Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Nimesoma andiko lako lote nimegundua udhaifu mkubwa kwenye hii kesi yako na hao wakubwa zako. Anyways msaada wako ulitakiwa kuishia tu kwa kumuelekeza mzazi (huyo Mama) kwa watawala ama wahusika ili afuatilie kila kitu mwenyewe kuanzia kwenye issue ya uhamisho wa binti mwenyewe. Kulichukua hilo jambo na kulifanya kama lako ama wewe ndo mzazi wa huyo binti ama mume wa huyo Mama ndo shida ilipoanzia. Wema una mipaka yake na kua makini na kufanya wema kwa mtu ambao una athari hasi kwa watu wengine specifically wakubwa zako. Kitendo cha kumwambia huyo Mama akareport hilo swala kwa katibu tawala kwako uliona ni msaada ila ulikua unawachomea utambi na kuwaharibia kazi wakubwa zako kitu ambacho wasingeweza kukubali kirahisi na hapo inamaana tayari ulikua ushaanzisha vita. Mbaya zaidi vita yako inahusisha mwanamke (huyo Mama) na mbaya kuliko vyote inahusisha mwanafunzi wa kike underage [emoji725] halafu uko kwenye kada ya elimu/ ualimu ambapo kimaadili na kiutumishi inakubana sana ukihisishwa na jambo hilo. Sijui kama kuna vitu umeficha lakini kama ulichoeleza ndo ukweli ulivyo basi fuatilia ngazi za juu hata Wizarani utachomoka tu japo itachukua muda ila haki yako itapatikana. Kwa maisha ya sasa acha kila mtu ahangaike na watu/ familia yake maswala ya kujifanya mwema sana tena wema wenyewe unahusisha mwanamke/ mtoto wa kike utaharibu tu future yako Mzee.
 
 
Wewe utakuwa umetembea na huyo mwanafunzi,haiwezekani utengenezewe zengwe kubwa namna hyo. Kwa faida ya nani? Usitafute kujisafisha hapa.
Mimi nahisi issue inaweza hata sio kutembea na huyo mwanafunzi. Issue iko kwa huyo Mama mwenye mtoto. Hapo kuna yule Mwalimu mwenzie alomtaka kimapenzi huyo Mama, kuna Mwalimu Mkuu, jamaa mwenyewe na mume wa huyo Mama. Hapo kuna kufanyiana visa tu kupitia huyo Mama. Mwalimu Mkuu na yule Mwalimu mwingine wamemchonganisha jamaa kwa mume wa huyo Mama na kwakua kesi ya watu wazima kumhusisha huyo Mama kimapenzi na jamaa yetu ni nyepesi na itaisha tu kimazungumzo maana ngumu kumkamata ugoni imebidi jamaa atengenezewe zengwe la kutembea na mwanafunzi wakijua hapo jamaa hachomoki leo wala kesho watakua washamkomoa ila kwa mtazamo wangu chanzo ni maslahi ya kimapenzi kwa hao wote watatu kwa huyo Mama naona kila mmoja kwa wakati wake alikua anamtaka huyo Mama wakazidiana maarifa then wameishia kokomoana
 
Hakuna haki nchi hii kama ni hivyo, inawezekanaje niwatreat wenye matatizo na wasiokuwa na matatizo the same?
Kwamba ilibidi nimuache mtoto mwenye shida ya Usajili kwa kuwa tu ni binti?
Changamoto sana!
1. Ni kweli haki huwa inapindishwa na ndio maana inatakiwa uchukue tahadhari kubwa kwenye mazingira unayokuwapo ili uwe salama. Acha kila mtu afanye kazi yake usipitilize.
Pia hukutoa taarifa takukuru hapo mwanzoni kabisa. ( Sijui kwanini)

2. Ndio, ilibidi uachie wataaluma na walimu wa malezi.

3. Hata ukifanikiwa kurudi kazini, punguza ukaribu uliopitiliza na wanafunzi wa Kike. Hii umefukuzwa kazi lakini Worst case scenario unaweza kufungwa au kupoteza maisha kabisa.
 
