuna, angeachia suala hilo lionekane mbele ya mahakama, na liibuliwe na mawakili wa upande wa utetezi.
 
well said, hivyo ndivyo na mimi nilifikiri.. lakini sasa kafanya kazi ya utetezi kuwa rahisi kweli...
 
Mwendapole nakubaliana nawe,na naamini ndivyoitakavyokuwa.

Mwanakijiji usisahau mnonge hana haki.Kwa machinga mambo hayawezi kuwa kama unavyotumaini.
 
Uhuru 2/16/2007

KONDAKTA Thomas Mwita aliyeshuhudia kifo cha dereva wake, amedai kuwa mshitakiwa Ditopile Mzuzuri (58), aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, alimzaba vibao na kumtishia kwa bastola dereva wa akiba kabla ya kumuua Hassan Mbonde.Mbali na Mwita abiria aliyekuwa amekaa kiti cha mbele katika basi hilo, Masasi Luenge, alidai Ditopile alimtishia kumpiga risasi na kumtukana baada ya kumueleza aache kumuamuru dereva Mbonde ashuke chini.
Kauli hizo ni maelezo ya mashahidi wa upande wa mashitaka yaliyosomwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Michael Luguru aliyesikiliza maelezo ya mashahidi hao 24 yatakayotumika katika kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa Mahakama Kuu.
Akisoma maelezo ya Mwita, Mwendesha mashitaka Gilvanus Muhume alidai Luenge alizambwa vibao baada ya kushuka kuangalia jinsi gari la Ditopile lilivyoharibika baada ya ajali hiyo.
" Aliposhuka alikutana na mshitakiwa (Ditopile) aliyemuuliza unafanya nini, ambapo Luenge alimjibu 'samahani mzee naangalia tulipo gonga' ghafla Ditopile alimzaba vibao na kumuamuru aondoke huku akimuonyeshea bastola kichwani," alidai Mwita katika maelezo yake.
Mwita ambaye ni kondakta wa daladala hilo lenye namba za usajili T 816 AGT, alidai siku ya tukio walikuwa wakielekea Tegeta saa moja usiku njia panda ya Kawe, wakati wakiwa kwenye foleni lilikuja gari aina ya Prado ambalo lilienda 'kuchomekea' ghafla mbele ya gari yao, ambapo kwa bahati mbaya gari lao liligonga tairi ya akiba iliyokuwa nyuma ya gari.
Alidai baada ya kuona mwenzake amenyooshewa bastola, aliondoka na kuingia ndani ya gari, huku Ditopile akizunguka dirisha alilokuwa amekaa dereva na kumlazimisha ashuke.
Mwita alidai Mbonde alimjibu: "Samahani mzee siwezi kushuka kwa kuwa gari lipo kwenye kilima na breki siyo nzuri hivyo nitaua abiria."Kwa mujibu ya maelezo ya Mwita, baada ya marehemu kujibu hivyo, Ditopile alimwambia kuwa anajali abiria kuliko gari lake na kumlazimisha asishuke ambapo alipandisha vioo na 'kuloki' mlango wake.
Ditopile baada ya kuona hivyo 'alikoki' bastola na kumfyatulia dereva Mbonde risasi mbili za kichwa.
Alidai baada ya kumpiga risasi, abiria walianza kulia huku wakipiga kelele kuwa ameua ndipo mshitakiwa alipoingia na kumgusa dereva huyo.
Mwita alidai abiria walianza kumzonga huku yeye akimshika kwa nguvu asitoroke kwa ajili ya kumpeleka polisi.
Alidai wakati wakimzuia, alitokea dereva wa Ditopile ambaye naye alichomoa bastola na kuwanyooshea huku akiwakataza kumshika bosi wake na hivyo kufanikiwa kuondoka naye katika eneo la tukio. Shahidi Masasi Luenge ambaye alikuwa abiria katika daladala hilo, alidai dereva wa Ditopile ndiye 'aliyechomekea' na kusababisha ajali hiyo.
Luenga ambaye alikuwa amekaa kiti cha mbele alidai baada ya marehemu kupigwa risasi alimuangukia na kufa papo hapo.
Alidai kabla ya kushambuliwa, marehemu alimuomba msamaha na kueleza sababu za kutoshuka.
Hata hivyo, alidai Ditopile alimtukana na kumuelekezea bastola.Kwa upande wake, dereva wa akiba katika daladala hiyo, Edward Girvas ambaye siku hiyo alikuwa kama kondakta, alidai alitishiwa kupigwa risasi ya kichwa na Ditopile, baada ya kushuka na kumuomba msamaha wakati marehemu alipogonga gari lao.
Alidai mshitakiwa kabla ya kumonyeshea bastola alimpiga vibao na kumtaka aondoke haraka.
Shahidi mwingine aliyetoa maelezo yake mahakamani hapo ni daktari Mgaya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, na kuthibitisha kuwa marehemu aliuawa kwa kupigwa risasi mbili.Alidai risasi hizo zilipitia upande wa kulia na kutokea kushoto na kwamba kipande cha risasi kilibaki katika kichwa cha marehemu.
Kamishna msaidizi wa polisi, Abdallah Mssika, katika maelezo yake alidai Ditopile alimueleza kwamba hakudhamiria kumuua dereva Mbonde, lakini bastola aliyokuwa akimtishia ilifyatuka na kusababisha mauaji hayo.
Akisoma maelezo ya shahidi huyo (Mssika), aliyemhoji Ditopile, Muhume alidai katika maelezo hayo, mshitakiwa alimueleza kuwa
hakuwa na nia ya kufyatua risasi bali alishtukia risasi zimetoka zenyewe baada kugonga dirisha.
Kulingana na Ditopile, hali hiyo ilisababishwa na bastola hiyo ambayo ni 'Automatic'.
Alidai kitendo cha yeye kutoa bastola hiyo, kilitokana na marehemu (dereva) kumsonya(matusi makali yaliyomfanya apoteze uwezo wa kujitawala - Mwanakijiji) na kugoma kushuka, baada ya kumgonga huku kondakta wa akiba akimtamkia maneno kwamba 'mzee hiyo ndiyo imetoka' matamshi aliyoyaona ni dharau kwake.
Mssika aliendelea kudai katika maelezo hayo kuwa Ditopile, baada ya kugundua risasi imefyatuka, aliamua kutoa risasi zote katika bastola yake ili isilete madhara zaidi.
Alidai baada ya kuhakikisha bastola yake iko salama, aliingia ndani ya basi hilo kuangalia jinsi dereva alivyoumia ili aweze kumsaidia ikiwa ni pamoja na kumpeleka hospitali.
Mssika alidai katika maelezo yake kwamba, Ditopile hakupata ushirikiano kutoka kwa abiria na badala yake walianza kumzonga na kumuambia 'umeua mwenyewe na umbebe kumpeleka hospitali' huku wengine wakimpiga.
Alidai katika kujiokoa kondakta wa gari hilo, alichukua chuma na kutaka kumpiga kichwani, lakini mshitakiwa alifanikiwa kukinga kwa kutumia mkono wake.
Kutokana na hilo, mshitakiwa alilazimika kukimbia huku akipiga kelele kuomba msadaa kutoka kwa dereva wake.
Mssika alidai kabla ya kuchukua maelezo ya Ditopile, mshitakiwa alimpigia simu kwa lengo la kutaka kujisalimisha na kumueleza juu ya tukio hilo.
Kamanda Mssika alidai baada ya kujisalimisha alichukua maelezo yake mbele ya wakili wake Ringo Tenga.
Akisoma maelezo ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, Mwendesha mashitaka Naima Mwanga alidai Tibaigana alieleza kushangazwa kumuona mshitakiwa akifika nyumbani kwake usiku wa manane akiwa na Mssika.
Naima alidai Kamanda Tibaigana alimkaribisha Ditopile kwa kumueleza 'Karibu Mheshimiwa na yeye alijibu kuwa mimi siyo mheshimiwa tena bali ni muuaji' na kuanza kumsimulia tukio hilo na kusisitiza kuwa hakuwa na nia ya kufanya hivyo.
Tibaigana alidai kuwa lalamiko kubwa la Ditopile ni kitendo cha dereva (marehemu) kumtukana na kukaidi kushuka ili waweze kufikia makubaliano.
Mbali na maelezo ya mashahidi hao, pia upande wa mashitaka utawasilisha vielelezo vitano ikiwemo taarifa ya daktari, maelezo ya ungamo la mshitakiwa, taarifa ya uchunguzi wa ripoti ya mlio wa risasi, ramani ya eneo la tukio na fomu ya gwaride la utambulisho.
Hata hivyo, upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili Nimrod Mkono, uliomba dhamana kwa mteja wao, na kumueleza hakimu kuwa ana uwezo wa kutoa dhamana ingawa hana mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hata hivyo Hakimu Lugulu alikataa kusikiliza ombi hilo na kuwataka kuliwasilisha Mahakama Kuu.
Ditopile ambaye jana alikuwa akiendeleza mtindo wake wa kuingia mahakamani huku akiwa amevaa 'pama' kuficha uso jana alisomewa shitaka jipya la kuuawa bila kukusudia.
Katika shitaka hilo, anadaiwa kuwa Novemba 4, mwaka jana, njia Panda ya Kawe na Bagamoyo alimuua bila kukusudia Hassan Mbonde.
Awali, alishitakiwa kwa kosa la mauaji kabla ya kubadilishiwa shitaka hilo na Mkurugenzi wa Mashitaka mwishoni mwa Januari.


