Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Nafikiri Mzee P, umenena kuwa huyu mzee anahitaji kuwa defense lawyer wa Blaza Dito,

Sasa vipi watuhumiwa wote wakiamriwa na daktari kwenda kukaaa HOTELINI?
Hiii Saloon ni ya nani na inamota toka wapi na kumrudisha wapi? Rais anawezaje kutoa msaada tu kwa familia ya marehemu bila ku-condemn kitendo kilichosababisha kifo cha huyo marehemu?

Hakuna raia waliomvamia mshitakiwa maana tunajua kuwa wananchi wote walitimka na kukimbia baada ya dereva kupigwa risasi, sasa bastola iko wapi?

Viongozi hawakwenda siku ya mazishi walikuwa wanaogopa nini? Kamam nji yetu ingekuwa haina historia ya ujanja wasingeogopa, wameogopa kwa sababu baada ya kifo hawakusema kitu, kwa sababu rais alikuwa hajasema kitu, mbona viongozi wa upinzani hawakupigwa na walikuwepo?

Mzee Moshi ninajua kuwa wewe ni mzee wa mahesabu, hii siasa na sheria ya
bongo bro, ni mazingaombwe ambayo sisi tunayafahamu, tuna historia ya watoto wa RUPIA, KINGUNGE, na juzi MUNGAI, hii naona hukuigusa hii, naona huuu sio upande wako bro, tusichotaka ni hayo mazingaombwe kurudiwa tena, na tayari tumeshaona hapa mazingara yanatayarishwa ya kucheza hayo mazingaombwe,

logic zako ni safi lakini kwa nji za huko majuu sio bongo, huko bongo hizo logic ziliacha kufanya kazi siku nyingi sanaa, na wewe unaelewa kuwa ni bongo tu ambako bajeti ya matumizi ya furniture ya ofisi wa waziri mkuu, ni makubwa kuliko bajeti nzima ya elimu!

Kwa hiyo tutaendelea tu kukataa mazingaombwe kwenye hii kesi, mpaka marehemu apatiwe haki kisheria, halafu hata kama ni msaada shilingi laki tano ni ndogo sana!
 
Augustine,

Maelezo yako yote ni ya kufikirika na hayana ukweli wowote ingawa yanaonekana kama ni sahihi:

(1) Mimi nilivyokuwa nimesoma gazetini nilikuwa nimeelewa kuwa hakimu alikataa kuwa mtuhumiwa atatibiwa chini ya utaratibu uliopo kuhusu watuhumiwa na wafungwa. Endapo baadaye ilikuja badilika na hakimu akakubali mtuhumiwa apelekwe kwa daktari kama raia huru ni kinyume cha taratibu. Mahabusu pamoja na wafungwa wote hupata matibabu yao chini ya ulinzi. Daktari hawezi kuamuru mtuhumiwa (au mfungwa) akapumzike nyumbani kwake au hotelini kama unavyosema; ni lazima mtuhumiwa aendelee kusimamiwa na vyombo vya dola akiwa amefungwa pingu hata kama atafanyiwa operation kubwa.

(2) Kitendo cha silaha kupotea na jeraha dogo alilokuwa nalo mkononi bwana Dito bado ni kitendwaili. Kwa vile alikwa na silaha iliyokuwa na risasi na alikuwa ameshaua mtu, si rahisi watu kumsogelea. Nilishawahi kuinonja hali hiyo wakati majambazi yalipoingia kwenye baa moja pale Sinza na kufyatua risasi angani halafu yakatuamuru wote tulale chini. Hakuna aliyefurukuta, tuliyaacha yakatatuchukulia viatu saa na pochi zetu kilaini. Kudai kuwa watu walimshambulia ni hadithi isiyokuwa ya kweli ingawa ni hadidhi inayoweza kumsaidia katika utetezi wake. Kumbuka kuwa wanachi wenye hasira pale Dar es Salaama wakiamua kujichukulia sheria huwa wanaua kabisa. Kama wangemnyang'anya ile bunduki ni dhaihiri kuwa wangemfyatulia risasi pia. Hata kwa kipigo tu, bwana Dito hangekuwa hai kwa sasa hivi.


(3) Rais aliye makini hawezi kutumia njia za kinafiki kama kupeleka mchango na kujitanganza kwa ajili ya cheap political points kama unvyoashiria. Jambo la muhimu alilotakiwa kulifanya wakati huo ilikuwa ni kumvua madaraka kwa muda (suspend) mara moja mtuhumiwa hata bila kumsubiri ajiuzulu. Kwa vile ukuu wa mkoa ni madaraka ya kuteuliwa na rais, hakukuwa na haja kwa rais kusubiri Dito ajiuzulu wakati yuko chini ya polisi. Angemsimamsiha kwa muda hadi hapo mahakama itakapoamua hatima yake. Endapo mahakama ingemkuta Dito hana hatia basi rais angekuwa na uhuru wa kumrudisha madarakani bila swali.

(4) Kwa serikali inayowajibika kwa wananchi wake haiwezi kutumia pesa za walipa kodi wake kulipia gharama zitokanazo na makosa ya mtu binafsi hata kama ni kiongozi wa serikali. Angalia mfano Rais Bill Clinton ambaye hadi leo bado analipa gharama za mawakili wake binafsi waliomtetea katika kesi yake ya ngono ingawa katika impeachment proceedings hakukutwa na hatia.

Kwa jumla katika bajeti ya serikali yetu hakuna fungu la kulipia gharama za namna hiyo.

(5) Viongozi wa serikali kutofika kwenye mazishi haikuwa kwa sababu ya usalama kama unavyodai, ni kwa vile walikuwa consummed na future ya mwenzao. Watanzania siyo watu wa fujo kama unavyotaka kuonyesha kuwa kama viongozi wangefika pale wangepigwa au kuumizwa. Katika mazishi yale alikuwepo mkuu wa Polisi wa wilaya ya Kinondoni ambaye aliruhusu magari mawili ya polisi kusaidia katika mazishi yale. Kamanda yule eliheshimiwa sana na waliokuwapo na baadaye alitoa hotuba kuwaomba wanachi watulie wakati sheria inachukua mkondo wake na walimsikiliza. Je huyu hakuwa kiongozi wa serikali? Hiyo unayozungumza ya vurugu na wanajeshi ilikuwa ni barabarani ambako wapiga debe walikuwa wakiomba michango kutoka kwa wapita njia. Kama bwana Luhanjo angefika na kutoa hizo Shs 500,000 za ubani pamoja na kueleza msimamo wa serikali kuhusu Bwana Dito, mambo yangekuwa tofauti.

