Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

I can understand it being an accident if the daladala driver was 20 or 30 meters away...lakini that was close to being point blank.Sasa yeye Dito hakujua kuwa alichoshika ni silaha? He is a trained military man,he is well aware of all the safety features and procedures.Wengi tumepitia JKT, na tunajua vizuri kitu cha kwanza muhimu kwenye silaha ni usalama.
Kwa hio in other words tukisema hii ni accident,then arent we setting a precendent? Wenye silaha binafsi(bastola) ni zaidi ya 10,000 hapa Tz If only a 3rd of those practised the same irresponsibility as did Dito and claim ni ajali,tutakuwa wapi?Tuangalie the whole process ya bastola kufyatua risasi: kwanza it has to be drawn,then it has to be cocked(bullet in chamber,it is dangerous having it there without intent of firing),the safety has to be off,vitu vyote hivi Dito kafanya kabla ya kuifyatua hio risasi.sasa kama kweli alikuwa anataka kumtishia,kwa nini asingepiga risaisi hewani?Kwangu mimi hapa sioni alichukua precautions gani za kutojaribu kumdhuru marehemu,hivyo kwa maoni yangu ni kwamba alidhamiria.Na bastola ni muhimu kwenye kesi ya mauaji,maana lazima iende kwenye kitengo cha ballistics polisi ili waweze ku-determine kuwa ile risasi iliyomuua marehemu ilitoka kwenye bastola ya mtuhumiwa.
 
RC wa Tabora, anasafiri kwenda Bagamoyo, anachukua bastola ikiwa na risasi zake, njiani gari lake linagongwa katika ajali ya magari, dereva wake anakwenda akuangalia hasara iliyotokea na kurudi ndani ya gari RC, anatoka na bastola mkononi mbele ya hadhara na kuanza kumtishia nayo dereva wa basi lililomgonga, dereva kwa kuhofia maisha yake anaanza kufunga viooo na mlango,

RC anafyatua risasi na kumuuuua dereva huyo hapo hapo na kumuuuuua, huku umma ukishuhudia, yaani kwa maneno mengine hiyo ilikuwa ni excution style, halafu RC anaokota ganda za risasi aliyoitumia na kurudi kwenye gari lake na kuondoka, huku akiacha wananchi wakitimka kwa kuhofia maisha yao.

eti explaination yake ni kwamba RC huyo, aliyetoka Tabora hadi DAR na bastola yake mfukoni na hatimaye kuitumia kwa kumuuua dereva asiyekuwa na hatia mbeele ya kadamnasi, ameua kwa AJALI, hakukusudia?

Haya vijana hebu tufundisheni hii shule mlizosoma maana huenda sisi wengine hatukwenda hizo shule kama zenu?
 
Mzee Es said:
Ala! kumbe una shida nyingine, samahani hiyo siwezi kukusaidia, na sitakujibu tena on this kwa sababu wewe unataka kuharibu huu mjadala, hiyo sitakupa nafasi kabisaa,

Mjadala hapa ni Blaza Ditopile Mzuzuri na mimi binafsi kutaka kuhakikisha haki inatendeka hiyo tu ndiyo nia yangu, na nimeshituka pale

alipokuja mahakamani na Saloon, Bastola kupotea, na yeye kudai ameumia baada ya kushambuliwa na wananchi, na kusikia viongozi wanajipanga kwa marehemu baada ya mazishi, hizo tu mzee wangu ndio shida zangu, yasingetokea hayo usingenisikia kabisaaa ningesubiri kama ulivyosema innocent until proven guilty, na sitaacha mpaka hukumu itakapotolewa, na promise nitaenda mahakamani kila itakapolia nitakuwepo nijionee mwenyewe, ukweli,

Kuhusu hayo matatizo yako mengine, I am lost hata yamefikaje humu kwenye mjadala wa Ditopile, unless kuna kitu sielewi ila anzisha mada nyingine sio ndani ya hiii!, yaani haya makubwa hebu sema mzee imekuwaje kuna mtu anawa-bully watu asiowaona, anzisha mada bro! anyway msimamo wangu niliusema mapema, mada mbili zilipohamishwa hapa na baadhi ya hoja zangu kufutwa nilisema yote wewe nenda utafute hiyo mada utakuta msimamo wangu na siwezi kurudia wala kugusa hilo tatizo lako, sitaki!

