Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 9,138
- 22,236
Mkuu kwenye hii hospital ninayofanyia kazi siku hizi tunaingia ofisi 07:30 then tunakuwa na vikao vya Morning Report mpaka 09:00 hadi 09:30.Upo sahihi sana. mimi nampenda sana mama samia ktk utendaji wake ila la hili la nidhamu ya moyoni kwa watumishi wa umma mama aliangalie vizuri.Kuchelewa kazini, kutokatoka hovyo kuzurula, kwenda kucheza kamali wakati wa kazi na vijiwe vya mpira vinashusha sana nidhamu ya kazi ktk secta zote.utakuta 80% ya watumishi wa umma wanastahili kufukuzwa kazi kila siku kwa utovu wa nidhamu.
utakuta wizara zote za serikali zina cheo kiitwacho ofisi supevisor maajabu yake ofisi supevisor hafuatilii watoro kazini, wacheza kamali, wafanyao ngono maofisini wala kuwabana wachelewaji. Hwa maO.S, utakuta siku zote ni father X-mass tuu na hupenda kununua stationary tuu!matokeo yake katika wizara zote za serikali huwezi kumtuka mfanyakazi aitwae workaholic(yaani yule aketie kitini na kujituma kazini mpaka anaambiwa nenda nyumbani kinguvu}
mimi binafsi namuomba sana mama awe mkali sana na avae ndita muda wote maana tupo katika kipindi cha heated economy la sivyo wajanja watamuangusha kisawasawa..
Hapo mtaenda kuhudumia wagonjwa hadi kwenye 10:30 halafu watu wanaenda canteen kunywa chai. Chai inanyweka huku stori zinapigwa hata mpaka 12:00 hivi au zaidi.
Mkirudi mnafanya kazi saa moja au moja na nusu mnarudi canteen kupata lunch ndio mpaka saa 15:30 watu wanarudi ku-sign out. Siku imeisha.
Hiyo ndio nidhamu ya moyoni ya hawa Watanzania hapa nilipo. Enzi za Magufuli tulinyooshwa na kazi zilifanyika kwa weledi knowing ukizingua imekula kwako.
RIP Magufuli.