Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Dogo mbishi. Tunamwambia bado anakuwa mbishi.Hapa ndio maswali huja jamii ni ngumu kukurlewa hata kama ulikuwa na nia njema
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dogo mbishi. Tunamwambia bado anakuwa mbishi.Hapa ndio maswali huja jamii ni ngumu kukurlewa hata kama ulikuwa na nia njema
Dogo mbishi. Tunamwambia bado anakuwa mbish
Pia kawa muhanga wa laana ya familia Pana watu wenye laana ukishiriki nao Kwa jambo lolote unaunganishwa nao laanaNimesoma andiko lako lote nimegundua udhaifu mkubwa kwenye hii kesi yako na hao wakubwa zako. Anyways msaada wako ulitakiwa kuishia tu kwa kumuelekeza mzazi (huyo Mama) kwa watawala ama wahusika ili afuatilie kila kitu mwenyewe kuanzia kwenye issue ya uhamisho wa binti mwenyewe. Kulichukua hilo jambo na kulifanya kama lako ama wewe ndo mzazi wa huyo binti ama mume wa huyo Mama ndo shida ilipoanzia. Wema una mipaka yake na kua makini na kufanya wema kwa mtu ambao una athari hasi kwa watu wengine specifically wakubwa zako. Kitendo cha kumwambia huyo Mama akareport hilo swala kwa katibu tawala kwako uliona ni msaada ila ulikua unawachomea utambi na kuwaharibia kazi wakubwa zako kitu ambacho wasingeweza kukubali kirahisi na hapo inamaana tayari ulikua ushaanzisha vita. Mbaya zaidi vita yako inahusisha mwanamke (huyo Mama) na mbaya kuliko vyote inahusisha mwanafunzi wa kike underage [emoji725] halafu uko kwenye kada ya elimu/ ualimu ambapo kimaadili na kiutumishi inakubana sana ukihisishwa na jambo hilo. Sijui kama kuna vitu umeficha lakini kama ulichoeleza ndo ukweli ulivyo basi fuatilia ngazi za juu hata Wizarani utachomoka tu japo itachukua muda ila haki yako itapatikana. Kwa maisha ya sasa acha kila mtu ahangaike na watu/ familia yake maswala ya kujifanya mwema sana tena wema wenyewe unahusisha mwanamke/ mtoto wa kike utaharibu tu future yako Mzee.
Mimi nahisi issue inaweza hata sio kutembea na huyo mwanafunzi. Issue iko kwa huyo Mama mwenye mtoto. Hapo kuna yule Mwalimu mwenzie alomtaka kimapenzi huyo Mama, kuna Mwalimu Mkuu, jamaa mwenyewe na mume wa huyo Mama. Hapo kuna kufanyiana visa tu kupitia huyo Mama. Mwalimu Mkuu na yule Mwalimu mwingine wamemchonganisha jamaa kwa mume wa huyo Mama na kwakua kesi ya watu wazima kumhusisha huyo Mama kimapenzi na jamaa yetu ni nyepesi na itaisha tu kimazungumzo maana ngumu kumkamata ugoni imebidi jamaa atengenezewe zengwe la kutembea na mwanafunzi wakijua hapo jamaa hachomoki leo wala kesho watakua washamkomoa ila kwa mtazamo wangu chanzo ni maslahi ya kimapenzi kwa hao wote watatu kwa huyo Mama naona kila mmoja kwa wakati wake alikua anamtaka huyo Mama wakazidiana maarifa then wameishia kokomoanaWewe utakuwa umetembea na huyo mwanafunzi,haiwezekani utengenezewe zengwe kubwa namna hyo. Kwa faida ya nani? Usitafute kujisafisha hapa.
1. Ni kweli haki huwa inapindishwa na ndio maana inatakiwa uchukue tahadhari kubwa kwenye mazingira unayokuwapo ili uwe salama. Acha kila mtu afanye kazi yake usipitilize.Hakuna haki nchi hii kama ni hivyo, inawezekanaje niwatreat wenye matatizo na wasiokuwa na matatizo the same?
Kwamba ilibidi nimuache mtoto mwenye shida ya Usajili kwa kuwa tu ni binti?
Changamoto sana!
Ni sahihi, kuna kitu anaficha huyu mwalimu.Mh maelezo yanatia uwalakini kidogo. Iweje watu wote hao wakubaliane kirahisi na uongo wa mkuu wa shule?
