Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali

Nimecheka kwa nguvu, kwahiyo picha ya rais iko ukutani maana ni Mungu?! Kwahiyo ukizingua hakuna sheria za kukuwajibisha, bali mpaka rais akuchukulie hatua kali?
Ahaaa, hizo sheria na taratibu zinafuatwa kwa niaba ya rais. Hujui hilo?
 
Peleka upuuzi huko!
Sio kazi ya mkuu wa nchi kufanya micromanagement!
Huhitaji kunyooshwa na ng'ombe yoyote. Wewe na mkuu wako wa kazi jifunzeni majukumu yenu.
Hii nchi imejaa ujinga sana.
 
Sasa hakuna nchi duniani iliyoendelea kwa mfumo huo mnaotaka wa Rais kuwa msimamizi wa madaktari, manesi, walimu, TRA, polisi, immigration, kilimo n.k
Tafufuteni mfumo mwingine, miaka 60 imetosha kuwapa funzo.
Actually Rais ni msimamizi wa kila mmoja.

Akiwa imara huko juu chain itashuka mpaka chini. Vice versa is true.

Mfano mzuri angalia uongozi hodari wa JPM.
 
Nachojua mm Rais was Nchi alikufa mwaka Jana.
 
Usukuma unakusumbua haki! 'Sang'udi'
Usukuma unaingiaje hapa?

Kwani Wasukuma wote wanampenda Magufuli?

Makabila mengine hawampendi?

Halafu unajua Magufuli mwenyewe hata hakuwa Msukuma!!!
 
Peleka upuuzi huko!
Sio kazi ya mkuu wa nchi kufanya micromanagement!
Huhitaji kunyooshwa na ng'ombe yoyote. Wewe na mkuu wako wa kazi jifunzeni majukumu yenu.
Hii nchi imejaa ujinga sana.
Enzi za Magufuli hakuwahi kuja hospitalini kwetu ila kulikuwa na nidhamu ya kutosha! Ukiwa kiongozi imara na taasisi zote zinakuwa imara.
 
Unapata taasisi imara kwa kuwa na katiba mpya ambayo imeandikwa kwa kusimamia misingi ya utu na demokrasia.
Uwajibikaji na kujielewa, muhimu sana. Sio kufoka na ukali uchwara.
 
Jiandaeni kushuka na kuwa nchi maskini tena, muda si mrefu subiri IMF wafanya kikokotoo chao, mtatafuta pa kujificha
 
Kwani Katiba ya JMT ya mwaka 1977 inasemaje kuhusu sifa za Rais? Je haul unayoyataja yapo?
 
Kinachotakiwa si UKALI na kutisha tisha viongozi waliochini yako hapana, bali ni kuweka mifumo imara ya utawala wa nchi ambayo inaanzia kwenye Katiba.
 
Mbona Raisi wa Zambia sio mkali na nchi inatembea anatimiza ahadi alizowaahahid wananchi kipind cha kampeni mzee sio lazima uwe mkali kuendeleza nchi zinaitajika strategies katika kuiongoza sio ukali fatilia siasa za Botswana afu uje uandike upuuzi wako tena
 
Haya ndiyo yanayotokea hivi sasa hapa nchini, Mama yu mpole akisingizia vita vya Ukraine na urusi na sasa swaumu eti hataki kuwakaripia viongozi useless serikalini. Matokeo yake sasa huko serikalini tumerudi kwenye zama zile zile za awali, wafanyakazi wako incomptent, rushwa imeshamiri kila upande tena nje nje. Mama anaturudisha nyuma sana kimaendeleo.
 
Hakuna Mtanzania anayependa kufanya kazi bila kusukumwa.

Ndio maana sasa hivi ubora wa huduma za umma umeshuka sana.

Tunapewa majibu ya hovyo na hatuna cha kuwafanya.
huo upumbavu pelekeni chato sio kwa watu wenye akili utupeleke kama mbuzi
 
Ndio Magufuli alikuwa Hana hayo yote ila hatukuwahi kuona umeme unakatika hovyo , inflation rate Leo Ni kubwa kuliko miaka mitano nyuma.

Jana nimeenda dukani nimekuta sabuni ya unga ya 1,000 inauzwa 1,200 na Soda ya 500 inauzwa 600.

Maji ya Uhai ya 500 yanauzwa 600. Kama huna Cha kujifunza hapa Basi.


Magufuli alikuwa na mapungufu Yake kama binadamu ila Kuna mazuri mengi alifanya.
 
Ulimwengu ulioendelea ajira nyingi za utumishi wa umma zinatolewa kwa mikataba ya muda maalum na kunakuwepo na tathmini ya utendaji kila baada ya muda fulani, ukiwa chini ya viwango vya utendaji unatimuliwa na bodi baada ya bosi wako kufikisha ripoti yako.
Huku kwetu kesi ya nesi, daktari, mwalimu, polisi, mwanajeshi wa ngazi za chini inafanywa suala la wizara.
 
Kama unapenda maisha ya unyapara nenda kaishi jela. Fullstop.
 
Huyo kilaza hajui hata hakuna sheria ya nchi inayoamrisha kuweka picha za Rais maofisini
Nimecheka kwa nguvu, kwahiyo picha ya rais iko ukutani maana ni Mungu?! Kwahiyo ukizingua hakuna sheria za kukuwajibisha, bali mpaka rais akuchukulie hatua kali?
 
Usukuma unaingiaje hapa?

Kwani Wasukuma wote wanampenda Magufuli?

Makabila mengine hawampendi?

Halafu unajua Magufuli mwenyewe hata hakuwa Msukuma!!!
Magufuli alikuwa Mrundi, huu ndio ukweli na utabaki hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…