The rest ni mazungmzo baada ya habari nimezowea, mambo ya complex hayo yako mimi sina kabisaa matatizo bro, maana ninaelewa nguzo moja muhimu ya hizi forum, ni BURUDANI! alisema mzee Mwanakijiji na ninakubali, kuwa hapa sio bunge wala mahakama, ni bulogu ya burudani, that is all!

Wallah I love it more!



You can do better than this
 
Zanaki,

Well said, vile vile let say bastola yake haikua na usalama (some revolvers za kizamani hazina usalama), WHY AIMING bastola yako unayojua haina usalama kwa kijana Mbonde?? Dito being ex-Kapteni wa Jeshi for sure he knew what was going on. Dito alaaniwe

Bob Mkandara
Mfano wako wa penati, ni sahihi kabisa, naanza kuona dalili za mlalahoi kupiga na Dito kudaka, impact ya mpira (kifungo) inategemea mlalahoi alikuwa na nguvu gani kwenye miguu yake.
 
Mzee Es, Zanaki na wengineo Upambuzi yakinifu wenu kuhusu suala zima la Mzee Dito Vs Marehemu Mbonde unanifanya nione kwamba kuna wazalendo wengi kama nyinyi wanalitazama suala hili kwa macho yote mawili,na kupigia mistari kila kinachosemwa/fanywa na serikali kupotosha ukweli wa kesi hii nyeti!,Sisi ndio ndugu wa kweli wa Mbonde!TUSIKOME Tupambane mpaka mwisho ili tuone sheria inachukua mkondo wake sawa sawa.Hata hao wanaosemwa kupinda utaratibu wa sheria wanaingia humu na kujua misimamo ya watu.Tujadili issue hii kwa nguvu ya hoja na tusitukanane wala kukashifiana,kwani michango yetu humu ina nafasi kubwa ktk HUKUMU.Ni vigumu kulikubali hilo lakini ndio ukweli.
 
Je ilikuwa ni ajali?
"Ajali haina kinga" waswahili walisema, kale kadaladala kugonga gari la RC yawezekana kuwa ajali (ingeweza kuwa gari la mtu yeyote kwani hiyo ni mashine tu), lakini kitendo cha mtu kuamua kutoka ndani ya gari lake, kujibizana na dereva, kumfuata hadi kwenye gari lake, kuweka kidole kwenye trigger, kulenga mahali pa kichwa na kufyatua huwezi kuita ajali, unless neno "ajali" limepoteza maana yake!!

Je aliua kwa kukusudia?
Jibu langu ni ndiyo. Hakuna mtu anayenyosha bastola iliyo na risasi, na kuweka kidole kwenye trigger huku ameielekeza kwa mtu/watu na baadaye kufyatua, mtu/watu wakafa halafu huyo mtu aseme hakukusudia kuua!! Kama lengo lake ilikuwa ni kumtishia huyo kijana, angefanya kama wanavyofanya mapolisi au hata watu wengine kabla ya kuamua kumlenga mtu kujitetea. Wanafyatua risasi hewani kutishia!!! Unapozidiwa nguvu hapo ndipo unapoua ukitetea maisha yako, and that is a defence.

Je ni mauaji ya kujitetea maisha?
Hilo lingekuwa na ukweli endapo tu, yule kijana angetajwa mahali popote kuwa alibeba silaha (ya aina yoyote) na kumtishia Bw. Mkuu wa Mkoa. Hadi hivi sasa hakuna ushahidi wowote kuwa Hassan alifanya hivyo. Kinachojulikana alipigwa risasi (iwe moja, mbili, au kumi) akiwa ameketi kwenye kiti cha gari huku amefunga vioo!

Je Bunduki inahitajika kuonesha nia ya kosa (mens rea)
La hasha, mazingira peke yake yanatosha kuonesha kama mtu alikusudia kutenda tendo ovu (actus reus) au la. Mtu akikutwa juu ya paa la nyumba ya mtu mwingine huku akiwa ameshikilia gudulia la petroli akimimina, na baadaye kushika kiberiti na kuwasha nyumba hiyo na baadaye akakutwa amesimama pembeni anaangalia huku nyumba inaungua, mkononi amebakia na njiti zilizoungua, na ana harufu ya mafuta na mashahidi wapo waliomuona akifanya hivyo, na ikathibitika kuwa ndani ya nyumba kulikuwa na mtoto wa miaka 4 aliyeuawa kwa moto, polisi hawahitaji guduria la mafuta lililotumika kumwaga mafuta!!!