Kumbuka kuwa mazishi yalifanyika siku ambayo Dito alifikishwa mahakamani ikiwa ni siku mbili tangu mauaji yafanyike. Dito alijiuzulu madaraka yake baada ya kutolewa hapo mahakamani ambapo Rais alitanganza kukubali kujiuzulu kwa Dito kesho yake, halafu ubani wa Rais umepelekwa baada ya siku kama mbili/tatu/nne hivi tangu Dito ajiuzulu. Hiyo timeline inaonyesha lapses nyingi sana katika maamuzi ya rais na wasaidizi wake kuhusu swala hili.
 
Ajabu zaidi mwenzetu kisha toa hukumu kuwa familia ya marehemu itunzwe na kusomeshwa hadi chuo kikuu kama vile haijui Bongo!...

Mchango wa fedha za ubani kwa marehemu hazikutolewa kwa sababu ya uchungu ama samahani ila political motivated!... wapinzani waliisha livalia njuga swala hili na ktk kuuzima moto, CCM wameona nao wajiunge ili kuondoa moto na hakika mzee baba wa marehemu kesha anza kusema ni - Kazi ya Mungu. Imani potofu ambayo mimi kamwe sintakubaliana nayo kwani nafasi ya Shetani inasimama wapi ktk swala hili?...
 
Mzee Kichuguuu,

Wewe ni kukuwekea fomu ya ubunge tu bro!!, maana wewe huko bongo hakuna kazi yoyote unaweza fanya zaidi ya ubunge! Damn!!!!!!!!
 
Kichuguu,
Well said. Mzee ES, mimi nilitaka kumpa kazi ya uwakili. Lakini ubunge ni sahihi zaidi.
 
Notice: Jamani nitawajia na taarifa za jinsi gani tunaweza kuisaidia familia hiyo hata kesho jioni.. kuna mtu nataka niwasiliane naje (mtu anayeheshimika sana kwenye jamii):

Kuna mambo kadhaa ya kuangalia:

a. Hii kesi iko mahakamani na tumeambiwa tusimhukumu Dito. Kitendo cha Rais kumtuma Katibu, na kitendo cha viongozi wa serikali kwenda kutoa rambirambi huko, ni kitendo cha kuonesha kukiri kuwa aliyemuua Hassan ni kiongozi wa serikali na kwa kufanya hivyo, ni wao wanaotoa hukumu (kwa matendo yao) kuwa Dito anawajibika kwa kifo cha kijana huyo. Wakati mwandishi wa The East African alipouawa ni wangapi walisikia serikali na viongozi wa serikali walijipanga mstari kwenda kutoa pole? Inawezekana walienda kule kama mtu binafsi, lakini vyombo vya habari havikuzipa uzito rambi rambi hizo kwa vile aliyemuua alikuwa hajulikani. Ni kujidanganya kuwa viongozi hawa wanatoa rambi rambi kwa vile kijana aliuawa!! Wanatoa rambirambi na wanatoa ahadi za kuisaidia familia hiyo kwa sababu anayetuhumiwa kuuwa ni kiongozi mwenzao!!! Kama anayetuhumiwa angekuwa Filipo wa Gongo La Mboto, mnadhani viongozi hao wangetokea kwa mzee Mbonde?

b. Kinachotolewa siyo rambirambi tu kama wengi wanataka tuamini. Hivi kesi ya Dito ikifika kutolewa hukumu na mzee akaambiwa aseme maneno machache, unadhani kweli atataka jamaa apewe adhabu kali akikumbuka misaada toka kwa Rais (rafiki wa mtuhumiwa) na viongozi wengine ambao wako tayari kuisaidia familia? Hizi rambirambi lengo lake si kufanya tukio zima kuwa ni "ajali" na "mapenzi ya Mungu", badala ya kuliita kwa jina lake "mauaji ya kinyama"? Je kwa viongozi kujitangaza kwenda kutoa rambirambi na pole lengo siyo kupindisha maoni ya watu juu ya Dito na kwa namna fulani kuinfluence mchakato wa upatikanaji wa haki?

Mlingano wa Mob justice na kitendo anachotuhumiwa Dito:

1: MJ na KAD vinatokana na hisia kuwa kibaka na yule dereva ni kero (nuissance) kwa jamii hivyo wanastahili adhabu ya papo kwa papo.

2: MJ na KAD vinamfanya mtu aliyedhurika na kitendo chao (aliyeibiwa na Dito) kuona kuwa jambo dogo ni kubwa!! Aliyeibiwa shilingi mia mbili na aliyegongewa gari lake, vitendo hivyo viwili ni vikubwa mno, ingawa kwa mtu mwenye mawazo sawa, shilingi mia mbili na taa za gari ni vitu vidogo ukilinganisha na maisha ya mtu!

3: MJ na KAD vinawafanya walioridhika kudhani kuwa wakienda polisi au wakifuata taratibu za kisheria itachukua muda, hivyo kwa vile wanajua aliyewadhuru (kibaka kwenye MJ, na Hassan kwenye KAD) basi ni bora wachukue sheria mikononi mwao. Katika vitendo vyote viwili hisia ya kuwa vyombo vya sheria viko mbali inatawala. Hata hivyo mara nyingi polisi hawako mbali kwani mara nyingi hufika kwenye tukio dk chache mtu akishakufa!!!

4: Kwa wale waliodhurika na vitendo vya vibaka na dereva, kwao adhabu ndogo haistahili (kumpeleka mtu polisi akalipa faini na kifungo maybe cha miezi mitatu) kwa wakosaji. Kwao adhabu kubwa zaidi ni ya lazima na ni fundisho kwa watu wengine. Adhabu kwa wakosaji ni kifo!!! watu mtaani watamchoma mtu na kaka Dito anatuhumiwa kumlipua mtu!!

Hivyo Moelex, kuzungumzia suala la tuhuma dhidi ya Dito ni mfano dhahiri wa Mob justice!! Je tofauti kati ya MJ na TAD ni nini!!!?

Tofauti ni kuwa kwenye Mob Justice watuhumiwa wanaotoa adhabu hiyo ni wengi na hawajulikani! Katika kesi dhidi ya Ka' Dito mtuhumiwa ni mmoja na anajulikana!! Kwa bahati mbaya (au nzuri kwa upande wake) yeye ni rafiki wa karibu wa Rais!!!!!!

