Sifa zilizotajwa hapa ni kuwa na masters,jee hiyo ni sifa ya kuwa mkuu wa wilaya? Pia sifa nyingine ni kugombea ubunge viti maakumu, jee hiyo nayo ni sifa ya kufaa kuwa mkuu wa wilaya? Au hiyo ya kuwa HR Tanroad, tujiukize aneingia Tanroad mwaka gani na kaingiaje maana tunajua Tanroad iko chini ya wizara gani na wizara hiyo ilikuwa chini ya nani.
Kuna makosa makubwa yanafanyika kwa kufanya U DC kama kazi ya kutokea wakati kazi hiyo ni muhimu sana hasa kwa maeneo ya vijijini na inahitaji mtu mwenye busara nyingi kwani ina madaraka makubwa hata ya kunweka mtu korokoroni.
Binafsi sipingi kupewa uDC huyo kijana lakini kama anamahusiano na mteuzi basi lazima awe na sifa na uzoefu wa ziada usio na shaka vinginevyo hiyo ni dosari kubwa kwa mteuzi.
Wachangiaji wengi wanaonyesha kubisha kwa ushabiki tuu na kutoa mifano ya Museveni na Marais watangulizi, hayo ni makosa kosa kulilinganisha na kosa