Je kitendo cha viongozi kwenda kutoa rambirambi ni kuokoa vurugu?
Kwa nje kitendo hicho kinapongezwa, ni cha kibinadamu na ni cha kiungwana. Hata hivyo, ukichunguza kwa karibu utaona kuwa ndani ya kitendo hicho kumejaa unafiki, uzandiki, na wa hali ya juu. Lengo lake ni moja tu nalo kumuonesha mtuhumiwa kuwa anajutia tendo lake (kitu ambacho hakibadilishi uzito au ubaya wa tendo hilo) na kujaribu kwa namna fulani kumuombea msamaha kwa wafiwa. Kitendo cha viongozi kutoa ahadi za kuisaidia familia n.k kina lengo moja tu nalo ni kuwanyamazisha wanafamilia (siyo kuzuia vurugu). Je watu waliokuwa wanalia mwanzoni kuwa famiilia imempoteza mtu pekee ambaye ndiye alikuwa anawasaidia kwa kila inahitaji nini zaidi ya mtu kuwapa uhakika wa chakula na malazi ya hapo baadaye?

Je ni watu wangapi ambao wanafiwa na baba zao, jamaa zao wanaosadia familia zao lakini huo RAis, makamu, meya, mawaziri, n.k wakijipanga msururu kuahidi misaada?

Ukweli ni kuwa, viongozi hawa wote wanafanya wanayofanya si kwa sababu wana uchungu kuwa Mbonde ameuwa kinyama, siyo kwa sababu familia inahitaji msaada sana, siyo kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuwasaidia tena.. La hasha!! Viongozi hawa wanafanya wanachofanya kwa sababu anayetuhumiwa kuua ni NANI.

UKWELI NI HUU
Kama muuaji wa Hassan angekuwa Mmachinga fulani, jambazi fulani n.k unadhani viongozi hawa wangepanga foleni kwenda huko Kawe? Je alipouwa yule mwandishi wa habari wa The East African, viongozi wangapi wangazi za juu walienda kutoa pole kule na kuahidi kuisadia familia yake? Sitashangaa kuna viongozi walioenda kutoa pole, sitashangaa kuna mawaziri walioenda kutoa rambirambi kule, ila WANGAPI KATI YA HAO WALIKWENDA WAKIFUATANA NA WAANDISHI WA HABARI NA WAPIGA PICHA?

Kama hamuyaoni mazingaombwe, basi inabidi mkalie ndimu!!!

M. M. Mwanakijiji
 
Shukran Mwanakijiji,Hakuna la nyongeza hapo.Kwa nini usipate nafasi ya kujiunga katika timu ya Prosecutors ili mpambane vyema na akina Ringos ambao wapo hapo kuinua profile zao?.Mimi sijui sheria,lakini kwa logic tu ,huyu Bwana ameua kwa kukusudia!
 
jamani,
mimi naomba nichukue mtazamo tofauti na wengine ,mnaweza kuniona mimi ni kichaa lakini ndio uhuru wenyewe wa kutoa mawazo yako.

hapa kuna mambo kadhaa ya kuangalia.
kwanza: viongozi wengi wa serikali(mawaziri,rc na dcs) na hasa wale waliowahi kupitia jeshi huwa wanatembea na silaha.hii ni kwa ajili ya self defence na mimi sioni tatizo na hilo.
hivyo basi rc ditopile kwa wadhifa wake atakuwa ametembea na silaha kwa zaidi ya miaka 15+ (kama kapteni wa jeshi, waziri,mkuu wa mkoa).
kwahiyo siku ya tukio kama siku nyingine ditopile alikuwa na silaha na wala hakunuwia kuwa siku hiyo anaenda kuua mtu.
tena unaona ilikuwa ni majira ya saa mbili pengine ndio alikuwa arudi kupumzika.
sasa pale imetokea ajali.(prado yake mpya imegongwa) hivi nani kati yenu prado yake imegongwa na ataanza kucheka au kumbembeleza mtu aliye gonga prado lake?
lazima pale jamaa alikasirika sana, sasa baada ya hapo anaamua kushuka na kwenda kukabiliana na dreva wa daladala, unategemea aiche silaha yake ya ulinzi (take into consideration the behaviour of daladalas youngmen who smoke marijuwana?).
baada ya hapo nawaachia mahakama iamue ila mimi huu ndio mtazamo wangu.

halafu na mwisho naomba tusisahau kuwa hawa madreva wa daladala wanasababisha vifo vya watu wengi tu kila siku,
kwahiyo sio tunalalama tu kwa kifo hicho cha dreva mmoja wakati tunasahau tabia mbovu za madreva wa daladala wanaosababisha vifo vya watanzania kila siku kwa sababu zisizo za msingi,
hawa madreva na makonda wao wengi ni wavuta bangi, wabwia unga. we need to be carefull here.
 