Ni sahihi, kuna kitu anaficha huyu mwalimu.
 
Fanya issue nyingine mshahara wenyewe kiduchu Si uwabwagie likazi lao?
 
Ndugu zangu, naombeni sana mnielewe kuwa najua umuhimu wa kuwa muwazi. Nimejieleza sana kwenye comment zilizopita, huo ndio uhalisia wangu ndugu zanguni!
Mimi pia nimeshangazwa na hili ndio maana nimekuja humu kuwaomba msaada
 
Sawa mkuu. Nashukuru sana
 
Ushauri mzuri lakini Kwa kesi ilipofikia RAS na DAS Hawana msaada tena kwake, sema Kwa nature ya suala lake kama kweli kosa ndo Hilo ilibidi awe amefukuzwa kazi na kapelekwa mahakamani akisubiria mvua 30
 
Inaonesha wewe mwl ulikuwa karibu na huyo mwanafunzi, kuna shida mahali haiwezekani kila kiongozi awe against wewe
Hata kama angekuwa karibu vip, huwezi fukuzwa kazi Kwa tuhuma hiyo,ingethibitika bila shaka huyo angekuwa yupo gerezani maana Sheria Iko straight ukitembea na mwanafunzi ikathibitika ni miaka 30 jela, sasa mbona yupo uraiani?
 


Mambo ya kuzingatia kwa waajiriwa:

1. Ukiwa kazini angalia salary yako tu.
2. Ufisuate mambo ya watu.
3. Acha uana harakati wa haki.
4. Wema usipitilize.

Either :

1. Hao jamaa kuna namna mna ugomvi wa chini chini na wameamua kukuangamiza, inaonekana wamefanikiwa.

2. Umeteleza kweli na kukula mtoto wa rafiki yako na sasa mambo kwisha haribika, pole sana, (Sikuhukumu, ni hisia tu.

Achana na hivi vita, kwa hapo ulipofikia, wewe ngoja barua ijibiwe na maisha lazima yaendelee, anza harakati nyingine za kutafuta kipato.

Nitarudia:

- Wema ni mzuri, ila usipitilize na kuingilia sana mambo mpaka utengeneze uadui na watu.

- Watu wanao amini katika ajira mara nyingi huwa na mapambano sana, wivu, chuki na vinyongo.
 
Mkuu

Ukiondoka hapo shuleni mkuu wa shule anapata faida fani?

Ukibaki hapo shuleni mkuu wa shule anapata hasara gani?
Ndugu Kuna watu wanaroho mbaya sana hujajua tu hapati faida yoyote ila anakuwa comfortable tu wewe kufukuzwa kazi.kama upo kwenye utumishi wa umma huwezi shangaaa hivi vitu
 
Ndugu Kuna watu wanaroho mbaya sana hujajua tu hapati faida yoyote ila anakuwa comfortable tu wewe kufukuzwa kazi.kama upo kwenye utumishi wa umma huwezi shangaaa hivi vitu
Ni kweli sipo kwenye ajira.

Lakini wanaume hua tunagombana kwaajili ya ishu mbili tu. Wanawake au pesa.

Chimbuko la ugomvi wetu huanzia hapo. Kama mtu hauzuii pesa yake na hauna time na mwanamke wake ni atakuchukia tu ila hatoenda extreme hadi kukuzushia kesi ufukuzwe.
 
Shukrani sana. Maelezo yako yamekaa sawa na nimeyaelewa vizuri. 🙏
 
mie nahis mkuu alitaka rushwa katika regstration ya mtoto .ndo hyu ticha akampa mfumo wa siri wakufika ngazi za juu ..mkuu akaona anaharibiwa dili hapo...
Makox hebu clear hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…