TANZIA Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wakili Avod Mmanda afariki Dunia. Atazikwa Mtwara na Serikali na wahudhuriaji wasiozidi 10

TANZIA Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wakili Avod Mmanda afariki Dunia. Atazikwa Mtwara na Serikali na wahudhuriaji wasiozidi 10

COVID-19 anahusika..?

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda 90%
Screenshot_2020-04-27-14-00-39.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa wilaya ya mtwara Evord Mmanda amefariki dunia alfajiri ya leo.

Huyu kiongozi kwao ni mkoani Kilimanjaro lkn kwa mujibu wa watu wa karibu tunaelezwa atazikwa huko mkoani mtwara.

Poleni wafiwa.

In God we Trust
 
RIP Wakili Mmanda nilikuwa Mpenzi mtazamaji wa Ijue Sheria...ITV

Nilikupotezea ulipojinasibu wewe ni CCM na kuchukua Fomu ya kura za Maoni.kugombea Ubunge Rombo... Ulipolipwa Fadhila kwa KUJINASIBU kwako... Niliacha kukufuatilia... RIP
 
“Tumekubaliana na familia kwamba sisi Serikali ndiyo tutakaosimamia mazishi yake…na hakutakuwa na kusafirisha mwili…atazikwa hapa Mtwara…na hatazikwa na zaidi ya watu kumi,” Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akielezea taratibu za mazishi ya liyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda aliyefariki dunia Aprili 26, 2020 katika Hospitali ya Rufaa Ligula alipokuwa akipatiwa matibabu.

#AzamTVUpdates
Mbona leo asubuhi highway dodoma-mwanza nimekutana na costa imebeba jeneza na wafiwa, inasafirisha kutoka dar kwenda huko shinyanga. Inamaana hao serikali imewaruhusu ila huyu mkuu wa wilaya serikali imeamua azikwe mtwara! Ummy Wekeni takwimu vzr ili zisaidie kuokoa walio hai.
 
Sio kweli. Credible information ni kuwa amefariki kwa Corona.
And by the way, watu bado wanakusanyika misikitini na makanisani, mbona serikali inaruhusu.
Ni kweli Coronavirus kabisa. Maana kweli kwa nini familia yake iombwe kuja Mtwara kumzika ?
 
Inasemekana mazishi yameshafanyika tayari. Duh hii corona ina set standards..

Sent using iphone pro max
 
Mbona leo asubuhi highway dodoma-mwanza nimekutana na costa imebeba jeneza na wafiwa, inasafirisha kutoka dar kwenda huko shinyanga. Inamaana hao serikali imewaruhusu ila huyu mkuu wa wilaya serikali imeamua azikwe mtwara! Ummy Wekeni takwimu vzr ili zisaidie kuokoa walio hai.
Mr ukifa kwa ugonjwa wa kawaida unasafirishwa tu, Juzi hapa kuna rafiki yangu amefariki akiwa dar es salaamu kasafirishwa hadi mbeya kwenda kuzikwa amezikwa ijumaa iliyopita,
Hapo hesabu tu kua DC kaenda na Covid- 19

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom