Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameielekeza Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kushusha mara moja bei za maji

Mpk wakuu wa wilaya nao wanatoa matamko hizi teuzi mama aziangalie kwa jicho la tatu..!!
Anyway bro mtatiro uwe unampa kazi kaka Luka akupambe hii ya kuja mwenyewe front unajichoresha 🤣🤣🤣🤣
Luka mpaka akukubali kwanza

Utasikia Mtatiro awatoa machozi ya furaha wanashinyanga
Huku wakibubujikwa na machozi walijotekeza kwa wingi 😄😄😄😄
 
Uzalishaji wa maji na kuyatibu unatofautiana sehemu moja na nyingine.

Hapo gharama za uendeshaji lazima zitofautiane, ndipo inaibuka bei tofauti.

Hata mafuta yanatofautiana bei kati ya mkoa na mkoa

Bei ya maji nchi nzima lazima iwe moja, issue ya gharama ya treatment na uzalishaji kutofautiana sio sbb hata kidogo..

Alafu una compare eti bei za mafuta na maji ku back up pointless yako ya utofauti wa bei? Hivi can you do such a comparison kweli? Ya maji na mafuta why their cap prices differ from one place to another?
 
duuuh kwahyo hataki kabsaa serikali ipate mapato??
 
MTATIRO ASHUSHA BEI ZA MAJI SHINYANGA VIJIJINI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameielekeza Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kushusha mara moja bei za maji kwenye kata mbalimbali za jimbo la Shinyanga Vijijini na kutaka bei mpya ziwe sawa na zile za Shinyanga Mjini mara moja.

Akiwa katika Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi, DC Mtatiro ameelekeza kuanzia tarehe 04.04.2024 bei za maji zishuke.

Mwakilishi wa Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola amekiri kupokea maelekezo hayo kwenye mkutano huo na kuanza kuyatekeleza mara moja.

Kuanzia sasa Bei za Maji kata za Didia, Tinde na Iselamagazi zenye jumla ya wakazi takribani 55,000 itakuwa shilingi 1,490 kwa wanaotumia uniti 1 - 5 kwa mwezi na shilingi 1,700+ kwa wanaotumia uniti 6+.

Wananchi wa kata hizi kwa miaka mitatu mfululizo wamekuwa wakilipa bili za maji kwa uniti moja shilingi 2,525 na hakukuwa na suluhu kwa sababu SHUWASA na EWURA walikuwa wanavutana katika kufanya uamuzi husika.

Katika mkutano huo, DC Mtatiro amekiri kumpigia simu Waziri wa Maji Juma Awesso ambaye ameunga mkono mapendekezo ya Wakili Mtatiro.

DC Mtatiro anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa zote 6 za Wilaya ya Shinyanga, ikiwa ni wilaya yake ya pili kuwa Mkuu wa Wilaya tangu Rais Samia amhamishe kutoka Tunduru Mkoani Ruvuma.
View attachment 2954245

Hivi Mtatiro una IDs ngapi humu?
 
Luka mpaka akukubali kwanza

Utasikia Mtatiro awatoa machozi ya furaha wanashinyanga
Huku wakibubujikwa na machozi walijotekeza kwa wingi 😄😄😄😄
😂😂😂😂 kaka Luka kikubwa uzingatie kuweka mafuta kwenye namba yake ya simu, atakusifia asubuhi, mchana na usiku
 
MTATIRO ASHUSHA BEI ZA MAJI SHINYANGA VIJIJINI

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameielekeza Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kushusha mara moja bei za maji kwenye kata mbalimbali za jimbo la Shinyanga Vijijini na kutaka bei mpya ziwe sawa na zile za Shinyanga Mjini mara moja.

Akiwa katika Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi, DC Mtatiro ameelekeza kuanzia tarehe 04.04.2024 bei za maji zishuke.

Mwakilishi wa Mkurugezi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola amekiri kupokea maelekezo hayo kwenye mkutano huo na kuanza kuyatekeleza mara moja.

Kuanzia sasa Bei za Maji kata za Didia, Tinde na Iselamagazi zenye jumla ya wakazi takribani 55,000 itakuwa shilingi 1,490 kwa wanaotumia uniti 1 - 5 kwa mwezi na shilingi 1,700+ kwa wanaotumia uniti 6+.