So, lets talk about both situations if you get my drift
 
ES na Jasusi,

Kazi za ubunge na uwakili siziwezi, mimi ni kichuguu tu. Ila kazi ya kutoa machozi nikililia amani na haki ninaziweza sana hasa pale inapoonekana wazi kuwa kanuni hizo zinavurungwa au zinaelekea kuvurugwa.
 
Haya Mzee Bob,

EL anakuja huko next week kula naye sahani moja akifanya mkutano wa bongo!,

Mzeee Kichuguuuuu,

Wewe ni Mlima bro, kile kichuguu chenye kumbi kumbi hakikufai bro I am impressed bro, wewe ukifika ma-bongo nishtue maana damn!!!!!!!!, huko bungeni bro kuna watu fulani kazi ni kulala tu na kukoroma mle, na kutuma vikaratasi vya matusi tu,

tunahitaji watu walio macho na makini bro, hiyo posting yako juu ni siasa na sheria ya bongo included, maana siasa na sheria ya bongo, haiko dunia nzima only in bongo, hakuna kulala mpaka tuone Blaza Dito, anapata what he deserve, nothing personal but just stupid rule of law!

Keep it up bro Kichuguuuuu, damn!!!
 
Kwa Latest news nilizozipata sasa ni kwamba

Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein ametoa mkono wa pole kwa mama mzazi wa Marehemu Hassan mbonde, maarufu kwa jina la mama mbonde, aliyeuwawa kwa kupigwa risasi. wakati alipofanya ziara maalum kwa kwenda kuwafariji wafiwa hao huko nyumbani kwako kawe jijini dar es salaam leo.

dada pamoja na ndugu wa marehemu walikuwepo..


Dr. Shein alii itikia dua ya pamoja na wazee wa familia ya marehemu.

kwa habari na picha zitawajia hivyi karibuni..
 
Makala hii nimeiona kwenye mtandao mmojawapo ya kublogu mwandishi anasema imetoka gazeti la jana la mtanzania, is this PR machinery at work au ni honest expression of thought?



NDUGU Kapteni Ukiwaona Ditopile Ramadhan Mwinshehe Wa Mzuzuri. Jina lake tu lilitosha kumpandisha juu kisiasa. Nililisikia kwa mara ya kwanza kupitia redio wakati ningali shule ya msingi miaka ile ya 80.

Ilikuwa ni kwenye moja ya chaguzi za ndani za CCM. Nayakumbuka majina mawili tu katika uchaguzi ule uliotangazwa moja kwa moja redioni. Ni majina ya Ndugu Ukiwaona Ditopile na Ndugu Idd Simba. Maana, jina la Ukiwaona Ditopile likikuwa refu mno na lenye kuvuta sikio. Wajumbe wa Mkutano ule Mkuu wa CCM nao walionekana kuvutwa na jina lake hata kabla hajatoa maelezo yake binafsi. Na mara ile jina la Ndugu Idd Simba lilipotamkwa, zililipuka kelele za Simba! Simba! Simba! Kana kwamba ilikuwa ni kwenye mechi ya Simba Uwanja Wa Taifa.

Nakumbuka yalisomwa maelezo binafsi ya Ukiwaona Ditopile kama mtu aliyeanzia kwenye utangazaji redioni na baadae kujiingiza kwenye siasa. Bila shaka, Ditopile angependa apande na kubaki juu kisiasa. Na hata kama kushuka kisiasa, basi asingependa iwe kama ilivyomtokea. Ditopile hakushuka, ameanguka na labda ameporomoka kisiasa.

Anayeshuka kisiasa walau anajua akanyage wapi katika ngazi za kuteremkia. Ditopile, kwa kutumia lugha na mazingira ya kwao Pwani, ni kama mtu aliyekwea kwa taabu sana mnazi mrefu. Amefika kileleni, amekwanyua nazi zake kwa mikono yake. Ameangusha chini, nazi moja baada ya nyingine.
Umewadia muda wa kuteremka mnazi akusanye nazi zake, ghafla amejikuta anaanguka chini ardhini. Sio tu ameanguka kwa kishindo kikubwa, bali pia amejeruhiwa vibaya mno. Katika yote mazuri aliyoyafanya kwa chama chake, serikali na kwa watu wa nchi hii, Ditopile ana hatari ya kukumbukwa daima kwa tukio analotuhumiwa sasa; kumwua kwa bastola dereva wa Daladala, Marehemu Hassan Mbonde.

Naam. Ditopile anatuhumiwa kwa mauaji. Nchi hii ina sheria zake. Tuna imani mkondo wa sheria utafuatwa ili haki itendeke. Hata hivyo, Ditopile anabaki kuwa ni binadamu kama wewe na mimi, hakukamilika. Na kama binadamu, inatupasa kujaribu kuingia kwenye hali yake na kujaribu kumwelewa yuko katika hali gani kwa sasa.

Huu si wakati wa kila mtu kutoa hukumu yake wakati kuna waliosomea kazi hiyo. Mathalan; kuandika magazetini vichwa vya habari kama vile; “ Ditopile kunyongwa!” Ditopile amerogwa!” na mengineyo yasiyo uthibitisho si kumtendea haki Ditopile. Kunazidi kuwaingizia simanzi zaidi ndugu zake wa karibu hata jamaa na marafiki zake. Hayo si maadili mema.

Tafsiri za tukio lile la mauaji zaweza kuwa nyingi. Lakini ukweli unabaki, kuwa Ukiwaona Ditopile anatuhumiwa kwa kumwua dereva wa daladala, ni mwananchi wa kawaida kabisa, mlalahoi. Siamini kama Ditopile alitaka mwisho wake wa kisiasa uwe ni namna ile. Lililomtokea ni dhahma na labda janga kubwa katika maisha yake binafsi, lakini pia kwa wote wenye kumhusu. Kama binadamu anastahili kupewa pole.

Hatujui kilichokuwa kikimzunguka Ditopile kwenye ubongo wake hadi kufikia kutenda jambo lile. Iko siku, katika utetezi wake, naye atapata fursa ya kuuelezea umma wa Watanzania juu ya usiku ule wa tukio uliopelekea mwisho wa huzuni na wenye majonzi kwa wengi, wenye kumhusu Ditopile na wale wenye kumhusu Marehemu Hassan Mbonde.