Quarz

Sehemu ya kwanza ya maelezo yako ina mantiki kidogo. Hata hivyo tatizo kubwa hapa ni kwamba kama ameitumia silaha hiyo miaka zaidi ya kumi na tano na hajkwahi kumnyooshea mtu, hapo ndipo upande wa mashitaka unaweza kusisitza kuwa huyu bwana alikusudia hasa kwa vile anajua sana matumizi na usalama wa silaha. Upande wa mashitaka pia unaweza kuonyesha kuwa mtuhumiwa alikuwa na motive ya kufanya uhalifu huo baada ya kuomna victim amegonga Prado yake mpya. Hakufanya hivyo spontaneously kwa vile alitelemka kutoka kwenye gari lake, akamfuata dereva victim ambaye wakati huo huenda alikuwa amepigwa na butwaa; akachomoa bunduki yake na kufungua safety pin kabla ya kumfyatulia victim. Hayo yote yalitokea wakati mlango wa gari ya victim umefungwa, kwa hiyo victim hakuwa amemkabili mtuhumiwa.


Sehemu ya pili ya maelezo yako nadhani hukuwa makini katika kuiandika kwa vile umeonyesha kuchukulia kuwa madereva wote wa daladala ni wavuta bangi na watu wasiokuwa na thamani kiasi kuwa ni haki yao wauwawe kinyama hivyo. Ingawa ni kweli baadhi ya madereva ni wakorofi, kuna madereva wengi ambao ni watu wenye heshima zao; madereva wengine wanendesha magari yao wenyewe. Tunaweza kuwa tunatofautiana madaraka na uwezo kipesa, ni vizuri tujenge tabia ya kuheshimu uhai wa watu wengine hata kama ni watu wa chini sana kijamii.
 
Quarz

Sehemu ya kwanza ya maelezo yako ina mantiki kidogo. Hata hivyo tatizo kubwa hapa ni kwamba kama ameitumia silaha hiyo miaka zaidi ya kumi na tano na hajkwahi kumnyooshea mtu, hapo ndipo upande wa mashitaka unaweza kusisitza kuwa huyu bwana alikusudia hasa kwa vile anajua sana matumizi na usalama wa silaha. Upande wa mashitaka pia unaweza kuonyesha kuwa mtuhumiwa alikuwa na motive ya kufanya uhalifu huo baada ya kuona victim amegonga Prado yake mpya. Hakufanya hivyo spontaneously kwa vile alitelemka kutoka kwenye gari lake, akamfuata dereva victim ambaye wakati huo huenda alikuwa amepigwa na butwaa; akachomoa bunduki yake na kufungua safety pin kabla ya kumfyatulia victim. Hayo yote yalitokea wakati mlango wa gari ya victim umefungwa, kwa hiyo victim hakuwa amemkabili mtuhumiwa.


Sehemu ya pili ya maelezo yako nadhani hukuwa makini katika kuiandika kwa vile umeonyesha kuchukulia kuwa madereva wote wa daladala ni wavuta bangi na watu wasiokuwa na thamani kiasi kuwa ni haki yao wauwawe kinyama hivyo. Ingawa ni kweli baadhi ya madereva ni wakorofi, kuna madereva wengi ambao ni watu wenye heshima zao; madereva wengine wanendesha magari yao wenyewe. Tunaweza kuwa tunatofautiana madaraka na uwezo kipesa, ni vizuri tujenge tabia ya kuheshimu uhai wa watu wengine hata kama ni watu wa chini sana kijamii.

Ni kweli jambo hili watu tunalijadili kulingana na taarifa zinazopatikana lakini hatuna uwezo wa kutoa uamauzi. Ukweli wote utatolewa mahakami.
 