Kuanzia mzazi, mwanafunzi, mratibu, afisa elimu na tcs? Hata walimu wenzio wanaojua ukweli walishindwa kabisa kupenyeza taarifa kwa wahusika au ndo wote hao walipangwa na mkuu wa shule au wote hao wana chuki? Kufukuzwa kazi serikalini siyo ishu rahisi hata kidogo kuna jambo nyuma ya pazia ambalo hauko tayari kuliweka wazi
Fanya issue nyingine mshahara wenyewe kiduchu Si uwabwagie likazi lao?Mimi ni Mtanzania mwezenu, nimeandika na kuweka katika jukwaa hili ili niweze kujengewa uwezo na ushauri na yeyote atakayeguswa na habari yangu; kama kuna sehemu haitaeleweka nipo kwa ajili ya ufafanuzi. Tafadhari siyo sawa kutumia lugha za matusi, kejeli na dharau kwani kila mtu ana changamoto yake.
Nimekuwa mtumishi wa Serikali katika kada ya ualimu tangu 2013-2023 mwezi wa tano. Nikiwa katika utekelezaji wa majukumu yangu nimekutana na changamoto nyingi sana za kawaida ambazo ni muhimu kazini.
Changamoto iliyonileta hapa ni hii sasa ambayo ni hatari kwa maisha yangu, familia yangu na jamii kwa ujumla.
Nilianza kanzi katika kituo xx, nikiwa huko nilikuwa karibu sana na mfanyakazi mmoja Askari wa Maliasili, nikiishi naye vizuri mpaka nahama kule mwaka 2017. Kwa bahati mbaya yule askari alikuja kupata changamoto za kiafya na akili na hivyo kupelekea familia yake kuyumba sana na hatimaye ndoa yake kuvunjika.
Mwaka 2022 january, nikiwa naendelea na majukumu nilikutana na Mke wa rafiki yangu(Yule Askari) akiwa amekuja shuleni kufuatilia taratibu za kumhamishia pale mtoto wake aliyetakiwa kuanza kidato cha kwanza shule niliyokuwa nafundisha awali, alifurahi sana kuniona kwani hakufahamu kama nilihamia pale. Baada ya kusalimiana alinijulisha juu ya changamoto alizopitia mpaka ndoa kuvunjika na tayari alikuwa ameolewa na mtu mwingine hatimaye tukaja kwenye changamoto ya uhamisho wa mtoto wake.
Kwa maelezo yake alifanikiwa kupewa namba za simu za makamu mkuu wa shule ili aweze kuomba nafasi, kwa bahati mbaya alipewa majibu kuwa nafasi zimejaa lakini atampatia namba za mwalimu mwingine ajaribu kuongea naye. Mama baadae alitumiwa namba hizo na kufanya mawasiliano na mwalimu huyo.
Majibu ya mwalimu yalikuwa Ahadi ya kupatikana kwa nafasi endapo mama [mzazi] atafanikiwa kuwapata watoto wengine angalau watatu ili wawe wanne na watatakiwa kulipia nafasi hizo kwa Tsh.20000 ili jumla iwe 80000. Majibu ya mzazi ilikuwa haiwezekani kutokana na ugeni wa mazingira na kutokufahamu ni nani mwenye uhitaji huo kwa haraka.
Basi yule mwalimu akamtaka mzazi atoe 50000 kwa ajiri ya nafasi ya mtoto. Kutokana na ugumu wa maisha ilionekana pesa kuwa ni nyingi mno, wakakubaliana kulipana 40,000/=, Lakini kadri muda ulivyozidi kwenda bado haikuwezekana kupatikana kwa pesa hiyo. Baada ya kuona hivyo mzazi ilibidi atoe taarifa hiyo kwa huyo mwalimu. Mwalimu aliyapokea majibu na kuamua kubadirisha masharti hayo na kumtaka yule mzazi kingono kwa siku tatu mfululizo ili ampatiye nafasi.
Kwa mujibu wa mzazi ilikuwa ni vigumu kwake kukataa na kukubali pia, lakini kutokana na uhitaji wake alikubali kufanya hivyo ili mtoto apate haki nafasi ya masomo, japo aliamini kuwa ingemuathiri sana kisaikolojia.
Hivyo siku niliyokutana naye pale shuleni ni siku aliyohitaji kuja kuonana na mwalimu kwa kuwa hawakuwahi kuonana.
Baada ya kunipa maelezo hayo nilimwuliza kama anamfahamu angalau kwa jina, akasema hamfahamu. Nikaamua kuomba namba yake, ilikuwa ni ngeni kwangu, lakini baada ya kuangalia kwenye mtandao wa M-Pesa niligundua kuwa ni namba ya mwalimu niliyemfahamu.
Kwa kumsaidia yule mama nikamwambia yule mama namfaham mwalim huyo, na nikaahidi kumuunganisha naye kwa masharti kuwa amwambie hayupo tayari kuwa naye kingono, ila ampe hiyo nafasi ya mtoto na kuhusu pesa amwambie aje achukue kwangu. (Nilisema hivyo kwa kuwa nilijua kuwa asingeweza kuja kunidai pesa hiyo, kwani alitambua kuwa mimi nilikuwa najihusisha na masuala ya kuzuia na kupambana na Rushwa shuleni hapo nikiwa ni Mlezi wa Klabu ya wanafunzi).
