Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali

Mkuu kwenye hii hospital ninayofanyia kazi siku hizi tunaingia ofisi 07:30 then tunakuwa na vikao vya Morning Report mpaka 09:00 hadi 09:30.

Hapo mtaenda kuhudumia wagonjwa hadi kwenye 10:30 halafu watu wanaenda canteen kunywa chai. Chai inanyweka huku stori zinapigwa hata mpaka 12:00 hivi au zaidi.

Mkirudi mnafanya kazi saa moja au moja na nusu mnarudi canteen kupata lunch ndio mpaka saa 15:30 watu wanarudi ku-sign out. Siku imeisha.

Hiyo ndio nidhamu ya moyoni ya hawa Watanzania hapa nilipo. Enzi za Magufuli tulinyooshwa na kazi zilifanyika kwa weledi knowing ukizingua imekula kwako.

RIP Magufuli.
 
Kwa hiyo hiyo hospitali mnasubiri Rais aje awaambie jinsi ya kutumia muda?

basi hiyo ni hospitali ya vichaa kuanzia Director/Incharge mpaka mfagizi.
 
Mwanzo tuliamini anapotoshwa lakini kadiri siku zinavyozidi kuongezeka tunaanza kushawishika vinginevyo.
 
Kwa hiyo hiyo hospitali mnasubiri Rais aje awaambie jinsi ya kutumia muda? basi hiyo ni hospitali ya vichaa kuanzia Director/Incharge mpaka mfagizi.
Siyo lazima aje Rais. Kipindi cha Magufuli hata bila Rais kuja kulikuwa na usimamizi mzuri.

Kila mtu aliwajibika ipasavyo huku akijua asipofanya hivyo atakuwa kwenye matatizo.

Sasa hivi hakuna anayesimamia... Jana ndio tumeambiwa hii ni nidhamu ya moyoni.
 
kwani sasa hivi hamuwi kwenye matatizo? siku yakikukuta utashukiwa individually.

Hata kipindi cha Magu walikuwepo nunda kama wewe, ndio maana leo tunawaona Makonda na Sabaya wakitiwa akili.

Wangekuwa wameisha watu wa hovyo basi jiwe asingekuwa anafukuza/simamisha watu kila leo.

Concern ya Rais ni smart sana,tusimamie taratibu kama wasomi na sio nguruwe mpaka aswagwe.

Tujenge taasisi imara za kusimamiana,rais atapita lakini taasisi smart zitabaki. Mf mzuri Hayati amesepa halafu mnabaki na nini?hayati angekuwa smart angeimarisha taasisi na sio kukaza kichwa tu kama vile utakuwepo milele
 
Huo ni ushamba
 

Usichanganye ukali na jazba. Mkali ni kuchukua hatua stahiki dhidi ya kosa halali au uzembe, na haya hufanyika pasi na kinyongo wala kusaka sifa za kijinga.

Jazba ni kuchukua hatua za kukomoa, na wakati mwingine ni kuchukua hatua kwa nia ya kukomoa ama kudhalilisha na kupandikiza vitisho na nidhamu ya woga.

Mfano mrahisi, Nyerere alikuwa mkali, lakini Magufuli alikuwa na jazba.
 

Kutuma vyombo vya dola kuteka watu na kuwabambikia kesi?

Kuagiza wakurugenzi kunajisi uchaguzi hiyo ni nidhamu ya dhati au woga.
 
Hakuna sehemu nimesema nimefanya hivyo.

Halafu actually hapo hakuna jinai yoyote ila usimamizi.

Na mkuu wa nchi amesharuhusu, na hiyo ndio hali halisi ya Watanzania - hatupendi kazi.
 
Kutuma vyombo vya dola kuteka watu na kuwabambikia kesi? Kuagiza wakurugenzi kunajisi uchaguzi hiyo ni nidhamu ya dhati au woga.
usipindishe mada kuleta mambo irrelevant; swala hapa ni usimamizi wa subordinates.

Mambo hayo mengine ni speculations zako tu, kwani kwani serikali haifanyi kazi za kesi na uchaguzi tu.
 
Hakuna kitu kinachoitwa nidhamu ya moyoni!
Nadhani mama amesahau kwamba wabongo ni watu wanaotaka kulazimishwa kufanya kazi.

Enzi zile bwana Lyatonga ilibidi awe anatoa viti vilivyokutwa wazi maofisini, wenyenavyo wako kitaa tu kula bata wakati wa kazi.

Wakati wa Kikwete nidhamu ya kazi ilishuka kupita kiasi kwa sababu rais hakuwa serious with anything, zaidi ya kuchekeana na kukwaa pipa kwenda kula bata majuu.

Wakati wa JPM nidhamu ya kazi ilirudi, japo ilikuwa ya woga, lakini watu walianza kufanya kazi na ufanisi wa utendaji ukaongezeka, na sisi makapuku tukawa tunahudumiwa humo maofisini.

Sasa Samia anahubiri nidhmu ya moyoni, mi naona tunarudi kwenye enzi za awamu ya 4!
 
usipindishe mada kuleta mambo irrelevant; swala hapa ni usimamizi wa subordinates. Mambo hayo mengine ni speculations zako tu, kwani kwani serikali haifanyi kazi za kesi na uchaguzi tu.
speculations kwako,sio kwa kila mtu. si huyu Lissu kasema alipigwa risasi na kitengo cha ikulu?
 
usipindishe mada kuleta mambo irrelevant; swala hapa ni usimamizi wa subordinates. Mambo hayo mengine ni speculations zako tu, kwani kwani serikali haifanyi kazi za kesi na uchaguzi tu.

Unataka mjadala uwe ndani ya utashi wako boss?
 
You are too local and too mannual.

Siku hizi inaongoza akili, teknolojia na uchumi imara sio kufoka foka.

Achana na hawa watu wamezoea kuchunga ng'ombe, wanafikiri na binadamu anachapwa tu mijeledi kama ngombe,

Ndo maana nyumba nyeupe hawatakaa wapate bahati tena ya kuingia!
 
Msameheni tu huyu ndugu zanguni.

Hajui na wala hajawajua WAHUNI wapoje. WAHUNI wameshamteka tayari. Nchi imerudi kwa WAHUNI.
Tukumbuke:-

*Angekuwepo JPM, umeme usingekuwa unakatika katika kama ilivyo sasa.

*Angekuwepo JPM, mbolea na bidhaa zingine zisingekuwa zimepanda bei kwa kiasi hiki cha 120%.

*Angekuwepo JPM, Ajali nyingi zinazotokea zisingekuwepo.
Kilichomsaidia JPM kudhibiti upumbavu huu ni ukali wake.

Maana ilikuwa akiongea tu, hadi sisimizi wanasikia sauti yake.

Nashangaa kuona kiongozi anasema tena hadharani eti hataweza kumkaripia mtu aliyekosea.

Tafsiri yake ni kwamba, Dereva ameachia usukani, kwa hiyo kila abiria apambane na hali yake ili kujinusuru.
 
..Na ni lazima atese na kuua wapinzani wake.

..pia awe mbaguzi na apendelee eneo anakotoka.
 
Nchi imara itakayostahimili majaribu ya muda haijengwi kwa ukali wa kiongozi mmoja, hujengwa na mifumo na taasisi imara.

Haya mambo ya kufokeana na ukali ndio yakafanya hadi ma-DC na RC wajitoe ufahamu ili waonekane ni watendajj bora kwa kufokea watumishi mbele ya camera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…