Kwa hiyo kwa maneno yako ni kwamba tuanzishe sheria maalum kwa ajili ya madereva wa dala dala wakigonga mtu tu, adhabu yao iwe kupigwa risasi hapo hapo na yule waliyemgonga,

au tuwaanzishie viongozi sheria maalum, wakigongwa na dala dala tu! iruhusiwe kuwapiga risasi madereva hao wa dala dala, kama alivyofanya blaza Dito?

Mzee WooooooooooooH!

Ahsante kwa ujumbe ila kama nilivyosema, hii mada ni muhimu kwangu kuliko hayo matatizo yako, I cannot help you!, kwa hiyo nitaendelea kulia na mada, na ninasubiri siku ya kesi nitakuwa wakwanza pale mahakamani nijioneee mwenyewe mzizi wa fitina ukikatwa, tena hadharani!
 
Dr.WHO,
Mechi imeanza pale magari yalipogongana.

Pili, bado hunielewi kuwa Guilty tunayozungumzia sisi ni hiyo ya MITAANI sio KORTINI. Kama vile tunavyomhukumu Ossama na 9/11 hali korti na wanasheria wangesema - he is not guilty until.....bra bra bra. Well, Afghanstan na Iraq wanalia leo hii hali korti zipo na bado watu tuna judge matendo yao ama ya Marekani. Na huko nyuma tume judge sana kuhusu Sadaam na wengine kusherehekea pindi alipokamatwa hali hatufahamu lolote zaidi ya kuona ktk TV. Korti imeamua he is Guilty lakini wapo wanaoamini he is not. Madai yao ile ilikuwa vita na Mashia walitaka kupindua serikali yake! Haya bado nikupe nyingine.... Je, kweli hatuwezi kusema yale mauaji ya Pemba serikali yetu ilikuwa guilty ati kwa sababu uamuzi ni wa korti?.
Kwa hiyo jaribu kuelewa tu kwamba hapa kijiweni sii mahakamani bali ni Mtaani na hakuna kati yetu anayesema AUAWE!.. no tunasema Dito ni mkosa, upo uwezekano mdogo sana wa sheria kuchukua mkondo wake kwa sababu ambazo zimeanza kujitokeza. Sababu hizo ndizo zinazoendesha mjadala huu.
Ebu jaribu kufikiria kwa nini aliokota ganda la risasi yake - If he didn't intend to!... Tena inasemekana baada ya tukio risasi zaidi zilipigwa hewani kuwasambaza watu. Well, mimi sina la kuongezea isipokuwa naamini he is guilty na adhabu gani inatakiwa, hapa nawaachia mahakama.

Ogah,
Bastola nyingi za kizamani zilikuwa safety yake Kukoki! kuna kitu kwa juu kimekaa kama kinyundo. Kinavutwa kwa dole gumba la mkono huohuo unaoshika bastola. Kumbukia sinema za Clint Eastwood!. Za siku hizi ambazo zinatumika sana unavuta top part hadi inapo click kisha unaiachia... hapo maneno twende kazini. Mara nyingi bastola hazina safety kama ya bunduki baada ya kukoki.
Haya, penalty miguu 12 halafu mpigaji mwenyewe kisha pewa hela za ubani! mshikaji hapa sijui...Pia sheria hiyohiyo inaruhusu Mawakili wanaruhusiwa kukata deal kama vile manslaughter... hapa mshikaji goli hakuna atapelekwa Tenende mwenye miguu pasi nanuu wala Dito hana haja ya kuchupa.
Mpira unapita juu!..
 
Mheshimiwa Quarz kweli umeniacha hoi.
Kwanza hakuna mtu hapa ambaye amelalamikia kitendo che Dito kuwa na silaha,wote tunajua kuwa anaimiliki kihalali,hilo halina mjadala.
Na lingine ni kuwa kuna kitu kinaitwa insurance,ambayo gari la Dito lazima lilikuwa nayo,na kama ni kosa la daladala,yote huwa yana 3rd party insurance,ambayo ingelitengeneza hilo Prado(kwa mweleo wangu),kwa hio alikuwa ana right ya kuchukia,lakini alijua that was an accident na kuna suluhisho lake,yeye ni mkuu wa mkoa na mtoto wa town,kwa hio kila kitu kingeenda chapchap.
Sasa kama kweli yeye alikwenda akiwa na fikira kama ulivyosema hapo juu kuwa anaenda ku-deal na mvuta bangi,sio simply dereva wa daladala then bado tatizo limeanzia kwake! Na kama kweli tuta-generelise kuwa madereva wa daladala ni wabwia unga na wavuta bangi,basi tatizo pia liko kwa wanao waajiri...ambao wengi ni haohao the likes of Dito and so forth.Where do we draw the line kuwa kaua huku akijua kuwa alikuwa anafanya nini,kutokana ni vigezo vilivyowekwa hapa na wanabodi? Labda mtu angesema wakati akigonga kioo cha marehemu Mbonde miwani yake ikaanguka,akawa haoni na akahisi marehemu kampiga kibao,then kwenye kujihami akajikuta anapiga ris....,au labda alihisi Mbonde anatoka na mkewe...au kasikia raisi anataka kumpa marehemu Mbonde ukuu wa mkoa Tabora.....yaani hata haijipi,hata ikiwekwa vipi! G U I L T Y ! ! !
 