Kwa bahati nzuri baada ya wawili hao kukutana na mzazi kutoa maelezo hayo, Mwalimu alishtushwa sana kuona mzazi akinitaja, alilalamika na hatimaye kumwambia yule mzazi ameharibu utaratibu wao, hivyo amlete mtoto hivyo hivyo aje aanze masomo.
Nilipewa mrejesho wa mazungumzo hayo na yule mzazi, nilifurahi kwani kilichokuwa kikihitajika pale ni nafasi ya masomo na kuzuia rushwa. yote yaliwezekana.
Kuhusu kumleta mtoto shule maandalizi yalikuwa yamefikia hatua nzuri isipokuwa kulikuwa na upungufu wa daftari 4 counter book quire 2. Kwa kuzingatia ukaribu wa mzazi huyo na mimi, nilianua kucgukua daftari nne dukani kwangu na kumkabidhi yule mzazi ili mtoto aanze masomo yake kwa wakati.
Kweli mtoto kesho yake aliletwa tayari kuanza masomo na muda wote nilikuwa naye karibu kama mtoto wangu.
Alisoma kidato cha kwanza kwa mahudhurio mazuri bila kufanya kosa lolote la kinidhamu Japo kwa upande wa utawala walikuwa wakisua sua sana kukamilisha uhamisho huo mtandaoni wakidai Hawana PREM-NUMBER ya mwanafunzi huyo. Baada ya kupewa taarifa hiyo kwa haraka nilishughulikia na uhamisho ukakamilishwa.
Mwaka 2023 Shule zilifunguliwa na mwanafunzi aliendelea na masomo yake ya kidato cha pili. Kutokana na utaratibu wa shule ilikuwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ni lazima wakae kwenye kambi zilizoandaliwa shuleni baada ya kukamilisha michango yao. Mwenzi wa pili mkuu wa shule alitangaza kuwa wanafunzi wote wasiohamia kambini waende wakafuate mahitaji kwa wazazi wao.
Mwanafunzi wangu naye akaondoka akaenda kufuata michango hiyo, kwa bahati mbaya ilikuwa ni wiki ya mwisho wa Usajili kwa ajili ya mitihani ya kidato cha pili, hivyo akiwa hajarudi shuleni wezake walipigwa picha kwa ajili ya usajili huo.
Siku ya mwisho ya usajili nilipewa taarifa ya kukosekana kwa picha ya mwanafunzi huyo na kuwa ilikuwa siku ya mwisho ya usajili. Baada ya kupewa taarifa niliamua kufanya mawasiliano na mzazi, ili ampige picha na anitumie ili niwakabidhi waweze kumsajili.
Hatukufanikiwa kupata picha siku hiyo kwani kule kijijini hakukuwa na mtu mwenye simu kubwa (Simu janja).
Niliamua kumtaarifu mwalimu aliyekuwa akishughulikia usajili huo, nikaambiwa mfumo umeshafungwa hivyo mwanafunzi itabidi akariri darasa.
Nilimpa taarifa baba mlezi wa mtoto(MAMA ALIKUWA AMESAFIRI) naye akaniomba nimshauri nini afanye ili mtoto asajiliwe. Baada ya kazi nilimtafuta akanielekeza kwake nikaenda kufanya mazungumzo ya kumsaidia mtoto. Tulikubaliana mimi nifuatilie kwa ngazi ya hapo shuleni ili utawala waone jinsi gani wanatatua tatizo hilo.
Niliwasilisha ombi ofisi ya Taaluma, na Mtaaluma akalipokea na kwenda kuliwasilisha kwa Mkuu wa Shule, Kwa bahati mbaya majibu ya mkuu wa shule yalikuwa Mimi niache kufuatilia tatizo la mtoto kwa madai kuwa hanihusu.
Nilipokea mrejesho huo kwa huzuni kubwa sana kutokana na mazingira halisi ya mtoto yule na kumtaarifu baba mlezi wa mtoto kwa kuwa wakati huo Mama mzazi alikuw nje ya mkoa kwa shughuli za kifamilia.
Baba mlezi aliendelea kufuatilia huku tukipeana ushauri kwa ukaribu mkubwa. Siku moja mlezi akiwa ofisini kwa mkuu wa shule ilionekana Mkuu wa Shule anamshauri mlezi amkaririshe mtoto baada ya kwenda kwa daktari wakatengeneze vielelezo vya kuthibitisha kuwa mtoto hakusoma vizuri kidato cha kwanza kutokana na kuumwa sana. Mzazi alikuwa tayari kwa hilo lakini mwanafunzi hakutaka kurudia kidato kimoja akiamini ni aibu kwa wanafunzi aliokuwa akisoma nao. Hivyo mkuu wa shule akasema basi itabidi wamhamishe aende akakariri katika shule nyingine.