Wananchi wa kata hizi kwa miaka mitatu mfululizo wamekuwa wakilipa bili za maji kwa uniti moja shilingi 2,525 na hakukuwa na suluhu kwa sababu SHUWASA na EWURA walikuwa wanavutana katika kufanya uamuzi husika.

Katika mkutano huo, DC Mtatiro amekiri kumpigia simu Waziri wa Maji Juma Awesso ambaye ameunga mkono mapendekezo ya Wakili Mtatiro.

DC Mtatiro anaendelea na ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa zote 6 za Wilaya ya Shinyanga, ikiwa ni wilaya yake ya pili kuwa Mkuu wa Wilaya tangu Rais Samia amhamishe kutoka Tunduru Mkoani Ruvuma.
View attachment 2954245
Na hapa wanatuuzia maji yaliyochanganywa na maji ya tope.
Watumiaji wa maji ya ziwa Victoria sehemu nyingine zote wanafaidi shy tunatumia maji yana harufu ya vyura
 
Hongera kwake,

Unit Moja Kwa 2500 ni kubwa mno, matumizi ya familia Moja hutumia Si chini ya unit 10 ambayo ni 20,000 Kwa mwezi.

Hata Hilo punguzo Bado, Inatakiwa unit 1 angalau iwe 1,300/=
Unit 1 kwa Shs 2,500 maana yake ndoo moja ya Lita 20 ni sawa na Shs 50, fedha hizi zinatumika kulipia umeme, kununua madawa ya kutibu maji, kulipia mishahara ya watumishi, kufanya matengenezo ya miundombinu ya maji pale inapoharibika, kufanya upanuzi wa miundombinu ya maji kwa wateja wapya. Je unaona hela hiyo inatosha? Lakini nikuulize, wewe kwa siku unakunywa Lita ngapi za maji ya kununua kwenye chupa? Mbona unaponunua maji ya chupa ya Lita 1.5 kwa sh 1000 au 1500 haulalamiki? Nafikiri kabla ya kuandika tujitafakari au tuulize kwanza tuelewe.
 
Maji ya chupa ya 500 ml kuuzwa 1000 Kwa Lita hiyo SI hoja.

1. Nikikuuliza kwanini maji unayodai mnayagharimia kuyatibu kwanini hayana ubora wa kunyweka kama maji salama ya kunywa kama S. Afrika utajibu ?

2. Iweje shinyanga unit 1 iuzwe 2,500 wakati maji hayo hayo Kutoka ziwa hilo Hilo Mza yanauzwa 1200 Kwa unit 1?

Majibu tafadhali 🙏
 
Unit 1 kwa Shs 2,500 maana yake ndoo moja ya Lita 20 ni sawa na Shs 50, fedha hizi zinatumika kulipia umeme, kununua madawa ya kutibu maji, kulipia mishahara ya watumishi, kufanya matengenezo ya miundombinu ya maji pale inapoharibika, kufanya upanuzi wa miundombinu ya maji kwa wateja wapya. Je unaona hela hiyo inatosha? Lakini nikuulize, wewe kwa siku unakunywa Lita ngapi za maji ya kununua kwenye chupa? Mbona unaponunua maji ya chupa ya Lita 1.5 kwa sh 1000 au 1500 haulalamiki? Nafikiri kabla ya kuandika tujitafakari au tuulize kwanza tuelewe.
Ingekuwa kila sekta inapiga hesabu kijinga kama hivi nchi isingekalika!
 
Hawajakomaga tu kufanya maamuzi kwenye majukwaa? Nchi hii tuna viongozi wa hovyo hovyo!
 
Uzalishaji wa maji na kuyatibu unatofautiana sehemu moja na nyingine.

Hapo gharama za uendeshaji lazima zitofautiane, ndipo inaibuka bei tofauti.

Hata mafuta yanatofautiana bei kati ya mkoa na mkoa
Ni vyema wakatafuta bei ya wastani. Wa kijijini apunguziwe na wa mjini wa ongezewe ili wote walipe bei sawa.
 
Nchi ya kipuuzi sana hii! Bei tofauti Kila Mahali? Hovyo sana!
 
Back
Top Bottom