Ditopile, popote alipo, siyo tu ni mtu anayeshinikizwa na maradhi yake ya moyo na kisukari, bila shaka anashinikizwa na mzigo mzito wa fikara juu ya mustakabali wa maisha yake na ya wale wote wenye kumhusu. Ditopile anatuhumiwa kuyaondoa duniani maisha ya binadamu mwenzake ambaye hakuwa tu dereva wa daladala, bali pia alikuwa ni baba, kaka na mjomba wa wengi. Ana wenye kumpenda na kumtegemea.

Vivyo hivyo, kwa Ukiwaona Ditopile, naye hakuwa Mkuu Wa Mkoa na mwanasiasa tu. Ditopile ni Baba, babu, kaka na mjomba wa ndugu zake wengi. Nao pia wanampenda na kumtegemea.


Naamini, Ukiwaona Ditopile ni mhanga wa mfumo alioshiriki kuujenga. Mfumo uliopelekea kupitisha Sheria ya mauzo ya silaha; (Arms and Ammunition Act No.2, 1991) . Kwa kosa analotuhumiwa kulitenda Ditopile , anatusaidia kuamsha tena mjadala juu ya suala la uuzaji na umilikaji wa silaha hapa nchini. Tuna lazima ya kuufanya kuwa ni mjadala wa kitaifa.Suala si kuwapima akili wanaomilikishwa silaha kama inavyotakiwa na baadhi ya wabunge wetu. Wengi wa wanaomilikishwa silaha tunaamini huwa ni wenye akili nzuri kabisa kabla ya kushika silaha hizo. Lakini mara tu wakiwa na silaha kwenye makoti yao ndipo hapo baadhi yao akili huwaruka na kudhani kuwa wao ndio mwanzo na mwisho. Hawakawii kutishia watu; “ Nitakupiga risasi!” hata kama amedhulumiwa chenji ya elfu moja tu!. Huo sasa ndio uwendewazimu ambao mtu huyo hakuwa nao kabla ya kumilikishwa silaha. Mjadala huu wa silaha unahitaji makala yake.


Turudi kwenye mada. Hakika Ukiwaona Ditopile si mwanasiasa wa msimu mmoja. Ditopile ni mwanasiasa wa misimu yote. Ana uzoefu wa miaka mingi katika mapambano ya kisiasa. Haikuwa ajabu kwamba Jakaya Kikwete alimtumia ipasavyo katika kinachoitwa Mtandao wake.

Mwanazuoni Profesa I. K. Bavu kwenye kitabu kiitwacho; Tanzania; Democracy In Transition alichoandika na wanazuozi wenzake anaulezea mchuano wa kisiasa kati ya wagombea wawili wa CCM katika uchaguzi wa mwaka 1985; Ni Martha Wejja aliyekuwa anatetea kiti chake na Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyekuwa anajaribu kibarua kilimchomshinda mtoto mwenzake wa mjini; Mzee Kitwana Kondo kwenye uchaguzi wa mwaka 1980. Kitwana Kondo alishinda uchaguzi, lakini baadae Mahakama ilitengua matokeo na kumpa ushindi Wejja.

Ditopile ana uwezo wa kunusa kisiasa na hata kusoma mwelekeo wa upepo. Kwamba siku moja tu kabla ya kufikishwa mahakamani, Ditopile amemwandikia Rais barua ya kujiuzulu inaonyesha pia uelewa na uzoefu wake wa kisiasa. Yeyote mwenye kufikiri kwa undani anafahamu kuwa hata bila kuandikwa kwa barua ile, Ditopile alistahili kujiuzulu, kwa kuandika barua ya kujiuzulu kabla ya kushinikizwa kufanya hivyo , Ditopile amejiongezea pointi kwenye vita ya maoni. Wengi mitaani wanaamini kuwa Ditopile amechukua hatua ya kistaarabu kujiuzulu na hilo lina athari chanya kwake juu ya mwelekeo wa maoni ya wananchi.

Katika kitabu kile cha Profesa I. K. Bavu na wenzake, inaandikwa zaidi jinsi Ditopile alivyopambana na kupanda juu kisiasa. Kuwa, mara tu Ditopile alipohutubia kwenye mkutano wa kampeni ya ubunge pale Pugu Kajiungeni mwaka 1985 , alisikia wanafunzi wale wa Sekondari ya Pugu wakiimba. “ Kura Zetu! Tumpe Wejja! Ditopile alisikika akiwatamkia wapambe wake; “ That is a lost territory!” Akiimanisha eneo hili tumeshalipoteza!

Kwenye mkutano wa kampeni Kariakoo, kwa Ditopile ilikuwa ni kama kuchezea uwanja wa nyumbani. Zilitumika mbinu ngumu za kisiasa kummmaliza Wejja. Mathalan, liliulizwa swali gumu kutoka kwa mpiga kura lenye kumtaka Wejja afafanue kwanini ametoa maelezo yenye kutofautiana juu ya mahala alipozaliwa kwa uchaguzi wa 1980 na ule wa 1985.

Na katika mkutano mwingine wa kampeni wa Ilala, Ditopile aliomba Bwana mmoja aliyejulikana kama “Sharifu”, aondolewe mkutanoni. Inaandikwa, kuwa “Sharifu” yule kwenye mkutano wa kampeni wa Mchikichini alisikika akitamka kuwa mkutano wa Ilala utakuwa wa mwisho kwa Ditopile kutokea hadharani. Wakati huo ilibaki mikutano sita ya hadhara kabla ya uchaguzi. Matokeo ya uchaguzi ule Ditopile alimshinda Martha Wejja na kuingia bungeni. ( I. K. Bavu, Tanzania : Democracy in Transition; Uk. 88-100)

Naam. Kwa ufupi tu, huyu ndiye Ukiwaona Ditopile Ramadhan Mwinshehe Wa Mzuzuri. Ni dhahiri, kwa sasa ana wakati mgumu katika maisha ya kawaida na maisha ya kisiasa. Lakini, kwa kuiangalia historia ya mtu huyu Ukiwaona Ditopile, nasita kuandika, kuwa ukurasa wa mwisho wa historia yake kisiasa umeshaandikwa
 
NONESENSE!

Marehemu Mzee Kisoki, alipouwa aliwekwa rumande bila ya huruma wala hadithi, wala hela za serikali kwa ndugu ya marehemu aliyeuliwa na Rc huyo, na hatukuona hizi hadithi za abunuwasi, na alinacha, why now?

Blaza Dito kumshinda ubunge mama mnyonge kama Mama Wejja, in the 80s what that has to do na Ditopile mkuu wa mkoa kumuua dereva wa basi juzi bila ya kosa?

Yes, binadamu wote tuna mapungufu, so what? sheria zote za nchi ziondolewe basi, na mahakama zivunjwe na majela yote bongo yafungwe, maana this time arround tunatakiwa na huyu mwandishi tuelewe kuwa Blaza Dito, kapitiwa tu na tunapaswa kuelewa maana wote tuna mapungufu!

Who cares huko aliko Blaza Dito anachofikiria? At least bado anaouna mchana vipi marehemu? Vipi mkewe? Vipi watoto wake? Wazazi wake vipi nao? Ndugu zake vipi? Wakati yeye Blaza Dito anaenda mahakamani na Salooon, ndugu za marehemu wanafanya nini?

Halafu look at more NONESENSE, mwandishi anamsifia muuaji Ditopile, kwa kuandika barua ya kujiuzulu kwa rais, badala ya kumuuuliza mbona mpaka leo hajaandika barua kwa ndugu wa marehemu? How about us the people? or the public at large, hivi kweli haoni kuwa tunahitaji an apology?

Huyu Mwandishi analilia tu kuanguka kisiasa kwa blaza na the humiliaton, kama ndiyo kigezo tosha cha kutufanya tumuoneee huruma na hata ikibidi kumsamehe, na kwamba wananchi tusitoe maoni yetu, yaani ni IDIOTIC hivi huyu mwandishi anajua kuwa rumande za bongo kuna mahabusu wangapi wanaoshukiwa kwa mauaji, tena wengine hata bila ya hatia? Yaani kwake huyu Blaza Dito ni more binadamu kuliko wengine wote huko rumande?

Anasema habari za rais kumtumia wakati wa kampeni za mtandao, man! go home yaani sasa wale wote walioshiriki katika kampeni za mtandao they are juu ya sheria? kwa hiyo from now on wanamtandao wote wavunje tu sheria maana walimsaidia rais kampeni? What a jerk huyu mwandishi is?

RC au gavana wa mkoa, amesafiri toka mkoa wa Tabora, mpaka Dar-es-Salaam, akiwa na bastola mwilini mwake, na hatimaye kumuua nayo dereva anayeendesha walalhoi tena mbele ya hadhara, na kuiokota risasi aliyoitumia na kurudi nayo kwenye gari lake, baadaye bastola imepotea, huyu mwandishi anayaita haya mapungufu? Na sisi wananchi tunatakiwa tu-understand na tusiseme kitu, maana tunamhuzunisha blaza Dito? Yaani haya ni matusi ya mchan kabisaaa!

Kiongozi wa taifa mwenye nafasi ya kuchaguliwa na rais, anapofanya vizuri katika uongozi ni wajibu wa wananchi kumjadili kwa ushujaa wake, kama tunavyomsifia Magufuli na wengine kina Rutabanzibwa, na anapofanya makosa pia wananchi wana haki ya kumjadili bila kuuulizwa, wala kutishwa, ni kweli at teh end of the day, atahukumiwa na mahakama kisheria, lakini in the meantime, ni haki yetu wananchi kuuuliza kwa nini analetwa Mahakamani na Salooon wakati wengine wote wanapanda ngarandinga? Na hiyo inatupa wasi wasi kuwa huenda hata huko rumande hayupo? Kwa hiyo ni lazima tuanze sasa ku-speculate if you will kulingana na sheria zetu, mtu anayetuhumiwa kama Blaza Dito, anatakiwa afanywe nini?

Wote tunajua kuwa Mwamwindi, alipomuuua mkuu wa mkoa wa Iringa, Dr. Kleruuu, ile kesi ilikuwa ni a home run kwa prosecutors, alihukumiwa kunyongwa, sasa this time mkuu wa mkoa wa Tabora, amemuuuwa dereva wa dala dala, je hukumu itakuwaje, ile ile au? safari hii itakuwa amepanda mnazi na ameanguka kisiasa, na he is going through a lot, na ni mwenzetu basi asamehewe?

`
 
Mzee ES

Baada ya kusoma hoja zako nyingi humu ndani kwa bahati nimeshajua kuwa una akili sana na haswa pale unapotoa majibu yanayo onesha jinsi gani umeelewa previous poster

Lakini kuna tatizo...

Uko very emotive na katika kuweka mada zako bayana na hili linachangiwa zaidi pale unapokuwa na personal attacks kwa waandishi na hiiinafanya yoooote uliandika mazuri kuonekana kuwa ni "nonesense" kama ulivyosema hapo juuu sasa mzee hebu rekebbisha hilo

kwani unamaoni gani kuhusu satatement hiii:

ONE IS INNOCENT UNTIL PROVED OTHERWISE BY THE COURT OF LAW BEYOND REASONABLE DOUBT?

Afterall TZ ni nchi yenye kufuata LAW&ORDER japo inaweza ikawa sio perfect lakin ndio msingi wa democrasia yetu au unasemaje Mzeee

hebu jaribu kuangalia mambo kwa kina basi...
 
Dr WHO,
ndugu yangu hapa sikubaliani kabisa na maoni yako kwa sababu nawe pia umezungumza ukiwa Emotive...that's the other side of this coin.

Mimi hutumia mifano ya kawaida kuleta tamu na chungu ya hoja. na mojawapo ni katika kukataa ushauri wako kuwa - ONE IS INNOCENT UNTIL PROVED OTHERWISE BY THE COURT OPF LAW BEYOND REASONABLE DOUBT?
Hii ni lugha inayotumika kortini na sio mtaani na wala sintaweza kukubali kwani zipo kesi ambazo hazifiki mahakamani...Je, hizi tuziweke ktk kundi lipi?
Je, wale waliokwisha ua na wakashinda kesi kwa kuhonga hatuwezi kusema they are Guilty? hali wenyewe kwa midomo yao wanasema mitaani kuwa - Mjomba pale zimenitoka sanaa lakini ukweli - I'm guilty.

