Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali

Kwa hiyo hiyo hospitali mnasubiri Rais aje awaambie jinsi ya kutumia muda?

basi hiyo ni hospitali ya vichaa kuanzia Director/Incharge mpaka mfagizi.
Hao watu ni sawa na ngombe hadi waswagwe.Miafrika tuna shida sana ndo maana huyo jamaa anaona ufahari kujisifia ujinga.
 
Sheria na taratibu za nchi hazifwatwi kwa niaba ya Rais au ili kumpendeza Rais. Utawala wa sheria upo ili watu waweze kuishi kistaarabu kwa haki na utu tofauti na hayawani ambao mwenye nguvu ndio anaamua chochote kinachomfaa.
Ahaaa, hizo sheria na taratibu zinafuatwa kwa niaba ya rais. Hujui hilo?
 
Siyo hospital yetu tu, hali ipo hivyo kote.

Hakuna nidhamu ya moyoni na kwa asili Waafrika hatupendi kazi, tunaona ni utumwa.

That's why tunahitaji kiongozi imara kama Magufuli anayeweza kusimamia vizuri.

Na hiyo ndio nidhamu yetu ya moyoni.
Kiongozi imara wakufoka utamtoa wapi kila mara?.Hatupendi kazi sio kwasababu hatuna kiongozi imara bali nikwasababu sheria na taratibu zinazosimamia maeneo yetu ya kazi hazijawekewa mifumo thabiti yakuwajibika.ndo maana wenye akili wanaona kuna huitaji wa katiba mpya itakayoweka taratibu kwenye kila idara kwa miaka mingi zaidi badaya yakusubiri binadamu aje kutukemea tupende kazi.
 
Na hapa ndio Katiba Mpya hutajwa
 
Nyumbu pekee ndio atatamani kufanywa hivi?👇

 
Magufuli hakuwahi kuja kutuambia tuwajibike, ila watu waliwajibika. Nani mjinga hapo?
 
Huyo "kiongozi wa kufokafoka" alitufanya tukazipenda kazi zetu.
 
Hakuna Mtanzania anayependa kufanya kazi bila kusukumwa.

Ndio maana sasa hivi ubora wa huduma za umma umeshuka sana.

Tunapewa majibu ya hovyo na hatuna cha kuwafanya.
Kuna watanzania wanajituma sana haswa kwenye sekta zenye kutoa maslahi bora kwa wafanyakazi. Kama mfanyakazi wa umma analipwa mshahara kama mkia wa mbuzi hata ukimsukuma ataharibu tu. Pili ili nchi yetu isonge mbele ni lazima tuwe na mifumo imara isiyotegemea utashi wa mtu mmoja. Mfumo wa sasa ambapo utashi wa mkuu wa nchi ushuka hadi kwa viongozi wa vitongoji hauna tija.
 
Mbona Magufuli hakuajiri wala kupandisha madaraja, ila huduma zilikuwa bora?
 
Itabidi ukamfufue jamaa yako aje kuongoza tena maana tumechoka na kelele zako.
 
Ziacheni hizo kazi zenu, kaeni pembeni, msubirini mwingine ambaye anaweza kufokafoka. Wapo wengi wanaozitaka hizo kazi zenu na wanaweza kuzifanya vizuri kwa weledi bila kufokewafokewa.
Huyo "kiongozi wa kufokafoka" alitufanya tukazipenda kazi zetu.
 
Maza anafikiri Chuo cha Uongozi ndiyo suluhisho. Sijui anafikiri wafanyakazi wote laki 5 atawapeleka huko.

Hii lugha ya kubembeleza bembeleza haitamsaidia.
 
Kwani huu umeanzisha ww hivyo unatembea na marking scheme, au ni wa mumeo hivyo una haki ya urithi kwenye kila kitu cha mumeo?
Matusi ya nini mzee; ninaelewa kuwa ni kawaida ya debe tupu kupiga kelele, lakini haikuwa ni lazima upige kelele nyingi.
 
Haya ndiyo yanaitwa mawazo mgando. Nchi yenye Katiba Bora lazima iwe na mifumo inayofanya kazi.

Kuwa na Rais anayefoka ni kielelezo cha mapungufu ya mfumo au ya Rais mwenyewe. Kwa nini UFOKE wakati una vyombo vyako vya kufanyia kazi.

Iko siku Nyankurungu2020 utakuja sema kuwa Tanzania inapaswa kuwa na Rais anayetafuna mahindi barabarani, au Rais anayenunua mapapai au Rais anayekaa vijiweni.

Hayo maujinga yote tumeyafukia na Mwendazake mwaka jana mwezi Machi pale Chato
 
Sasa huo ni uzembe wenu nyie msitujumuishe na sisi.
 
Nyerere hakuwa na hulka (compulsive) ya kufokea viongozi na watumishi ovyo ovyo tena hadharani. Ilifanyika kwa visa na nyakati maalum. Wala haikuingia mubashara kwenye media (magazetini na kwenye radio).

Mambo yalikuwa yakimalizwa katika mazingira ya kiofisi Ikulu. Wananchi walikuwa wakijionea matokeo tu na kukisia kuwa kuna mtikisiko umepita huko Ikulu, au wizarani au kwenye shirika au kwenye taasisi. Kinachofuatia ni kuvuja kwa udaku.

Hii ya awamu ya tano ni kipropaganda zaidi kama show biz vile. Maagizo ya kazi, maonyo, kejeli, vitisho, adhabu zinatangazwa hadharani hata kwenye taarifa ya habari. Ujinga huo haukuwepo wakati wa Mwalimu na nidhamu ilikuwepo.
 
Magufuli hakuwahi kuja kutuambia tuwajibike, ila watu waliwajibika. Nani mjinga hapo?
Wewe kinachokusumbua inaonekana uko kwenye kundi la legacy badala ya kuangalia mahitaji ya nchi.Unachoshindwa kurlewa ni kwamba kabla ya huyo magufuli kazi zilikuwepo na watu walifanya na zitaendelea kuwepo hadi mwisho wa dunia.Kwahiyo hakuna mtu special kwenye nchi.Ndo maana tunasema hakuitajiki kua na mtu wakutusukuma bali iwepo mifumo ili ifanye kazi miaka mingi zaidi umri ambao huyo mtu wako wakukufokea hawezi kufika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…