Wapi sheria za tanzania zinakataza uhuru wa kuabudu ikiwa mtu kavaa sare za kazini? Hivi unajua chochote kuhusu haki na uhuru wa kuabudu kama unavyolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kwa maana hiyo unataka kusema ni marufuku kwa jeshi au askari kusali akiwa kambini au kituoni? Au kuna tofuati gani akifanya ibada zake akiwa na hizo uniform? Kuabudu mtu anaabudu akiwa na vazi lolote lile kwa kadiri imani yake inavyomruhusu na hakuna sheria hata moja inayomzuia mtu kufanya hivyo. Ingekuwa hilo ni kosa kama unavyodhani basi angeshawajibishwa na hao wakubwa lakini badala yake ndo kwanza walimpandisha vyeo.na madaraka juu..Ila Mungu akaona amchukue mapema maana huwenda hivyo vyeo/madaraka visingekuwa na kheri kwake au ndo ingekuwa sababu ya kumuasi mola wake mlezi.