Naam maadam Dito kesi ipo mahakamani ina maana kacheza RAFU. Kipenga kimeisha pigwa na refa, na kazi iliyobaki ni mpira uwekwe miguu 12 ili penati ipigwe. Upo uwezekano mkubwa wa kukosa kufunga goli (which is Hukumu) kutokana na hizi sheria zetu za nje ya korti ambazo zinakubalika kortini (rushwa). Lakini bado itajulikana kuwa kulikuwepo na rafu (guilty) na penalty imepigwa!..
Alichosema Mzee ES hapo juu ni ukweli ambao haupindiki. Dito hajaomba kukutana na familia ya marehemu wala kuandika barua kwa wafiwa isipokuwa kazini kwake which sent signal kuwa haoni bado makosa yake na kisheria navyojua akikubali makosa basi kesi yake itakuwa ngumu. Na lazima kakatazwa na mawakili wake hali kisha sema kwa wandishi kuwa ilikuwa bahati mbaya. Then, why not tell the family!
Hakuna anayefikiria ama kuyasema mazuri ya marehemu jinsi alivyokuwa akisaidia familia yake!.. matatizo aliyoyapata hadi kufikia kuwa dereva n.k . hakuna anayezungumzia kuhusu watoto wa marehemu na familia yake jinsi wanavyo mkosa marehemu isipokuwa kunukuu maneno ya baba wa marehemu yanayompa nguvu Dito - Eti kifo cha Mbonde ni kazi ya Mungu!
Yaani hapa tunaondoa kabisa uchafu wa rafu hii!... kwa nini tusiseme ilikuwa shetani?
Dito ni mwanajeshi ambaye anafahamu kabisa sheria zote za silaha na anafahamu kuwa bastola haiwezi kufyatuka ghafla ikiwa safety ipo ON. Ilikuwaje akaiondoa safety ikiwa hakukusudia!..besides, why utoke ndani ya gari lako na bastola kumtishia kijana dereva wa basi hali wewe ni RC kiasi ambacho unaweza kupiga simu tu polisi na kijana akawekwa ndani na kusahaulika. He had so many option mbali na kubeba bastola kama vile anafukuza jambazi.
He was wrong na sisi tunasema amecheza rafu (GUILTY) kwa hiyo hata kama atashinda kesi kwetu tutasema tumeshindwa kufunga goli lakini rafu bado ilichezwa.
 
Mzee GENIUS WHO, sijakuelewa ninakuomba urudie tena, maana ninaona more NONESENSE kutoka kwako, I could care less kama unazo akili au huna, ninachojali ni hoja zako kama zipo kwenye hayo juu sioni kitu,

Kama ni sheria, inaonekana wewe umekaa majuu kwa muda mrefu, sasa sheria za bongo zimekuchenga kabisaa na siasa yake, maana Mwamwindi alipomuuua RC, Dr. Kleruuu, hata kabla hajahukumiwa tayari tulikuwa tunaimba nyimbo kwenye shule za msingi za kumlaani kwamba ametumwa na mabeberu,

pia kuna na mpaka wimbo wa Mbaraka Mwinshehe, unaolaani kifo hicho cha mwanamapinduzi, na ulitolewa hata kabla ya hukumu na kunyongwa kwa Mwamwindi, sasa kwa mtazamo wako which is more NONESENSE?

Hicho cheo cha kuamua nani ana akili na nani hana kwenye hii forum nani aliyekupa? Hebu nisaidie kuelewa toka uingie hii forum ni wangapi wenye akili na wasiokuwa nazo ninaomba unitajie bro? Na aliyesema wewe unazo akili ni nani? Unafikiri watu wote bongo wanaoandika articles kuhusu hiii kesi hawahjui kuwa innocent until proven guilty, ni wewe tu na mwandishi wa hiii articles ndio mnaojua?

Since mzee wangu una akili sana, zimekuzidi mpaka unaweza kujua walionazo na wasionazo, how do you describe ndugu wa marehemu waliokuwa wamebeba mabango kuwa " Kikwete tuomeona hii kasi mpya", na waandishi waliozitoa picha hizo magazetini unawaitaje mzee genius? Vipi hiyo article ni wewe uliyeiandika nini, mbona una jazba bro? Halafu kitendo cha mshitakiwa wa mauaji kuletwa kwa Saloon wakati wauaaji wengine kama yeye wamo kwenye ngarandinga wewe unakionaje? Mzee Genius ulitegemea hii article itaingia hapa na sisi tuishanglie ndio tuonekane tuna akili kama zako za u-genius?

Mzee Genius unaonaje ukirekebisha hayo, kwa staili zako za ki-GENIUS?, and also kama kwa kuandika kama ulivyoandika hapo juu kwa maoni yako ni kuwa genius, basi mi i hizo akili sizitaki kabisaaaaa, tafadhali ninakuomba unihesabu kama sina akili mzee wangu genius DR. WHO!


Wallah I love this forum!
 
Mkandara said:
Dr WHO,


Mimi hutumia mifano ya kawaida kuleta tamu na chungu ya hoja. na mojawapo ni katika kukataa ushauri wako kuwa - ONE IS INNOCENT UNTIL PROVED OTHERWISE BY THE COURT OPF LAW BEYOND REASONABLE DOUBT?
Hii ni lugha inayotumika kortini na sio mtaani na wala sintaweza kukubali

-Mindhali hii ndio lugha inayotumika huko mahakamani then hatuna budi kuifuata kwa sababu ndivyo sheria inavyosema na kuna maana kwa nini hizi sheria ziliwekwa inthe first place


Naam maadam Dito kesi ipo mahakamani ina maana kacheza RAFU. Kipenga kimeisha pigwa na refa, na kazi iliyobaki ni mpira uwekwe miguu 12 ili penati ipigwe. Upo uwezekano mkubwa wa kukosa kufunga goli (which is Hukumu) kutokana na hizi sheria zetu za nje ya korti ambazo zinakubalika kortini (rushwa). Lakini bado itajulikana kuwa kulikuwepo na rafu (guilty) na penalty imepigwa!..

-Kupelekwa mahakamani does not constitute kuwa mtu yuko guilty ndio maana huko wanatumia lugha ya kuwa INADAIWA
sasa kwa kutumia mfano wako nashangaa kuwa katika mechi hiyo inaanza kwa penalty sasa mechi ilichezwa saangapi mzee umeniacha hapo kidogo hebu fafanua


Alichosema Mzee ES hapo juu ni ukweli ambao haupindiki. Dito hajaomba kukutana na familia ya marehemu wala kuandika barua kwa wafiwa isipokuwa kazini kwake which sent signal kuwa haoni bado makosa yake na kisheria navyojua akikubali makosa basi kesi yake itakuwa ngumu. Na lazima kakatazwa na mawakili wake hali kisha sema kwa wandishi kuwa ilikuwa bahati mbaya. Then, why not tell the family!


