Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

Usigeuze JF kuwa chungu cha majungu! Ongelea uwezo wake, sio uhusiano wake...ungejisikiaje kama ungekuwa wewe unaomba kazi sehemu afu unanyimwa simply because wewe una undugu na rais...tuletee CV na track record ya performance sio mijungu
conflict of interest,,ukielewa maana ya neon hilo hungetoa comment hiyo
 
''The tragedy of Africa is that Africans are in the business of canonizing thieves and demonizing its saints.'' - Prof. PLO Lumumba
 

Wakuu wa wilaya kama wateule wengine wa rais serve at the pleasure of the president. Rais ana dira na viwango alivyopanga. Katika vigezo vitatu alivyo sema katibu mkuu kiongozi sijaona kugombea ubunge maalum kama kigezo. You are not telling the truth.

Suala la conflicts of interest ni legitimate argument lakini inanonekata Happy ana sifa za kutosha. Niambie ktk vigezo vilivyotajwa na Katibu Mkuu Kiongozi ni kigezo gani hana? Speaking of kuwa na Masters degree; yes, I will take that as an accomplishment.
 
Mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ajibidiisheje? Wakati hivyo ni vyeo feki! Havina faida yoyote, vinalitia taifa hasara.! Upweke wa kukosa kazi unawafanya kuwa vituko kwenye jamii. Utaskia mkuu wa wilaya kakesha usiku akikamata maDJ kwenye bar. Vyeo hivi hakika vinahitaji kufutwa.
 
dah kumbe mh raisi ana moyo safi sana amejitolea kumlea binti na akamsomesha mpk masters kwa hili mh raisi awe mfano wakuigwa
 
Chakaza kwani wale watoto wa museven wana shida gani kama ishu ni qualification tu, sie tunasema ile kulelewa tu na mteuzi imemuondolea sifa kabisa. La sivyo hakuna tofauti na hao akina museven
 
Kwani wale watoto wa marais wa angola na uganda hawakua na sifa au, kwann dunia nzima imewashangaa
 
Mtoa uzi huna taarifa za kutosha, na hivyo sioni tija kuamini chochote ulichoandika. Mfano unasema 2015 hakugombea viti maalumu? Aligombea na alifika mpaka ngazi ya taifa dodoma. Kama mh JPM angetaka kumbeba alishindwa nini? Kimsingi sifa za U-DC Happy anazo hivyo acha majungu. Naona unajitesa "why nt me?"
 
Kama sifa anazo apewe tuache majungu vijana
 
Bado hujaweka wazi, nafasi ya kazi aliyopata kufanya ni hiyo ya HR wa Tanroads kulingana na Maelezo yaliyopo hapa. Na huo ulikuwa ndani ya wizara ya "baba" yake na sii nafasi ya kisiasa. Nyingine ni "kugombea" ubunge na kushindwa.
Tupeni sasa katika huo u HR nini kikubwa kilikuwa kinafanyika kumfanya awe bora kwa sifa mnazo mpa? Labda hili tukilipata kutoka kwa watumishi wa Tanroads litatuweka sawa ili kuondoa hiyo sintofahamu inayosababisha wamlinganishe na Museveni ambaye hana rekodi nzuri.
Happy atafanya kazi yake kwa ufanisi ikiwa haya yatawekwa wazi na kumuondoa kwenye kundi la "mtoto wa baba"
 
Kwani wale watoto wa marais wa angola na uganda hawakua na sifa au, kwann dunia nzima imewashangaa

Dos Santos na Museveni wanajulikama kuwa ni watawala wa ki imla. US Attorney General wa John F. Kennedy alikuwa mdogo wake Robert F Kennedy. Alipoteuliwa hakuwa na uzoefu wala sifa za kuwa mwanasheria mkuu but he was very successful in fighting against organized crime. How do you explain that? Was JFK a dictator?
 
Kabla hatujamwangalia Happy tuanze na Rose Kamili, Atropia, Ruth Mollel ............
Kipimo cha ufanyaji kazi wa ccm ni chadema kwa muktadha huu, si ndio!!!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…