Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

Mkuu, kuna watu wameangalia hawakuona mapungufu kwenye huu uteuzi. Sasa wameanza kuja na hoja dhaifu kama hizi

kweli kabisa, wangeteuliwa wao au ndugu zao wasingekuja na na hizi weak reasons.
 
Mtoa sadaka mzuri uanzia nyumbani kwake sio utoe sadaka nje wakati kwako kuna njaa.
 
Hata sioni tatizo kama sifa anazo

Mkuu shida ipo maana likija swala la kumwajibisha lazima afikirie mara mbili. Hawezi kumchukulia hatua kama atakazomchukulia mtu ambaye hawana uhusiano.
Waliozungumzia "conflict of interest" hawakuwa wajinga.
 
Hilo sio kosa kama huyo binti sifa anazo ni haki yake naye kutumia fursa
 
Mkuu inabidi urudi darasani hujui nini maana ya conflict of interest. Mkuu wa wilaya ni mwakilishi wa rais wilayani. Unapozungumzia conflict of interest always Ina involves two parties. Sasa hiyo conflict of interest ni Kati ya Nani na nani

ni kati yake yeye na mkuu wa wilaya
 
Hii inaonesha Kama ni Tanzania Sio Republic, bali ni Indirect Kingdom! Coz Katika Rupublic Hakuna Kupeana Nafasi au Cheyo Kwa Sababu Ya Ufamilia, Lakina Katika utawala Wa Kifalme Ndiyo Kila Mwanafamilia Ana Nyadhifa Katika Ufalme.

Asante "His Majesty" Magu Kwa Kumchagua "Princess" Happyness Senenda William.
 
Mleta Uzi umetuletea mada fikirishi. Tukumbuke JK alisema serikali yake haina ubia na mtu lkn matokeo yake tumeyaona, maswahiba kwa utitiri na ndugu. Mwingine aliwekwa getini kazi yake ni kukuunganisha Bwana Mkubwa then unamlipa 5m ili upige picha na bosi wake kuwatishia TRA ofisini.

JPM amedai hana wa kumlipa fadhila lkn tumeona swahiba Kitwanga na yule mbunge wa Mwanza wakiteuliwa uongozini. Sasa tunajadili "mtoto wake" wa kufikia. Kwanza alikuwa Tanroad wizara ya "baba" kabla hajawa Rais. Sote tunajua urafiki wa KARIBU Kati na baina ya Magu na Bosi wa Tanroad. Utasemaje "mtoto" hakubebwa toka huko hadi sasa U-DC?

Hoja si uwezo maana wenye uwezo kama huo ni wengi. Hoja ni nchi iliyooza kwa nepotism namna hii kwa mtu uliyetangaza kwenda tofauti ni lazima tuhoji. Na je, ni huyo pekee? Huko Tanroad alishindanishwa na nani?? Mods, sasa mpige tu ban Uzi huu.
 
Kama ingekuwa ww unaishi na ndugu yako, sifa zoooooooote anazo, utaacha kumsaidia ?
 
Kwahiyo ukiwa mtoto au ndugu wa mkulu unapaswa kufanya kazi gani?
 
2015 JPM angembebaje wakati yeye mwenyewe alikuwa anasubiri kubebwa? hulijui hilo?
 
Naona umbea ndo kazi sasa
 
tena atafanya kazi kwa nidhamu asimwangushe mlezi wake
 
Umewahi kujiuliza idadi ya ndugu na close relative wa mtawala aliyepita waliowekwa kwenye power? Mmoja kajadiliwa sana humu
Ni shedah, undugulization
Umewa
 

So What? Hii Ina mantiki gani na tija ipi ?
 
Wengi wamezoea kumuita "Happy Magufuli" kwa sababu amekulia na kulelewa na huyu mzee na hata kumsomesha.Nafikiri alianza na Ualimu Kigurunyembe Morogoro,baadae akaenda UDOM akasoma BBA na kisha alienda nje ya nchi kufanya Masters

Mara ya mwisho alikuwa Tanga TANROADS....Watu wa TANROADS Tanga wanampata(Wizara ya Baba)
Kweli kapata Wilaya ya Kisarawe
 
Kwani huyo ni ndugu yake? By the way Magufuli hanaga hizo. Aliwahi kumfunga mdogo wake kwa kuiba ng'ombe wa wazazi wake
Hujui kitu wewe! Usisababishe watu wakamwaga hapa kisa kizima cha Huyo ndugu yake watu wakashika midomo bure! Tuyaache maana yalikuwa yao kindugu na walimalizana.
Ila ukienda Chato ukasema hicho ulichosema utazomewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…