* News Alert *

Habari zilizofika KLH News studio ni kuwa wazazi halisi wa kijana Hassan Mbonde aliyeuawa wiki kadhaa zilizopita na mtuhumiwa Ditopile Mzuzuri, wanatarajiwa kuwasili jijini Dar hivi karibuni kutoka kijijini kwao huko Singida. KLH News itaendelea kuwaletea habari hii inayoendelea kufunguka kila masaa yanavyozidi kupita!
 
mzee kichuguu,
mimi ninawaheshimu binadamu wote bila kujali kipato chao au la,binafsi ni mfuasi mkubwa sana wa sera za mwalimu, binadamu wote sawa na binadamu wote ni ndugu zangu.
katika hii isu ya ditopile intetion yangu ni kuangalia mambo kwa upana wake,ningependa tuende mbele zaidi kuangalia the root courses of the problems ambazo hilo tatizo moja la ditopile ni dalili ya matatizo mengi yaliyojificha ndani yake.
suala zima la daladala pale dar es salaam kwa ujumla wake ni KERO. madeleva wa daladala na makondikta wao ndio wasababishaji wa ajali nyingi katika jiji la dar,kwahiyo ndugu yangu kichuguu katika hilo la kutetea uhai wa binadamu tutee pia uhai wa watanzania wengi amabo maisha yao yanapotea kimyakimya kwa sababu hizo za ajali za uzembe.

mzee zanaki,
sina cha kuongeza kwasababu naona wewe umeshakuwa hakimu na umeshatoa hukumu tayari.

MZEE ES,
kugombea urais ni haki yangu kikatiba na majaliwa ya mungu mwaka 2020 nimeazimia kuchukua form ya urais kupitia chama cha CHADEMA.
kwahiyo naomba unitunzie kura yako ili tuweze kuondoa kero hizi kwa taifa hili.
 
Mkuu wa mkoa akerwa na maderva wa daladala

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, William Lukuvi, amesema sekta ya usafiri wa nchi kavu na majini mkoani hapa imegubikwa na matatizo mengi yakiwemo ya watoa huduma ya mabasi ya daladala kutoa huduma isiyoridhisha, ikiwa ni pamoja na kutoa lugha chafu kwa abiria.

Lukuvi alisema hayo jana kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri wa nchi kavu na majini, ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(Sumatra) na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Alisema kitendo cha watoa huduma ya usafiri, hasa wa mabasi ya daladala kutoa lugha chafu kwa abiria, kuwabughudhi wanafunzi na kutoza nauli wanazotaka, kumesababisha wakazi wa mkoa huo kukata tamaa na usafiri huo.

Alisema hali hiyo imekuwa kukichangiwa na mambo mengi yakiwemo ya miundombinu dhaifu iliyopo katika mkoa huo na utendaji mbaya wa mamlaka na taasisi husika katika kusimamia na kudhibiti watoa huduma ya usafiri.

Alisema tatizo lingine ni elimu ndogo ya haki na wajibu wa watumiaji katika kuboresha huduma za usafiri kama uzembe wa wahudumu na waendesha vyombo vya usafiri, kama vile madereva na makondakta kutofuata sheria za usalama barabarani na ukiukwaji wa sheria za uendeshaji biashara ya usafiri wa abiria.

Alisema mkutano huo wa wadau wa huduma ya usafiri wa majini na nchi kavu kumekuja wakati muafaka ambapo mkoa umepania kupunguza matatizo yanayotokana na huduma ya usafiri isiyoridhisha.

Hata hivyo, alisema hivi sasa mkoa wa huo una mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 5554.2.
 
Back
Top Bottom