-Dito kuandika barua au kutoandika barua kwa wanafamilia wa marehemu ni suala ambalo ni personal na sidhani kama kuna sehemu katika sheria inamlazimisha kufanya hilo,pili suandika barua ya kuresign sio lazima kuwa kakubali kaua lakini hiyo ni for simple reason kuwa utendaji wake wa kazi utakuwa unaingiliana na kesi hii hivyo alikuwa anakila right ya resign na pia kutokana na contract yake ya kazi,kisheria anatakiwa kufanya hivyo

Hakuna anayefikiria ama kuyasema mazuri ya marehemu jinsi alivyokuwa akisaidia familia yake!.. matatizo aliyoyapata hadi kufikia kuwa dereva n.k . hakuna anayezungumzia kuhusu watoto wa marehemu na familia yake jinsi wanavyo mkosa marehemu isipokuwa kunukuu maneno ya baba wa marehemu yanayompa nguvu Dito - Eti kifo cha Mbonde ni kazi ya Mungu!

-Sasa hayo aseme nani?inawezekana yashasemwa lakini hayapewi attention kwa sababu kuna hili suala zima la character assassination ambalo ni part time obessission kwenye media zetu bongo bila kuangalia facts ni zipi na fiction ni ipi



Yaani hapa tunaondoa kabisa uchafu wa rafu hii!... kwa nini tusiseme ilikuwa shetani?


-based on what evidence?


Dito ni mwanajeshi ambaye anafahamu kabisa sheria zote za silaha na anafahamu kuwa bastola haiwezi kufyatuka ghafla ikiwa safety ipo ON. Ilikuwaje akaiondoa safety ikiwa hakukusudia!..besides, why utoke ndani ya gari lako na bastola kumtishia kijana dereva wa basi hali wewe ni RC kiasi ambacho unaweza kupiga simu tu polisi na kijana akawekwa ndani na kusahaulika. He had so many option mbali na kubeba bastola kama vile anafukuza jambazi.

-I can agree na maswali uliyotunga na natumai upande wa mashtaka ushaangalia hii lione of questioning na ndio maana kesi ikaenda mahakamani ambako haya yote yatajibiwa na MTUHUMIWA



He was wrong na sisi tunasema amecheza rafu (GUILTY) kwa hiyo hata kama atashinda kesi kwetu tutasema tumeshindwa kufunga goli lakini rafu bado ilichezwa.


-Sasa kama ni gulty bila kuangalia evidence zote je, nchi zingine watuona sisi as jokers kwa sababu tunataka kuchukua sheria mikononi mwetu sasa tofauti yetu na wanyama iko wapi mkuu?
 
Mzee Es said:
Mzee GENIUS WHO, sijakuelewa ninakuomba urudie tena, maana ninaona more NONESENSE kutoka kwako, I could care less kama unazo akili au huna, ninachojali ni hoja zako kama zipo kwenye hayo juu sioni kitu,


-Actually wewe ndio ulianza kulitumia kwa TAFITI THEN JADILI na naona its becoming ur favourite word so far

Kama ni sheria, inaonekana wewe umekaa majuu kwa muda mrefu, sasa sheria za bongo zimekuchenga kabisaa na siasa yake, maana Mwamwindi alipomuuua RC, Dr. Kleruuu, hata kabla hajahukumiwa tayari tulikuwa tunaimba nyimbo kwenye shule za msingi za kumlaani kwamba ametumwa na mabeberu, pia kuna na mpaka wimbo wa Mbaraka Mwinshehe, unaolaani kifo hicho cha mwanamapinduzi, na ulitolewa hata kabla ya hukumu na kunyongwa kwa Mwamwindi, sasa kwa mtazamo wako which is more NONESENSE?


-NONESENSE ni kumhukumu mtu bila ya kumpa fursa ya kujitetea na ndio maana pale Arusha tuna mahakama ya wanaodaiwa kuuwa mahalaiki kule Rwanda

Hicho cheo cha kuamua nani ana akili na nani hana kwenye hii forum nani aliyekupa? Hebu nisaidie kuelewa toka uingie hii forum ni wangapi wenye akili na wasiokuwa nazo ninaomba unitajie bro? Na aliyesema wewe unazo akili ni nani?

-Hii ni mpya na kama umepata impression hiyo basi nadhani umepotoka ila nilichosema ni kuwa kwa nini tusiangalie mambo kwa kina ili kujua mchele ni upi na pumba ni zipi? Akili kila mtu anazo & that includes YOU sasa labda ungewatupia mpira ma moderators wa website wanaweza kukujibu hilo au unasemaje?

Unafikiri watu wote bongo wanaoandika articles kuhusu hiii kesi hawahjui kuwa innocent until proven guilty, ni wewe tu na mwandishi wa hiii articles ndio mnaojua?


-Actually kutokana na standard ya journalism iliopo bongo ndio hawajui na kama huamini tazama mfano mdogo wa IPPMEDIA wanakesi ngapi za madai mahakamani bongo? au hujui kama hao waandishi weyewe siku hizi wanshinda kwenye internet cafe kusoma mambo humu kisha wao wanajidai wanalatest...au uliza MKAPA aliwaambiaje waandishi wa habari bongo kuhusu standards za uandishi wao



Since mzee wangu una akili sana, zimekuzidi mpaka unaweza kujua walionazo na wasionazo, how do you describe ndugu wa marehemu waliokuwa wamebeba mabango kuwa " Kikwete tuomeona hii kasi mpya", na waandishi waliozitoa picha hizo magazetini unawaitaje mzee genius? Vipi hiyo article ni wewe uliyeiandika nini, mbona una jazba bro? Halafu kitendo cha mshitakiwa wa mauaji kuletwa kwa Saloon wakati wauaaji wengine kama yeye wamo kwenye ngarandinga wewe unakionaje? Mzee Genius ulitegemea hii article itaingia hapa na sisi tuishanglie ndio tuonekane tuna akili kama zako za u-genius?