Mlezi alinitumia taarifa ya mazungumzo hayo kwa njia ya ujumbe wa simu huku akiwa ndani ya osisi ya mkuu wa shule. MAJIBU niliyoyatoa ilikuwa ni mlezi kuomba ruhusa kwa mkuu wa shule kama usajili hauwezekani kwa ngazi ya shuleni basi aruhusiwe afanye mawasiliano na Katibu Tawala wa Mkoa au Baraza la mitihani, Mlezi akakubali na kuniomba nimpatie namba za watu hao atakapotoka ofisini.
NDUGU WANA JAMVI, HAPO NDIPO ULIKUWA MWANZO WA TATIZO. Siku hiyo ndipo mawasiliano yangu na mlezi yalipokoma na kesi zangu kuibuliwa ghafla. Nakumbuka hiyo ilikuwa ni tarehe 16/03/2023 nilipomshauri mzazi aombe ruhusa ya kufanya mawasiliano na ofisi za juu.
Tarehe 17/03/2023 mzazi aliitwa shuleni na mkuu wa shule na kuambiwa aandike barua ya kulalamika kuwa mimi nimekuwa nikimtongoza mtoto wake tangu alipoanza kidato cha kwanza na kumtumia kama mwuza duka wangu baada ya kusoma. Mzazi aliandika barua hiyo akithibitisha kuwa aliyafahamu mahusiano hayo,
Mtoto naye akaandikishwa barua kuwa nilikuwa nikimtongoza sana na kumpiga viboko vingi alipokuwa akinikataa.
TAREHE 20/03/2023 Mkuu wa Shule aliwatuma Walimu wa Nidhamu na Malezi wanihoji nikaitikia wito na kuhojiwa.
TAREHE 21/03/2023 Nilipewa barua na mkuu wa shule akitaka nijitetee kuwa sina mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo, niliipokea barua hiyo na kuijibu.
Baada ya siku chache nikaambiwa na mkuu wa shule nahitajika ofisi wa Afisa Elimu wa Kata (Mratibu kata), nilienda kule ofisini na kukuta wananisuburi ndani ya ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata na Afisa Mtendaji Kata akiwa ndiye mwenyekiti wa mazungumzo akiwa na Mkuu wa Shule na Mratibu. Alitumia nguvu sana kunilazimisha nikiri kumtaka kimapenzi mwanafunzi yule, sikuweza kukubali kwa kuwa haikuwa kweli. Mtendaji kata alipiga simu Polisi kumtaka askari aje aniweke chini ya ulinzi, baada ya Askari kufika na kupewa maelezo alihitaji ampate atakayekuwa mlalamikaji wa Kesi hiyo, Wote Watatu wakakataa na hivyo nikarihusiwa niondoke.
Baada ya wiki moja niliitwa na TSC Wilaya, nikapewa Notes na Hati ya Mashitaka tuhuma ikiwa ni “KUWA NA TABIA YA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI YANAYOASHIRIA KUTAKA KUFANYA NAYE TENDO LA NDOA).
Nilijibu na kuiwasilisha kwa wakati, waliunda tume ya uchunguzi wakaja kunihoji, na kuwahoji baadhi ya mashahidi mbele yangu, na wengine kwa njia ya simu.
JAMBO LA KUSHANGAZA waliandikishwa barua za maelezo kwa siri na kuambatanisha kwenye muhtasari wa mahojiano. Na yule mwanafunzi alikuwa ameshahamishwa hivyo mkuu wa shule akalazimishwa amsafirishe aje kuhudhuria mahojiano. Na mkuu wa shule akamwagiza mhasibu ahakikishe mwanafunzi huyo anasafirishwa tena kwa pesa ya shule.
Siku chache baadae niliitwa Tena ofisi ya TSC WILAYA NA KUPEWA BARUA YA KUFUKUZWA KAZI.
Kwa barua ile nilikata rufaa tangu mwezi July 2023 lakini mpaka sasa sijajibiwa kwa madai kuwa mpaka Raisi afanye uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Makao Makuu.
POLENI SANA NDUGU WANAJUKWAA KWA KUWACHOSHA NA MAELEZO HAYO MAREFU!
Aidha Nategemea kupata Ushauri na Misaada yenu ndugu zangu Nisije nikaishia kuwa Kichaa.
Sawa mkuu. Nashukuru sana1. Ni kweli haki huwa inapindishwa na ndio maana inatakiwa uchukue tahadhari kubwa kwenye mazingira unayokuwapo ili uwe salama. Acha kila mtu afanye kazi yake usipitilize.