hapa patamu
 
Patamu si mchezo. Ukisikia watu "kukojolea taaluma zao" ni kwenye hii kesi.
 
yaani, kama ushahidi wa konda na dereva wa akiba haukuweza kumfanya DPP kuendelea na mashtaka ya awali.. basi I quit!!
 
Lini nasi tutaanza kuheshimu maadili ya taaluma na utaalamu wetu badala ya kulinda cheo? Yaani hapa huhitaji hata chembe ya taaluma ya sheria kujua kuwa haki inapindishwa! Hivi akuna moral obligation kwa upande wa mawakili wa utetezi kiasi kwamba wanaweza kupindisha sheria kiasi hicho?
 
Nilipojenga hoja mwanzoni kuhusu "kusudio" la mtuhumiwa nilitilia mkazo sana suala la bastola, kifyatushi, na kulenga marehemu... sikujua maneno hayo ya mashahidi... but now I'm more convinced than ever that Dito alimchabanga risasi ili kumpa fundisho! Unfortunately, hatujui kama marehemu alilipata fundisho hilo au la!!! Na kwa mara ya kwanza tunasikia dereva wa Dito naye alikuwa na bastola na aliitoa hadharani!!....na katika maelezo hayo yote hatuambiwi kama bastola ilipotea isipokuwa Dito "alitoa risasi zilizobakia"....
 
Huyo jamaa kishapitishwa kuwa DPP mpya au anadhani akimsaidia mheshimiwa basi ataula kiulaini?
 
Jamani hivi vikundi vya Wanasheria na NGO vinafanya nini au navyo vimeshavamiwa na Mtandao.

Swala la msingi hapa ni: Je DPP anaweza kubadilisha kesi au mahakama ndiyo hupitia ushahidi na utetezi wa kosa na kuamua na kutoa hukumu.

Huyu DPP anataka kusema mimi nikimshitaki mtu kwa kuniibia, yeye anaweza kuabdili shitaka na kuwa mimi ndiye niliyeiba.

Nadhani ndiyo maana wakati mwingine nadhani "MOB JUSTICE is BETTER than our JUSTICE SYSTEM"

Nadhani wananchi wamepewa ushauri tosha kabisa kuwa "mwenye kosa aadhibiwe papo hapo" kwani kumpeleka polisi ni kupoteza muda na unaweza kugeuziwa kesi bure"

Wangetakiwa wa"Dito" pale pale kama vibaka wanavyofanyiwa.
 
Aljazeera.. the answer to your hypothetical question.. "mimi nikimshitaki mtu kwa kuniibia, yeye anaweza kuabdili shitaka na kuwa mimi ndiye niliyeiba." ni NDIYO! at least anaweza hata kuifuta hiyo kesi yako au kupunguza mashtaka unayotaka kushitaki!!
 
Back
Top Bottom