-Suala la mshitakiwa kupelekwamahakamani kwa saloon and so on sio issue amabyo naweza kuikataa au kuitetea lakini naamini kuwa kama sheria imefuatwa then thats ok kama haikufuatwa then asiyependa anayo right ya kufungua separate case kwa ajili hiyo.Ndugu wa marehemu wanayo kila right ya kumourn as long as itakuwa hayo mabango yao hayokuwa yanatukana watu nadhani still walikuwa ndani ya sheria majority ya waandishi wetu naweza kuwaita ni ma ROTWEILLER JOUNALISTS nadhani hiyo sums it up. Uzuri mimi sio REGINALD MENGI amabaye anataka kuban hata jina lake lisitajwe humu JAMBO FORUM na wala si condone hayo anayofanya na mimi huwa na advocate freedom of speech na hata kama kwa watu amboa hutuwapendi kiasi gani lakini its their basic right kujiexpress kwa namna wanayovyoweza as long as wanaheshimu wenzao..sina uwezo wa kukukataza usichangie humu na hata kama ningekuwa na uwezo huo ningekuchukulia kama challenge na hii yote ni nzuri


Mzee Genius unaonaje ukirekebisha hayo, kwa staili zako za ki-GENIUS?, and also kama kwa kuandika kama ulivyoandika hapo juu kwa maoni yako ni kuwa genius, basi mi i hizo akili sizitaki kabisaaaaa, tafadhali ninakuomba unihesabu kama sina akili mzee wangu genius DR. WHO!

-no sitokuhesabu kama huna akili ila naweza kukuhesabu kama mtu amabye anaweza kuchnganua mambo kwa kina bila ya kuendeshwa na hao waandishi wa habari wanaopenda udaku.sasa hili GENIUS naona nalo umelipenda mno lakini huoni kama unajionesha kuwa una inferiority complex kusema kukubali kuwa huna akili wakatu akili unazo au ndio unamwomba Mungu akufanye uwe huna akili?

Wallah I love this forum!

-I will love it more when they will stand up against bullying from R.MENGI
 

Attachments

  • JK.jpg
    JK.jpg
    19.3 KB · Views: 307
Ala! kumbe una shida nyingine, samahani hiyo siwezi kukusaidia, na sitakujibu tena on this kwa sababu wewe unataka kuharibu huu mjadala, hiyo sitakupa nafasi kabisaa,

Mjadala hapa ni Blaza Ditopile Mzuzuri na mimi binafsi kutaka kuhakikisha haki inatendeka hiyo tu ndiyo nia yangu, na nimeshituka pale

alipokuja mahakamani na Saloon, Bastola kupotea, na yeye kudai ameumia baada ya kushambuliwa na wananchi, na kusikia viongozi wanajipanga kwa marehemu baada ya mazishi, hizo tu mzee wangu ndio shida zangu, yasingetokea hayo usingenisikia kabisaaa ningesubiri kama ulivyosema innocent until proven guilty, na sitaacha mpaka hukumu itakapotolewa, na promise nitaenda mahakamani kila itakapolia nitakuwepo nijionee mwenyewe, ukweli,

Kuhusu hayo matatizo yako mengine, I am lost hata yamefikaje humu kwenye mjadala wa Ditopile, unless kuna kitu sielewi ila anzisha mada nyingine sio ndani ya hiii!, yaani haya makubwa hebu sema mzee imekuwaje kuna mtu anawa-bully watu asiowaona, anzisha mada bro! anyway msimamo wangu niliusema mapema, mada mbili zilipohamishwa hapa na baadhi ya hoja zangu kufutwa nilisema yote wewe nenda utafute hiyo mada utakuta msimamo wangu na siwezi kurudia wala kugusa hilo tatizo lako, sitaki!

The rest ni mazungmzo baada ya habari nimezowea, mambo ya complex hayo yako mimi sina kabisaa matatizo bro, maana ninaelewa nguzo moja muhimu ya hizi forum, ni BURUDANI! alisema mzee Mwanakijiji na ninakubali, kuwa hapa sio bunge wala mahakama, ni bulogu ya burudani, that is all!

Wallah I love it more!
 
jana tume observe one of humiliation of huminity,,i was watching tv na nikaona namna propaganda ya dito free campagne inavyoendelea..inakinaisha kumuona dr shein alivyoingia pale na vilio vilivyotawala,,,pale kwa mzee mbonde..leo mzee mzima mwenyekiti wa dito free campagne network..na rais wa jamhuri ya tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ,jakaya ..anatia team kwa ndugu mbonde.
naomba kuuliza swali nijibiwe,,utaratibu mufaka na wa heri wa maziko na msiba kiislamu ni upi??? maana ndugu zetu waislam wanamoja ya taratibu nzuri za msiba,,kwanza hawakawii kuzika ,,pili baada ya kuzika tanga huanuliwa haraka ,sasa pale kwa mzee mbonde mlala hoi mwenzetu amepata wapi feza za kukalisha watu msiba wiki ya pili hii wanalia ,wanakula na kulala hapo,,, au jk akishaenda leo ndio wataanua matanga rasmi na kutoa kauli ya shukrani,? je kuna heri kwa muislamu kulia wiki mbili mfululizo,,,maana nasikia mkirefusha msiba mnampunguzia marehemu dhawabu...
 
Kuna mnaotaka anyongwe, wengine mnataka afungwe, na wengine ahukumiwe kwanza.

Kesi hii haitakuwa na ugumu. Naamini mtuhumiwa hatakana kumuua marehemu, ila atadai ilikuwa ajali. Kwa hiyo, hakuna tatizo la kupotea bastola kwani hakutakuwepo na kupinga kwamba bastola iliyomuua marehemu ni ya mtuhumiwa, na mtuhumiwa ndiye alimpiga marehemu risasi.

Kama kutakuweko na ushahidi wa kuridhisha kwamba mtuhumiwa alipiga risasi ya kwanza ikavunja kioo kisha akapiga risaisi ya pili na ikamwingia marehemu, basi hakimu hataweza kuamua kwamba ilikuwa bahati mbaya, hata kama angependa kufanya hivyo.

Wengi mnasahau uwezekano wa vurugu kubwa kutokea wakati kiongozi anamuua mlalahoi. Huku kujitokeza viongozi kutembelea familia ya marehemu ni njia sahihi ya kuepusha vurugu.

There is no possibility that this was a premeditated murder, and so, forget about the death penalty. It was murder, but it was not premeditated. The only question that we must address is whether it was an accidental homicide. If the accused (yes, he is more than just a suspect at this stage, for he has been charged) fired two shots then I am satisfied that it was not an accidental homicide. If a single shot came out that terrible pistol then it may or may not have been accidental, and a thorough analysis of the evidence of eye witnesses will be need before we can know for sure.

Augustine Moshi
 
Back
Top Bottom