Pia hukutoa taarifa takukuru hapo mwanzoni kabisa. ( Sijui kwanini)
2. Ndio, ilibidi uachie wataaluma na walimu wa malezi.
3. Hata ukifanikiwa kurudi kazini, punguza ukaribu uliopitiliza na wanafunzi wa Kike. Hii umefukuzwa kazi lakini Worst case scenario unaweza kufungwa au kupoteza maisha kabisa.
Ushauri mzuri lakini Kwa kesi ilipofikia RAS na DAS Hawana msaada tena kwake, sema Kwa nature ya suala lake kama kweli kosa ndo Hilo ilibidi awe amefukuzwa kazi na kapelekwa mahakamani akisubiria mvua 30Hakuna kesi ya kufukuzwa kazi kwa ushahidi wa kufikirika na mwepesi kama huo hata kama ni kweli ulimtongoza huyo binti. Labda kama ungekuwa umemtafuna kweli, na ukakamatwa na vielelezo/vidhibiti vya kutosha! Mfano ujumbe mfupi kwenye simu, umekutwa naye ndani ya chumba chako na huyo mwanafunzi, umempa ujauzito, nk.
Wewe endelea kupigania haki yako. Ikiwezekana nenda kwa DAS, RAS, nk kutoa malalamiko yako. Na baada ya hapo fanya utaratibu wa kuomba kuhamia shule iliyo kwenye Kata/Tarafa nyingine ndani ya hiyo Halmashauri yako ili kuepukana na hizo changamoto.
Hata kama angekuwa karibu vip, huwezi fukuzwa kazi Kwa tuhuma hiyo,ingethibitika bila shaka huyo angekuwa yupo gerezani maana Sheria Iko straight ukitembea na mwanafunzi ikathibitika ni miaka 30 jela, sasa mbona yupo uraiani?Inaonesha wewe mwl ulikuwa karibu na huyo mwanafunzi, kuna shida mahali haiwezekani kila kiongozi awe against wewe
Awe mkweli kesi nyepesi sana hiyo kama kweli Hilo ndo kosa lililomuondoa kazinKama una uhakika hukuwahi kuwa na matamanio ya kimapenzi na siyo tabia yako kuwatongoza wanafunzi,weka wakili.
Hiyo kesi ni ya kutungwa.
Vp,Mwl uliyembania kula mbususu alikuwa ni huyo mkuu wa shule?
Mimi ni Mtanzania mwezenu, nimeandika na kuweka katika jukwaa hili ili niweze kujengewa uwezo na ushauri na yeyote atakayeguswa na habari yangu; kama kuna sehemu haitaeleweka nipo kwa ajili ya ufafanuzi. Tafadhari siyo sawa kutumia lugha za matusi, kejeli na dharau kwani kila mtu ana changamoto yake.
Nimekuwa mtumishi wa Serikali katika kada ya ualimu tangu 2013-2023 mwezi wa tano. Nikiwa katika utekelezaji wa majukumu yangu nimekutana na changamoto nyingi sana za kawaida ambazo ni muhimu kazini.
Changamoto iliyonileta hapa ni hii sasa ambayo ni hatari kwa maisha yangu, familia yangu na jamii kwa ujumla.
Nilianza kanzi katika kituo xx, nikiwa huko nilikuwa karibu sana na mfanyakazi mmoja Askari wa Maliasili, nikiishi naye vizuri mpaka nahama kule mwaka 2017. Kwa bahati mbaya yule askari alikuja kupata changamoto za kiafya na akili na hivyo kupelekea familia yake kuyumba sana na hatimaye ndoa yake kuvunjika.
Mwaka 2022 january, nikiwa naendelea na majukumu nilikutana na Mke wa rafiki yangu(Yule Askari) akiwa amekuja shuleni kufuatilia taratibu za kumhamishia pale mtoto wake aliyetakiwa kuanza kidato cha kwanza shule niliyokuwa nafundisha awali, alifurahi sana kuniona kwani hakufahamu kama nilihamia pale. Baada ya kusalimiana alinijulisha juu ya changamoto alizopitia mpaka ndoa kuvunjika na tayari alikuwa ameolewa na mtu mwingine hatimaye tukaja kwenye changamoto ya uhamisho wa mtoto wake.
Kwa maelezo yake alifanikiwa kupewa namba za simu za makamu mkuu wa shule ili aweze kuomba nafasi, kwa bahati mbaya alipewa majibu kuwa nafasi zimejaa lakini atampatia namba za mwalimu mwingine ajaribu kuongea naye. Mama baadae alitumiwa namba hizo na kufanya mawasiliano na mwalimu huyo.
