Tusishabikie tusichokijua. Hapa suala siyo uwezo wa mteuliwa bali ni kukiuka misingi ya uadilifu. Hii siyo kazi ya uwalimu, udaktari au uhasibu, ni nafasi ya uongozi wa kisiasa. Hapa kuna mgongano wa kimaslahi. Meneji wa kampuni ya umma akimpa tenda kwenye kampuni anayoiongoza mwanae, anakuwa ametenda kosa. Siyo kwa sababu mwanae hana uwezo wa kutekeleza tenda bali tunakuwa hatuna uhakika kama tenda amepewa kwa sababu ya uwezo (ambao anao) au kwa sababu ya mahusiano ya kifamilia.
Wenye uwezo na masters siyo huyo tu. Kwa nini hao wote hawakupewa? Kwa hiyo hizi teuzi haziangalii uwezo na elimu pekee yake bali ni pamoja na vigezo vingine, huenda vya upendeleo vikawa ni miongoni.
Kama ni kweli yaliyoandikwa, nijuavyo mimi ni kwamba, kiongozi mwadilifu kabisa kabisa, kamwe asingeweza kufanya hivyo. Ndiyo maana Viongozi waliowahi kuwa na uadilifu wa hali ya juu kama Mwalimu hawakuawahi, hata mara moja kuwapa uongozi wanafamilia kwenye nafasi za uteuzi zinazofanywa na Rais, hakuwahi kufanya hata siku moja. Na haya mataifa yenye demokrasia, huwezi kuona kitu kama hicho hata siku moja. Haya yanatokea Afrika, na bahati mbaya sana watu wanatetea vitu vinavyokiuka misingi ya utawala bora.