Majibu ya mwalimu yalikuwa Ahadi ya kupatikana kwa nafasi endapo mama [mzazi] atafanikiwa kuwapata watoto wengine angalau watatu ili wawe wanne na watatakiwa kulipia nafasi hizo kwa Tsh.20000 ili jumla iwe 80000. Majibu ya mzazi ilikuwa haiwezekani kutokana na ugeni wa mazingira na kutokufahamu ni nani mwenye uhitaji huo kwa haraka.
Basi yule mwalimu akamtaka mzazi atoe 50000 kwa ajiri ya nafasi ya mtoto. Kutokana na ugumu wa maisha ilionekana pesa kuwa ni nyingi mno, wakakubaliana kulipana 40,000/=, Lakini kadri muda ulivyozidi kwenda bado haikuwezekana kupatikana kwa pesa hiyo. Baada ya kuona hivyo mzazi ilibidi atoe taarifa hiyo kwa huyo mwalimu. Mwalimu aliyapokea majibu na kuamua kubadirisha masharti hayo na kumtaka yule mzazi kingono kwa siku tatu mfululizo ili ampatiye nafasi.
Kwa mujibu wa mzazi ilikuwa ni vigumu kwake kukataa na kukubali pia, lakini kutokana na uhitaji wake alikubali kufanya hivyo ili mtoto apate haki nafasi ya masomo, japo aliamini kuwa ingemuathiri sana kisaikolojia.
Hivyo siku niliyokutana naye pale shuleni ni siku aliyohitaji kuja kuonana na mwalimu kwa kuwa hawakuwahi kuonana.
Baada ya kunipa maelezo hayo nilimwuliza kama anamfahamu angalau kwa jina, akasema hamfahamu. Nikaamua kuomba namba yake, ilikuwa ni ngeni kwangu, lakini baada ya kuangalia kwenye mtandao wa M-Pesa niligundua kuwa ni namba ya mwalimu niliyemfahamu.
Kwa kumsaidia yule mama nikamwambia yule mama namfaham mwalim huyo, na nikaahidi kumuunganisha naye kwa masharti kuwa amwambie hayupo tayari kuwa naye kingono, ila ampe hiyo nafasi ya mtoto na kuhusu pesa amwambie aje achukue kwangu. (Nilisema hivyo kwa kuwa nilijua kuwa asingeweza kuja kunidai pesa hiyo, kwani alitambua kuwa mimi nilikuwa najihusisha na masuala ya kuzuia na kupambana na Rushwa shuleni hapo nikiwa ni Mlezi wa Klabu ya wanafunzi).
Kwa bahati nzuri baada ya wawili hao kukutana na mzazi kutoa maelezo hayo, Mwalimu alishtushwa sana kuona mzazi akinitaja, alilalamika na hatimaye kumwambia yule mzazi ameharibu utaratibu wao, hivyo amlete mtoto hivyo hivyo aje aanze masomo.
Nilipewa mrejesho wa mazungumzo hayo na yule mzazi, nilifurahi kwani kilichokuwa kikihitajika pale ni nafasi ya masomo na kuzuia rushwa. yote yaliwezekana.
Kuhusu kumleta mtoto shule maandalizi yalikuwa yamefikia hatua nzuri isipokuwa kulikuwa na upungufu wa daftari 4 counter book quire 2. Kwa kuzingatia ukaribu wa mzazi huyo na mimi, nilianua kucgukua daftari nne dukani kwangu na kumkabidhi yule mzazi ili mtoto aanze masomo yake kwa wakati.
Kweli mtoto kesho yake aliletwa tayari kuanza masomo na muda wote nilikuwa naye karibu kama mtoto wangu.
Alisoma kidato cha kwanza kwa mahudhurio mazuri bila kufanya kosa lolote la kinidhamu Japo kwa upande wa utawala walikuwa wakisua sua sana kukamilisha uhamisho huo mtandaoni wakidai Hawana PREM-NUMBER ya mwanafunzi huyo. Baada ya kupewa taarifa hiyo kwa haraka nilishughulikia na uhamisho ukakamilishwa.
Mwaka 2023 Shule zilifunguliwa na mwanafunzi aliendelea na masomo yake ya kidato cha pili. Kutokana na utaratibu wa shule ilikuwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ni lazima wakae kwenye kambi zilizoandaliwa shuleni baada ya kukamilisha michango yao. Mwenzi wa pili mkuu wa shule alitangaza kuwa wanafunzi wote wasiohamia kambini waende wakafuate mahitaji kwa wazazi wao.
Mwanafunzi wangu naye akaondoka akaenda kufuata michango hiyo, kwa bahati mbaya ilikuwa ni wiki ya mwisho wa Usajili kwa ajili ya mitihani ya kidato cha pili, hivyo akiwa hajarudi shuleni wezake walipigwa picha kwa ajili ya usajili huo.
Siku ya mwisho ya usajili nilipewa taarifa ya kukosekana kwa picha ya mwanafunzi huyo na kuwa ilikuwa siku ya mwisho ya usajili. Baada ya kupewa taarifa niliamua kufanya mawasiliano na mzazi, ili ampige picha na anitumie ili niwakabidhi waweze kumsajili.
Hatukufanikiwa kupata picha siku hiyo kwani kule kijijini hakukuwa na mtu mwenye simu kubwa (Simu janja).
Niliamua kumtaarifu mwalimu aliyekuwa akishughulikia usajili huo, nikaambiwa mfumo umeshafungwa hivyo mwanafunzi itabidi akariri darasa.
Nilimpa taarifa baba mlezi wa mtoto(MAMA ALIKUWA AMESAFIRI) naye akaniomba nimshauri nini afanye ili mtoto asajiliwe. Baada ya kazi nilimtafuta akanielekeza kwake nikaenda kufanya mazungumzo ya kumsaidia mtoto. Tulikubaliana mimi nifuatilie kwa ngazi ya hapo shuleni ili utawala waone jinsi gani wanatatua tatizo hilo.
Niliwasilisha ombi ofisi ya Taaluma, na Mtaaluma akalipokea na kwenda kuliwasilisha kwa Mkuu wa Shule, Kwa bahati mbaya majibu ya mkuu wa shule yalikuwa Mimi niache kufuatilia tatizo la mtoto kwa madai kuwa hanihusu.
Nilipokea mrejesho huo kwa huzuni kubwa sana kutokana na mazingira halisi ya mtoto yule na kumtaarifu baba mlezi wa mtoto kwa kuwa wakati huo Mama mzazi alikuw nje ya mkoa kwa shughuli za kifamilia.
Baba mlezi aliendelea kufuatilia huku tukipeana ushauri kwa ukaribu mkubwa. Siku moja mlezi akiwa ofisini kwa mkuu wa shule ilionekana Mkuu wa Shule anamshauri mlezi amkaririshe mtoto baada ya kwenda kwa daktari wakatengeneze vielelezo vya kuthibitisha kuwa mtoto hakusoma vizuri kidato cha kwanza kutokana na kuumwa sana. Mzazi alikuwa tayari kwa hilo lakini mwanafunzi hakutaka kurudia kidato kimoja akiamini ni aibu kwa wanafunzi aliokuwa akisoma nao. Hivyo mkuu wa shule akasema basi itabidi wamhamishe aende akakariri katika shule nyingine.
Mlezi alinitumia taarifa ya mazungumzo hayo kwa njia ya ujumbe wa simu huku akiwa ndani ya osisi ya mkuu wa shule. MAJIBU niliyoyatoa ilikuwa ni mlezi kuomba ruhusa kwa mkuu wa shule kama usajili hauwezekani kwa ngazi ya shuleni basi aruhusiwe afanye mawasiliano na Katibu Tawala wa Mkoa au Baraza la mitihani, Mlezi akakubali na kuniomba nimpatie namba za watu hao atakapotoka ofisini.
NDUGU WANA JAMVI, HAPO NDIPO ULIKUWA MWANZO WA TATIZO. Siku hiyo ndipo mawasiliano yangu na mlezi yalipokoma na kesi zangu kuibuliwa ghafla. Nakumbuka hiyo ilikuwa ni tarehe 16/03/2023 nilipomshauri mzazi aombe ruhusa ya kufanya mawasiliano na ofisi za juu.
Tarehe 17/03/2023 mzazi aliitwa shuleni na mkuu wa shule na kuambiwa aandike barua ya kulalamika kuwa mimi nimekuwa nikimtongoza mtoto wake tangu alipoanza kidato cha kwanza na kumtumia kama mwuza duka wangu baada ya kusoma. Mzazi aliandika barua hiyo akithibitisha kuwa aliyafahamu mahusiano hayo,
Mtoto naye akaandikishwa barua kuwa nilikuwa nikimtongoza sana na kumpiga viboko vingi alipokuwa akinikataa.
TAREHE 20/03/2023 Mkuu wa Shule aliwatuma Walimu wa Nidhamu na Malezi wanihoji nikaitikia wito na kuhojiwa.
TAREHE 21/03/2023 Nilipewa barua na mkuu wa shule akitaka nijitetee kuwa sina mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo, niliipokea barua hiyo na kuijibu.
Baada ya siku chache nikaambiwa na mkuu wa shule nahitajika ofisi wa Afisa Elimu wa Kata (Mratibu kata), nilienda kule ofisini na kukuta wananisuburi ndani ya ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata na Afisa Mtendaji Kata akiwa ndiye mwenyekiti wa mazungumzo akiwa na Mkuu wa Shule na Mratibu. Alitumia nguvu sana kunilazimisha nikiri kumtaka kimapenzi mwanafunzi yule, sikuweza kukubali kwa kuwa haikuwa kweli. Mtendaji kata alipiga simu Polisi kumtaka askari aje aniweke chini ya ulinzi, baada ya Askari kufika na kupewa maelezo alihitaji ampate atakayekuwa mlalamikaji wa Kesi hiyo, Wote Watatu wakakataa na hivyo nikarihusiwa niondoke.
Baada ya wiki moja niliitwa na TSC Wilaya, nikapewa Notes na Hati ya Mashitaka tuhuma ikiwa ni “KUWA NA TABIA YA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MWANAFUNZI YANAYOASHIRIA KUTAKA KUFANYA NAYE TENDO LA NDOA).
Nilijibu na kuiwasilisha kwa wakati, waliunda tume ya uchunguzi wakaja kunihoji, na kuwahoji baadhi ya mashahidi mbele yangu, na wengine kwa njia ya simu.
JAMBO LA KUSHANGAZA waliandikishwa barua za maelezo kwa siri na kuambatanisha kwenye muhtasari wa mahojiano. Na yule mwanafunzi alikuwa ameshahamishwa hivyo mkuu wa shule akalazimishwa amsafirishe aje kuhudhuria mahojiano. Na mkuu wa shule akamwagiza mhasibu ahakikishe mwanafunzi huyo anasafirishwa tena kwa pesa ya shule.
Siku chache baadae niliitwa Tena ofisi ya TSC WILAYA NA KUPEWA BARUA YA KUFUKUZWA KAZI.
Kwa barua ile nilikata rufaa tangu mwezi July 2023 lakini mpaka sasa sijajibiwa kwa madai kuwa mpaka Raisi afanye uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Makao Makuu.
POLENI SANA NDUGU WANAJUKWAA KWA KUWACHOSHA NA MAELEZO HAYO MAREFU!
Aidha Nategemea kupata Ushauri na Misaada yenu ndugu zangu Nisije nikaishia kuwa Kichaa.
Ndugu Kuna watu wanaroho mbaya sana hujajua tu hapati faida yoyote ila anakuwa comfortable tu wewe kufukuzwa kazi.kama upo kwenye utumishi wa umma huwezi shangaaa hivi vituMkuu
Ukiondoka hapo shuleni mkuu wa shule anapata faida fani?
Ukibaki hapo shuleni mkuu wa shule anapata hasara gani?
Ni kweli sipo kwenye ajira.Ndugu Kuna watu wanaroho mbaya sana hujajua tu hapati faida yoyote ila anakuwa comfortable tu wewe kufukuzwa kazi.kama upo kwenye utumishi wa umma huwezi shangaaa hivi vitu
Shukrani sana. Maelezo yako yamekaa sawa na nimeyaelewa vizuri. 🙏Mambo ya kuzingatia kwa waajiriwa:
1. Ukiwa kazini angalia salary yako tu.
2. Ufisuate mambo ya watu.
3. Acha uana harakati wa haki.
4. Wema usipitilize.
Either :
1. Hao jamaa kuna namna mna ugomvi wa chini chini na wameamua kukuangamiza, inaonekana wamefanikiwa.
2. Umeteleza kweli na kukula mtoto wa rafiki yako na sasa mambo kwisha haribika, pole sana, (Sikuhukumu, ni hisia tu.
Achana na hivi vita, kwa hapo ulipofikia, wewe ngoja barua ijibiwe na maisha lazima yaendelee, anza harakati nyingine za kutafuta kipato.
Nitarudia:
- Wema ni mzuri, ila usipitilize na kuingilia sana mambo mpaka utengeneze uadui na watu.
- Watu wanao amini katika ajira mara nyingi huwa na mapambano sana, wivu, chuki na vinyongo.
mie nahis mkuu alitaka rushwa katika regstration ya mtoto .ndo hyu ticha akampa mfumo wa siri wakufika ngazi za juu ..mkuu akaona anaharibiwa dili hapo...Ndio mkuu. Kwa madai yake amesingiziwa kumtaka huyo mwanafunzi na mwalimu mkuu akishirikiana na mzazi na mwanafunzi wamefanikisha kutengeneza ushahidi uliowezesha kumfukuza kazi.
Swali ni Kwanini mwalimu mkuu apate ushirikiano kutoka kwa mzazi na mwanafunzi kumuumiza mtu ambaye tangu wanamfahamu amekua akiwatendea wema na wamefanya hayo akiwa anajaribu kuwasaidia hitaji lao ambalo lilikuwa linakwamishwa na huyo huyo mwalimu mkuu?